MAAGIZO
- Jibu maswali yote
- Majibu yote ni lazima yaandikwe kwa lugha ya kiswahili
MASWALI
UFAHAMU
Soma makala haya ujibu maswali yafuatayo
Utotoni niliamini kwamba kusoma ndiko ufunguo wa kila kitu ulimwenguni kwa jinsi kunavyoonekana kuwatoa watu katika uzuzu, ukata na ugonjwa: na kuweka kwenye maisha bora ya mwangaza wa kujua kusoma na kuandika, utajiri wa kuweza kuvaa hata suti ya vipande vitatu, na kuwa na afya ya kuonekana kwa kitambi. Hizo ni zamani zile ambapo shule ya vidudu haikuwa sharti la mtoto kukubaliwa katika darasa la kwanza. Mtoto angelisha ama kusaidia kwa kazi za nyumbani mpaka kufika umri wa miaka kumi kisha, kufumba na kufumbua, afisa wa serikali angeonekana akishauriana na wazazi wa mtoto. Matokeo yangekua mtoto huyo kuanza safari ndefu ya kila siku, apate asipate chakula.
Mimi kwa upande wangu sikujali maisha pata-nenda shule, kosa-bado-neda-shule. Sikujali kero za baridi kali wala karaha za vua la asubuhi. Kuanzia utotoni niliwahusudu wenzangu waliokuwa wakirauka kiasi cha kufikiriwa walilala kwa shati na kaptula zao, au kwa blauzi na skati na kaptula zao. Nilipendezwa na unifomu zao nikatamani na hata kuapa kwamba siku moja nitavaa kama wao na kutembea kwa maringo kama wao. Zaidi nilitamani kufika walikokuwa wakienda na kufanya walivyokuwa wakifanya huko.
Penye nia hapakosi njia. Nia yangu ilidhihirika nilipojiunga na darasa la kwanza. Darasa la kwanza lilinisoma kisogo baada ya siku mbili tu. Nalo la pili likanipungia mkono baada ya juma moja. Miaka mitano baadae nilikutana na kiunzi cha kwanza kwenye mtihani wa kitaifa wa chumba cha saba uliokuwa kifungua mlango wa kuingia kidato cha kwanza.
Baada ya miaka minne nilikutana na mlango funge mwingine nilibisha na ukanifungukia kwa kutia fora katika mtihani wa kiwango cha elimu ya pili. Katika miaka miwili iliyofuatia nilijiunga na shule maarufu ya kitaifa siku hizo.
Masomo hayakuendelea kuwa mteremko kwangu kwani uchechefu wa karo na masurufu ulimaanisha kuwa siku nyingi nilikuwa nje ya kuta za darasa letu. Hata hivyo nilijifunga masombo. Hatimaye nilifunguliwa mlango wa kuingia ndaki.
Baada ya kuhitimu kwa shahada ya kimsingi ya uzamili, kisha uzamifu au daktari falsafa hatimaye, nilifanywa meneja kufikia leo. Hata nikiwa ukubwani bado nazidi kusoma na kutafiti ili nisiote ukurutu wa akili.
Cheo na madaraka haya ya umeneja yamaanisha kila siku nivae suti kamili na shati nyeupe pe, amabayo shingoni imeambatanishwa na kipande maalumu cha kitambaa kinacholewalewa kifuani. Nijiangaliapo kiooni hujifananisha na mtu ambaye amejitia jitanzi shingoni.
Nina kitambi ambacho labda ni taashira ya utajiri. Hata hivyo ingawa mimi si mwenye sauti kubwa kiuchumi, ninaweza kujivunia elimu yangu ilivyoniwezwsha kujimudu kidogo maishani. Sasa nina shamba langu mwenyewe, nyumba yangu mwenyewe ambayo imejaa mali yangu mwenyewe. Nina redio yangu mwenyewe, rununu yangu mwenyewe na wanyama wangu mwenyewe.
Lakini mwenzangu ambaye zilimwishia ukingoni katika shule za nasari, hana elimu, pesa wala mahali pa kuzikiwa wakati mpira utakapomwia mwingi.
MASWALI
- Eleza imani ya mwandishi kuhusu elimu (alama3)
- Taja dhiki zilizomkabili mwandishi alipokuwa shuleni (alama2)
- Onyesha uhusiano uliopo kati ya elimu, kazi na ukwasi kwa mujibu wa habari hii (alama3)
- Ukirejelea makala haya, fafanua msemo,’elimu ni bahari haina kikomo’ (alama3)
- Hatima ya wale ambao hawakupata elimu ni ipi? (alama2)
- Badala ya maneno yafuatayo mwandishi angetumia msamiati gani? (alama3)
- Nilijifunga masombo
- Ndaki
- Taashira
UFUPISHO (Alama 15)
Dhuluma kwa wanawake sio matokeo ya sasa baada ya uhuru, bali ni matokeo ya hali iliyokuepo tangu enzi za mababu zetu; kabla ya ukoloni. Kubaguliwa na kudhulumiwa kwa wanawake kiasi kunaoana na kunyonywa kwake kijamii kunakoshuhudiwa siku nenda miaka rudi.
Elimu ya jadi ilimwandaa mwanamke kuwa chombo kitiifu cha mwanamume. Mwanamke aliandaliwa katika unyago na katika mfumo mzima wa malezi kuwa chombo cha kutumikia mwanamume-kumstarehesha, kumfariji, kumlisha na kumzalia watoto. Mwanamke tangu jadi hakuruhusiwa kushiriki katika shughuli za kisiasa na utawala wala hakuna mtu aliyeamini kwamba mwanamke angeweza kushikilia wadhifa wowote wa uongozi.
Demokrasia ya jadi naihusudu sana; ambapo wazee walikaa chini ya mbuyu na kuamua mambo ya jumuiya. Mahakama ya kijiji ilikuwa aghalabu ni ya wazee na wanaume peke yao. Hakukuwa na mwaname aliyeshirikishwa, hata kama alikua ajuza. Sifa waliokua nayo wanawake ni ile ya usihiri na uganga. Mwanamke yeyote aliyezeeka alidhaniwa kuwa bingwa wa uchawi, ulozi na ushirikina. Kwa hivyo, wanawake ndio waliokuwa washirikina wakubwa, maana fursa ya kupata elimu pana zaidi hawakuwa nayo. Si ajabu kuwa mwanamke alipojitokeza na kusema jambo la busara, aliuupza na pengine kutukanwa hadharani.
Kwa bahati nzuri, kumezuka mwamko uliotuingiza katika enzi mpya. Vita vya wanawake vya kujihami na kujiendeleza katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume vimetapakaa kote katika kila sehemu ya dunia. Wanawake wengi wamekiuka misingi na mizizi ya utamduni na kung’oa asasi za kijamii na itikadi ambazo daima zimeendelea kumnyanyasa na kumuumbua utu mwanamke tangu jadi. Watetezi wa haki za wanawake zamani walilaumu suala la serikali za mataifa mwaka hadi mwaka. Huku maswala ya wanawake ya kijamii, uut na utamaduni yakishangiliwa kupitishwa, watetezi wameeleza wasiwasi wao ikiwa kupitishwa kwa maazimio kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wanawake kimataifa au katika nchi moja. Fauka ya hayo, baadhi ya wachunguzi wanaonelea kuwa maazimio mengi hayadokezi hatua za kufikiwa haki za wanawake.
Maazimio mengine yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake, kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa, na ushirikiano wa kimataifa, majukumu yao katika jamii, mfuko wa umoja wa Mataifa wa wanaweka (Unifem) na kuimarisha hadhi ya wanawake katika sekretariati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa shughuli nyingine katika mkabala huu.
Wanawake wameonyesha vipaji vyao katika nyanja mbalimbali za maisha; siasa, uchumi, utawala na kadhalika. Wanawake wamejikakamua na kudhihirisha kuwa wao pia wana jukumu muhimu la kutekeleza ili kuyaongoza maisha yao na ya watu wengi. Wadumishaji wa dhuluma za kijinsia hawana budi kusalimu amri na kuukubali ukweli huu, wapende wasipende. Mtazamo juu ya haki sawa unatokana na kukubaliwa na kuondolewa kwa aina zote za ubaya dhidi ya wanawake wanaojitolea mhanga kutetea hadhi yao pamoja na ya wanyonge wengine. Wao huonekana kama waasi, wapinga mila na watovu wa utii.
MASWALI
- Bila kubadilisha maana asilia, fupisha aya tatu za kwanza.(Maneno 45-55) (alama6)
Matayarisho
Jibu - Kwa kurejelea aya tatu za mwisho, pambanua hoja muhimu zinazoguziwa na mwandishi (Maneno 60-65) (alama9)
Matayarisho
Jibu
MATUMIZI YA LUGHA
- Andika maneno yenye vitamkwa vya sifa zifuatazo (alama2)
- Kikwamizo sighuna cha kaakaa gumu, irabu ya nyuma juu, kikwamizo ghuna cha kaakaa laini, irabu ya nyuma juu, kitambaza na irabu ya mbele juu.
- Taja sifa zinazonyesha usawa baina ya jozi hizi
/gh/ na /ng’/
/f/ na /v/
- Andika neno lenye muundo ufuatao wa tamko kamili katika neno (alama2)
K,KI,KKI
KiK - Ainisha mofimu katika neno hili (alama2)
Kifurahieni - Tunga sentensi ukitumia nomino uga (wingi) pamoja na kivumishi cha pekee cha kusisitiza na kielezi cha kiasi (alama2)
- Andika katika hali ya ukubwa (alama2)
Wanawake wale wana midomo mikubwa inayotisha - Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo (alama4)
- Mwanafunzi aliadhibiwa kwa kuwa alikosea mwalimu (badilisha maneno yaliyopigwa msitari kuwa nomino)
- Mapambano baina ya mwanadamu na mazingira yalizaa fasihi (anza kwa fasihi)
- Margret ni mkakamavu. Onyi ni mkakamavu pia. (unganisha iwe sentensi moja yenye kihusushi cha kulinganisha)
- Maji ambayo wanakunywa ni hatari (tumia hali ya mazoea bila ‘amba’)
- Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi kinachofanya kazi ya kiwakilishi (alama2)
- Andika wingi hali katavu (alama2)
Nyanya na babu : Sisi ndisi wakulima - Andika sentensi moja kwa wakati uliopita hali endelevu ukitumia kitenzi – P - katika kauli ya kutendana (alama2)
- Tumia kijalizo katika sentensi kama: (alama2)
- kiwakilishi
- kielezi
- Tunga sentensi moja kutofautisha maneno haya: taka na daka (alama2)
- Andika kinyume (alama2) Mjomba hakumtwika nyanyake mzigo hivyo akapata laana
- Onyesha kiima, chagizo na aina za shamirisho (alama2)
Mpodozi ambaye alikuja juzi alipaka kucha rangi jana jioni mara kadha wa kadha - Eleza matumizi ya ‘KU’ katika sentensi hii (alama2)
Alikusaidia kwenda kule wakati hukuwa na uwezo wa kusoma - Changanua sentensi hii ukitumia kielelezo cha msitari (alama2)
Hasikii la mwadhini wala mtekaji msikitini - Bainisha maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo (alama2)
Mwakuona angefuata somo angefaulu - Eleza matumizi mawili ya alama ya kibainshi (alama1)
- Tunga mfano mmoja wa sentensi kuzingatia muundo ufuatao (alama2)
S -¬ (RH + RH + t + N + V ) - Neema amekuwa kiduchu toka utotoni lakini mwenye akili nyingi akitazama unaona kama anayezisoma a akili zako (tumia methali mwafaka kuafiki maelezo hayo) (alama1)
- Jaza pengo (alama2)
- Mtu ni kwa mja, ukongo ni kwa ............................................ na kiate ni kwa ........................................
- Tunapotaka kuomba radhi kabla ya kutamka jambo ambalo linaweza kumuudhi mtu tunasema ..................................... ilhali tunapotamka kuonyesha mshtuko au jambo la hatari tunasema .....................................
ISIMU JAMII(alama10)
Jambo Kenya! Nachukua fursa hii kumkaribisha mheshimiwa Profesa Chan kutoka jamhuri ya watu wa Uchina. Kufikia hapo kila kitu ki barabara tunapoendelea kujadiliana kuhusu swala hili la mabadiliko ya hali ya anga ulimwenguni. Suala hili linaendelea kupunguza idadi ya watu duniani. Nawaomba tusimame kuwaheshimu walioondoka.
(anawaashiria wasimame)
Asanteni sana
-
- Tambua sajili hii (alama1)
- Eleza sifa za sajili uliotaja hapo juu ukizingatia kifungu (alama4)
- Order! Lazima kutii mpangilio! Katili hauruhusiwi kuongea bila ruhusa. Polisi, mpelekeni nje.
- Tambua sajili hii (alama1)
- Fafanua sifa zozote nne ambazo zingejitokeza iwapo mazungumzo yangeendelea (alama4)
MWONGOZO
- Kusoma ndiko ufunguo wa kila kitu
Hawatoa watu kwatika ujinga, uzuzu, umaskini na ugonjwa
Huwaweka watu kwenye maisha bora ya mwangaza
Huwaweka watu kwenye utajiri (alama3) - Kukosa chakula
Baridi kali
Mvua ya asubuhi
Ukosefu wa karo na masurufu mengine (alama2) - Elimu na kazi - mtu aliyeelimika aliweza kuajiriwa
Elimu na ukwasi – elimu humwezesha mtu kujimudu maishani ingawa sio lazima awe tajiri - Mwandishi ameelimika sana /amepata shahada mbalimbali na kufanywa meneja lakini anazidi kusoma na kufanya utafiti (alama3)
- Hakuna jibu
- Kutojimudu maishani
Kutojimudu kiakili - Nilijitahidi/nilijikakamua
Ndaki - chuo kikuu
Ishara/ dalili
UFUPISHO
- Dhuluma kwa wanawake ni hali ya tangu jadi
Elimu ya jadi ilimwandaa kama chombo cha mume
Taasubi ya kiume
Mwanamke kama msihiri na mganga
Kupuuzwa na kutukanwa hadharani
Demokrasia iliyomfungia inje (alama6) - Matokeo ya elimu ya kisasa
Mwanamke wa enzi mpya
Mwanamke kujiamini na kujiendeleza
Vipaji katika nyanja mbalimbali
Kikwazo cha itikadi na mila za kiasili
Wadumishaji wa dhuluma wasalimu amri
Mwanamke anayeongoza maisha yake
Hadhi ya mwanamke kukua (alama8,1mtiririko)
MATUMIZI YA LUGHA
-
- Shughuli (alama1)(1/0)
- Za kaakaa laini
Za mdomo meno (alama1)
-
- Mlango
- bin
- Ki – furahi – e - ni (alama2)
ngeli mzizi rai wingi - Nyuga zenyewe zilinadhifishwa mara kadhaa (alama2)
- Majanajike yale yana madomo makubwa yanayotisha (alama2)
-
- Adhabu iliyotolewa kwa manafunzi kwa kufanya makosa /Makosa ya mwanafunzi kwa mwalimu yalimfanya apewe adhabu/mwalimu alimpa mwanafunzi adhabu baada ya kufanya makosa (alama1)
- Fasihi ilizushwa na mapambano baina ya mwanadamu na mazingira (alama1)
- Magret ni mkakamavu sawa na /zaidi ya/kuliko/kama Onyi (alama1)
- Maji wanywayo ni hatari (alama1)
- Ambaye ni mlafi ameadhibiwa (alama2/0)
- Akina/kina nyanya na mababu : Sisi si wakulima (alama2/0)
- Watoto walikuwa wanapana chakula (alama2/0)
- kumbe/Ndiye huyu (W) (alama1/0)
Mtoto amekuwa sokoni (E) (alama1/0) - Taka - kuwa na haja ya kitu /jambo fulani (alama2)
- karibia kutokea
- uchafu
Daka - kamata kitukilichorushwa - Tunda changa
- Sehemu iliyokwenye ukuta kuwekea vitu
- Mjomba hakumtua nyanyake mzigo hivyo akakosa baraka (alama2/0)
- kiima - mpodozi ambaye alikuja juzi
chagizo - jana jioni mara kadha wa kadha
shamirisho kitondo - kucha
shamirisho kipozi – rangi (4marks) - Alikusaidia - nafsi ya pili umoja
Kule - mahali/ngeli ya PA-KU-MU
Hukuwa - wakati uliopita kanushi
Kusoma - kitenzi jina - S – KN(ø) + KT(T + W + N + U + W + N + E)
- Somo - Mwalimu wa jandoni/ukungani
- Maarifa
- Mtu ambaye wanarejelea kuwa jina moja
- Rafiki (alama2)
- Kutofautisha ng’ na ng
- Kufupisha maneno mfano `tu
- kufupisha miaka `98
- Miongoni mwa wanariadha wa Kenya kuna wanariadha hodari (alama2)
- Usione wembamba wa reli garimoshi hupita
-
- Maradhi/Uwele
Yatima (alama1) - Ashakum
Toba! (alama1)
- Maradhi/Uwele
ISIMU JAMII
-
- Sajili ya itifaki - Mheshimiwa profesa Chan anawakilisha jamhuri ya watu wa uchina
- Lugha ya adabu - naomba msimame
- Hutaja vyeo vya wahusika pamoja na nchi zao mfano; mheshimiwa profesa Chan kutoka Uchina
- Maneno machache ya utangulizi yasemwe kwa lugha ya mwenyeji m.f Jambo Kenya?
- Maneno sahili ili kufanikisha mawasiliano mfano; naomba msimame
- Huhitaji matumizi mwafaka ya shadda, toni na mkazo, mfano barabara
- Hutumia tafsida kuficha ukali wa lugha kwa mfano; swala hili linapungua idadi ya watu duniani
- Msamiati hulingana na mada mfano, haya ya anga ya ulimwengu
-
- Sajili ya mahakamani
-
- Kunukuu vifungu vya sheria kutoka kwenye katiba au kesi zilizo amriwa hapo awali Kwa mfano: Kwa mujibu wa sheria, kifungu nambari 12, ibara ya tano, sehenu ya A.....
- Matumizi ya msamiati maalum unaohusiana na shughuli zinazoendeshwa mahakamani; kama vile wakili, dhamana, rufaa
- Lugha ya heshima hasa hakimu na jaji anaporejelewa au kuzungumziwa na hata mawakili wanapozungumza wenyewe kwa wenyewe.
- Lunga ya kunyenyekea na inayodhihirisha kiwango cha heshima cha hali ya juu, kama vile Bwana jaji na Msomi rafiki yangu.
- Usakaji wa ushahidi kutoka kwenye matini na mashahidi ili kuwawezesha mahakimu kuafikia uamuzi ufaao.
- Matumizi ya udadisi kwa njia ya kuwahoji mashahidi.
- Matumizi ya maneno ya kukopa hasa ya kilatini kama vile nole proseque, harbeas corpus na amicus curie.
- Maelezo marefu au ya kimzunguko, kwa mfano; “wewe Kahindi wa Hindi, unashtakiwa kuwa tarehe 12 mwezi wa Desemba mwaka wa 2013, mkiwa na washukiwa wengine ambao hawako mahakamani mlihusika katika wizi wa kimabavu ambapo mliishambulia familia ya Bw. Pokoyoyo.....”
Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Cekana Mock Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students