MAAGIZO
- Jibu maswali manne pekee
- Swali la kwanza ni la lazima
- Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobakia yaani : Riwaya, hadithi fupi,ushairi na fasihi simulizi
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
- Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili
MASWALI
SEHEMU A: TAMTHILIA
Timothy M.Arege :Bembea ya Maisha
- LAZIMA
La! Kila mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu hutakasa sahani akijua itamfaa tena. Kinacholelewa hakina budi kulea.- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
- Changanua mtindo katika dondoo hili (alama3)
- Kauli iliyopigiwa mstari inaonyesha majukumu ya watoto kwa wazazi. Thibitisha kwa kuonyesha wazi alivyowajibika anayerejelewa na msemaji (alama4)
- Fafanua umuhimu wa msemaji katika kujenga tamthilia ya Bembea ya Maisha (alama4)
- Eleza sifa tano za msemewa (alama5)
SEHEMU B: RIWAYA
A. Matei: Chozi la Heri
Jibu swali la 2 au la 3
- ”Vipi, binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliyomwagika?”
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
- Tambua mbinu ya lugha iliyotumika (alama2)
- Jadili sifa tatu za msemaji (alama3)
- Hakiki jinsi binadamu alivyomwagikiwa na maji katika riwaya (alama11)
- “Nilipojaribu kuukata mkono niliostahili kuubusu yalinifika ya kunifika.
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
- Fafanua mambo mbalimbali yaliyomfika anayesema maneno katika dondoo hili (alama4)
- Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenye riwaya, onyesha jinsi udhaifu wa uongozi umebainika katika Jumuiya ya Chozi la Heri (alama12)
- SEHEMU C:HADITHI FUPI
MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINEj
jbu swali la 4 au la 5
Racheal Wangare:Fadhili za Punda
“Rudi, nyumbani mwanamke wewe! Nitakuja jioni tuyamalize haya.”-
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
- Fafanua hulka ya msemaji wa kauli hii (alama4)
- Huku ukizingatia hadithi hii, jadili maudhui ya mabadiliko yanavyojitokeza katika hadithi(alama7)
- Changanua mtindo katika dondoo hili (alama 5)
Alasiri ile, baada ya ibada mbili, mhubiri akawa hoi kwa mavune. Akatamani kufika nyumbani apumzike, kazi ya kuwalisha kondoo wa Mungu si kazi rahisi. Wamefika nusu safari, bintiye katulia kama maji ya mtungi. Akimtazama kipembe anamkumbusha marehemu mkewe. Miaka mitatu sasa na dhiki ya kuondokewa haijamwisha. Alihisi ukiwa, akatamani mwenziye. Sasa kazi kukilea kitoto chao, kibinti hiiki kilicho mlanda mamake kama shilingi kwa ya pili. Nyuma ilijaa kicheko alipokua hai mamake. Kama si bintiye ambaye ulimi wake hautulii, kiroho kingemvamia labda hata kumvuta kuelekea kaburini .
AU
-
- Winnie Nyaruri Ogenche; Sabina
“Ninaomba wazazi wenzangu muwape watoto wa kike elimu badala ya kuwaoza mapema. Hongera, mwanangu kwa kupata alama mia nne arubaini na saba”- Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kukuza hadithi husika (alama5)
- Tambua mbinu ya kimtindo iliyotumika katika dondoo hili (alama1)
- Fafanua jinsi mbinu yenyewe ilivyotumika ili kufanikisha utunzi wa hadithi (alama6)
- Fafanua changamoto zinazokabili jinsia ya kike kwa mujibu wa hadithi (alama8)
SEHEMU D :USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
- Nazuka mtunga mambo, na watunzi watungao
Wafungatao masombo, kushika msu na ngao
Naipiga ya ngambo, sauti ifike kwao
Wawapi wajigambao, tugambiyane vigambo?
Ni siku nyingi kitambo, ninyemele naja leo
Kama kweli wana nyimbo, nawaje niimbe nao
Na sababu ni vigambo, vya wale wajitwazao
Wawapi wajigambao,tugambiyane vigambo?
Iwapo mu wana nyimbo, na ungoi upasao
Musingewaonya mambo, waoga mwatishao
Mungefungata masombo, kuteta na wawezao
Wawapi wajigamboa, tugambiayane vigambo?
Wawapi fundi wa nyimbo, malengo wajitwazao
Wasemao kula jambo, kuwa walijua wao
Kuna kipambua pambo, chatafuta wapambao
Wawapi wajigambao,tugambiyane vigambo?
Musidhani ni msimbo, hayano nambano leo
Nawaeleza ni mambo, yamtaka atakao
Ajifungate msombo,mdudoateze nayo
Wawapi wajigambao, tugambiyane vigambo?
Imani wenya utambo, mutambao kwa matao
Muelewao mafumbo, na mbinu za wafumbao
Kuna ‘tomvu za ulimbo, tengani muruke nao
Wawapi wajigambao, tugambiyane vigambo?
Sasa tafunuwa wimbo, takasani masikio
Siimbi la mtu jambo, alojiweka kituo
Hili’ metunga no fumbo, n’ nao niwatakao
Wawapi wajigambao, tugambiyane vigambo?
Tamati enyi warembo, nasubiri matokeo
Hivi sasa sina jambo, ela naaga nendao
Ni mimi simba wa wimbo,marara ningurumao
Wawapi wajingambao, tugambiyane vigambo?
Maswali- Lipe shairi hili anwani mwafaka (alama1)
- Eleza muundo wa shairi hili (alama4)
- Taja na utoe mifano ya mbinu nne za kimtindo zilizotumika katika shairi hili (alama4)
- Fafanua uhuru wa kishairi katika ubeti wa nne (alama3)
- Andika ubeti wa pili katika lugha ya nathari (alama4)
- Tambua nafsi nenewa katika shairi hili ` (alama1)
- Taja toni la shairi hili (alama1)
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika ushairi (alama2)
- Wafungatao masombo
- Ninyemele
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali:
Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki,
Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki
Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni, usimwone ni rafiki
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka,
Wengine watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo,
Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakazifuata nyago,
Hadi kwenye wako ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka
Pindi kinunua kitu, hafurahi Shaitani, bali tajawa chukizo,
Mtu kiwa mtukutu, tanuna mtimani, kwalo lako tekelezo,
Tamko lake ‘Subutu’ Kuondoa tumaini, na kukuulia wazo,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka,
Aliye na taraghani, taabu kuishi naye, kazi yake kujidai,
Takusema faraghani, asosema kiwa naye, kupendeza maadui,
Hana faida nyumbani,ni mtu akuchimbaye, mradi usitumai,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka,
Kwa hakika ni balaa, kumkirimu mchawi, aliyejaa uchoyo,
Bahati ina hadaa, kukupa alo sadawi, aibatili rohoyo,
Mipangoyo kwake jaa, na nia ya ustawi, huwiza kuvunja kaninyo,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Ninacho changu kilio, ninalia sanasana, kinyesi nimetupiwa,
Ningetoa azimio, lakini uwezo sina, kwa matatizo kuambiwa,
Ama nitumie mbio, fuadini ninanena, akilini nazuiwa,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
MASWALI:- Lipe shairi hili anwani mwafaka (alama1)
- Fafanua mambo manne mabayo nafsineni analalamikia (alama4)
- Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama3)
- Idadi ya vipande katika kila mshororo
- Mpangilio wa vina katika kila ubeti
- Idadi ya mishororo katika kila ubeti
- Andika ubeti wa nne katika lugha nathari (alama3)
- Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili (alama2)
- Huku ukitoa mifano, onyesha mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (alama2)
- Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili (alama2)
- Fafanua muundo wa ubeti wa tano na sita (alama3)
SEHEMU E : FASIHI SIMULIZI
- .Niaje wazungu wanaweza kutunza vitu vikajaa kwenye friji. Yani nimeweka soda mbili tu kweye friji lakini akili haitulii hadi nizinywe. Niko sebuleni nazunguka tu. Najaribu kuwaza vitu vingine lakini wapi akili inaniambia ‘My friend, kunywa soda.’
- Bainisha kipera cha utungo huu (alama1)
- Fafanua aina tatu za taswira zilizotumika katika kifungu hiki (alama3)
- Utanzu wa kipera hiki huweza kuchukua nafasi muhimu katika fasihi simulizi. Thibitisha kwa hoja
zozote sita (alama6) - Ufanisi wa uwasilishaji wa utanzu huu unategemea fanani. Teteta kauli hii. (alama5)
- Ni changamoto zipi zinaweza kumkabili mwanafasihi mtafiti nyanjani? (alama5)
MWONGOZO
-
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- Msemaji ni Yona
- Msemewa ni Sara
- Alasiri nyumbani kwa Sara na Yona
- Yona anasisitiza kauli yake kuwa Sara anafaa kumwita mwanawc Neema aje ampeleke hospitali kwani wao walipanda mbcgu. (4x1=4)
- Changanua mtindo katika dondoo hili
- Nidaa- La!
- Istiara-Mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu huitakasa sahani yake akijua itamfaa tena. Yona analinganisha wanawe (Asna na Neema) na mbcgu, mazao yake, na mavuno. Pia, anawalinganisha na sahani ambayo aliitakasa imfae.
- Taswira-mtu hutakasa sahani (3×1=3)
- Kauli iliyopigiwa mstari inaonyesha majukumu ya watoto kwa wazazi. Thibitishakwa kuonyesha wazi alivyowajibika anayerejelewa na msemaji
- Amewafaa wanuna wake kwa hali na mali kwani; amewalipia wanuna wake karo. (“... Ninasikia kulipia elimu ya Chuo kiku si lelemarna”) uk.2
- Anagharamia matibabu ya Sara. (“Ugonjwa huu usingenibakisha hata nikaona leo hii. Ulikuwa umenila kiasi cha kuniacha chicha; chicha kavu kwenye mwako wa jua. Hadi akaja yeye na kunipeleka kwa wataalarnu... Leo nisingekuwako. “) uk.2
- Amewaajiria wafanyakazi (“Yona umesahau mara? Hukumbuki kuwa Neema alituajiria wafanyakazi kutusaidia...”) uk. 3
- Anamtumia Yona pesa za dawa na za kujumuika na wazee wenzake ili wasimuone shabiki, (‘... Hivi umesahau kuwa wewe anakutumia hela za kununua dawa? Hata sasa umetumia mapeni uliyotumiwa kwenda kwa wazee wcnzio ili wasikuone shabiki tu?”) (4x1=4)
- Fafanua umuhimu wa msemaji katika kujenga tamthilia ya Bembea ya Maisha
- Amedhihirisha masaibu ya uraibu wa pombe kama vile kuvuruga maisha ya mtu. Yona aliachishwa kazi kwa kukosa kuwajibika kazini.
- Anajenga maudhui ya mabadiliko. Mtazamo wa Yona unabadilika. Yona awali alikosa huruma kwa mkewe sara alipokuwa mgonjwa. Sasa yona anaonekana mwenye huruma.
- Ni kiwakilishi cha wale wanaothamini utamaduni katika jamii. Anaamini kwamba kila familia sharti iwe na mtoto wa kiume ili kuwa mrithi
- Ametumiwa kuonyesha namna ukatili unavyoendelezwa dhidi ya jinsia ya kike. Yona hana utu kwa sababu baada ya kumkuta bibi yake akiwa katika hali mbaya ya ugonjwa, bado anamuuliza kwa nini hajaanda mlo.
- Anadhihirisha suala Ia taasubi ya kiume kwani, tunamwona Yona aliyekinai na kukasirishwa na Sara arnbaye ameketi palepale ilhali hajamwandalia chakula (4×1=4)
- Eleza sifa tano za msemewa
- Mvumilivu Sara alivumilia mateso ya mume wake ambaye alimlaumu kwa kutopata rntoto wa kiume.Mume wake alimtesa kutokana na kosa ambalo kwa hakika halikuwa lake.
- Mpatanishi Sara ni mpatanishi kwa kuwa alimshauri bintiye amwelewe mume wake ambaye alitii
utamaduni uliomfanya asimkubali mkwe wake alale nyumbani kwao. Pia, alimshauri bintiye
amshukuru mumewe kwa kumruhusu kutumia hela zake kumtibu yeye aliyekuwa anaugua. - Mwenye utu Sara aliijali ndoa yake na kumpenda mumewe licha ya fujo zake. Alikataa kukaa
mjini na binti yake ili kumwepushia mume wake fedheha ya kujifanyia kazi zilizohusishwa na
wanawake kama vile kuchota maji kisimani. - Mwenye hekima -Maneno anayozungumza yana wingi wa hekima na busara.Anamweleza Asna
asichezc na akili zake ijapokuwa hakupata elimu sawasawa. - Mlezi mwema -Anawalea wanawe kwa kuwapa mawaidha ya busara.Anawanasihi kuheshirnu
ndoa, utamaduni na baba yao. - Mtamaduni Neema anatilia maanani tamaduni za jamii yakc. Kwanza tunamwona akisema kuwa
fimbo hurithiwa na mtoto wa kiume. Tena tunamwona akimtetea bwana yake kuhusiana na suala
Ia kazi za jikoni na kuteka maji kisimani. - Mwenye uhusiano mwema —Sara alikuwa na uhusiano mwema na Dina. Anapougua, Dina
anakuja kumsaidia kwa kuwa walikuwa na uhusiano mwema. - Mwenye msimamo thabiti hata baada ya kusutwa na kukejeliwa na wanajamii hakuyumbishwa
na maneno yao. Aliwapenda mabinti zake kwa dhati. Hata ingawa anachapwa kichapo cha mbwa
na bwana yake, hakutoka nyumbani kwake, alisimama kidete na familia yake.
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- ”Vipi, binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliomwagika?”
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- Haya ni maneno ya Mwanaheri
- Akimwambia Kairu na Umu
- Walikuwa katika shule ya Tangarnano
- Ni baada ya kukutana na kuanza kusimuliana kuhusu yaliyowafika hadi wakakutana pale zozote 4x 1
- Tambua mbinu ya lugha iliyotumika
- Swali balagha - vipi, binadamu anavyoweza kuyazoa maji yaliyomwagika?
- Methali-Maji yakimwagika hayazoleki.
- Jazanda-maji yaliyomwagika kutaja-1, 2x1
- Jadili sifa tatu za msemaji
- Mwenye mawazo mapevu. Mama yake angetafuta suluhu kwa mgogoro kati yake na wakwe zake badala ya kujiua
- Mwenyc busara - anaamini kuwa hakuna haja ya kushughulikia mambo ambayo hawezi kuyabadilisha
- Mwenye bidii - anatia bidii shuleni. Anafuata ushauri wa mwalirnu Dhahabu kwamba elimu
itamletea mabadiliko - Mshauri za kwanza 3x1
- Hakiki jinsi binadamu alivyomwagikiwa na maji katika riwaya
- Lunga kumwagikiwa na maji pale anapoachwa na mkewc Naomi
- Umu na nduguye wanamwagikiwa na maji kwa kuachwa mayatima wakati Lunga anapoaga
- Ridhaa anamwagikikwa na maji wakati anapoipoteza aila yake yote isipokuwa Mwangeka
- Mwangeka anamwagikiwa na maji kufuatia kifo cha mkewe na mtoto wake
- Zohali anamwagikiwa na maji pale anapotungwa mimba katika umri wa ujana na kupelekea afukuzwe shuleni na kuteswa na wazazi
- Waafrika wanamwagikiwa na maji pale wanapokatazwa na wakoloni kulima mazao yaletayo fedha huku ikiwalazimu kufanya vibarua kwao
- Baadhi ya vijana wa rika la Tuama wanakufa baada ya kupashwa tohara
- Hospitali inamwagikiwa na maji pale Selume analalamikia ukosefu wa mwangaza, ukosefu wa glavu na deni kutokana na usimamizi duni
- Wakaazi wa msitu wa mamba wanaharibikiwa pale wanapofurushwa huku vyakula walivyolima vikiibiwa na viongozi
- Vijana barobaro wanaotumiwa na wanasiasa kuandamana wanamwagikiwa na maji pale wanapomiminiwa risasi vifuani wa walinzi huku wakiuawa
- Kitoto kinachookotwa na Neema kilimwagikiwa na maji pale kilitupwa na mama mzazi badala ya kukilea
- Ridhaa anasimulia mwanawe Mwangeka vile walivyobomolewa nyumba zao kwenye mtaa wa Zari, hawakupewa fidia yoyote nao wale waliowauzia viwanja hivi waliingia mitini
- Lunga kufutwa kazi na mkurugenzi kwa kupinga mradi wa ununuzi mahindi
zozote 11 x 1 = 11
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- “Nilipojaribu kuukata mkono niliostahili kuubusu yalinifika ya kunifika.
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- Haya ni maneno ya Lunga akiwajibu watu waliomuuliza ilikoenda jazba ya kuhifadhi misitu aliyokuwa nayo. Anajibu akiwa kwake baada ya kupoteza kazi na mali yake na kukimbilia kwenye msitu wa Mamba. Mvuto wa kunawiri kwa mimea ya babake ulimsukuma kukata miti na kupanda mimea iliyomstawisha. (4× 1)
- Fafanua mambo mbalimbali yaliyomfika anayesema maneno katika dondoo hili
- Familia yake ilitimuliwa kutoka walikokuwa wakiishi kwenye shamba la tajiri wao Kiriri.
- Wanafunzi wenzake kama Kimondo walizoea kumkejeli shuleni kuwa yeye ni mtoto wa nyumba ya utajiri
- Alitimuliwa mara ya pili kutoka Msitu wa Mamba.
- Walipelekwa Mlima wa Simba ambako siku zote hakujua ni kitovu Chao.
- Mkewe Naomi alimtoroka. Baada ya mwaka alifariki.
- Watoto wake Dick na Mwaliko walitoroshwa na kijakazi naye Umu akatorokea jijini.
zozote (4×1=4)
- Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenye riwaya, onyesha jinsi udhaifu wa uongozi umebainika katika Jumuiya ya Chozi la Heri
- Utawala wa kiimla- yule kiongozi mwanamke katika visakale vya majirani anayewatumikisha wanaume huku wanawake wakiketi tu (uk. 17).
- Viongozi kusisitiza kudumishwa kwa haki ya mwanamke huku wakipuuza watoto wa kiume wanaolawitiwa (uk. 17).
- Viongozi wanawatazama wafuasi wao kwenye runinga wakizozana badala ya kuwakanya (uk 19).
- Matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Polisi wanawakabili wavunja sheria vikali. Wanawapiga risasi na kuwauwa baadhi yao (uk. 20).
- Uongozi kutobuni mfumo wa elimu unaowapa vijana stadi na umilisi wa kujiajiri. Baadhi wanahitimu shahada na hawawezi kujitegemea (Rejelea malamamishi ya mwanaharakati aliyevaa shati Iililoandikwa ‘Hitman’ (uk. 21).
- Viongozi wanawaelekeza vijana warudi mashambani huku wakijua kwamba hawamiliki chochote (uk. 21)
- Viongozi kuwapa wageni vipande vikubwa vya ardhi bila kujali mustakabali wa wenyeji (uk. 22). Wenyeji wanafukarishwa zaidi.
- Uundaji wa tume bandia za kuchunguza kashfa ya unyakuzi wa ardhi, kila mara raia wanapolalamika wakidai kuona ripoti za uchunguzi huu (uk. 22).
- Viongozi kuwatumia vijana kama nyenzo ya kuwafanyia kampeni.
- Mbinu hasi za uongozi - viongozi wanatumia unafiki kuwavutia vijana kwao Viongozi wanatiririkwa na machozi ya mamba wanapoona hali duni ya vijana (uk. 22).
- Ufisadi - viongozi wanawahonga vijana kuwapigia kura. Pia wanawahonga akina mama. Vijana wanahitajika kutoa hongo ili kupata kazi (uk. 133).
- Vijana badala ya kuwaelekeza akina mama kumpigia kiongozi afya wanawaelekeza kumchagua kiongozi fisadi (uk.23).
- Viongozi wanatoa ahadi za uongo-mwanaharakati mwenye shati lililoandikwa ‘Hitman’ anasema walikuwa wameahidiwa ubalozi (Uk. 23).
- Viongozi wanaendeleza unasaba. Hazina ya Jitegemee ambayo inanuiwa kuwapa vijana mtaji wa kuanzishia biashara imeandamwa na ukabila na unasaba (uk. 24).
- Uongozi kutobuni nafasi za kazi kwa Vijana - kijana rnwenye shati lililoandikwa ‘Hitman’ anasema mate yamewakauka kwa kufunga bahasha za kutumia maombi ya kazi. Shamsi analalamikia ukosefu wa nafasi za kazi (uk. 133).
- Ubaguzi katika utoaji wa nafasi za kazi - Shamsi anasema kwamba nafasi za kazi zilitwaliwa na ndugu za viongozi.
- Malalamishi ya wafanyakazi hayasikilizwi. Kina Shamsi wanapoomba nyongeza ya mshahara wanaambiwa ni vibarua wasiokuwa na ujuzi/stadi maalum.
- Viongozi wanawafuta wafanyakazi wanapolalamikia mshahara duni. Shamsi na wenzake wanafutwa kazi wanapoomba kufikiriwa kama wanataaluma wengine nafasi za kazi zikipatikana. Wanafukuzwa kutoka kwenye nyumba za kampuni kwa kuwaziwa kuifilisi kampuni (uk. 131).
- Uongozi hauhakikishii raia usalama wa chakula. Baba yake Shamsi anakufa kwa kula vijasumu vya mizizi mwitu (uk. 134).
- Huduma za kimsingi hazitolewi kwenye hospitali za wanyonge. Kijijini kwa baba ya Shamsi hakuna hospitali. Kadhalika hakuna dawa kwenye hospitali ya wanyonge mjini.
- Uongozi kutowapa wafanyakazi vifaa vya kimsingi vya kazi. Selume anakosa glavu kumhudumia mama anayejifungua (uk. 139).
- Uongozi wa hospitali kutowajibikia majukumu yake. Hawalipii huduma za Selume analazimika kupapasa kwenye giza (uk. 140).
- Ukosefu wa dawa unasababishwa na usimamizi mbaya wa hospitali. Selume hana dawa ya kumpoza mama usingizi (uk. 140).
- Wasimamizi wa hospitali wanaiba dawa na kuziuza kwenye maduka yao ya dawa huku wagonjwa wakifa kwa kukosa dawa (uk. 140).
- Maazimio ya makubaliano ya kazi hayatirnizwi. Kampeni dhidi ya polio inatingwa na hatua ya viongozi ya kuwauzia maskini wasiomudu kujilisha dawa hizi (uk. 140).
- Viongozi wananyakua dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na saratani ambazo zimetengewa wanyonge (uk. 141).
- Uongozi wa mahakama unatinga utekelezaji wa haki kwa kukawisha kesi. Tila anataka kuwajaji ili kesi ambazo zimeselelea mahakamani kwa miongo miwili ziamuliwe (uk. 45).
- Viongozi wanaendeleza uharibifu wa mazingira. Taka kutoka mitaa ya wenye nguvu zinaelekezwa kwenye mtaa wa mabanda wa Sombera (uk. 28). Makiwa anasema wanatoa sandarusi wanazotumia kama vyoo kwenye milima ya taka.
- Uongozi kutowajibikia raia makao mema. Nyurnba za bei nafuu zinazojengewa wakazi wa kitongoji duni cha Sombera zinanyakuliwa na viongozi (uk. 28).
- Viongozi wanawaangamiza wapinzani. Lunga anapopinga kuuziwa mahindi duni kwa raia anafutwa kazi (uk. 70-74).
- Uongozi unawapa raia hatimiliki katika Msitu wa Mamba huku wakijua kwamba mahali hapa ni marufuku kwa binadamu (uk. 76).
- Japo uongozi umewahamisha raia kwenye Msitu wa Mamba, bado unauhujumu msitu huu. Ukuzaji mahindi na ukataji mbao bado unaendelezwa; malori na matrekta hubeba shehena za mbao, makaa na mahindi (uk. 77).
- Uongozi unapowaharnisha raia kutoka Msitu wa Mamba, hauwapi fidia ya kutosha. Lunga hajapewa fidia ya kutosha kukidhi mahitaji ya familia yake kama awali. Watoto hawawezi kusomea kwenye Shule za awali.
- Uongozi unaruhusu ujenzi kwenye sehemu zilizotengewa ujenzi wa barabara, na baadaye kuyabomoa majumba hayo hayo. Majumba matatu ya Ridhaa yanabomolewa kwa amri ya Waziri Tendakazi (uk. 13).
- Viongozi wananyakua ardhi ambayo imetengewa upanzi wa chakula na kujenga majumba ya kifahari (uk. 68). Hili linasababisha kutojitosheleza kwa chakula. Viongozi wamenyakua misitu na kujenga viwanda (uk. 68). Hata Mlima wa Nasibu ambao ni madhabahu umenyakuliwa na kujengwa hoteli za kitalii (uk.69). (Za kwanza 12×1=12)
- Eleza muktadha wa dondoo hili
SEHEMU C:HADITHI FUPI
MAPAMBAZUKO YA MACHWEO NA HADITHI NYINGINE
Jibu swali la 4 au la 5
Racheal Wangare:Fadhili za Punda
- “Rudi, nyumbani mwanamke wewe! Nitakuja jioni tuyamalize haya.”
-
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- Msemaji ni Luka
- Msemewa ni Lilia
- Mahali ili Ofisini- sehemu ya mapokezini
- Baada ya Lilia kuamua kwenda kumtafuta Luka ofisini katikati mwa wiki baada ya uvumi kuhusu uhusiano wa Luka na wanawake wengine 4x1=4
- Fafanua hulka ya msemaji wa kauli hii
- katili anamehapa Lilia
- mpyaro amtukana Lilia
- Asiye na shukrani
- Mzinifu/ mkware anauhusiano wa kimapenzi na wanawake wengine
- Mwenye bidii - anatia bidii masomoni hadi anafaulu
- Mnafiki anajifanya kuwa anampenda Lilia hadi pale anapochaguliwa kuwa gavana. 4x1
- Huku ukizingatia hadithi hii, jadili maudhui ya mabadiliko yanavyojitokeza katika hadithi
- Uso wa lilia unabadilika kutokana na majeraha aliyoyapata kutokana na kipigo cha mumewe
- Maisha ya Lilia ya furaha yanabadilika na kuwa ya huzuni kutokana na madhila ya Luka
- Maisha ya Luka yanabadilika anapokutana na familia ya lilia- anaanza masomo
- Luka anaacha kazi ya kuhubiri na kuwa mwanasiasa
- Mtazamo wa Luka mabadilika-jinsi alivyomwona lilia akiwa rnrembo sasa amuona kuma asiyependeza. “ona umbo lako sasa
- Baada ya Luka kuchaguliwa kama gavana anasahau rnke wake, lilia
- Maisha ya lilia yanabadilika baada ya kulazwa hospitalini anaamua kumwacha Luka
- Maisha ya Luka yanabadilika baada ya kupata ajali anawapoteza marafiki. 7x1
- Eleza muktadha wa dondoo hili
- Changanua mtindo katika dondoo hili
- Jazanda-Kondoo- wafuasi wa kidini
- Tashbihi—katulia kama maji mtungini.
landa mamake kama shilingi kwa ya pili. - Mbinu rejeshi — anamkumbusha marehemu
Uhuishi-kihoro kingemvamia - Taswira-nyumba iliyojaa kicheko 5x1
-
- Winnie Nyaruri Ogenche; Sabina
“Ninaomba wazazi wangu muwape watoto wa kike elimu badala ya kuwaoza mapema. Hongera, mwanangu kwa kupata alama mia nne arubaini na saba”- Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kukuza hadithi husika
Mrejelewa ni Sabina- Ametumiwa kuendeleza na kukuza ploti ya hadithi kutokana na mgogoro baina yake na familia ya Ombati..
- Ni kielelezo bora cha wanajamii wanaoenzi masomo na wanaojitolea sabili ili kupata ufanisi katika maisha yao ya halali.
- Mwandishi amemtumia kukashifu ukiukaji wa haki za watoto na kukandarnizwa kwao.
- Ametumiwa kudhihirisha maudhui ya uwajibikaji, elimu na ukiukaji wa haki za watoto mayatima.
- Ametumiwa kudhihirisha matatizo yanayopitiwa na watoto mayatima.
- Amechimuza sifa ya Ombati na Yunuke kama katili.
- Ametumiwa kufanikisha methali baada ya dhiki faraja kwani anajipitia magumu mwanzoni lakini baadaye maisha yake yanaendelea. (5x1=5)
- Tambua mbinu ya kimtindo iliyotumika katika dondoo hili
- Kinaya (alama 1)
- Fafanua jinsi mbinu yenyewe ilivyotumika ili kufanikisha utunzi wa hadithi
- Ni kinaya ombati na Yunuke kumtumikisha Sabina kwa kufanya kazi za sulubu ilhali ni mtoto yatima.
- Ombati kumfahamisha mwalimu mkuu kuwa anampa Sabina muda tosha kujiandaa kwa mtihani wa kitaifa.
- Yunuke kumrejelea Sabina kama baradhuli ilhali ndiye baradhuli.
- Ombati kutaka kumwoza Sabina licha ya kuwa mwenye umri mdogo tena mwanafunzi wa shule ya msingi.
- Ombati kujitanua kuwa ametunukiwa kumlea mwana mwerevu masomoni, Sabina.
- Ombati kudai kuwa Sabina anapenda kufanya kazi shambani ilhali ni kumtumikisha.
- Ombati kuwaomba wazazi wawape watoto wao wa kike elimu badala ya kuwaoza mapema ilhali ndivyo alivyo dhamiria kufanya.
- Ombati na Yunuke kutotaka kukaa mbali na Sabina baada ya kufaulu kwake masomoni licha ya kuwa kikwazo.
- Yunuke kumfokea Sabina hata kumwambia kuwa hana akili masomoni.
- Yunuke kumwambia Sabina ana tabia sawa na za mamake (mwasherati) ilhali ni mwadilifu. (6x1)
- Fafanua changamoto zinazokabili jinsia ya kike kwa mujibu wa hadithi
- Sabina kusongwa na mawazo kabla ya mtihani wa kitaifa (wa darasa la nane )kuwadia
- Sabina kufanyishwa kazi za sulubu na Yunuke
- Nyaboke (mamake Sabina ) kupata ujazito akiwa umri mdogo
- Sabina kulelewa na mzazi mmoja akiwa na umri mdogo
- Nyaboke kulazimika kuacha shule baada ya kupata mimba
- Babake Sabina kumkana Sabina baada ya kumkana Sabina mchana peupe
- Sabina kuachwa yatima baada ya kifo cha mamake. Analazimika kuishi na babu na nyanya.
- Wanajamii kumtenga Sabina wakidai familia yao iliandamwa na mikosi na nuksi.
- Sabina kudhulumiwa kwa kupigwa na Yunuke
- Sabina kupangiwa njama ya kuozwa mapema hata kabla ya kumaliza masomo yakc
- Sabina kudharauliwa na kuonekana bure na hata kuambiwa kuwa juhudi zake hazingefua dafti na Yunuke. (8x1=8)
- Eleza umuhimu wa mrejelewa katika kukuza hadithi husika
- USHAIRI
Maswali- Ipe shairi hili anwani mwafaka
- Wawapi wajigambao
Majigambo/vijigambo
- Wawapi wajigambao
- Eleza muundo wa shairi hili
- Mishororo minne kila ubeli
- Urari wa vina; mbo, o
mbo, o
mbo, o
mbo, o - vipande viwili katika kila mshororo- ukwapi na utao
- mizani 16 kila mshororo
- kibwagizo- wawapi wajigambao, tugambiyane vigambo (4x1=4)
- Taja na utoe mifano ya mbinu nne za kimtindo zilizotumika katika shairi hili
- Swali balagha-kibwagizo ni swali
- Msemo/nahau — napiga ya mgambo
- Kufungata masombo
- Taswira—tomvu za ulimbo tengani,
- Istiara — mimi simba wa wimbo
- Fafanua uhuru wa kishairi katika ubeti wa nne
- Tabdila — kulla- kula
- Inkisari — wawapi-wako wapi
- Lahaja — tugambiyane (3x1=3)
- Andika ubeti wa pili katika lugha ya nathari
- Mshairi amesema kuwa amenyamaza siku nyingi kutokana na vigambo vya wenye
mazoea kujitapa leo anavunja kimya chake kwa kuwa dhubutu wajitokeze awaonyeshe ubingwa wake (4x 1=4)
- Mshairi amesema kuwa amenyamaza siku nyingi kutokana na vigambo vya wenye
- Tambua nafsi nenewa katika shairi hili
- Nafsinenewa –wajigambao ,wenye maringo (1×1=1)
- Taja toni la shairi hili
- Toni — kukejeli! dharau / dhihaka (1x1=1)
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama lilivyo tumika katika ushairi
- Wafungutao masombo — wajifungao kibwebwe
wanajizatiti/wanajitahidi
Ninyemele — nimenyamaza (2x 1=2)
- Wafungutao masombo — wajifungao kibwebwe
- Ipe shairi hili anwani mwafaka
- Shairi la kiarudhi
- Lipe shairi hili anwani mwafaka
- Binadamu hatosheki / Binadamu ana tamaa / tamaa ni hatari (alama 1/0)
- Fafanua mambo manne mabayo nafsineni analalamikia
- Mtu aliye na tama huwa hatari kama nyoka
- Unafiki wa mtu asiyeaminika
- Masengenyo
- Balaa ya kumkirimu mchawi ni kutupiwa kinyesi (Za kwanza 4x1=4)
- Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
- Idadi ya vipande katika kila mshororo
- Tumbuizo — kila mshororo una vipande vitatu — ukwapi. utao. mwandamizi ambavyo vinatoshana kwa urefu -- kila kimoja kina mizani nane
- Mpangilio wa vina katika kila ubeti
- Ukaraguni — vina vya kila kipande vinaofautina katika shairi nzima
- Idadi ya mishororo katika kila ubeti
- Tarbia — kila ubeti una mishororo minne
- Idadi ya vipande katika kila mshororo
- Andika ubeti wa nne katika lugha nathari
- Ni taabu kuishi na mtu aliye taraghani kwani kazi yake ni kujidai.
- Atakusema faraghani asivyosema ukiwa naye kuwapendeza maadui zako
- Ni mtu akuchimbaye. Hana faida nyumbani. Mradi usimtumai.
- Mtu aliye na tamaa wa kutaka kisicho chake ni hatari kama nyoka.
(Alama 3x1=3 jibu Iiandikwe kwa aya moja au atuzwe 0)
- Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
- Takriri - Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
- Tashbihi/tashbiha — ni hatari kama nyoka
- Tashihisi/uhaishaji/uhuishi — bahati inahadaa bahati kupewa uwezo wa kudanganya
- Litifati — Subutu’ kumwacha mtu ajisemee
- Nahau — kinyesi nimetupiwa
(Za kwanza 2x1=2 atolee mfano au atuzwe 0)
- Huku ukitoa mifano, onyesha mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi
- Inkisari — ukweliye badala ya ukweli wake, kiso badala ya kisicho n.k
- Miundo ngeu ya kisintaksia / kuboronga sarufi / kufinyanga sarufi — ninacho changu kilio badala ya ninacho kilio changu (Za kwanza 2×1=2ataje, atolee mfano na asahihishe au atuzwe 0)
- Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili
- Urudiaji wa neno — kweli,
- Urudiaji wa sauti —a — balaa, hadaa. jaa. tamaa
- Urudiaji wa mstari - Mtu kuwa na tamaa. akitaka kiso chake. ni hatari kama nyoka.
- Urudiaji wa silabi — ki, ki, ki (Za kwanza 2x1=2 atolee mfano au atuzwe 0)
- Fafanua muundo wa ubeti wa tano na sita
- Mistari / mishororo minne katika kila ubeti
- Vipande vitatu katika kila mshororo
- Vina vinabadilika kulingana na ubeti
- Mizani 8,8,8=24 katika kila mshororo
- Mshororo wa mwisho unarudiwarudiwa/ kibwagizo (lazima atolee mfano Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka) (Zozote 3x1=3)
- Lipe shairi hili anwani mwafaka
SEHEMU E : FASIHI SIMULIZI
- Niaje wazungu wanaweza kutunza vitu vikajaa kwenye friji. Yani nimeweka soda mbili tu kweye friji lakini akili haitulii hadi nizinywe. Niko sebuleni nazunguka tu. Najaribu kuwaza vitu vingine lakini wapi akili inaniambia ‘My friend, kunywa soda.’
- Bainisha kipera cha utungo huu
- Kichekesho (1x1)
- Fafanua aina tatu za taswira zilizotumika katika kifungu hiki
- Taswira ono- kujaa kwenye friji
- Taswira muonjo-kunywa
- Taswira mwendo-nazungumza tu
- Taswira sikivu- inaniambia
- Utanzu wa kipera hiki huweza kuchukua nafasi muhimu katika fasihi simulizi. Thibitisha kwa hoja zozote sita
- Huburudisha watazamaji na waigizaji wenyewe. Burudani hii mara nyingine hupumbaza.
- Huhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jamii kama vile upashaji tohara, matambiko, majigambo, ngoma, miviga na michezo ya watoto hudumishwa kupitia maigizo.
- Ni kitambulisho cha jamii; kila jamii ina Sanaa ya maigizo ya jamii husika. Miviga na sherehe za arusi na mazishi hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.
- Hukuza umoja na ushirikiano wa watu wanapojumuika kushiriki katika maigizo. Hao hujitambulisha kama jamii moja
- Ni nyenzo za kupitisha maarifa na amali za jamii kupitia michezo ya jukwaani. Husawiri mtazamo wa jamii kuhusu masuala mbalimbali kama vile woga, wizi na usaliti.
- Hukuza ubunifu madhalan watoto wanaposhiriki michezo ya watoto, hujifunza kubuni michczo wakiwa wachanga na pia Sanaa ya uigizaji.
- Ni njia ya kuimarisha urafiki. Kwa vile mizaha na utani katika malumbano hukuza urafiki na uhusiano bora
- Huongoza jamii kupambana na mazingira wanamojipata. Kutegemea imani ya wanajamii,matambiko yanaweza kuondoa matatizo katika jarnii kama vile njaa, ugonjwa na ukame kwa kuomba Mungu
- Maigizo huelimisha kupitia maudhui na hulka za waigizaji na kushauri nafsi zao, kuiga au kukashifu hulka hizo. (6x1=6)
- Ufanisi wa uwasilishaji wa utanzu huu unategemea fanani. Teteta kauli hii.
- Huwa mchangamfu na mchcshi kwa hadhira yake ili kuwafanya wapcndezwe na hadithi
- Anafahamu utamaduni wajamii yake
- Anaifahamu hadhira yake vizuri na kusimulia kulingana na mapendeleo yao. wasichana au wavulana? vijana au wazee?
- Huwa na uwezo wa ufaraguzi - uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila kujifunga na muundo asilia.
- Mwenye kumbukumbu nzuri - uwczo wa kukumbuka
- Mwenye uwezo wa kuigiza kwa kutumia viungo vyake, uso (ishara-uso) na sauti(kiimbo
- Mwenye uwezo wa kujenga taharuki kwa kusita kidogo ili kuvuta nadhari ya hadhira yake.
- Hushirikisha hadhira yake katika nyimbo n.k
- Mtambaji hodari na mkwasi wa lugha.
- Ni changamoto zipi zinaweza kumkabili mwanafasihi mtafiti nyanjani?
- Gharama ya utafiti-huenda gharama ikawa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu. Baadhi ya mafanani au wahojiwa huenda wakadai walipwe kabla ya kutoa habari zozote.hivyo ikiwa mtafiti hana hela basi utafiti wake utakwamizwa.
- Mtazamo hasi wa wanajamii kuhusu ujazaji wa hojaji huenda ukawafanya wengi wao kutojaza hojaji zao. Wanajamii wengine huweza kushuku kwamba mtafiti anawapeleleza na wakakataa kutoa habari.
- Vizingiti vya kidini ambavyo hutokea pale ambapo baadhi ya wahojiwa wanaamini kwamba matendo ya fasihi simulizi k.v matambiko na uimbaji wa taarabu yanaenda kinyume na imani yao ya kidini.
- Uchache wa wazec au wataalamu wa fasihi simulizi ,kukosckana kwa wazee wanaoweza
kutamba ngano ama kueleza vipera vingine k.v vitendawili. - Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi ikiwa mkusanyaji analazimika kwenda mbali kukusanya
habari,hasa katika sehemu kame itakuwa vigumu iwapo hana gari. - Ukosefu wa usalama ,huenda mkusanyaji wa fasihi simulizi akavamiwa ,baadhi ya watu si
wakarimu na huenda wakamshuku mtafiti na kuvamiwa. (5x1=5)
- Bainisha kipera cha utungo huu
Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Cekana Mock Exams 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students