MAAGIZO
- Andika insha mbili: insha ya kwanza ni ya lazima
- Chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Zingatia sarufi.
- Onyesha nambari ya insha unayoandika.
- Andika tahariri kuhusu sababu za kudorora kwa usalama katika gatuzi lako.
- Fafanua hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa nchini kukabiliana na umaskini nchini.
- Andika insha inayooana na methali mchuma janga hula na wa kwao.
- Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo.
...niliyagugumia maji hayo kwa pupa na kung’amua kuwa maji ni uhai.
MARKING SCHEME
- Kichwa
jina la gazeti
Siku na tarehe
Mada
Utangulizi – aya ya kwanza itoe maelezo ya jumla kuhusu suala la kudorora kwa usalama
Maudhui- Kuwepo kwa makundi haramu/makundi ya kigaidi
- Uhaba wa kazi kwa vijana
- Watu kumiliki silaha kinyume na sheria
- Uchochezi wa wanasiasa/siasa za migawanyiko
- Ukabila
- Wizi wa mifugo baina ya jamii mbalimbali
- Kuzembea kwa vyombo vya usalama
- Uhusiano mbaya kati ya polisi na raia
- Athari hasi za dawa za kulevya/vileo
- Giza/kukosekana kwa taa za usalama mijini
- Idadi ndogo ya polilsi/walinda usalama
- Kisasi cha ukatili wa kitambo
- Kutoaminiana kwa wanandoa
- Kudorora kwa usalama mipakani
- Ushindani wa kupata mamlaka
- Misongamano ya watu mijini
Aya ya mwisho iwe ya hitimisho. Mtahiniwa atoe kauli yake ya mwisho labda kwa kufupisha maelezo yake ya hapo juu.- Jina la mwandishi
- Cheo chake
- Kichwa
Hoja/maudhui- Kuhimiza upangaji uzazi
- Kuwapa watu ajira
- Kufanya biashara
- Kuwa na maendeleo endelevu nchini
- Kudhibiti ufisadi
- Kupunguza mikopo/ukopaji kutoka ughaibuni
- Kuboresha usalama katika kila janibu ya nchi
- Kufanya maendeleo mashambani
- Kuboresha kilimo ili kuwa na utoshelezaji wa chakula
- Kuhimiza uwekezaji utaohakikisha maendeleo na nafasi za kazi
- Kuwapa watu mishahara inayolingana na gharama za maisha
- Kuweka mtalaa wa elimu unaoona na mahitaji/gharama ya maisha.
- Mchuma janga hula na wa kwao
Hii ni insha ya methali
Chuma ni kufanya kazi na kupata faida/ tungua matunda kutoka mtini.
Janga-balaa /baa /mataka / shida / hatari / taabu
Ajitafutiaye shida huathirika na jamii / jamaa yake .
Mtahiniwa asimulie kisa /visa vitakavyoafikiana na methali.
Asipinge methali.
Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokeza;- Mhusika kushiriki raha za kilimwengu, akaambukizwa magonjwa yasotibika,hatimaye anarejea nyumbani anakogua , mzigo wa kumtunza unakuwa kwa familia yake.
- Mhusika aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni au shirika fulani, anacheketwa labda kutokana na uzembe au utovu wa maadili ya kikazi,anarejea nyumbani kwa familia yake; kule hana chochote hivyo basi anaishia kutegemea jamma zake, huu unakuwa mzigo mkubwa kwa watu wake.
- Mtoto ambaye anatokea kuwa mhalifu, anafikishwa kortini na kutozwa faini kubwa.Hii inakuwa gharama kwa familia yake kwa vile ndio wanaotakiwa kulipia.
- Mwanafunzi ambaye anakosa kuwajibika masomoni shuleni , anafeli mtihani, maisha ya halafu yanakuwa magumu kwa hivyo jamaa zake wanalazimika kuingilia kati ili kumuauni kwa mahitaji ya kila siku
-
- Mtahiniwa aandike kisa kinachoonyesha mtu ambaye anateseka sana labda kutokana na kutekwa nyara.
- Mtu huyu asawiriwe kama ambaye alikuwa karibu kufa/kukata tamaa na baadaye kwa bahati nzuri anapata maji.
(Alama zituzwe kutokana na mwongozo wa kudumu wa kusahihisha insha kama inavyopendekezwa na Baraza la Mitihani ya Kitaifa Nchini (KNEC) )
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Momaliche Post Mock 2020 Exam.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students