MAAGIZO KWA MTAHINIWA
- Jibu maswali yote.
- Majibu yote yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.
- UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ilikuwa jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa kusikiliza taarifa ya habari.
Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe kiinuamgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.
Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, waziri wa kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia la kilo tisini. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu.
Baada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga ekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wakati wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.
Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazo bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani.
Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua na kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.
Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapitanjia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’
Bila taarifa wala tahadhari, mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi. Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tuko lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.
Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuns, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa. ‘MAHINDI GUNIA 900/=.’ Niligutuka usingizini.
Maswali- Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari. (alama 1)
- Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika? (alama 2)
- Taja matatizo matatu yaliyotishia mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi
(alama 3) - Eleza maana za methali zifuatazo kwa mujibu wa taarifa
- Usikate majani, mnyama hajauawa (alama 1)
- Muumba ndiye muumbua (alama 1)
- Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia. (alama 4)
- Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu? (alama 1)
- Eleza maana za;
- Kinuamgongo (alama 1)
- Manyakanga wa kilimo (alama 1)
- UFUPISHO(ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ufupishe kwa mujibu wa maswali uliyopewa
Utafiti umebaini kuwa pana uwiano baina ya lugha inayotumiwa kwa lugha rasmi na kiwango cha umaskini katika nchi, na pia kiwango cha ustawi. Kwa mfano, nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikitumia lugha za wakoloni waliozitawala kama lugha rasmi. Nchi hizi zimekuwa zikitumia lugha hizo katika shughuli rasmi, kutoa mafunzo na kupitishia sera muhimu zinazoathiri maisha ya wananchi wote. Kile wasichozingatia ni kuwa, raia wao wengi hawazielewi.
Idadi kubwa ya raia barani Afrika ni wakulima au wasakatonge katika sekta za juakali, uchukuzi na biashara ndogondogo ambao hawana umilisi wa lugha hizo za kigeni. Watu hawa aghalabu huendesha shughuli zao za kila siku kwa kutumia lugha zao za asili, au kama hapa Afrika MAshariki, hutumia Kiswahili ambacho aghalabu hawazingatii usanifu wake. Je, kwa nini tusiokoe na kuauni idadi hii kubwa ya watu ili kuimarisha hali zao kiuchumi, kijamii na ambazo hawazielewi; lugha zinazotumiwa na kufahamika na wachache?
Manufaa ya kutumia lugha inayoeleweka ma kufahamika na wengi kama lugha rasmi ni lukuki yakilinganishwa na maumizi ya lugha za kigeni kama kiingereza, kifaransa, kijerumani au kimandarin. Kwanza, matumizi yake huwawezesha watumiaji kujieleza wakaeleweka vizuri kwa kuwa mkondo wa fikra unatumia lugha wanayoijua, na hivyo wana nafasi ya kuwa wabunifu. Kwa mfano, matumizi ya lugha asili katika utoaji elimu yatahakikisha kuwa wanafunzi wanashiriki kikamilifu katika shughuli zote za kielimu. Hawatakuwa wanafunzi wanaongojea kuelezwa kila kitu bali watajisakuria ili kujizidishia maarifa.
Matumizi ya Kiswahili, lugha inayoeleweka na idadi kubwa ya watu, huhakikisha kuwa ujuzi na maarifa yanayopitishwa si himaya ya kundi dogo tu lililoelimika bali hata wale wasiobahatika kuzielewa lugha hizo za kigeni. Hii ni kwa sababu anayesema kwa lugha ya kigeni husema na ubongo, naye asemaye kwa lugha asili husema na moyo, hivyo basi akaeleweka zaidi katika yale ayasemayo. Aidha, matumizi haya hutoa nafasi sawa kwa wengi na kuepusha utegemezi wa wakalimani ambao aghalabu hawaeleweki kutokana na kasi ya mazungumzo, au wakatoa fasiri isiyo sahihi. kila mmoja ataweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa kutokana na uwezo wa kufasiri sera za serikali na kutoa uamuzi wao wenyewe ikilinganishwa na wakati ambapo sera hizi zinawasilishwa kupitia lugha za kigeni.
Fauka ya haya,matumizi ya lugha inayoeleweka na wengi huwawezesha watu kushiriki na kuchangia katika uimarishaji wa demokrasia kutoka vijijini, hadi kitaifa. Hata hivyo, itashangaza kumwona mzungu akizungumza na wanajamii kwa Kiswahili, naye mwakilishi wa jamii hiyo akiwazungumzia kwa kiingereza. Hii ni njia mmoja ya kuwatenga raia wasioelewa lugha hiyo ya kigeni. Matumizi ya lugha kama hii huhujumu mtagusano baina ya watu. Kwa hivyo, hakisalii tu kuwa lugha rasmi katika katiba bali katika uhalisia.
Maswali- Fupisha aya ya kwanza kwa kutumia maneno 35-40 (alama 5)
Nakala chafu
__________________________________________________________________________________________________________________________________________Nakala safi
__________________________________________________________________________________________________________________________________________ - Kwa maneno kati ya 100-110, eleza manufaa ya kutumia lugha inayoeleweka na watu wengi kama lugha rasmi katika nchi. (alama 10)
Nakala chafu
__________________________________________________________________________________________________________________________________________Nakala safi
__________________________________________________________________________________________________________________________________________
- Fupisha aya ya kwanza kwa kutumia maneno 35-40 (alama 5)
- SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
- Taja vipasuo viwili vya kaakaa laini. (alama 2)
- Andika neno lenye sauti mwambatano. (alama 1)
- Weka shadda katika neno lifuatalo ili itoe maana mbili tofauti. (alama 2)
ala - Tumia kiimbo katika sentensi mbili tofauti ili kudhihirisha. (alama 2)
- Ombi/rai
- Amri/kuamuru
- Tambulisha vipashio vinne vya sarufi ya Kiswahili. (alama 2)
- Tunga sentensi kwa kutumia kiwakilishi huru nafsi ya tatu wingi. (alama 2)
- Tumia kivumishi cha pekee katika sentensi kuonyesha umilikaji. (alama 1)
- Tumia vihusishi kuonyesha uhusiano wa wakati na kiwango. (alama 2)
- Weka maneno haya katika ngeli zake. (alama 2)
- Miwani
- Wema
- Ainisha mofimu katika neno lifuatalo. (alama 3)
Hakuwakaribisha - Bainisha tofauti kati ya mzizi huru na mzizi funge kwa kutoa mifano. ( alama 2)
- Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika senensi ifuatayo. (alama 2)
Utakapomkabidhi barua hii, nipashe habari - Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Ilitumwa kumlimia nyanya shamba - Yakinisha sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea. (alama 2)
Hakuwasaidia wala hakuwakaribisha kwake. - Tambua kirai kihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Jino la Tamma linauma mara kwa mara. - Tunga sentensi ukitumia neno zawadi kama kitenzi (alama 2)
- Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
“Nitamwalika mtondogoo.” Fatuma akasema. - Changanua sentensi hii kwa kutumia matawi. (alama 4)
Darasa lilojengwa limefunguliwa leo alasiri. - Kanusha (alama 1)
Sisi ndisi wanafunzi - Tunga sentensi moja ukitumia kiambishi –po- kudhihirisha mahali dhahiri. (alama 1)
- ISIMU JAMII (ALAMA 10)
- Eleza maana ya lugha ya taifa. (alama 2)
- Eleza sababu tatu zinazofanya watu kubadili na kuchanganya ndimi. (alama 3)
- Eleza hatua tano ambazo zimesaidia kukuza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru nchini Kenya. (alama 5)
MARKING SCHEME
- UFAHAMU
- Mashaka ya kilimo cha mahindi
- Shilingi elfu saba na mia tatu (200,000 – 192,700=7,300)
-
- Tisho la korongo na vidiri kufukua mbegu.
- Kiangazi
- Mvua ya barafu
- Gharama kubora (1x3=3)
- Eleza maana za methali zifuatazo kwa mujibu wa taarifa
- Usikate majani, mnyama hajauawa (alama 1)
Haikuwa vizuri kufurahia faida kabla ya kuuza mavuno. - Muumba ndiye muumbua (alama 1)
Mungu ana uwezo wa kuleta barafu na kiangazi na kustawisha mimea.
- Usikate majani, mnyama hajauawa (alama 1)
- Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia. (alama 4)
- Kiwango cha chini cha mavuno
- Kushuka kwa bei (2x2=4)
- Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu? (alama 1)
Mahindi aliyodhani yameangamizwa na kiangazi yalinawili tena. - Eleza maana za;
- Kinuamgongo (alama 1)
Malipo ya kustaafu. - Manyakanga wa kilimo (alama 1)
Wataalamu wa kilimo.
Makosa sita ya sarufi adhibu = 3
Hijai adhibu = 3
- Kinuamgongo (alama 1)
- MAJIBU YAUFUPISHO
- Fupisha aya ya kwanza kwa kutumia maneno 35-40 (alama 5)
Hoja muhimu- Utafiti umebaini kuwepo uwiano baina ya lugha rasmi na kiwango cha umaskini na utajiri katika nchi.
- Kutumiwa kwa lugha za wakoloni katika shughuli rasmi zinazoathiri wengi ilhali hawazielewi kunawafanya wasiweze kufasiri sera za serikali ifaavyo.
(1X5=5)
- Kwa maneno kati ya 100-110, eleza manufaa ya kutumia lugha inayoeleweka na watu wengi kama lugha rasmi katika nchi. (alama 10)
Hoja muhimu- Wanaoitumia wanaweza kujieleza wakaeleweka vizuri.
- Huwawezesha kushiriki katika shughuli zinazowaathiri.
- Huwafanya watumiaji wakahisi kutambulika.
- Huhakikisha kuwa ujuzi na maarifa hayasalii kuwa nilki ya walioelimika tu bali pia wasioielewa lugha ya kigeni.
- Huhakikisha kuwa wengi wanaelewa kinachowasilishwa.
- Huondoa utegemezi wa wakalimani.
- Huwezesha watu kuchangia katika uimarishaji wa demokrasia.
- Hutoa nafasi sawa kwa kila mtu kushiriki katika ujenzi wa kitaifa.
- Huimarisha mtagusano.
(10X1=10)
Makosa sita ya sarufi adhibu = 3
Hijai adhibu = 3
- Fupisha aya ya kwanza kwa kutumia maneno 35-40 (alama 5)
- SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
- Taja vipasuo viwili vya kaakaa laini. (alama 2)
/k/
/g/ (1X2=2) - Andika neno la silabi moja lenye sauti mwambatano. (alama 1)
Ndama. Suti mfano nz,mb,nd,kw,zw - Weka shadda katika neno lifuatalo ili itoe maana mbili tofauti. (alama 2)
ala- ala – aina ya mfuko unaotiwa kisu/panga.
- ala- zana ya kazi.
- Ala! – mshangao
- Tumia kiimbo katika sentensi mbili tofauti ili kudhihirisha. (alama 2)
- Ombi/rai
Tafadhali nifungulie mlango. - Amri/kuamuru
Ondokeni hapa!
- Ombi/rai
- Tambulisha vipashio viwili vya sarufi ya Kiswahili. (alama 2)
- Sauti
- Silabi
- Neno
- Sentensi
- Tunga sentensi kwa kutumia kiwakilishi huru nafsi ya tatu wingi. (alama 2)
- Wao hawana heshima.
- Nafsi ya tatu yeye (umoja) wingi wao.
- Tumia kivumishi cha pekee katika sentensi kuonyesha umilikaji. (alama 1)
- Matumizi ya enye.
- Mwenye gari amewasili.
- Tumia kihusishi kuonyesha uhusiano wa wakati na kiwango. (alama 2)
- Vihusishi vya wakati toka, hadi, mpaka, kabla ya, mwishoni mwa n.k
- Vihusishi vya kiwango mfano zaidi ya
Amefanya kazi zaidi ya (kiwango) Tamima kabla ya (wakati) mwalimu kutoka
- Weka maneno haya katika ngeli zake. (alama 2)
- Miwani
I - I - Wema
U –U
- Miwani
- Ainisha mofimu katika neno lifuatalo. (alama 3)
Hakuwakaribisha
Ha – kikanushi cha nafsi
ku – kikanushi wakati uliopita
wa – watendewa
karib – mzizi
ish – kauli
a – kiishio - Bainisha tofauti kati ya mzizi huru na mzizi funge kwa kutoa mifano. ( alama 2)
- Mzizi huru ni neno zima lialojitegemea kimaana bila viambishi mfano sahau, jadili,rudi,jadili na sanduku.
- Mzizi funge au tegemezi ni ule ambao huhitaji kuambishwa ili kudhihirisha maana kamili mfano piga, a-na-chez-a
- Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika senensi ifuatayo. (alama 2)
Utakapomkabidhi barua hii, nipashe habari
Utakapomkabidhi barua hii – kishazi tegemezi.
Nipashe habari – kishazi huru. - Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Ilitumwa kumlimia nyanya shamba
I – shamirisho ala
nyanya – kitondo
shamba - kipozi - Yakinisha sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea. (alama 2)
Hakuwasaidia wala hakuwakaribisha kwake.
Huwasaidia na kuwakaribisha kwake. - Tambua kirai kihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Jino la Tamima linauma mara kwa mara.- La Tamima
- Tunga sentensi ukitumia neno zawadi kama kitenzi (alama 2)
Juma alimzawadia mtoto - Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
“Nitamwalika mtondogoo.” Fatuma akasema.
Fatuma alisema kwamba angemwalika siku tano baadaye. - Changanua sentensi hii kwa kutumia matawi. (alama 4)
Darasa lilojengwa limefunguliwa leo alasiri. - Kanusha (alama 1)
Sisi ndisi wanafunzi(atumie kikanushi cha ndi)- Sisi si wanafunzi (kikanushi huru)
- Sisi sisi wanafunzi (kikanushi ambata)
- Tunga sentensi moja ukitumia kiambishi –po- kudhihirisha mahali dhahiri. (alama Patazamwapo na watalii panavutia.
Anapopalima patajengwa.
Makosa sita ya sarufi adhibu = 3
Hijai adhibu = 3
- Taja vipasuo viwili vya kaakaa laini. (alama 2)
- ISIMU JAMII (ALAMA 10)
- Eleza maana ya lugha ya taifa. (alama 2)
Ni lugha iliyoteuliwa kama kitambulisho cha utamaduni na ustaarabu wa taifa zima. (1x2=2) - Eleza sababu tatu zinazofanya watu kubadili na kuchanganya ndimi. (alama 3)
- Kusisitiza ujumbe.
- Upungufu wa msamiati wa lugha moja.
- Kutaka kudhihirisha uko kundi Fulani la watu. (1x3=3)
- Eleza hatua tano ambazo zimesaidia kukuza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru nchini Kenya. (alama 5)
- Kuwekwa kwa sera.
- Kueuliwa kwa Kiswahili kama lugha ya taifa.
- Vyombo vya habari na mawasiliano mfano taifa leo.
- Shughuli za biashara.
- Uchapishaji wa vitabu.
- Shughuli za kidini.
- Kampeni za kisiasa vilitegemea matumizi ya Kiswahili.
(1x5=5)
Makosa nne ya sarufi adhibu alama mbili
Hijai adhibu alama mbili
- Eleza maana ya lugha ya taifa. (alama 2)
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Momaliche Post Mock 2020 Exam.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students