- UFAHAMU
- Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
- Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
- Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (al.2)
- Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
- Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (al.2)
- Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (al.3)
- Kubisha hodi
- Kukolewa
- Makurutu
- UFUPISHO
- Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (al.9) Mtiririko alama 1
- Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (al.6) Mtiririko alama 1
- SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
- Tambua sauti.
Kipasuo ghuna cha kaakaa laini (al.1) - Unda neno lenye muundo ufuatao wa sauti (al.1)
KKKKI - Eleza maana ya istilahi zifuatazo za sauti (al.4)
- Kiimbo
- Konsonanti mwambatano
- Tunga sentensi moja ukitumia neno –zuri kama kiwakilishi, kivumishi na kielezi (al.3)
- Eleza tofauti kati ya sentensi hizi (al.2)
Ningesoma kwa bidii ningepita mtihani.
Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani - Tunga sentensi moja sahihi itakayotumia vitenzi vifuatavyo (al.3)
-wahi, -enda, -ona - Huku ukitumia mifano mwafaka, tofautisha silabi wazi na silabi funge (al.2)
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya yakinishi (al.2)
Wanafunzi wasiposoma kwa bidii hawatapita mtihani - Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (al.2)
Gaidi aliyelipua guruneti ile ametiwa mbaroni - Andika katika msemo wa taarifa: (al.2)
“Wakazi wa eneo hili ni wafugaji stadi wa sungura” kakangu aliniambia. - Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo (al.3)
Sheria hizo mpya zilitundikwa juu ya ukuta usiku wa manane. - Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
- Sali
- La
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi (al.4)
Jengo lijengwalo kwenye msingi thabiti hudumu sana. - Andika katika kauli ya kutendesha (al.2)
Amani alikunywa pombe mpaka akalewa sana - Andika kwa udogo (al.2)
Njia iendayo mbinguni ni nyembamba - Neno changa lina maana ya kutoa kitu au fedha ili kukusanya kwa makusudi Fulani. Eleza maana zingine mbili (al.2)
- Taja nahau zingine mbili sawa na “Enda ahera” (al.2)
- Andika kwa wingi (al.1)
Zigo la kuliwa halilemei
- Tambua sauti.
- ISIMU JAMII (alama 10)
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
“Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”
- Tambua sajili inayorejelewa (al.2)
- Tambua sifa zinazobainisha sajili yenyewe (al.8)
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- UFAHAMU
- Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
- Kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi 1x1=1
- Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
- Kuimarisha utendakazi katika kikosi ambacho kwa muda mrefu kimelaumiwa kwa kulowa ufisadi na uvunjaji wa haki za kimsingi
- Unaashiria mwanzo wa mageuzi makubwa yanayonuiwa kukipatia kikosi hicho sura mpya
- Kuwapa maafisa wa polisi mafunzo mapya
- Kuunda kikosi imara chenye nidhamu na kinachoheshimu haki za kibinadamu 4x1 = 4
- Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (al.2)
- Ukosefu wa nidhamu
- Kutoheshimu haki za binadamu/kimsingi
- Kukolea kwa ufisadi
- Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
- Maafisa wa polisi kupokea mafunzo kwa kipindi cha kati ya miezi 15 na 21 kinyume na awali ilipochukua miezi 9
- Alama za kujiunga na kikosi hicho zimeongezewa kutoka D hadi C
- Asilimia 10 ya makurutu wawe na digrii kutoka chuo kikuu ili kuhitimu naibu wa inspekta wa polisi
- Usawa wa jinsia kuzingatiwa katika uajiri wa maafisa wa polisi 3x1 = 3
- Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (al.2)
- Jopo iliyoteuliwa na Rais mwaka wa 2003
- Taasisi ya elimu
- Wakufunzi kutokea chuo cha mafunzo cha Kiganjo
- Wataalam wa maswala ya usalama kutoka Uswizi 2x1 =2
- Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (al.3)
- Kubisha hodi
- Kuingia/kutukia
- Kukolewa
- Kuendeleza/kushamirisha
- Makurutu
- Wanafunzi wanaojiunga na kikosi cha polisi
- Kubisha hodi
- Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (al.1)
- UFUPISHO
- Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (al.9)
- Serikali kuwasilisha bajeti
- Kueleza jinsi mabilioni yalivyotumiwa
- Serikali ya Kenyatta kusema itatumia shilingi 1.6 trilioni kwa maendeleo.
- Makadirio kuwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni
- Kukosa kueleza jinsi ya kupata kitifa hicho
- Habari hizi kunipa wasiwasi
- Kenya kudaiwa shilingi 1.8 trilioni na wafadhili
- Kutolaumu wale wasiolewa ukubwa wa deni hili
- Kugawanya deni hili kwa Wakenya wote
- Kila Mkenya kadaiwa shilingi 45,000
- Kenyatta kurithi deni kutoka kwa Kibaki
- Deni kumkosesha usingizi Rais
- Kutafuta njia ya kulipa bila kuathiri uchumi
9x1 = 9
Mtiririko alama 1
- Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (al.6)
- Serikali kutenga fedha nyingi kuwalipa wafanyikazi
- KRA kutokusanya kiwango kinachohitajika
- Ukusanyaji wa ushuru kutatizwa na hofu wakati wa uchaguzi
- Serikali za kaunti kupendekeza kutumia mabilioni ambayo hawana
4x1 = 4
Mtiririko alama 1
- Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (al.9)
- SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
- Tambua sauti.
Kipasuo ghuna cha kaakaa laini (al.1)- /g/
- Unda neno lenye muundo ufuatao wa sauti (al.1)
KKKKI- Mchwa
- Eleza maana ya istilahi zifuatazo za sauti (al.4)
- Kiimbo
- Kupanda na kushuka kwa sauti mtu anapozungumza
- Konsonanti mwambatano
- Mfuatano wa konsonanti mbili au zaidi katika silabi unapotamka
- Kiimbo
- Tunga sentensi moja ukitumia neno –zuri kama kiwakilishi, kivumishi na kielezi (al.3)
- Vizuri vile ni vya watu wazuri walioandikiwa vibaya
- Eleza tofauti kati ya sentensi hizi (al.2)
Ningesoma kwa bidii ningepita mtihani.- Kuna uwezekano wa kitendo kutendeka/wakati uliopo
Ningalisoma kwa bidii ningalipita mtihani
- Hakuna uwezekano/wakati uliopita
- Tunga sentensi moja sahihi itakayotumia vitenzi vifuatavyo (al.3)
-wahi, -enda, -ona- Aliwahi kwenda kumuona afisini mwake (1x3=3)
- Huku ukitumia mifano mwafaka, tofautisha silabi wazi na silabi funge (al.2)
- Silabi wazi ni zile zinazoishia kwa irabu k.m. ru + ka ba + ba
- Funge ni zile zinazoishia kwa konsonanti k.m. m + t u Da - k - ta - ri
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya yakinishi (al.2)
Wanafunzi wasiposoma kwa bidii hawatapita mtihani- Wanafunzi wakisoma kwa bidii watapita mtihani
- Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (al.2)
Gaidi aliyelipua guruneti ile ametiwa mbaroni- Gaidi aliyelipua guruneti – k – huru ametiwa baroni – Kishazi tegemezi
- Andika katika msemo wa taarifa: (al.2)
“Wakazi wa eneo hili ni wafugaji stadi wa sungura” kakangu aliniambia.- Kakangu aliniambia kuwa wakazi wa eneo hilo ni wafugaji stadi wa sungura.
- Bainisha aina za virai katika sentensi ifuatayo (al.3)
Sheria hizo mpya zilitundikwa juu ya ukuta usiku wa manane.- Sheria mpya – Kikundi nomino
- Zilitundikwa juu ya – Kikundi tenzi
- Juu ya ukuta – Kikundi kihusishi
- Usiku wa manane – Kikundi kielezi
1x4 = 4
- Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo (al.2)
- Sali
- Sala, msala, msalihina,
- La
- Chakula, mlo, mlaji, ulaji
- Sali
- Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi (al.4)
- Andika katika kauli ya kutendesha (al.2)
Amani alikunywa pombe mpaka akalewa sana- Pombe ilimlevya Amani
- Andika kwa udogo (al.2)
Njia iendayo mbinguni ni nyembamba- Kijia kiendacho mbinguni ni chembamba 1x2 = 2
- Neno changa lina maana ya kutoa kitu au fedha ili kukusanya kwa makusudi Fulani. Eleza maana zingine mbili (al.2)
- Umwa viungoni au mishiopani kama ugonjwa wa biridi ya bisi
- Siyokomaa/siyopevuka
- Taja nahau zingine mbili sawa na “Enda ahera” (al.2)
- Kata kamba
- Aga dunia
- Ipa dunia kisogo
- Enda jongomeo
- Andika kwa wingi (al.1)
Zigo la kuliwa halilemei- Mizigo ya kuliwa hayalemei
- Tambua sauti.
- ISIMU JAMII (alama 10)
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
“Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”- Tambua sajili inayorejelewa (al.2)
- Sajili ya michezo/kandanda/kambumbu
- Tambua sifa zinazobainisha sajili yenyewe (al.8)
- Lugha changamfu/cheshi/porojo
- Kupiga chuku/kutiwa chumvi
- Lugha shawishi
- Utohozi/mf. Foul, Horse power
- Lugha mseto/kuchanganya ndimi/msimbo
- Matumizi ya tamathali za usemi
- Lugha nyepesi inayoeleweka
- Kuhamisha ndimi
- Huchanganywa na nyimbo
- Matumizi ya msamiati teule wa kambukambu
- Kauli/sentensi fupi fupi
- Sentensi zisizokamilika
- Uradidi/takriri/urudiaji
- Matumizi ya lakabu
- Sifa kemkem kwa wachezaji
Zozote nane 1x8=8
Adhabu
Makosa ya sarufi ya kwanza manne yaondolewe alama 2 4x1/2 =2
Makosa ya hijai hadi manne 4x1/2 =2
Jumla alama 4
- Tambua sajili inayorejelewa (al.2)
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download KISWAHILI PAPER 2 - FORM 4 END TERM 1 EXAMS 2020.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students