MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
Maswali
- SWALI LA LAZIMA
Andika barua kwa waziri wa kilimo kupitia kwa katibu wa kilimo huku ukipendekeza jinsi nchi ya Kenya inavyoweza kukabiliana na janga la njaa. - Maasi ya vijana yameleta madhara mengi kwa wanafunzi wa shule za upili. Jadili sababu na suluhisho la janga hili.
- Andika kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali; Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
- Andika insha itakayomalizia kwa; ......hapo ndipo nilipong’amua kwamba mzazi ni kitu cha thamani.
Mwongozo Wa Kusahihisha
- SWALI LA LAZIMA
Andika barua kwa waziri wa kilimo kupitia kwa katibu wa kilimo huku ukipendekeza jinsi
nchi ya Kenya inavyoweza kukabiliana na janga la njaa.
Insha izingatie- Hii ni barua rasmi
- Iwe na muundo ufuatao
Anwani ya mwandishi
Anwani ya mwandikiwa
Kupitia kwa anwani ya katibu wa kilimo
Kwa Bwana/Bi
YAH: MAPENDEKEZO YA KUKABILIANA NA JANGA LA NJAA
Hoja
- Kuhifadhi maji wakati wa mvua ili kutumika nyakati za kiangazi.
- Wananchi kufunzwa namna ya kuzingatia kilimo bora ili kupata mavuno ya kutosha.
- Sheria ziwekwe za namna ya kuhifadhi na kutunza misitu kwani huvuta mvua.
- Maghala ya kuhifadhi mavuno yajengwe.
- Jamii zinazohamahama zihimizwe kulima na kuweka mifugo wanayoweza kutunza.
- Kukuza zao Fulani maalum katika eneo.
- Wakulima kupewa misaada ya vifaa na mbolea ya kukuza chakula.
- Wakulima kupewa mitaji kutoka kwa serikali.
Sahihi
Nakala kwa:- Waziri wa kilimo
Anwani - Katibu wa kilimo
Anwani - Idara husika- anwani
- Maasi ya vijana yameleta madhara mengi kwa wanafunzi wa shule za upili. Jadili sababu na suluhisho la janga hili.
- Visababishi
- Dawa za kulevya
- Shiniko la kikundi/rika.
- Filamu mbaya
- Kudhibitiwa kupita kiasi
- Kukosa nidhamu
- Malezi mabaya/udekezaji
- Kubomoka kwa msingi wa jamii
- Ufukara kusababisha kujiunga na makundi haramu
- Kukata tamaa
- Suluhisho
- Kujiondoa kundini
- Kuwashauri vijana
- Kujenga udhabiti wa jamii
- Utiifu na unyenyekevu
- Kuwa na usemi
- Kuvumiliana na kusameheana
- Kutochagulia watoto taaluma na wachumba
- Wazazi kutolazimisha watoto taaluma au kozi wasizotaka
- Kutopendelea na kulinganisha watoto kiuwezo
- Kutotumia dawa za kulevya/hamasisho kuhusu athari za mihadharati
- Kuomba pamoja
- Baba kutimiza majukumu yake ya kukimu jamii
- Kutodhibiti mke na watoto kupita kiasi
- Uadilifu
- Visababishi
- Andika kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali; Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
- Mtahiniwa aandike kisa kitakachoana na methali hii.
- Mwanafunzi azingatie sehemu zote mbili za methali.
Maana ya methali - Malezi ya kudekeza watoto huleta majuto kwa wazazi baadaye. Mzazi akimdekeza mtoto bila kuwelekeza vyema akiwa na tabia mbaya na kuelekea kuasi bila kumtia adabu, mzazi atakuja kutaabika mwenyewe.
TANBIHI
Akigusia upande mmoja wa methali atuzwe alama 10
- Andika insha itakayomalizia kwa; ......hapo ndipo nilipong’amua kwamba mzazi ni kitu cha thamani.
- Lazima mtahiniwa amalize kisa kwa maneno aliyopewa; asipomaliza kwa maneno hayo ataadhibiwa kimtindo.
- Kisa kiwe cha kusisimua ajabu.
- Mtahiniwa aonyeshe hali ya huzuni (kutendeka kwa jambo la kuhuzunisha)
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Prediction.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students