MAAGIZO
- Jibu maswali yote
- UFAHAMU (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ithibati ya maendeleo ya kiteknoloJia nchini Kenya tayari ipo.
Binafsi, nimeshuhudia teknolojia ya juu katika miundo ya simu na kompyuta, mifumo ya malipo ya kidijitali, mawasiliano na matumizi ya roboti yakizidi kurahisisha kazi katika sekta nyingi humu nchini.
Kila mwanauchumi atakubaliana nami kwa kuwa teknolojia ni nguzo muhimu katika kuongeza kiwango cha uzalishaji.
Lakini mbona uzalishaji umepungua katika miongo michache iliyopita ,katika kipindi ambapo teknolojia nyingi zilivumbuliwa? Sababu ni nini?
Nikichunguza data katika mataifa mengi ,hasa ya kiafrika,uzalishaji umepungua tangu mwanzo wa karne ishirini ya moja(21). Kumekuwa na sababu nyingi zilizochochea kushuka kwa utengenezaji wa bidhaa viwandani.
Sababu si teknolojia zenyewe bali ukosefu wakueneza teknolojia hizo kufikia kila mwananchi kwa mfano, program ya “my dawa” ni nzuri lakini ni wakenya wangapi wana uwezo wa kumiliki simu ya kisiasa ilikufaidika na huduma zake?
Ili kila mkenya aweze kumudu bei ya simu ya kisasa, basi uchumi wafaa kuimarika kiasi cha kuwa na hela za ziada za kununua vifaa vya kiteknolojia.
Kila mkenya na tambua kuwa ufisadi umelemaza kila sekta ya uchumi wetu,lakini hiki si kikwazo pekee cha teknolojia kukosa kuwafikia wananchi wamatabaka ya chini.
Hali hii pia inasababisha kampuni saba zilizokuwa zimeorodheshwa katika soko la hisa la Nairobi (NSE) kuondolewa kutokana na mapato ya chini kama licha ya kutumia teknolojia kuimarisha uzalishaji.
Kudorora kwa uzalishaji kunahusiana moja kwa moja na kupanuka kwa pengo na mapato baina ya matabaka mbalimbali ya kiuchumi. Kwa mfano ,kampuni ya Safaricom inapata faida kubwa zaidi kwa sababu teknolojia yake ya M-pesa imeenea kote,huku kampuni pinzani zikiumia.
Hivyo ,serikali kupitia mamlaka ya ushindani yafaa kuondoa vikwazo vinavyozua ushindani,nakuweka kanuni zinazozima ukiritimba.
Tukiachia kampuni chache umiliki wa soko husika, tutakuwa tunazuia kufurahia matunda yateknolojia, hakuna haja ya wagonjwa kukwama mashinani eti kwa sababu hawana simu za kupata huduma za kiafya kidijitali.
Teknolojia haitakuwa na maana iwapo mamilioni ya wakulima hawana uwezo wamiliki simu yenye apui na ya waunganishana soko la mazao yao pamoja na kuwaelekeza kwa maduka yenye dawa na mbegu za bei nafuu. Utazidi kuumia iwapo tutaachia Safaricom idhibiti soko la kutuma hela kidijitali.
Sera kuhusu teknolojia nchini zafaa kuboreshwa ilikuvumisha ubunifu na kueneza hadi mashinani.Kuna raha gani kuwa teknolojia nyingi zisizo saidia kukuwa kwa uchumi wetu? Teknolojia isiyoenea itazidi kulemaza uzalishaji tusipochukua hatua.
Maswali- Yape makala uliyoyasoma anwani mwafaka. (alama.1)
- Toa sababu za teknolojia kulemaza uzalishaji wa mali. (alama. 4)
- Kwa mujibu wa makala haya ni nini umuhimu wa teknolojia.? (alama.2)
- Ni hatua ipi serikali inastahili kuchukua ili kuzuia ukiritimba (alama.2)
- Ni nini msimamo wa mwandishi kuhusu teknolojia (alama.2)
- Fafanua msamiati huu kimuktadha (alama.2)
- Idhibati……………………………………………………………………………
- Ukiritimba…………………………………………………………………………
- UFUPISHO (alama 15)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalo kumba ulimwengu wa sasa, hasa katika nchi zinazoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi za ulimwengu huu. Kuna idadi kubwa ya watoto wanaoajiriwa katika nyanja mbalimbali za jamii. Zipo sababu nyingi zinazo wasukuma watoto kutafuta ajira barani Afrika kwa mfano, familia nyingi huishi maisha ya ufukara hivi kwamba hushindwa kuyatimiza mahitaji muhimu hususan kwa watoto. Kupanda kwa gharama ya maisha kuna zidisha viwango vya umasikini. Ukosefu wa lishe pia huwafanya watoto kutoroka nyumbani kutafuta ajira. Janga la UKIMWI limesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya mayatima wanaoishia kutafuta ajira ili kuyakimu maisha. UKIMWI umezifanya familia nyingi kuwaondoa watoto shule iliwaweze kuajiriwa kwa lengo la kuanzisha pato la familia hizo. Watoto wengine hutoroka makwao kwa sababu ya maonevu. Maonevu haya ni kama vile kupigwa, kutukanwa kila wakati, kunyanyaswa kijinsia na kadhalika. Huko nje hutaabishwa kimwili na kiakili. Hufanyizwa kazi za sulubu zenye malipo duni au wasilipwe kabisa. Hili huwasononesha na kuathiri afya yao.
Uundaji wa umoja wa Afrika hivi majuzi ni hatua muhimu ya kushughulikia matatizo ya Afrika kama vile ajira ya watoto, kuzorota kwa miundo misingi, magonjwa, njaa, umaskini, ufisadi na ukabila. Katika kushughulikia haki za watoto, nchi za Afrika hazina budi kuzingatia masharti yalivyowekwa na umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto. Nchi nyingi za Afrika ziliidhinisha mkataba wa masharti hayo ikiwemo nchi ya Kenya.
Nchi hizi basi lazima zishughulikie haki za watoto kupitia sheria za nchi. Watoto ni rasilmali muhimu na ndio tumaini la kuwepo kwa kizazi cha binadamu.
Maswali.- Eleza mambo yote muhimu anayozungumzia mwandishi katika aya ya kwanza. (maneno 6, 1 mtiririko)
Nakala chafu
Nakala safi - Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwisho. (maneno50 - 55)
(alama 7, 1 mtiririko)
Nakala chafu
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nakala safi
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
- Eleza mambo yote muhimu anayozungumzia mwandishi katika aya ya kwanza. (maneno 6, 1 mtiririko)
- MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo(alama 2)
- Kikwamizo hafifu cha ufizi,irabu ya mbele kati,nazali ya midomoni,irabu ya chin ikati
- Nazali ya ufizi,Irabu ya juu mbele, kipasuo hafifu cha midomo,irabu ya nyuma kati
- Ainisha mofimu katika maneno yafuaatayo: (alama 2)
- Asemavyo
- Mwangwi
- Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi `ni` (alama 2)
- Ainisha vitenzi katika sentensi: (alama 3)
Ndege yu taabani, hata hivyo anajaribu kujinasua. - Tunga sentensi ukitumia kirai kihusishi kama kielezi. (alama 1)
- Unapo adhirika na jambo unasema hewala! Unaposhangilia timu yako kwa kupata ushindi unasema……………………………………..na unapotaka kitu kinusurike unasema………………. (alama 2)
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kinyume: (alama 2)
Wakimbizi walihama na wakavunja kambi. - Tunga sentensi yenye muundo ufuatao (alama 2)
Nomino ya jamii, kirai kihusishi ,kitenzi kishirikishi, kielezo cha mahali. - Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
Mtoto huyo mzuri alifika shuleni asubuhi na mapema. - Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (alama 2)
Wachezaji walishinda mechi wakatuzwa. - Tunga sentensi na ubainishe shamrisho kitondo, kipozi na ala . (alama 3)
- Onyesha miundo miwili ya nomino katika ngeli ya A-WA (alama 2)
- Yakinisha sentensi ifuatayo katika nafsi ya pili umoja. (alama 2)
Hataenda shuleni kesho. - Eleza dhima ya tatu za viambishi tamati mbali na kauli ya kutenda/kiishio. (alama 3)
- Tunga sentensi moja katika wakati uliopita hali ya mazoea. (alama 2)
- Changanua sentensi zifuatazo kwa kielezo cha mistari.
- Huyu wake alikuwa amefika lakini hatukumjua. (alama 2)
- Mtoto wa Shangazi hucheka sana. (alama 1)
- Eleza maana tatu zinazojitokeza katika sentensi. (alama 3)
Niliona mamba. - Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo. (alama 2)
Madebe hayo yatasafirishwa pamoja na nyundo hizi.
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo(alama 2)
- ISIMU JAMII (ALAMA 10)
Wewe ni mfanyibiashara katika Soko la Kongomawe. Fafanua sifa kumi za lugha utakayotumia ilikuwavutia wateja wako.
Mwongozo wa Kusahihisha
- UFAHAMU
- Teknolojia
- Malipo ya kidigitali ni ya juu
- Teknolojia kutofikia kila mwananchi
- Kutokuwa na uwezo kumiliki simu ya kisasa yenye apu
- Ufisadi
- Kampuni kuondolewa kutoka soko la hisa
- Kulinda matumizi
- Vikwazo vikali kupitia kwa mamlaka ya ushindano (CAK)
- Sera zafaa kuboreshwa ili kuvumisha ubunifu na kueneza hadhi mashinani
-
- Mabadiliko
- Kuwa na uwezo mkuu kwa kampuni moja
- UFUPISHO
-
- Ajira ya watoto ni tatizo sugu ulimwenguni.
- Wengi huajiriwa katika nyanja mbalimbali.
- Familia nyingi ni maskini (fukara)
- Kupanda kwa gharama ya maisha huzidisha umasikini.
- Njaa huwatorosha nyumbani.
- Ukimwi umezidisha mayatima.
- Wengine hutoroshwa makwao na maonevu.
- Wengine huondolewa shuleni.
- Huko hutaabishwa kimwili na kiakili / hufanyishwa kazi za sulubu / hulipwa malipo duni au wasilipwe kabisa.
- Hili huwasononesha na kuathiri afya yao. (al 6 1 ya mtiririko)
-
- Watoto wengine hujiingiza katika jinai wanapokosa ajira
- Wengine hujikuta mandanguroni.
- Uundaji wa umoja wa Afrika ni hatua ya kushughulikia matatizo barani.
- Nchi za Afrika lazima zizingatie masharti ya umoja wa mataifa kuhusu watoto.
- Nyingi zaidhinisha watoto kupitia sheria zao.
- Lazima zishughulikie watoto kupitia sheria zao.
- Watoto ni rasilimali na tamaini la kizazi. (alama 7 1 ya mtiririko).
Utuzaji
Sehemu a – 7
Sehemu b - 6
Utiririko alalma - 2
15- Adhabu – ondoa alama moja kwa kila ziada ya maneno 10 baada ya kumtuza
- Ondoa alama ½ kwa kila kosa la hijai na sarufi (6h na 6s) baada ya kumtuza
- Anayekosa kuandika matayarisho na jibu kwa haya moja asipewe alama za utiririko
-
- MATUMIZI YA LUGHA
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo (alama 2)
- Kikwamizo hafifu cha ufizi,irabu ya mbele kati,nazali ya midomoni,irabu ya chini kati
- sema
- Nazali ya ufizi,Irabu ya juu mbele, kipasuo hafifu cha midomo,irabu ya nyuma kati
- nipo
- Kikwamizo hafifu cha ufizi,irabu ya mbele kati,nazali ya midomoni,irabu ya chini kati
- Ainisha mofimu katika maneno yafuaatayo: (alama 2)
- Asemavyo
a-sem-a-vyo
a-mofimu tegemezi ya nafsi ya tatu umoja
sem-mzizi
a-kiishio
vyo-mofimu tegemezi ya -o -rejeshi tamati - Mwangwi
Mw-angwi
Mw-mofimu tegemezi ya umoja
Angwi-mzizi
- Asemavyo
- Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi `ni’ (alama 2)
- nafsi ya kwanza umoja
- Niliwasili jana.
- mahali
- Twende kanisani.
- kitenzi kishirikishi kipungufu
- Yeye ni daktari.
- wingi
- Tokeni nje.
- Kama kiulizi
- watakani?
- nafsi ya kwanza umoja
- Ainisha vitenzi katika sentensi: (alama 3)
Ndege yu taabani, hata hivyo anajaribu kujinasua.- Yu-kitenzi kishirikishi kipungufu
- Anajaribu-kitenzi kisaidizi
- Kujinasua-kitenzi kikuu
- Tunga sentensi ukitumia kirai kihusishi kama kielezi. (alama 1)
- Mtoto ameanguka chini ya meza.
- Unapoadhirika na jambo unasema hewala! Unaposhangilia timu yako kwa kupata ushindi unasema hoyee/ huree/ hoyee/ oyee,/hario,/ripiripu. unapotaka usikivu unasema aisee/ ati/ebu,/hebu/ jamani, (alama 2)
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya kinyume: (alama 2)
Wakimbizi walihama na wakavunja kambi .- Wakimbizi waliishi na wakakita kambi.
- Tunga sentensi yenye muundo ufuatao (alama 2)
Nomino ya jamii, kirai kihusishi ,kitenzi kishirikishi,kielezo cha mahali.- Kicha cha funguo ki mezani.
- Bainisha kiima na chagizo katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
Mtoto huyo mzuri alifika shuleni asubuhi na mapema.- Mtoto huyo mzuri-kiima
- Asubuhi na mapema-Chagizo
- Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo (alama 2)
Wachezaji walishinda mechi wakatuzwa.- Wachezaji walishinda –Kishazi huru
- mechi wakatuzwa-Kishazi tegemezi
- Onyesha shamrisho ,kitondo, kiponzi na ala katika sentensi ifuatayo (alama 3)
Mwanafunzi alimbebea mwalimu mzigo kwa gari.- mzigo-shamirisho kipozi
- mwalimu-shamirisho kitondo
- gari-shamirisho ala
- Onyesha miundo miwili ya nomino katika ngeli ya A-WA (alama 2)
M-WA
Mtu -Watu
M-MI
Mtume-Mitume
KI-VI
Kiwete-Viwete
CH-VY
Chura-Vyura - Yakinisha sentensi ifuatayo katika nafsi ya pili umoja. (alama 2)
Hataenda shulenj kesho.
- Utaenda shuleni kesho.
- Eleza dhima ya tatu za viambishi tamati mbali na kauli ya kutenda/kiishio. (alama 3)
Ukanusho – haji
Kauli ya kutendea – som- e- a
Undani/kielezi – darasa-ni / mahali asimama-po
Wingi / amrisho – amke-ni, cheze-ni
Unominishaji/uzoefu – ushona-ji
Kiendelezi – amk-e-ni
Wakati acheza-po (Za kwanza 3×1=03) - Tunga sentensi moja katika wakati uliopita hali ya mazoea. (alama 2)
- Mwanafunzi alikuwa akisoma/asoma/anasoma kwa bidii shuleni.
- Changanua sentensi zifuatazo kwa kielezo cha mistari.
- Huyu wake alikuwa amefika lakini hatukumjua. (alama2)
S — S1 + S2
S1 — KN + KT
KN — W + V
W — Huyu
V — wake
KT — Ts + T
Ts — alikuwa
T — amefika
U — lakini
S2 — KN(O) + KT
KN — O
O — hatukumjua
KT — T
T — hatukumjua - Mtoto wa Shangazi hucheka sana. (alama 1)
S — KN + KT
KN — N + H + N
N — Mtoto
H — wa
N — Shangazi
KT — T + E
T — hucheka
E — sana
- Huyu wake alikuwa amefika lakini hatukumjua. (alama2)
- Eleza maana tatu zinazojitokeza katika sentensi. (alama 3)
Niliona Mamba.- Mamba-aina ya Nyoka
- Mamba-mnyama aishiye majini/Ngwena
- Mamba-magamba ya samaki
- Mamba-magome ya mti yaliyomeguliwa
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo. (alama 2)
Madebe hayo yatasafirishwa pamoja na nyundo hizi.- Vijidebe/videbe hivyo vitasafirishwa pamoja na vijinyundo hivi.
Ondoa makosa ya hijai na sarufi ipasavyo
- Vijidebe/videbe hivyo vitasafirishwa pamoja na vijinyundo hivi.
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo (alama 2)
- ISIMU JAMII
Sajili ya matangazo ya biashara.- Lugha ya kuvutia hutumiwa, bidhaa moto moto ili kuvutia wateja.
- Lugha shawishi mno hutumiwa, bidhaa nyororo sana ili kuwavutia wanunuzi.
- Kuna matumizi ya takiriri bei rahisi, bei rahisi, bei rahisi, ili kusisitiza bei ya bidhaa.
- Kuchanganya ndimi, bei ni affordable ili kuvutia wateja wengi.
- Athari za rangi hutumiwa ili kuvutia wateja wengi.
- Athari za muziki hutumiwa, kuvutia wateja.
- Huwa na ucheshi na porojo ili kuwavutia wateja.
- Lugha isiyo sanifu hutumika ili kuwasilisha ujumbe kwa wote kwa urahisi.
- Ubora wa bidhaa husisitizwa, ili kuwavutia wateja.
- Kuna upigaji chuku mwingi ili kuwavutia wateja.
- Sentensi fupi fupi hutumika kurahisisha mawasiliano.
- Kuna matumizi ya michoro kuvutia wateja.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - KCSE 2022 Prediction.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students