MAAGIZO
- Swali la kwanza ni la lazima.
- Maswali mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki;, riwaya,hadithi fupi na fasihi simulizi,
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
- Majibu yote lazima yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.
Maswali
SEHEMU YA A: TAMTHILIA - KIGOGO P. KEA (alama 20) SWALI LA LAZIMA
- “Lisilowezekana ni kukama ndume…………hujafa hujaumbika.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
- Taja na ueleze mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili. (al.2)
- Fafanua umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. (al.4)
- Jadili mbinu zozote kumi walizozitumia wanasagamoyo kujikomboa kutoka uongozi dhalimu katika jimbo la Sagamoyo. (al.10)
SEHEMU YA B: (CHOZ LA HERI)- K. MATEI
Jibu swali la 2 au la 3
- Riwaya
“ Tumeendelea kuwakwaza akina dada huku tukididimiza nguzo ya jamii yetu. Na kuwe huko kumtoa mekoni, lakini hili la kumpa jukumu la kuiongoza jamii nzima! Itakuwa kukivisha kichwa cha kuku kilemba.”- Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
- Eleza mifano mitatu ya kukwezwa kwa mwanamke na mitatu ya kutwazwa kwa mwamume kama anavyodai nafsineni. (al.6)
- Jadili umuhimu wa mandhari katika kujenga riwaya hii kwa kurejelea shule ya Tangamano. (al.10)
- “Ukiukaji wa haki za kibinadamu ni jambo la kawaida katika jamii ya Chozi la Heri. Jadili. (al.10)
SEHEMU YA C: (TUMBO LISILOSHIBA)- ALIFA CHOKOCHO
(Jibu swali la 4 au 5)
-
- MAME BAKARI- Mohammed Khelef Chassany
“Ubahimu naotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake.” Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya Mame Bakari. (al.10) - MASHARTI YA KISASA – Alifa Chokocho
“Hatimaye Dadi ilimbidi kuusikitikia ule uzuri ambao unapeleka kwingine wala si kwake. Na tazama ile kanzu jinsi ilivyomfika magotini kidada. Tazama anavyoiacha wazi ile miguu na miundi yake yenye kuvutia. Ndiyo, hata yeye Dadi akifuatana na mkewe Kidawa, wakipitana njiani wanawake wanaovaa hivyo huwatambulia macho. Kwa nini basi wanaume wengine wasimtumbulie macho mke wake yeye? Na Kidawa akimwona mumewe anawatumbulia macho wanawake hubwata kwa kimombo “Stop your gaze!” Na yeye humwuliza, ndio anasema nini? Na Kidawa hujibu, “Acha kudolea wanawake macho. Kwa nini wasiwe na uhuru wa kuvaa wanavyopenda? Au huelewi wanawake wana uhuru? “My dress my choice!” Lakini yeye hatimaye hujiuliza: Itakuwaje dunia iwapo watu wote (sio wanawake tu ) watavaa wanavyopenda?.- Jadili aina nne za taswira zinazojitkeza katika dondo hili. (al.4)
- Kando na taswira, tambua mbinu sita za kimtindo katika dondoo. (al.6)
Au
- MAME BAKARI- Mohammed Khelef Chassany
- Ukirejelea hadithi zifuatazo kwenye Diwani, eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza. (al.20)
- Tumbo Lisiloshiba.
- Mapenzi ya kifaurongo.
- Ndoto ya mashaka.
- Mtihani wa maisha.
SEHEMU YA D: (USHAIRI)
Jibu swali la 6 au 7
- Shairi la kwanza
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Maendeleo ya umma
Sio vitu maghalani
Kama tele vimesaki
Lakini havishikiki
Ama havikamatiki
Bei juu
Maendeleo ya umma
Sio vitu gulioni
Kuviona madukani
Kuvishika mikononi
Na huku wavitamani
Kama tama ya fisi
Kuvipata ng’o
Maendeleo ya umma
Sio vitu shubakani
Dhiki ni kwa mafakiri
Nafuu kwa mafakiri
Ni wao tu washitiri
Huo ni uistimari
Lo! Warudia
Maendeleo ya umma
Ni vitu kumilikiwa
Na wanyonge kupatiwa
Kwa bei kuzingatiwa
Bila ya kudhulumiwa
Na hata kuhadaiwa
Hiyo ni haki.
Maendeleo ya umma
Dola kudhibiti vitu
Vijapo nchini mwetu
Na kuwauzia watu
Toka nguo na sapatu
Pasibakishiwe na kitu
Huo usawa.
Maendeleo ya umma
Watu kuwa na kauli
Katika zao shughuli
Vikaoni kujadili
Na mwisho kuyakubali
Maamuzi halali
Udikteta la.
Maendeleo ya umma
Watu kuwa waungwana
Vijakazi na watwana
Nchini kuwa hakuna
Wote kuheshimiana
Wazee hata vijana.
Maswali- Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
- Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
- Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
- Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya. (al.2)
- Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
- Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
- Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
- Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
- Andika ubeti wanne kwa lugha nathari. (al.4)
Au
- Shairi la pili
Joseph Kiponda : Taifa ni Ushuru
Lau kama ingakuwa, madhali tuna uhuru
Watu kodi kutotowa, na kuifanya kufuru
Vije nchi ingakuwa, taifa bila ndururu
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Hivi taifa kumea, nakuendelea mbele
Kwamba lajitegemea, haliwategei wale
Yataka kujitolea, ushuru bila kelele
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Wafanyikazi wa umma, mfano mwema walimu
Wauguzi mahashuma, daktari wahadimu
Bila hizi darahima, vipi wangalihudumu?
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Si vyema kuombaomba, kwa wageni kila mara
Huwa twajifunga kamba, na kujitia izara
Adha zinapotukumba, kujitegemea bora
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.
Miradi ya maendeleo, yahitaji darahima
Ndo tufikie upeo, ulio dunia nzima
Wadogo na wenye vyeo, bila kodi tutakwama
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Ushuru si kwa wanyonge, wasokuwa na uwezo
Watozwe hata wabunge, na wengine wenye nazo
Yeyote asijitenge, kodi akalipa bezo
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru
Kwetu kutoa ushuru, ndiko kujitegemea
Pasiwepo na udhuru, sio wa kuelea
Huwa ni kama kiguru, asenao kutembea
Taifa halingakuwa, bilashi bila ushuru.
Maswali- Ujumbe unaowasilishwa katika shairi hili, una hadhira legwa. Zitaje. (al.3)
- Kwa kutolea mifano, eleza aina tatu za idhini ya kishairi alizozitumia mshairi. (al.3)
- Huku ukitoa mifano, taja aina tatu za takriri zinazojitokeza katika utungo huu. (al.3)
- Fafanua bahari zinazojitokeza katika shairi hili. ( al.4)
- Andika ubeti wa nne katika lugha nathari. (al.4)
- Taja mbinu tatu za kifani zilizotumika katika shairi hili. (al.3)
- SEHEMU YA E:(FASIHI SIMULIZI
Soma kifungu kifutacho kisha ujibu maswali yanayofata.
Basi kizito Matukio alipewa Cheo kikubwa kutokana na uchapakazi wake. Shirika alilokuwa akifanya kazi likawa na matumaini makubwa. Kizito naye badala ya kuchapa kazi akawa anajigamba na kujitapa mitaani. “Ukubwa ninaujua miye. Mimi ndiye Kizito hapa. Kizito Mzito mimi, akaringa. Akawadharau akina Wanjiku. Amina na Shikuku. Akajitosa kwenye raha bila kujali na kuvaa suti nzito alizoagizia kwa fedha za shirika. Muda si muda shirika likaingia hasara. Mwishowe ametimuliwa kazini na wazito wenyewe. Ameondoka na mkoba mzito wa madeni na fedheha: nguo sasa anavaa za matambara mazito! Jamani uzito unakowapeleka wazito.
MASWALI- Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (al.4)
- Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu. (al.2)
- Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (al.4)
- Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (al.3)
- Eleza hasara nne za miviga? (al.4)
- Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa. (al.3)
Mwongozo wa Kusahihisha
SEHEMU YA KIGOGO
- Swali la kwanza
“ Lisilowezekana ni kukama ndume……………….hujafa hujaumbika”- Eleza muktadha wa dondoo.
- Usemi wa Babu
- Msemewa ni majoka
- Majoka alikwa kwenye chumba cha wagonjwa na anazungumza na Babu katika dondoo hili
- Taja na uelezi mbinu moja ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili.
- Jazanda – lisilowezekana ni kukama dume
- Methali – Hujafa hujaumbika
- Fafanua umuhimu wa msemaji wa dondoo hili
- Msemaji ni Babu
- Ametumika kuonya umma kuwa si vyema kutedea wengine mabaya maana maovu yana mwisho.
- Kielelezo cha washauri wenye maarifa wanaokashifu viongozi dhidi ya maovu yao.
- Ametumiwa kuonyesha kuwa wazee wana jukumu la kuwashauri viongozi waliopotoka ili watawale vyema.
- Ametumiwa kufufua matumaini kwani analenga kumbadilisha.
- Majoka kuleta mabadiliko
- Ametumika kuonyesha tofauti za kiutawala – viongozi waanzilishi
- Waliongoza kwa nia njema lakini waliofuata wamejaa ubinafsi.
- Kujenga wahusika kama majoka
Hoja zozote 4 x1 = Alama 4
- Jadili mbinu zozote kumi walizozitumia wanasagamoyo kujikomboa kutoka uongozi dhalimu katika jimbo la Sagamoyo.
- Maandamano: Wananchi wanaamua kuandamana kudai haki zao wakati ule bei ya vyakula inapopanda.
- Uanaharakati : Wananchi wanajitolea ili kuihamasisha jamii kuhusu haki yao na udhalimu. Tunu anaenda mangweni ili kujaribu kuchochea ari ya kupigania haki akiwa na Sudi na siti.
- Migomo:: Walimu na wauguzi wanagoma kulalamikia ile hali duni ya utendaji kazi na mshahara duni.
- Mitandao ya kijamii:Wanajaribu kurusha matukio mubashara (live coverage) kupitia mitandao hii. Hali hii inasaidia kusambaza habari kwa urahisi.
- Matumizi ya runinga na televisheni: Runinga ya mzalendo inaangazia matatizo yanayowakumba wanasogamoyo. Inaripoti taarifa mbalimbali zinazohusu udhalimu wa serikali. Majoka anapanga njama ya kuifunga idhaa hiyo.
- Mshikamano wa wanyonge: Tunu naSudi wanatumia umoja wao kuwa nguzo muhimu ya kujikwamua uongozi dhalimu.
- Matumizi ya magazeti: Kuna magazeti yanayoandika habari mbalimbali juu ya harakti za kudai haki za wanasogamoyo.
- Sudi kuwatia hofu viongozi dhalimukwamba matendo yao yanamulikwa na matendo na washikadau kama vile jumuiya ya kimataifa.
- Kuwazindua wanyonge kuhusuhila za viongozi. Sudi anadhamiria kuwazindua Boza na Kombe.
- Kuchunguza mienendo ya viongozi dhalimu. Ashua na tunu wanatmbua kwamba kuna mkutano wa Kenga na kutaka kujua wachopanga.
- Kuwakusanya /kuwaita na kuwaongoza watu wasikilize wao na kukabili viongozi dhalimu.
- Kuwakubali viongozi moja kwa moja na kuwaambia makosa yao. Ashua anamkumbusha majoka kuwa hakuna asiyelipa kodi na kuwa hela hizo zingesafisha soko.
- Mikutano ya mhadhara na ya wachache kwa mfano hotuba ya tunu kwa wanadabari ilivyoangazia ukiukaji ya haki za wanasagamoyo.
- Kuamua kuunga mkono uongozi ufaao bila kuzingatia tabaka, hisia au umri- raia wanamtetea na kumuunga mkono Tunu, Sudi kukataa kuchonga kinyango cha majoka na kuchonga cha Tunu.
- Ashua kukataa ajira kwa majoka.
- Kususia mikutano ya majoka.
- Upelelezi wangerejelea kuchunguza kifo cha jabali
- Ufadhili wa nje kwa wapigania haki.
- Tunu kusomea uanasheria na kupigania haki za wanasagamoyo.
Hoja zozote 10 x 1= alama 10
- Eleza muktadha wa dondoo.
SEHEMU YA B: RIWAYA YA CHOZI LA HERI
-
- ni maneno ya mwanaharakati Tetei, yakinukuliwa na Kaizari katika masimuluzi yake kwa mwamu wake Ridhaa na wengine ya jinsi vita vilivyozuka baada ya kutawazwa kiongozi mpya mwanamke.
- Kukwezwa mwanamke – affirmative action na a third should be women, kupigania elimu kwa mtoto wa kike, haja ya kuwainua akina mama kiuchumi.
- Kutawazwa kwa mwanamume- hukumu ya kifo kwa mwanamume kumbaka mkewe, kutotetewa kwa wanaaume wanaoteseka katika ndoa kutokana na mapigo na dhiki za kisaikolojia kutoka kwa wake zao, kujeruhiwa na kudhalilishwa na wanawake kwa kupigwa.
- Kuchimuza mtiririko wa vitushi- Jinsi umu alijiunga na shule hii
- Kujenga mtindo/ploti kupitia hotuba, barua ya mwanaheri.
- Kuchimuza sifa za mwalimu Dhahabu, wanafunzi.
- Kujenga maudhui ya umaskini kupitia wanaunzi kama Kairu
- Kufafanua jukumu la elimu- kuleta maingiliano kati ya wanafunzi , kuwafanya kujua taabu za wenzao na kukubali jaala zao –umu, Kairu chanda chema.
- Ukiukaji wa haki za kibinafsi.
- Biashara ya watoto ikiongozwa na Bi. Kangara na Sauna
- Utekwaji nyara wa watoto – Sauna.
- Ajira kwa watoto Mf Dick anaajiriwa na Buda kuuza mihadarati.
- Wazazi kujihusisha kimapenzi na wanao mf. Sauna.
- Ubakaji mf Lime na mwanaheri.
- Utelekezaji watoto mf. Naomi anamwachia mumewe uangalizi wa wanao.
- Vijana wengi wanapoteza maisha katika ghasia za baada ya uchaguzi wengine wakiuawa na maafisa wa polisi.
- Dhuluma kwa wafanyikazi mf. Mwajiri wa Naomi.
- Visingizio mf Lemi.
- Utelekezaji wa watoto wachanga baada ya kujifungua mf Riziki Immaculate.
- Wizi na uporaji wa mali yaw engine mf. Katika ghasia za baada ya uchaguzi kwa maduka ya wahindi, waarabu na hata ya waafrika.
- Uavyaji wa mimba mf. Sauna anaavya mimba ya babake.
- Ndoa za mapema-uozwaji wa wasichana kwa wazee kv Pete kwa Fungo.
SEHEMU YA C: HADITHI FUPI TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
- MAME BAKARI – Mohammed Khelef Chassany
“ Ubahimu anaotendewa mwanmke unakuwa na athari mbaya kwake,” Jadili ukweli wa kauli hii ukirejelea hadithi ya mame Bakari
- Husababisha maumivu ya kimwili.
- Ilimfanya Sara kulia na kulaani/kujihurumia
- Mimba za mapema
- Kutengwa na watu /wanafunzi wenzake.
- Hofu ya kufukuzwa nyumbani (baba)
- Kulaumiwa na jamii
- Hofu ya kufukuzwa shuleni /kukatiziwa masomo.
- Kulaaniwa
- Kuoteza fahamu.
- Kusutwa
- Shida za kisaikolojia.
Hoja zozote 10 x 1 = alama 10
MASHARTI YA KISASA – Alifa Chokocho
Hatimaye Dadi ilimbidi kuusikitikia ule uzuri ambao unapelekwa kwingine wala si kwake. Na tazama ile Kanzu jinsi ilivyomfikia magotini kidawa. Tazama anavyoiacha wazi ile miguu na miundi yake yenye kuvutia. Ndiyo, hata yeye Dadi, akifuatana na mkewe Kidawa, wakipitana njiani wanawake wanaovaa hivyo huwatumbulia macho kwa nini basi wanaume wengine wasimtumbulie macho mke wake yeye? Na Kidawa akimwona mumewe anawatumbulia macho wanawake hubwata kwa kimombo “Stop your gaze!” Na yeye humwuliza, ndio anasema nini? Na Kidawa hujibu, “Acha kudolea wanawake macho. Kwa nini wasiwe na uhuru wa kuvaa wanavyopenda? Au huelewi wanawake wana uhuru? “My dress my choice!” Lakini yeye hatimaye hujiuliza: Itakuwaje dunia iwapo watu wote (sio wanawake tu ) watavaa wanavyopenda?.- Jadili aina nne za taswirs zinazojitokeza katika dondoo hili.
- Taswira hisi- Dadi kuusikitikia ule uzuri.
- Taswira mwendo – ambao unapelekwa kwingine.
- Taswira oni- Tazama Dadi akifuatana na mkewe, tazama anavyoiacha wazi.
- Taswira sikivu – hubwata kwa kimombo
- Na yeye humuuliza.
- Kando na taswira, tambua mbinu sita za kimtindo katika dondoo.
- Uzungumzi nafsia – Dadi anajihoji
- Maswali ya balagha –kwa nini wasiwe na uhuru wa kuvaa wanavyopenda?
- Nidhaa – My dress my choice
- Kuchanganya ndimi/kuhamisha msimbo – stop you gaze.
- Kinaya – Dadi kuwatumbulia macho wanawake ilhali hafurahii.
- Kidawa akitumbuliwa macho.
- Nahau- Tumbulia macho.
- Jadili aina nne za taswirs zinazojitokeza katika dondoo hili.
-
- Ukirejelea hadithi zifuatazo kwenye Diwani, eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza. (al.20)
- Wenyeji wa madongoporomoka waliishi kwa vibanda.
- Walikosihi watu wepesi wasio na mashiko.
- Watu wadogo (maskini) wanawekewa mitego na vikwazo vya sheria ili mali yao inyakuliwe.
- Maskini wanafinywa kama takataka na matajiri, jambo linalowakasirisha- mzee mego
- Ardhi ya maskini (wasiokuwa na nguvu ) lazima inayakuliwe.
- Eneo la madongoporomoka (wanakoishi) Lina vibanda vinavyozungukwa na uozo na bubujiko la maji machafu.
- Mzee mego na wenzake wanakumyua chai kwenye mkahawa mshenzi (hali duni)
Hawakuhusishwa /kushauriwa katika ujenzi wa taifa.
- Mapenzi ya kifaurongo.
- Dennis anaweza kuhuzu asili yake ya kimaskini.
- Wazazi wa Dennis huamka asubuhikutafuta vibarua vya kuwalimia matajiri mashamba.
- Dennis anasema kuwa wazazi wake hawana mahitaji.
- Shuka zilizotandikwa kitandan imwa Denis zimezeeka na kuchanikachanika.
- Dennis anatafunwa na njaa – mchele umekwisha, anapika uji
- Ndoto ya mashaka
- Mashaka anafanya kazi za vibaraua almuradi wajikimu na mamake (biti Kidebe)
- Walipewa vishamba vya kulima ili wapate chakula.
- Mashaka na waridi wanapoona hawakuwa na chochote (siku hiyo hatuna hili na lile).
- Waliishi kwa chumba kimoja kwa muda mrefu tangu waowane.
- Chumba cha kupangwa (watu tisa)
- Mabinti walibanana kwenye kitanda kidogo na wavulana walioweza kwa jirani.
- Walikaa karibu na choo ambacho hufurika mvua inaponyesha.
- Mashaka anakula kiporo wakati wa chamcha
- Mtihani wa maisha
- Samueli anatembea kilomita sita kwenda shule kutwa.
- Samueli anatazamia kukwamua familia yake kwenye umaskini.
- Baba Samueli anauza ng’ombe kumsomesha Samueli.
- Ukirejelea hadithi zifuatazo kwenye Diwani, eleza jinsi maudhui ya umaskini yanavyojitokeza. (al.20)
SEHEMU YA D: USHAIRI
-
- Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
- Anadhamiria kuonyesha wanyonge wanastahili usawa na haki – na wanyonge kupatiwa kwa bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa – ubeti wa 4
- Baininsha tamathali mbili za usemi katika shairi hili. (al.2)
- Tashbihi – ni kama la moto, wavitamani kama tama ya fisi
- Takriri – Maendeleo ya umma
- Nidaa – Lo!
- Eleza umuhimu tatu wa usambamba katika shairi hili. (al.2)
- Maendeleo ya umma (urudiaji wa fungu) – kusisitiza ujumbe
- Urudiaji wa silabi …..ni, ki – kuleta ridhimu
- Urudiaji wa neno.
- Onyesha jinsi maendeleo ya umma ulivyo kinaya. (al.2)
- Ni kinaya kuwa tuna vitu tele lakini bei I juu
- Ni kinaya kuviona vitu madukani lakini kuvipata ng’o
- Eleza mambo ambayo mshairi nachukulia kuwa maendelo halisi ya umma. (al.4)
- Vitu kumilikiwa na wanyone kupiwa.
- Bei kuzingatiwa bila kudhulumiwa
- Dola kudhibiti vitu vijapo nchini mwetu.
- Watu kuwa na kauli katika shughulika zao.
- Watu kuwa waungwana.
- Tambua matumizi ya mstari mishata kwa kutolea mifano. (al.2)
- Mishororo ambayo si toshelezi katka shairi
- Maendeleo ya umma
- Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (al.1)
- Ni mzalendo/mwananchi-nchini mwet ubeti 5
- Mtetezi wa haki – ubeti 4
- Fafanua toni ya shairi hili. (al.1)
- Kuhamasisha
- Kuzindua
- Andika ubeti wanne kwa lugha nathari. (al.4)
- Maendeleo ya umma ni kutafuta vitu na kuwauzia wanyonge kwa bei nafuu pasi na kunyanyasua wala kudanganywa na hivyo kulinda haki zao
- Eleza dhamira ya shairi hili. (al.2)
-
-
- Wafanyikazi wa umma
- Maskini na tajiri
- Wadogo na wenye vyeo.
-
- Inkisari –maendeleo , ndo/ndio
- Tabdila – Kutotowa /kutotoa
- Kuboronga sarufi-Kujitegemea bora/bora kujitegemea.
-
- Takriri neno-shuru ubet 2
- takriri sialbi – vina katikati kila ubeti
-
- Mathnawi- vipande 2 kila mshororo
- Ukaraguni – vina vinabadilika ubeti hadi mwingine
- Kibwagizo- mshororo wa mwisho umerudiwa kila ubeti .
- Tarbia – mishororo 4 kila ubeti.
-
- Si vizuri kuomba misaada ya kigeni kila wakati.
- Hivyo ni sawa na kuwa mateka
- Ni vyema kujitegemea kwa shida zetu
- Taifa haliwezi kuimarika bila ushuru
-
- Maswali balagha – vipi wangalihudumu
- Jazanda /sitiari- twajifunga kamba/ kiguru
- Tashbihi – ni kama kiguru
-
SEHEMU YA E:(FASIHI SIMULIZI )
- Onyesha kwa nini kipera hiki ni soga (al.4)
- Wahusika katika soga huwa ni wa kubuni
- Wahusika hupwa majina ya watu wanaopatikana katika jamii husika.
- Huwa na ukweli Fulani unaowahusu wanajamii
- Ucheshi unaotumika huwa muhimu kama njia ya kupunguza ukali wa ukweli uliomo.
- Fafanua vipengele viwili vya kimtindo vilivyotumika katika utungo huu. (al.2)
- Uradidi –nzito nzito
- Jazanda – mkoba mzito
- Taswira – nguo sasa navaa za matambara.
- Eleza matatizo utakayokumbana nayo nyanjani ukikusanya kazi ya kipera hiki (al.4)
- Gharama ya utafiti
- Mtazamo hasi kwa wanajamii
- Vizingiti vya kidini
- Kikwazo kutoka kwa watala
- Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi
- Ukosefu wa usalama
- Uchache wa wazee au wataalamu
- Taja mifano mitatu ya ngomezi za kisasa (al.3)
- Kengele zinazotumiwa kupigia hodi kwenye majumba.
- Toni katika rununu
- Milo kwenye ambulensi
- Eleza hasara nne za miviga? (al.4)
- Baadhi ya niviga kama vile kutiwa unyagoni kwa wasichana umepitwa.
- Baadhi ya miviga ukinzana na malengo ya taifa mf unyago
- Hujaza hofu mf kafara ya binadamu.
- Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa
- Fafanua umuhimu wa misimu ya kisasa. (al.3)
- Ni kitambulisho cha kundi Fulani la watu. Mfano misimu ya mabaharia huwatambulisha mabaharia wengine.
- Misimu huhifadhi siri za wanaotumia.
- Hutumiwa kuibua hisia mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji.
- Hukuza ushirikiano , uzalendo na uaminifu miongoni mwa wanaotumia.
- Huongeza haiba au ladha katika lugha-kuondoa ukinaifu unaotokana na kutumia msamiati uliozoeleka miaka nenda.
- Hupunguza makali katika lugha /kutasfidi lugha.
- Hukuza lugha zaidi-baadhi usanifisha na au kuwa lugha rasmi.
- Hufadhi historia na utamaduni wa jamii.
- Kielelezo cha mpangilio (mfumo) wa jamii Fulani, kijamii na kuchumi –matabaka.
- Hutumiwa kuondoa urasmi katika mazungumzo.
- Hukuza uwezo wa kufikiri na kutathmini au kudadisi.
Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - KCSE 2022 Prediction.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students