Kiswahili Maswali na majibu kutoka kwa Mocks

Share via Whatsapp
  1. Bainisha sauti mbili aina ya likwidi.

    Likwidi/Vilainisho:- Hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati ala za sauti zinapokaribiana na kutatiza hewa kwa namna maalum. Hutamkwa huku hewa ikiendelea kupita. Wanaisimu wamebainisha aina mbili za likwidi, ambazo ni vitambaza na vimadende.

  2. Andika upya sentensi ifuatayo ukitujmia -0- rejeshi tamati.
    Debe ambalo humwaga maji lina tundu

    Debe limwagalo maji lina tundu.

  3. Unda nomino mbili kutokana na kitenzi ‘dhalimu’

    mdhalimu, udhalimu

  4. Neno ‘kiongozi’ ni mofimu aina gani?

    Mofimu huru

  5. Ainisha yambwa katika sentensi :

    babake - yambwa tendewa
    simu - yambwa

  6. Huku ukitoa mfano, eleza maana ya sentensi tatanishi.

    Sentensi tatanishi ni sentensi pandikizi, yaani ambazo zinabebana kupitia matumizi ya kuwa na kwamba.

    Maria na Juma walipoona kuwa baba yao amewasili, walikimbia kuenda kumlaki.

  7. Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha jumla katika ngeli ya KI-VI.
    Vyote vilivyoraruka vimechomwa.

  8. Ainisha virai katika sentensi ifuatayo.
    Amefundushwa kupika vizuri na mamake.

    Amefundishwa kupika - Kirai kivumishi
    vizuri - kirai kielezi
    na mamake - kirai nomino

  9. Iweke nomino ‘pua’ katika ngeli yake.
    LI-YA

  10. Nini maana ya nomino dhahania.
    Ni nomino ambazo hazionekani haziwezi kushikika k.v huzuni
  11. Taja na ueleze aina ya kielezi kilichotumika katika sentensi. (ala2)
    Wanafunzi waadilifu washauriwa watembee makundimakundi.
    makundimakundi: kielezi cha idadi

  12. Andika kinyume cha sentensi hii. (ala2)

    Kijakazi alihuzunika mtoto alipopotea.
    Mtwana alifurahi mzee alipopatikana

  13. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    “Mzee, gari la moshi huondoka hapa saa ngapi?’’ Mgeni aliuliza

    Mgeni alikata kujua wakati ambao gari la moshi huondoka kutoka kwa mzee.

  14. Isimu Jamii

    Toa ushahidi kuwa Kiswahili ni lahaja ya Kibantu.

    Majibu yake:

    http://goo.gl/M4ApX7
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Maswali na majibu kutoka kwa Mocks.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 36226 times Last modified on Thursday, 12 November 2020 08:25
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest