Maagizo
- Jibu maswali yote
- UFAHAMU: (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Kijiji chetu kilikuwa kimeanza kuingiwa na wasiwasi. Katika kipindi cha miaka michache iliyopita tulikuwa tumewapoteza watu kadha na hakuna aliyeelewa kiini hasa cha majanga haya. Wazee walisikika wakisemezana kwa sauti za chini. Hatukujua hasa walichosema lakini ilikuwa bayana kuwa kijiji chetu kilikuwa juu ya mchongoma.
Kijijini kwetu kuna mambo yatokeayo yakaonekana miujiza.Tunabaki kutapatapa kuelezea chanzo chake na wesemavyo, akili ni nywele kila mtu ana zake. Ila zipo nywele za koto na za singa. Lakini kuna watu wenye kuandamwa na tata, mti wowote uliokuwa karibu ulishikiliwa kwa tumaini la kuleta nafuu. Ndiyo, nafuu. Na ndivyo ilivyotokea kiasi cha kila mtu kuwa bingwa wa kufasiri asili ya janga na suluhu yake. Hali hii iliendelea mpaka walipofika wataalamu kijijini kwetu na kufanya utafiti wa kisayansi uliotufumbulia asili ya dhiki zetu.
Siku hiyo ya kutolewa matokeo ya utafiti, kijiji kizima kilijumuika kwenye uwanja wa shule mapema. Hakuna aliyeonyesha uso wa furaha. Ilikuwa kama tuliokuwa mahakamani tunasubiri hukumu ya kesi ya jinai dhidi yetu. Siyakumbuki yote aliyosema yule mtaalamu lakini yapo yaliyotugusa sote.
“Najua mna hamu ya kujua tatizo liko wapi. Kabla ya kulieleza tatizo lenyewe ningependa kusema poleni kwa misiba iliyowaandama. Kuwapoteza wapendwa si pigo kwa familia tu, bali pia kwa kijiji na taifa. Na kuanzia sasa ninawaomba tushirikiane kuibadilisha hali hii. Hatuwezi kuendelea kuishi hivi," alisema huku wanakijiji wanamtazama kwa masikitiko makubwa.
"Binadamu yumo katika awamu ya kujiangamiza", aliendelea, "amefanya uvumbuzi wa teknolojia aali lakini ambayo sawa na mwaridi, ina miba. Miba hii sasa inamchoma kila aitundaye teknolojia. Kwa sababu ya wingi wetu, sasa tunataka kuzalisha mazao yetu haraka. Kwa sababu ya ongezeko kubwa la idadi ya watu walaji ni wengi lakini ardhi inazidi kujibana. Njia ya pekee ya kuongeza lishe ni kupitia uzalishaji zaidi wa vyakula. Katika ulimwengu ambapo vipando vile vile hurudiwa kupandwa kwenye ardhi ile ile, pato lake hupungua. Jibu la kuinua pato ni teknolojia. Teknolojia hii imebuni uzalishaji wa mbolea ya kemikali ambazo huchochea rotuba kwenye ardhi. Urutubishaji wa ardhi yetu ndogo umetuwezesha kuzalisha chai, kahawa, mahindi na mazao mengine kwa wingi ili kukidhi haja yetu ya chakula. Zamani ardhi ilipokuwa kubwa na idadi ya watu ikawa ndogo, haja hii ya mbolea haikuwepo. Ardhi iliachwa kujirutubisha yenyewe. Madhara tuyaonayo sasa hayakuwepo wakati huo."
"Leo hii utashi wetu wa kujitosheleza umetusukumizia ukingoni mwa maisha. Vyakula yvetu sasa vina kemikali hatari kutokana na mizizi ya mimea kufyonza virutubisho vyenye nitrojeni. Virutubisho hivi hustawisha mimea. Hata hivyo mimea hii tunayoila ina kemikali hatari kwa miili yetu. Kemikali hizi vilevile huingia kwenye nyasi ambazo huliwa na mifugo wetu. Mifugo hao hudhurika, nasi tunapofaidi bidhaa zao tunadhurika. Hata mito yetu na visima hupokea mikusanyiko ya kemikali hizi hatari, nasi tunazinywa kupitia kwa maji. Kemikali hizi husababisha saratani, na hili ndilo tatizo la kijiji hiki."
Kauli hii ya mwisho iliutikisa umati ule. Sauti za wanakijiji zilisikika zikinong'onezana. Wengi wa wanakijiji waliona kama kila kitu pale kijijini kilikuwa chanzo cha adhabu ya kifo kwao.
Baada ya kule kutanabahishwa, ilisikika sauti ya mlevi mmoja aliyesema kwa sauti kubwa kabisa, "Ni hivi, ama tule hivyo vibaya tufe polepole au tuache kuvila tufe mara moja."
Tamko hili la mlevi liliwasisimua wote waliokuwa pale, wakapata walau sababu ya kucheka. Kucheka huku kuliwatia watu matumaini, wakaanza kuuliza maswali. Kwa nini mbolca itengenezwe kutokana na kemikali hatari? Hivi dunia haijui kuwa ipo hatari kwenye mboica hizo? Je, waache kunywa maji na kutupa vyakula walivyokuwa navyo? Waliuliza maswali haya na mengine mengi.
Yule mtaalamu hakuwa na mengi ya kusema kwa sababu alifahamu kuwa kila aina ya teknolojia ina faida na madhara yake. Kwa hivyo alieleza kwa ufupi.
"Kemikali hizo ndizo huchochea rutuba ya ardhi ambayo huiwezesha mimea kukua na kutupa mazao mengi. Dunia inafahamu fika madhara ya kemikali zinazotumiwa kwenye mbolea lakini ifanyeje? Watu watakao kulishwa ni wengi. Ardhi imepungua kwa sababu ya wingi wa watu. Watu wanataka kula ilhali ardhi hiyo ndogo haina tena rutuba. Hata maji hayo yaliyoathirika mtayanywa tu bado. Mtaishije bila maji? Mtapika vipi? Mtakunywa nini? Hali hii tunaweza kuiondoa polepole kwa kuwekeza kwenye ufugaji wa kuku, ng'ombe na mbuzi wengi ili tutumie mbolea yao kurutubisha ardhi yetu. Wanasayansi wanasema itachukua yapata miaka mitano kuirejesha ardhi katika hali yake asilia."
Maelezo ya mtaalamu yule yalileta nafuu ya namna fulani kwa wanakijiji. Mzee mmoja alipewa nafasi kuzungumuza kabla ya kikao kufungwa. Mkutano ulipomalizika kijiji kilijua tatizo lilipokuwa na kuumaliza uvumi uliokuwa unaoteshwa kila leo.- Eleza sababu mbili za wanakijiji kuuona ugonjwa uliozuka kuwa miujiza. (alama 2)
- Eleza madhara manne ya kemikali za mbolea kulingana na kifungu. (alama 4)
- Bainisha mambo matatu yanayochochea kubuniwa kwa teknolojia mpya kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)
- Andika mambo mawili yanayoonyesha kuwa wazee wa jamii hii walikuwa na hadhi. (alama 2)
- Fafanua maana ya 'nywele za koto na 'nywele za singa' kwa kurejelea kifungu hiki. (alama 2)
- Kipe kifungu hiki anwani mwafaka. (alama 2)
- UFUPISHO: (Alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha wjibu maswali.
Demokrasia ni mfumo wa utawala ambapo wananchi huwa na mamlaka ya kuwachagua wawakilishi wao moja kwa moja. Demokrasia ni utawala wa umma. Utawala huu ni tofauti na utwala wa mtu mmoja au wa kundi dogo. Katika serikali ya kidemokrasia, umma huhakikishiwa haki fulani za kimsingi ambazo haziwezi kukiukwa au kutupiliwa mbali. Kwa kawaida haki hizo hutambuliwa na kudhibitiwa kimataifa.
Kwa mujibu wa Larry Diamond, demokrasia ina mihimili kadhaa. Demokrasia inashirikisha kuchagua na kubadili serikali kupitia chaguzi za huru na haki. Inahusu pia kuhusika kikamilifu kwa umma katika siasa na masuala ya kijamii kwa jumla. Kadhalika, demokrasia inahusu kulindwa kwa haki za kibinadamu za wananchi. Ni utawala ambao huongozwa na sheria, na ambapo sheria na taratibu zake hutumiwa kwa namna sawa kwa wananchi wote. Ni muhimu kutaja kwamba, kila nchi huifasiri dhana ya demokrasia kwa namna inavyoifaa yenyewe. Kwa mfano, katika taifa la Kenya, demokrasia ni serikali ya wananchi ikiongozwa na wananchi kwa niaba ya wananchi.
Zipo aina mbalimbali za demokrasia. Demokrasia ya moja kwa moja huhusu wananica kupigia sera fulani kura moja kwa moja bila kupitia kwa wajumbe au wawakilishi. Aina hii ya demokrasia huwezekana pale ambapo nchi ina idadi ndogo ya watu, hasa ambao wamesoma na wana mambo mengi yanayoshabihiana. Aina hii ya demokrasia ndiyo inayotumiwa Uswisi.
Kuna mataifa ambapo wananchi huwachagua wawakilishi wao wa bunge. Hii huitwa demokrasia ya uwakilishi au isiyo ya moja kwa moja. Hii ndiyo aina ya demokrasia inayotumika sana na hutilia mkazo ulinzi wa haki za wote; wawe wachache au wengi. Hutilia maanani matakwa ya watu binafsi kuliko yale ya taifa zima. Mfano mzuri wa demokrasia hii ni India. Demokrasia ya uwakilishi huweza kujitokeza kwa namna tofautitofauti kutegemea matakwa ya nchi mahususi.
Demokrasia ya Urais ni aina mojawapo ya demokrasia ya uwakilishi. Aina hii ya demokrasia humpa rais mamlaka makuu juu ya serikali. Rais huchaguliwa ama kwa njia ya moja kwa moja, au kwa kutumia wawakilishi. Yeye hawi tu kiongozi wa taifa, bali pia wa serikali kama ilivyo Kenya, Marekani na Ajentina. Hali kadhalika, kuna Demokrasia ya Bunge. Aina hii huipa bunge mamlaka makubwa. Kitengo cha utekelezi cha serikali hupata mamlaka yake kutoka bungeni. Kiongozi wa taifa na kiongozi wa serikali huwa watu tofauti na wenye viwango tofauti vya mamlaka. Kwa kawaida, kiongozi wa serikali huwa na mamlaka makubwa zaidi kama ilivyo Uingereza. Demokrasia ya kimabavu huelekea kupingana na dhana halisi ya demokrasia. Katika demokrasia hii tabaka la juu pekee ndilo lenye haki ya kuchagua wawakilishi wa taifa. Umma hauna haki hiyo. Mfano wa demokrasia hii ni Urusi.
Demokrasia ina manufaa mengi. Demokrasia hulinda masilahi ya wananchi wote; si walio wengi, si walio wachache, si wenye nguvu, si wanyonge...Demokrasia pia husaidia kugatua mamlaka, hivyo kuzuia kundi dogo kuwa mamlakani daima. Hili hufanikishwa na chaguzi za mara kwa mara. Kwa vile sheria haibagui, demokrasia basi hukuza usawa kwa wote. Walo wanaochaguliwa hujaribu kuweka sera mwafaka kwa kuwa hawadumu mamlakani. Kuhusishwa kwa umma katika kuamua watakaowatawala na kuwepo kwa kipindi mahususi cha kuhudumu hupunguza uwezekano wa kutokea kwa mapinduzi.
Hali kadhalika, demokrasia huchochea mabadiliko katika nchi kwa kuwa kila utawala huwa na kipindi chake maalumu ambapo umma hupata nafasi ya kuubadilisha, na hivyo kubadili sera na mwelekeo wa nchi. Demokrasia huipa umma nafasi ya kujifunza mambo mengi kuhusu siasa. Wakati wa uchaguzi, wagombeaji hunadi sera na rawaza zao, na hivyo kuelimisha umma. Demokrasia pia huwafanya watawala kuwa na tahadhari na kuwajibika kwa kuwa umma ulioerevuka kisiasa unawatia kwenye mizani na huenda usiwachague tena.
Ni dhahiri kwamba demokrasia ina dhima kuu katika maendeleo ya nchi. Hivyo ipo haja ya kuthamini na kuendeleza mifumo ifaayo ya kidemokrasia ili kuhakikisha kwamba haki ya kila raia imelindwa.- Fupisha ujumbe wa aya tano za kwanza kwa maneno 110. (alama 10; 1 ya mtiririko)
Matayarisho............................
.............................................
Nakala safi..............................
............................................. - Kwa maneno 50 eleza masuala amabayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho (alama 5; 1 ya mtiririko)
Matayarisho............................
.............................................
Nakala safi..............................
.............................................
- Fupisha ujumbe wa aya tano za kwanza kwa maneno 110. (alama 10; 1 ya mtiririko)
- MATUMIZI YA LUGHA: (Alama 40)
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)
- irabu, konsonanti, konsonanti irabu, konsonanti, irabu
- konsonanti, konsonanti, irabu, irabu
- Ainisha mofimu katika maneno yafuatayo: (alama 2)
- asemavyo
- mwangwi
- Onyesha aina za nomino katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
Shule nzima ilifurahia ukarimu wa Shirika la Tugawane. - Andika sentensi ifuatayo katika wingi. (alama 1)
Seremala aliulainisha ubao huo ili kutengeneza kasha amuuzie mlinzi huyo. - Tunga sentensi ukitumia vivumishi vinavyotoa maana zifuatazo:
- Nafasi katika orodha (alama 1)
- Kutobagua (alama 1)
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa. (alama 1)
Mtu huyo alifuata njia iliyomwelekeza mjini. - Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo bila kupoteza maana.
- Mhandisi alikarabati mtambo.
Mtambo ulikuwa kiwandani.
(Unganisha kuwa sentensi moja bila kutumia kiunganishi.) (alama 1) - Kembo alishona fulana hiyo vizuri sana. (Tumia kielezi cha kiasi badala ya vile vilivyopigiwa mstari.) (alama 1)
- Mhandisi alikarabati mtambo.
- Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi. (alama 2)
Mkurugenzi alisema kwamba wangetoa nyongeza ya mshahara mwaka ambao ungefuata. - Geuza sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu. (alama 1)
Ni wazi kwamba gharama ya maisha itapanda bei ya mafuta ikipanda. - Andika sentensi ifuatayo katika hali yakinishi. (alama 1)
Badi huwa hapitii hapa, huenda usimpate. - Zuri ni kwa baya, aminifu ni kwa .......... na vivu ni kwa................ (alama 2)
- Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani? (alama 2)
- sukari ........
- teo .............
- Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari (alama 2)
Mvua imepusa na watu wameanza kuondoka. - Vyakula viliandaliwa. Vyakula vilikuwa na viinilisha muhimu.
(Unganisha kuunda sentensi changamano.) (alama 2) - Bainisha yambwa na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alama3)
Zumari alimtunzia Keto watoto hao kwa upendo. - Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi 'ku' (alama 2
- Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
Usalama ukiimarishwa watalii wengi watakuwa wanazuru humu. - Unaporidhika na jambo unasema hewala, unaposhangilia timu yako kwa kupata ushindi unasema ....... .... na unapotaka usikivu unasema .............. (alama 2)
- Jepesi ni kwa rahisi, ukuta ni kwa. ................... na njia ni kwa ................. (alama 2)
- Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya dua na tua. (alama 2)
- Mzee Pumu ni mraibu wa vileo. Baada ya muda watoto wake wawili wanakuwa watumizi sugu wa vileo. Andika methali inayoweza kutumiwa kuelezea (alama 1)
- Tunga sentensi ukitumia kiunganishi cha uteuzi. (alama 1)
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)
- ISIMU JAMII: (Alama 10)
Wewe ni mhubiri katika Maabadi ya Shamu. Umealikwa kuwahubiria wanafunzi wa Shule ya Upili ya Lulu. Fafanua sifa kumi za lugha utakayotumia.
MAJIBU
- UFAHAMU
-
- Walikuwa hawaujui.
- Watu wengi walifariki.
2 x1 = 2
- Madhara ya kemikali ya mbolea
- Hudhuru afya za watu/husababisha magonjwa/ husababisha kansa/saratani
- Huwadhuru wanyama/ mifugo
- Hutia sumu kwenye mimea.
- Huchafua visima na mito.
- Husababisha vifo vya watu na mifugo.
4x1=4
- Mambo yanayochochea teknolojia mpya kubuniwa:
- Kupungua kwa mashamba/ ardhi inazidi kujibana
- Kuzorota kwa rutuba na kupunguza uzalishaji/vipando hurudiwa.
- Ongezeko la watu watakao lishe/ wingi wa watu.
- Kutoipa ardhi nafasi ya kupumua na kujirutubisha.
3x1=3
- Wazee wana hadhi kwa sababu.
- Jamii inataka kujua wanachokifikiria kuhusu janga jamii inatambua mchango wao katika usuluhishaji wa changamoto..
- Mzee mmoja anapewa nafasi kuhitimisha kikao
2 x1 = 2
- 'Nywele za koto' inarejelea wenye mawazo finyu au ya kubabaisha na 'nywele za singa' inarejelea wenye mawazo ya kina/mapevu./Kila mtu ana uelewa wake; Viwango vya uelewa havifanani.
1x 2 = 2 - Anwani mwafaka kwa kifungu.
- Madhara ya mbolea Hofu kijijini
- Janga la saratani/Saratani
- Madhara ya teknolojia
1 x 2 = 2
-
- UFUPISHO
-
- Demokrasia ni mfumo wa utawala wa kuwachagua wawakilishi moja kwa moja.
- Demokrasia ni utawala wa umma.
- Umma huhakikishiwa haki fulani za kimsingi ambazo haziwezi kukiukwa.
- Haki hizo hutambuliwa na kudhibitiwa kimataifa.
- Demokrasia hushirikisha uchaguzi ulio huru na wenye haki.
- Huwezesha kuhusika kikamilifu kwa umma katika siasa na masuala mengine ya kijamii.
- Husisitiza kulindwa kwa haki za kibinadamu na za wananchi.
- Huwa ni utawala wenye usawa wa kisheria/ni utawala ambao huongozwa na sheria.
- Kila nchi hufasiri dhana ya demokrasia kwa namna inayoifaa yenyewe.
- Kuna demokrasia ya moja kwa moja: raia hupigia sera fulani kura bila kupitia kwa wajumbe.
- Kuna demokrasia ya uwakilishi - demokrasia ya uwakilishi ya urais, demokrasia ya uwakilishi ya bunge na demokrasia ya uwakilishi ya kimabavu.
9x1=9
1 ya mtiririko Jumla 10
-
- Demokrasia hulinda maslahi ya raia wote.
- Hugatua mamlaka na kuzuia kundi dogo kudumu mamlakani.
- Hukuza usawa kwa wote kwa kuwa sheria haibagui.
- Wanaochaguliwa huweka sera mwafaka.
- Kuhusishwa kwa raia hupunguza uwezekano wa kutokea mapinduzi.
- Hukuza mabadiliko kwa kuwa uongozi huwa na kipindi maalumu cha kuhudumu.
- Demokrasia hufunza watu kuhusu siasa hasa wakati wa kampeni.
- Watawala huwa na tahadhari na kuwajibika.
- Demokrasia ina dhima muhimu kwa nchi hivyo inafaa kuendelezwa.
5x1= 5
-
- MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
-
- Ondoka, ongoka, anguka, atwaza
1/0 (alama 1) - Ndoa, ngao, mbao, twaa
1/0 (alama 1)
- Ondoka, ongoka, anguka, atwaza
-
-
- a - nafsi ya tatu/mtenda/ ngeli/kiambishi cha umoja/ kiambishi cha kiima
- sem- mzizi.
- a - kauli tenda/ kiishio/ kimalizio
- vyo - kirejeshi/namna
- 1/0 (alama 1)
- mw - umoja
angwi - mzizi
1/0 (alama 1)
-
- Shule - nomino ya jamii/ makundi / ya kawaida
ukarimu - nomino dhahania
Shirika la Tugawane - nomino ya pekee
3x1 = 3 - Maseremala walizilainisha mbao hizo ili kutengeneza makasha wawauzie walinzi hao.
1/0 -
- Mungla alikuwa wa kwanza katika mbio hizo.
1/0 - Kuli yeyote anaweza kupakia mizigo hiyo chomboni.
1/0
- Mungla alikuwa wa kwanza katika mbio hizo.
- Jitu hilo lilifuata jia/ jijia lililolielekeza jijini.
1/0 -
-
- Mhandisi alikarabatia mtambo kiwandani.
Au - Mtambo ulikarabatiwa kiwandani na mhandisi.
Au - Kiwandani kulikarabatiwa/mlikarabatiwa/palikarabatiwa mtambo na mhandisi.
Au - Mtambo uliokuwa ambao ulikuwa kiwandani ulikarabatiwa na mhandisi.
1/0
- Mhandisi alikarabatia mtambo kiwandani.
-
- Kembo alishona fulana hiyo tena.
Au - Kembo alishona fulana hiyo mara nyingi maradufu/daima/mara nyingine.
1/0
- Kembo alishona fulana hiyo tena.
-
-
- "Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao," Mkurugenzi akasema.
Au - "Watatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao," Mkurugenzi akasema.
Au - "Mtatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao," Mkurugenzi akasema.
Au - Mkurugenzi: Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao.
2/0
- "Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao," Mkurugenzi akasema.
-
- Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda baada ya kupanda kwa bei ya mafuta.
Au - Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.
Au - Ni wazi kwamba gharama ya maisha ingekuwa imepanda iwapo bei ya mafuta ingekuwa imepanda.
Au - Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda bei ya mafuta ilipopanda.
1/0
- Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda baada ya kupanda kwa bei ya mafuta.
- Badi huwa anapitia (hupitia) hapa, huenda ukampata/umpate/utampata.
1/0 - aminifu - saliti 1/0
vivu - kakamavu/ shupavu 1/0 -
- sukari - I-I, I-ZI( aina nyingi) 1/0
- teo - U-ZI 1/0
- Mvua imepusa na watu wameanza kundoka.
KN(N) KT(T) U KN(N) KT(Ts+T)
Au
S — S1 + U +S2
S1 — KN+KT
KN — N
N — Mvua
KT — T
T — imepusa
U — na
S2 — KN+KT
KN — N
N — watu
KT — Ts +T
Ts — wameanza
T — kuondoka
au
KN(N) KT(T) + U + KN(N) + KT(Ts + T)
2 x1 = 2 -
- Vyakula vilivyokuwa na viinilishe muhimu viliandaliwa.
Au - Vyakula vilivyoandaliwa vilikuwa na viinilishe muhimu.
Au - vyakula ambavyo viliandaliwa vilikuwa na vinilishe muhimu.
2/ 0
- Vyakula vilivyokuwa na viinilishe muhimu viliandaliwa.
- Keto - yambwa tendewa / kitondo
watoto hao-yambwa tendwa/kipozi
kwa upendo-Chagizo.
3x1 = 3 -
- Ku-nafsi ya pili umoja
- Baba anakupenda. - Mahali/ ngeli ya mahali/ mahali kusikodhihirika
- Huku kwao kunapendaza. - Kitenzi jina/ ngeli ya kitenzi-jina
- kucheza kule kunavutia. - Wakati uliopita wakati uliopita hali ya kukanusha
- wageni hawakufika mapema.
2x1=2
- Ku-nafsi ya pili umoja
- Usalama ukumarishwa - kitegemezi 1/0
Watalii wengi watakuwa wanazuru humu - huru. 1/0 - hoyee! huree!/hario!/ oyee! 1/0
jamani!/jama! enyi!/nyungwa! aisee! 1/0 - ukuta - kiambaza/ kizuizi/kizingiti/ngome/boma 1/0
njia - baraste/namna/mbinu/mtindo/jinsi/ sampuli 1/0 - dua-ombi
tua sita, pumzika, tulia, aibu, weka mzigo chini.
Tanbihi: Sentensi sharti ibainishe maana hizi.
2 x1=2
Mfano: Msafiri alitua mzigo akapiga magoti na kumpigia Mola dua. -
- Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
Au - Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina.
Au - Samaki huanza kuozea kichwani.
1/0
- Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.
-
- Doto hakula wala kunywa kwa siku kadha.
- Je, utakula wali au sima?
- Ama usome kwa bidii au ufeli mtihani wako.
1/0
-
- ISIMUJAMII (Alama 10)
- Msamiati wa kidini/ matumizi ya msamiati teule wa kidini
- Lugha ya kuwashawishi kumtii Mungu.
- Kurejelea vifungu vya vitabu vitakatifu.
- Kuchanganya ndimi/ kubadili msimbo.
- Lugha inaweza kuwa rasmi au isiyo rasmi.
- Lugha yenye toni kali ya kuonya.
- Kuwasawiri kama viumbe ambao ni wategemezi kwa Mungu.
- Maswali ya balagha ili kuwahusisha zaidi/kuteka hisia zao.
- Lugha ya mafumbo/matumizi ya majazi.
- Kurudia vifungu/baadhi ya maneno kama vile Amina'.
- Anaweza kutumia misimu ya vijana ili kujinasibisha nao.
- Matumizi ya ucheshi/ utani kiasi cha haja.
- Lugha ya unyenyekevu/ upole/ kusihi.
- Kutumia lugha sahili kulingana na kiwango cha wanafunzi.
- Matumizi ya msamiati wa shuleni
10 x 1 = 10
Tanbihi
Mifano sharti itolewe ili mtahiniwa apate alama 1.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download KCSE 2019 Kiswahili Paper 2 Questions With Marking Scheme.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students