KISWAHILI KARATASI YA 1 Marking Scheme - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
  1. Insha ichukue muundo wa ilani.

    GAZETI LA SAUTI,
    Jumanne, 25 – 6 – 2017,

    IDARA YA TRAFIKI WILAYA YA MUEMBE MMOJA,
    SANDUKU LA POSTA 22100 – 00100,
    MUEMBE MMOJA
             ILANI
    TAREHE 25 – JUNI – 2017
    KUH: ONGEZEKO LA AJALI BARABARANI

    Hoja za kuzingatiwa
    Mwanafunzi aeleze sababu za ongezeko la ajali na suluhu yake.
    • Madereva kuendesha magari kwa kasi.
    • Gari zingine kukosa vidhibiti mwendo.
    • Madereva kutofuata na kutozingatia alama za barabarani.
    • Madereva wengine kuendesha magari wakiwa walevi
    • Madereva kukosa vyeti na utaalaamu unaofaa kwa dereva yeyote.
    • Wananchi / wapita njia wanaovuka barabara kwa maeneo ya hatari
    • Matumizi ya magari kuchwara / mabovu na makuukuu barabarani
    • Hali duni ya barabara
    • Magari kubeba abiria kupita kiasi
      Suluhu
    • Idara ya trafiki kuwatahadharisha wanaokiuka sheria za barabarani watanaswa na kamera za siri zilizowekwa
    • Kunyang’anywa leseni
    • Kufunguliwa mashtaka
    • Kutozwa faini au kufungwa
    • Ukarabati wa barabara
    • Magari mabovu kuondolewa barabarani
    • Ukaguzi wa magari mara kwa mara kuakikisha magari yana vidhibiti mwendo na mikanda ya usalama
    • Wananchi kuhamasishwa umuhimu wa kutumia mikanda ya usalama na sheria nyingine za barabarani.

      Wenu mwaminifu,
      Sahihi
      Jina (Kristino Luvuno)
      Afisa mkuu wa trafiki
  1. Mbinu za kubuni nafasi za ajira nchini
    • Kutoa elimu inayofaa kwa vijana kama vile ufundi na teknolojia
    • Kuanzisha na kusambaza viwanda na karakana mashinani
    • Kuimarisha kilimo kwa kutumia mbinu mwafaka za kilimo, kutoa mikopo na pembejeo
    • Kuhifadhi maji ya mvua kutumika katika kilimo
    • Kuhimarisha sekta ya jua kali
    • Kuwapa mikopo kwa riba ya chini
    • Kuanzisha miradi ya kazi kwa vijana kama vile kupanda miti, kukarabati barabara
    • Kuzingatia miundo misingi, faafu kama vile barabara
    • Kusambaza umeme mashinani
  1. Methali inaamanisha kuwa mtu anapopatwa na janga / shida huathiri watu wa ukoo wake au usaidiwa na jamaa zake.

    Mwanafunzi asimulie kisa kuhusu mhusika aliyepatwa na msiba / janga au tatizo na marafiki wakamkimbia / wakamwambaa lakini jamaa yake walimsaidia.
    Anayefanya mambo maovu au mabaya hayamwathiri peke yake bali huwafikia jamaa zake pia.
    Tanbihi
    Si lazima mwanafunzi aeleze maana ya methali. Kisa kisichooana na mada atuzwe. D- (maki 01 – 02)
  1. Kianzo cha insha kionyeshe maneno yale yale asipoanza kwa kifungu amejitungia swali.
    Insha hii itafutiwe kichwa mwafaka.
    Mwanafunzi anaweza kueleza kisa kilichosababisha madhara au maagamizi kwa wenzake. Kama vile ajali barabarani, moto, dawa za kulevya, maporomoko.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 1 Marking Scheme - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest