KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

SEHEMU YA A:

USHAIRI

  1. Lazima
    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuatia

    Na ujenge nyumba yako, jingi jasho likuoshe,
    Ufyeke, upime na uweke nguzo,
    Kisha paa uweke na ukandike,
    Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.

    Wataanza kutalii mpaka mende usiku,
    Nje na ndani ya nyumba watazunguka,
    Bila woga, bila ruhusa ulichonacho watakula,
    Masaha yatakuwa yako, ijara ya kaziyo.

    Na nyingi dawa uweke, nyumba nzima uihame,
    Ukae nje nzima siku usubiri,
    Wazima wamelala ukindi usiku,
    Vichwa vigumu hawafii mende rahisi.

    Kifo cha mende sharti miguu juu,
    Kichwa ukikanyage kipasuke usikie,
    Na kisha wengine usiku mchana uwasake,
    Mpaka watakapokwisha. Usiseme nao.

    Maswali
    1.  
      1. Hili ni shairi la aina gani?       (alama 1)
      2. Tetea jibu lako.        (alama 3)
    2. Eleza jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake katika utenzi wa shairi hili.   (alama 4)
    3. Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi na uzitolee mifano. (alama 4)
    4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.        (alama 4)
    5. Eleza ujumbe wa shairi.          (alama 2)
    6. Toa mfano mmoja wa mstari mshata. (alama 1)
    7. Kichwa gani kinaliafiki shairi hili?  (alama 1)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA.

AREGE

MSTAHIKI MEYA

Jibu swali la 2 au la 3

  1. “Changamoto zinazokumba Cheneo ni sawa na zile za mataifa yanayoendelea ya bara la Afrika”.
    Jadili kauli hii.    (alama 20)
  1. “Ni hatari kuwaongoza watu wenye kukosa haya mawili.” 
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.   (alama 4)
    2. Fafanua haya mawili.  (alama 4)
    3. Eleza sifa mbili mbili za wahusika katika dondoo hili.    (alama 4)
    4. Fafanua migogoro yoyote minne katika tamthilia hii.    (alama 8)

SEHEMU C: HADITHI FUPI

WALIBORA NA S.A MOHAMMED (Wah)

DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE

Jibu swali la 4 au la 5

  1. “Nashangaa vile kwetu wanavyowaabudu watu hao wasiotujali.” Kwetu wapi? Ahaa! You guys are our brothers.
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake.  (alama 4)
    2. Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zilizotumika katika donddoo hili.  (alama 4)
    3. Jadili swala la ubaguzi katika hadithi hii. (alama 12)
  1. Fafanua maudhui ya utabaka katika ndoa ya Samani.   (alama 20)

SEHEMU YA D: RIWAYA

KEN WALIBORA

KIDAGAA KIMEMWOZEA

Jibu swali la 6 au la 7

  1. “Wajua bara la Afrika lataka watu waliosoma sana kulikombia toka kwenye utumwa wa…..”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.  (alama 4)
    2. Eleza mbinu iliyotumika katika dondoo hili.   (alama 3)
    3. Je, bara la Afrika lataka kukombolewa kutoka utumwa wa mambo matatu. Yataje.           (alama 3)
    4. Thibitisha ukweli kuwa jamii ya msemaji inakabiliwa na uhaba wa elimu kwa kutoa mifano riwayani.   (alama 10)
  1. Taja na ufafanue methali kumi zilizotumila katika riwaya hii.  (alama 20)

SEHEMU E:

FASIHI SIMULIZI

  1.  
    1.  
      1. Eleza maana ya miviga.    (alama 2)
      2. Taja sifa tano za miviga.   (alama 5)
      3. Taja hasara tatu za miviga.    (alama 3)
    2.  
      1. Eleza maana ya ngomezi. (alama 2)
      2. Toa mifano miwili ya ngomezi za kisasa.     (alama 2)
      3. Taja changamoto tatu za ngomezi za kisasa.       (alama 6)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2017 KITUI MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest