KISWAHILI KARATASI YA 3 Marking Scheme - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

kidagaa kimemwozea – Ken Walibora

  1. Maudhui ya utu
    • Amani anampa DJ shati baada ya kaptura yake DJ kuliwa na fahali
    • DJ anajitolea kuwapeleka Amani na inami kwa Nasaba bora na majisifu kutafuta ajira
    • Amani anachukua kitoto alicholazimishiwa na Nasaba Bora
    • Bi Zuhura anamkumbusha Nasaba Bora kuwa akiwa mtemi ana wajibu wa kulipa hifadhi kitoto kilichotupwa mlangoni mwa Amani
    • Bi Zuhura anaendelea kuwasaidia akina Amani an Imani kwa hali na mali kukilea kitoto uhuru.
    • Imani anajisabilia kuacha kazi kwa majisifu kuja kumsaidia Amani kumtunza uhuru
    • Bi Zuhura anamwomba mumewe kumsaidia mama mjamzito anayejifungulia njiani
    • Imaani anamuuguza Amani hospitalini na nyumbani mwa majisifu
    • Amana anamkinga na kumtetea Nasaba Bora dhidi ya shambulizi la Gaddafi(Oscar kambona)
    • Bi Zuhura anamtafutia mtemi Nasaba Bora kasisi na hata kuhudhuria mazishi yake licha ya maovu alitotendewa.
    • Amani anawagawia maskini ardhi pia anamfidia matuko weye kwa kumpa kasri la majununi   (10 x 2 =20)

Mstahiki meya

  1.  
    1. msemaji - meya
      Msemewa – madiwani I,II na III
      Mahali – Ofisi ya meya
      Sababu – meya aliwaita madiwani kupata ushauri wao kuhusu jinsi ya kuliongoza baraza. Meya anasema hali si ya kawaida na kuwa kuna baadhi ya madiwani wanaochochea watu kuwa baraza limeshindwa kutimiza majukumu yake (4 x 1 = 4)
    2. maudhui – Tamaa ya uongozi. Meya ansema mara hiyo hangetaka kusikia mtu amekufa kwani jambo hilo lingemletea tatizo wakati wa uchaguzi (2 x 1 = 2)
    3. ufisadi uliokithiri ndio uliokuwa msingi wa matatizo ya cheneo
      • matumizi ya pesa za umma kuwatumbuiza rafikize k.m. meya anamwambia Bili kuwa ana ‘entertainment vote’ ya meya yangoja ualishi tu.
      • unyakuzi wa ardhi ya umma.
      • kutupilia mbali kanuni za utendakazi k.m. kukatiza kandarasi ili meya ampe mtu wake mwenyewe.
      • hongo meya kusema kuwa baraza linagharamia petrol ya mhubiri akienda kuliombea
      • mali na vitu vya thamani kutoweka k.m. Bili anapendekeza wauze fimbo ya meya.
      • kutumia rasilimali za umma kwa faida ya kibinafsi k.m. watoto wa madiwani kupelekwa shuleni kwa magari ya baraza na hata kulipiwa karo na baraza.
      • kazi kutolewa kwa mapendeleo k.m meya anasema mhazili wake hakustahili kupata kazi ile ila alimpigania.
      • kutumia mahakama kuidhinisha uhalifu k.m kuacha kesi kufika mahakamani kisha kugawana fidia. (zozote 7 x 2 = 14)
  1. kama kiongozi mkuu wa Baraza lamji wa cheneo, meya Sosi anasahau kuwa alichaguliwa na watu kuwatumikia.
    • Ana kiburi k.m. alikataa kufuata ushauri mzuri wa Daktari siki na diwani wa III
    • Ana ubinafsi uliomfanya kuyajali maslahi yake tu na marafiki wake.
    • Tama ilimpofusha akajilimbikizia mali hata kuunga mkono mipango ya kuuza fimbo ya meya.
    • Ana mawazo/upeo finyu na hatambui anapokuwa akipotoshwa.
    • Anawadharau waliomchagua kama wasiostahili kusikilizwa wala kuheshimiwa.
    • Jiji lake lilikubwa na migomo ya wafanyakazi hivyo basi kuathiri maendeleo.
    • Sauti za waliogoma zilimnyima amani na utulivu.
    • Rafikiye Bili anamhepa wakati wa shida.
    • Aliathiriwa na mazingira machafu/uvundo wa takatak jijini.
    • Aliishi kwa hofu na kuhisi salama tu askari wanapofika.
    • Hatimaye aliitwa nguvuni kutokana na uongozi wake mbaya (zozote 10 x 2 = 20)
  2. USHAIRI
    1. kichwa
      • mabadiliko
      • Hayawi hayawi huwa
      • Hayawi huja yakawa (1 x 2 = 2)
    2.  
      1. methali
        • Hayawi hayawi huwa
        • kimya kingi kina mshindo
      2.  tashbihi
        • hata walioonewa kama taka za gereji
        • Ja taka ulimjaji
      3. Taswira
        • tope likang’ang’aniwa (zozote 2 x 2 = 4)
    3.  
      • lengo lake ni kuwatadharisha wale wanaowadharau wenzao wa tabaka la chini, wasaidiwe.
      • kuwapa moyo wasiokuwa nacho kuwa kesho huenda wakawa nacho (2x 1= 2)
    4. umbo
      • mishororo mine kwa kila ubeti
      • lina beti tano
      • Lina mizani kumi na sita kwa kila mshororo.
      • Vina vya kati vinatiririka isipokuwa vya mwisho
      • Lina kibwagizo (4 x 1=4)
    5. methali – Hatawi hayawi huwa (1 x 2 = 2)
    6.  
      1. ujaji – uamuzi
      2. Walotakwa – waliotakiwa kuwa (2 x 1 = 2)
    7.  
      • inkisari k.m. walotakwa – waliotakiwa; WaloKuwa – waliokuwa
      • Tabdila k.m. kumbaguwa – bagua; Hukutambuwa – tambua
      • Utohozi  k.m gereji –‘garage’; Ujaji – ‘judge’ (2 x 1 = 2)
  3. Damu nyeusi
    Uozo
    Maeko
    • Unywaji wa pombe kupindukia
    • Duni kuwasumbua wanakijiji kwa nyimbo zake.
    • Ubinafsi salim kumshauri jamila awache duni amwoe yeye
    • Duni kumpiga mkewe jamila.

    Kikaza
    • Ufisadi wa Bw. Mtajika na Bi.Mtajika
    • Usaliti wa baadhi ya wanakijiji kama vile machupa.
    • Mtajika kuwandanganya wanakjiji kwa kuwapa ahadi za uongo
    • Wanakijji kukosa uwajibikaji kwa kutojishughulisha na athari za chaguo lao la uongozi
      DamuNyeusi
    • Dereva kukataa kumbeba fikirini kwa vile ni mweusi
    • Fikirini kutozwa faini bure
    • Fikirini kuitwa na polisi kwa kutofunga zipu
    • Wanafunzi na mhadhiri kumbagua fikirini
    • Fiona kuwa katili kwa fikirini
      Samaki wa nchi za joto
    • Christine kuavya mimba.
    • Christine kujihushisha na mapenzi kiholela na peter
    • Bisahara haramu: ubadilishanaji wa fedha
    • Peter kuwapunja wavuvi
    • Wazungu kujihusisha katika uasherati
      Gilasi ya mwisho makaburini
    • Itikadi za ushirikina
    • Ukaidi wa vijana kama serikali na josefina kukataa maonyo ya msoi
    • Vijana kujihusisha na anasa
    • Wakora kuwaibia wateja na wahudumu wa baa ya makaburini (4 x1 = 4),(5x4=20)
  1. Fasihi simulizi
    1.  
      1. Ayari- Hekaya – Ayani ni mdanganyifu au mtu anayetumia ujanja/hila kulaghai wengine (al.2)
      2. Misimu- maneno yanayozuka na kutumiwa katika mazungumzo na makundi maalum ya watu katika jamii. Hatimaye hupotea ni machache tu yanayodumu. (al.2)
      3. Nyiso- ni nyombo zinazoimbwa jandoni (wavulana) na unyangoni(kwa wasichana). Kila jamii ina desturi zake zinazozingatiwa kama kigezo cha kuvusha vijana kutoka utotoni na kuingia utu uzima (al.2
      4.  Mbolezi- Nyimbo za matanga. Huimbwa wakati mtu amefariki au wakati wa maafa (al.2)
      5. Mbazi- Ni hadithi ambazo huwa za kimafumbo na mafunzo, hutolewa kwa kutumia kielelezo hasa wakati wa maongezi k.m. katika Bibilia.(al.2)
      6. Lakabu- Ni jina la kupanga ambalo mtu hujibandika ama hubandikwa kutokana na sifa zake za kimaumbile, kutabaka, tabia au kimatendo.
    2. Njia/mbinu za kukusanya fasihi simulizi
      • Kusikiliza- mhusonyaji anaweza kusikiliza wasanii katika jamii wakitamba.
      • Kushiriki- aweza kujipanga na jamii kwa kushiriki katika ngoma, soga, masimulizi n.k.
      • Kurekodi – kwa vinasa sauti, video, filamu
      • Kutazama – kushuhudia kwa macho fasihi Fulani, ikiendelezwa.
      • Kutumia hojajo
      • Mahojiano (zozote 4 x 2 = 8 )
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 3 Marking Scheme - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest