SEHEMU A:KIDAGAA KIMEMWOZEA – KEN WALIBORA
- Lazima
Kwa kutoa mifano, fafanua maudhui ya utu kama yanavyojitokeza katika riwaya ya kidagaa kimemwozea. (al. 20)
SEHEMU B:MSTAHIKI MEYA – T AREGE
Jibu swali la 2 au 3
- “Mwaka wa kuomba kura utakapofika sitataka mizuka yao kuniandama.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
- Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili (al.2)
- Ufisadi uliokithiri ndio uliokuwa msingi wa matatizo ya cheneo. Thibitisha kwa mifano mwafaka(al. 14)
- “Majuto ni mujukuu huja baadaye.” Thibitisha ukweli wa methali hii ukitoa mifano kutoka kwenye tamthilia ya mstahiki Meya. (al. 20)
SEHEMU C: USHAIRI
- SHAIRI
Hayawihujayakawa, walinena wanenaji
Nyuma walotakwa kuwa, wakawa ndo wajuaji
Nao mbele walokuwa, wakazikosa soseji
Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa.
Mwendo usimwone waw, damu yake sileleji
Kwa watu akikosewa, kwamba hajipi ujaji
Kimya kikuu angawa, kishindo ukitaraji
Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa.
Hawanacho walokuwa, huja kuwa wasemaji
Wakawa wanatakiwa, kule wasikotaraji
Hata walioonewa, kama taka za gereji
Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa.
Hayawi huja yakawa, ulijuwe mjuwaji
Matope waloumbiwa,huziishi za saruji
Na saraji walokuwa, tope likang’ang’aniwa
Hufika ya wanenaji,hayawi huja yakawa.
Mwovu huyo angakuwa, kampe japo kilaji
Sijipe kumumbaguwa,hwenda atawale mji
Kiwa hukumtambuwa, jataka ulimjaji
Hufika ya wanenaji, hayawi huja yakawa- Andika kichwa mwafaka cha shairi hili (al. 2)
- Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mtunzi wa shairi hili (al.4)
- Eleza dhamira ya mshairi (al.2)
- Eleza umbo la shairi hili (al.4)
- Taja methali inayotawala katika shairi (al. 2)
- Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kwenye shairi
- ujaji
- walotakwa
- Onyesha matumizi mawili ya uhuru wa mshairi (al.2)
SEHEMU D: DAMU NYEUSI NA HADITHI NYINGINE
- Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii (al. 20)
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI (AL. 20)
-
- Eleza istilahi zifuatazo: (al. 12)
- Ayani
- Misimu
- Nyiso
- Mbolezi
- Mbazi
- Lakabu
- Fafanua mbinu nne za kukusanya fasihi simulizi (al. 8)
- Eleza istilahi zifuatazo: (al. 12)
Download KISWAHILI KARATASI YA 3 - 2017 MURANG'A MOCK EXAMINATION.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students