MAAGIZO:
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha moja nyingine kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue Maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe ya lugha ya Kiswahili
MASWALI
- SWALI LA LAZIMA
Andika tahariri kwa Gazeti la Mwanga wa Jamii kuhusu manufaa ya mfumo wa elimu ya umilisi (CBC) nchini. - Mfumo wa serikali za Kaunti umeleta faida nyingi kuliko hasara. Jadili.
- Andika kisa kitakachoafiki methali hii;
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. - Andika kisa kitakachoanzia kwa maneno yafuatayo.
Mambo ni kangaja huenda yakaja. Tulikuwa tumefanya mazoezi kwa wiki moja mfululizo. Siku ikawadia. Tuliamka mafungulia ng’ombe….
MWONGOZO
- SWALI LA LAZIMA
- Sura au mtindo wa tahariri uzingatiwe.
- Kichwa kiwe na jina la gazeti (Mwanga wa Jamii), tarehe na mada ya uhariri.
- Mwili wa insha ufuate kwa maudhui manane kuhusu mada husika.
- Hitimisho ionyeshe msimamo kuhusu mada iliyojadiliwa.
- Kimalizio kiwe na;
- Jina la mhariri,
- Cheo chake mhariri
- Jina la gazeti (sio lazima kwa maana kichwa kina jina la gazeti)
- Mtahiniwa atumie wakati uliopo hali timilifu.
- Mfano wa kichwa;
GAZETI LA MWANGA WA JAMII
JUMATATU, JULAI 18, 2023
MANUFAA YA MFUMO WA ELIMU YA UMILISI NCHINI
Baadhi ya hoja ni;
Manufaa ya elimu ya umilisi- Huwasaidia wanafunzi kutambua, kukuza na kutumia talanta zao.
- Wanafunzi wataweza kujitegemea katika maisha yao ya usoni.
- Inasaidia nchi kujiendeleza kiuchumi na kuepuka kuagiza bidhaa nje ya nchi.
- Inasaidia katika kuendeleza utamaduni.
- Uchafuzi wa mazingira unapungua.
- Mfumo huu unasisitiza utendaji kuliko nadharia.
- Wanafunzi wako na uhuru wa kufanya watakachotaka katika maisha yao ya usoni.
- Hukuza utangamano miongoni mwa mwanafunzi wanapotekeleza wajibu pamoja.
- Inawezesha wanafunzi kuwa wabunifu wanapotumia vitu vinavyopatikana kwenye mazingira yao.
- Matumizi ya teknolojia yanapanuka kwa vile wanafunzi wanaitumia katika masomo.
- Wanafunzi wanapata ujuzi wa mambo mengi wakiwa wangali wadogo.
- Serikali za Kaunti zimeleta changamoto nyingi kuliko ufanisi. Jadili.
- Hii ni insha ya mjadala.
- Mada ishughulikiwe kwa kina, kila hoja aya yake.
- Maudhui yajitokeze vilivyo.
- Mtahiniwa atumie msamiati bora na lugha yenye mnato.
( lazima aangazie pande zote mbili)
Baadhi ya hoja ni hizi;
Ugatuzi ni hali ya kugawa mamlaka/ raslimali kutoka kwa serikali kuu hadi kwa serikali za mashinani.
Kuunga/ Ufanisi wa mfumo wa ugatuzi- Nafasi za ajira zimebuniwa.
- Raslimali zimefikia raia mashinani.
- Mali asili imezalishwa zaidi.
- Makundi na makampuni mbalimbali yanaweza kufanikiwa kupata kandarasi. mbalimbali kama vile za ujenzi wa barabara, maofisi, mabwawa za taifa nk
- Ugavi sawa wa raslimali za kitaifa kwa kaunti zote.
- Huduma za serikali zimeletwa karibu na wananchi.
- Wananchi wamepata fursa ya kuendeleza kaunti zao kama inavyofaa kutegemea mahitaji yao.
- Imekuwa rahisi kumulika namna ambavyo pesa zilizotengewa kaunti zinavyotumiwa.
- Imeokoa wakati wa kushughulikia maswala fulani kwani hakuna kutafuta huduma mbali.
- Nafasi katika taasisi za elimu ya juu zimeweza kunufaisha wenyeji kinyume na ilivyokuwa hapo awali.
- Huduma nyingi za kijamii na za kimsingi zimeletwa karibu na wanaoishi katika kaunti husika.
- Wananchi wanahusishwa vilivyo katika kufanya maamuzi muhimu katika maeneo yao, kwa mfano kuhusishwa katika bajeti, miradi ya shule, barabara nk.
- Ushindani chanya baina ya kaunti/maeneo mbalimbali.
- Ushirikiano wa kibiashara baina ya kaunti mbalimbali.
Kupinga/ Changamoto za mfumo wa ugatuzi- Ufisadi miongoni mwa maafisa wa kaunti hasa wakati wa kupeana zabuni.(Ufisadi umegatuliwa)
- Ukabila na mapendeleo kwa mfano kwa misingi ya ukoo au sehemu anayotoka kiongozi.
- Kaunti zingine ni changa sana kiuchumi na kimaendeleo.
- Mfumo huu ni swala geni zaidi nchini – kuna changamoto kwani hakuna tajriba ya awali ya kurejelea.
- Huenda maeneo mengine katika kaunti yakatengwa au kupuuzwa huku mengine yakipendelewa.
- Kunaweza kutokea chuki, kutoelewana na kutoaminiana miongoni mwa watu wa maeneo mbalimbali wakiwemo viongozi.
- Ushindani usio na manufaa baina ya serikali za kaunti na serikali kuu.
- Kunyosheana kidole cha lawama kati ya magavana na maafisa katika serikali kuu kuhusu kutokuwepo kwa miundo msingi bora.
- Matumizi mabaya ya pesa kwa kutoa huduma zinazofanana kati ya serikali kuu na zile za kaunti.
- Ubadhirifu na matumizi mabaya ya raslimali.
- Wengi wanaoshikilia nyadhifa mbalimbali katika serikali za kaunti hawana tajriba ya kutosha.
- Kuzorota kwa baadhi ya huduma kama vile ya afya.
- Methali; Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- Hii ni insha ya methali.
- Maana yake ni kwamba mtu anayeenda huku na huko kwenye ufuo wa bahari hakosi kitoweo.
- Hutumika kutufunza kwamba anayehangaikia jambo fulani lazima mwishowe atafanikiwa/ lazima ataambulia kitu.
- Kisa kionyeshe hali ambapo mhusika anafanya juhudi za hapa na pale na mwishowe azoe matunda.
- Hapa kufanikiwa lazima kutokane na bidii.
- Kisa lazima kionyeshe pande mbili za methali: kujibiidisha hapa na pale, na kule kufanikiwa.
- Anwani ya insha iwe ni methali yenyewe.
- Andika kisa kitakachoanzia kwa maneno yafuatayo.
Mambo ni kangaja huenda yakaja. Tulikuwa tumefanya mazoezi kwa wiki moja mfululizo. Siku ikawadia. Tuliamka mafungulia ng’ombe….
Mtahiniwa ako na uhuru wa kubuni kisa chochote kitakachoanzia kwa maneno haya bila kubadilisha.
Yaweza kuwa ni siku ya michezo iliyokubwa na mashaka.
Aidha hakukuwa na mashaka lakini matokeo yakawa kinyume cha walivyotarajia.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Nginda Girls Mock Examination 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students