Maagizo
- Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
MASWALI
- Mauaji katika ndoa yamekita mizizi katika taifa letu. Umeteuliwa na rais wa jamuhuri kuwa katibu wa Tume ya Uwiano wa Kijamii kuchunguza sababu za mauaji haya na hatua za kukabiliana na janga hili. Andika Ripoti. Alama 20
- Kama mwanafunzi bora katika shule yako umepata nafasi ya kuzuru kwenye mbuga la wanyama la Masai Mara kwa siku tano ambapo umejifundisha mengi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi misitu katika mfumo ikolojia. Andika shajara. Alama 20
- Tunga kisa kitakachodhihirisah ukweli wa methali:
Asiyemjua simba atazame mtegowe. alama 20 - Nilipoipokea simu nilisikia: “Njoo upesi kwenye kituo cha afya cha Kamaliza kuna dharura…” Endeleza. Alama 20
MWONGOZO
- Mauaji katika ndoa yamekita mizizi katika taifa letu. Umeteuliwa na rais wa jamuhuri kuwa katibu wa Tume ya Uwiano wa Kijamii kuchunguza sababu za mauaji haya na hatua za kukabiliana na janga hili. Andika Ripoti. Alama 20.
Sababu za mauaji:- Ukosefu wa ushauri nasaha- vijana kujiingiza katika ndoa kabla hawajaelewa yaliyomo.
- Vijana kukimbilia maisha ya ndoa wangali wadogo.
- Matumizi ya dawa za kulevya.
- Kupanda kwa gharama ya maisha – vijana wanashindwa kupata mahitaji ya kimsingi
- Vijana kutegemea wazazi wao kwa kila kitu hivyo basi, wanapokuwa wakubwa wanashindwa kujitegemea.
- Mifano mibaya ya wazazi wanaoishi maisha ya kuzozana.
- Ukosefu wa nafasi za ajira miongoni mwa vijana na hivyo kupata mzongo wa akili.
- Utumiaji mbaya wa mali na ubadhirifu wa mali ya taifa.
- Mfadhaiko wa moyo/msongo wa kimawazo.
- Ukosefu wa uaminifu katika ndoa.
- Wanandoa kutelekeza majukumu yao ya kinyumba- kutoshughulikia mahitaji ya kimsingi ya familia kama, lishe
- Ushirikina /imani potovu za kidini
- Taasubi ya kiume/kike.
Hatua za kukabiliana na tatizo hili- Wanandoa kupewa ushauri nasaha kabla na wakiwa katika ndoa
- Kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto katika ndoa. Wazazi kufunza watoto kujitegemea.
- Kuimalisha demokrasia katika jamii.
- Kuimarisha hali ya kiuchumi kwa wanandoa ili kuwa na uwezo wa kukudhia mahitaji ya kimsingi.
- Hatua kali za kiserikali kwa wale wanaotekeleza unyama huu zichukuliwe.
- Kukabiliana na dawa za kulevya.
- Viongozi wa kidini kuwajibikia majukumu yao ya kuelekeza jamii.
- Vijana wafunzwe kuwa wavumilivu.
- Talaka – kumwacha mwanandoa ikiwa mmeshindwa kusuluhisha yaliyoko.
- Kufufua mila na desturi za kiafrika kuhusu mivigha ya ndoa.
- Kama mwanafunzi bora katika shule yako umepata nafasi ya kuzuru kwenye mbuga la wanyama la Masai Mara kwa siku tano ambapo umejifundisha mengi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi misitu katika mfumo ikolojia. Andika shajara. Alama 20
Umuhimu wa misitu kwenye mfumo ikolojia:- Huwa asili ya chakula na matunda kwa binadamu na wanyama
- Huwa maskani ya wanyama.
- Huvuta mvua
- Viwanda hupata malighafi kutoka kwa misitu.
- Misitu huleta dawa za kienyeji.
- Huzuia mmomonyoko wa udongo.
- Hurebesha mandhari kutokana na rangi yake ya kijani.
- Huleta hewa safi.
- Ni kivutio cha watalii.
- Hufanya vivuli vinavyokinga watu na wanyama
- Huwa ni chanzo cha miti na chemchemi za maji.
- Huzuilia upepo mkali uvumao kwa kasi.
- Tunga kisa kitakachodhihirisah ukweli wa methali:
Asiyemjua simba atazame mtegowe. alama 20
Matumizi ya methali:
Kabla ya kujiingiza katika jambo fulani au shughuli fulani inatupasa kuchunguza hatari zilizopo.
Mtahiniwa aweze kuonyesha mtu ambaye hakukadiria hatari ya shughuli fulani na hivyo basi baada ya kuingilia akajipata katika matatizo mengi. - Nilipoipokea simu nilisikia: Njoo upesi kwenye kituo cha afya cha Kamaliza kuna dharura. Endeleza. Alama 20
Mtahiniwa aonyeshe ni kwa nini aliitwa na alipoenda cha dharura kilikuwa kipi?
Kisa chake kijenge taharuki kutoka mwanzo hadi mwisho.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Wahundura Boys Mock Examination 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students