Maagizo
- Jibu maswali yote.
MASWALI
UFAHAMU
Somo kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Muhula wa kwanza wa kidato cha tatu ulipoanza, kama ilivyokuwa desturi katika shule ya Askofu Timotheo, wanafunzi walichunguzwa hali na Sista. Sista akaandika nakala ya matokeo ya uchunguzi wake na kumkabidhi mwalimu mkuu wa shule Bi. Margaret. Mwalimu mkuu akafanya lililomjuzu. Akaandikia waraka wazazi kwa wasichana waliuokuwa katika nakala ya matokeo ya Sista.
Jumatatu ya juma la tatu ilianza kama siku nyinginezo. Wanafunzi walijumuika gwarideni. .Maombi ya asubuhi yalifanywa. Mwalimu wa zamu akawakumbusha wanafunzi majukumu yao na bendera ikapandishwa. Zamu ya mkuu wa shule ilitimia. Aliwakumbusha wanafunzi umuhimu wakuwajibikia vitendo vyao. Baada ya hilo, aliita majina ya wanafunzi watatu na akatangaza kwamba baada yakufumukana wafike ofisini mwake. Vicheko vya chini kwa chini vilianguliwa. Sababu ya kuitwa kwa wanafunzi wale ilikuwa dhahiri.
Sela na wenzake walipofika ofisini walielekezwa wasubiri katika chumba cha mapokezi. Ingawa walifahamu sababu ya kuitwa pale, mpango uliokuwapo ulikuwa usiku wa giza. Hakuna aliyezungumza na mwenziwe kutokana na muemeo wa mawazo. Wote waliinamisha nyuso zao.
Baada ya nusu saa hivi, ofisini mliigia wazazi wawili; wa kike na kiume. Walikuwa wazazi wa Sela ; Mzee Butali na mkewe. Wao walionekana kuemewa na fikira. Kutokana na urasmi wa muktadha ule, hapakuwa na mazungumzo baada ya salamu. Mara kwa mara, Mzee Butali alitupia bintiye jicho la uhasama kabla ya mhazili kumfahamisha mwalimu mkuu kuhusu mjo wa wazazi wale.
Ofisini, Bi. Margaret alitia udibaji , “ Asanteni kwa kuja. Sisi kama walimu na wazazi hukabiliana na mengi. Tukio lililowaleta hapa ni la kawaida kwetu. Ingawa sisi hufanya tuwezavyo kuwalinda wanetu, mara nyingi tabia zao hutupiga chenga…”
Wakati huu wote wazazi wa Sela walikuwa wamenyamaza. Mamake Sela alikuwa akimtazama Bi. Margaret huku Mzee Butali akiwa ameinama. Bi. Margaret alipohitimisha usemi wake, Mzee Butali aliinua uso wake na kumtazama mwalimu mkuu.
“Mwalimu nina swali moja ambalo ningetaka unijibu. Je, ni kwa nini sisi huwaleta watoto shuleni?” mzee Butali aliuliza kwa sauti iliyojaa uchungu.
Baada ya mazungumzo kati ya mwalimu mkuu na wazazi wa Sela, uamuzi ulitolewa. Sela na wenzake wawili hawangeweza kusoma pamoja na wengine baada ya hali yao kubainika. Bi. Margaret alipendekeza watafutiwe shule za kutwa karibu na watokako ili waendelee kusoma huku wazazi wakiwatunza. Alikuwa amewaandikia barua za mapendekezo ili wapokelewe katika shule ambazo wangechagua. Sela aliondoka shuleni na wazazi wake.
Boma la Mzee Butali liligeuka jahanamu baada ya kutoka shuleni. Mzee Butali aliwazulia majojo Sela na mama yake. Majirani nao walishuhudia bughudha hizo kwa mbali.
“ Leo ndio mtanitambua. Mama gani anayemtaza mwana akigeuka afriti? Sikutumia hela zangu mimi katika elimu yake hadi nikaitwa pangu pakavu? Mtwae kilicho chenu mniondokee!” mzee Butali aliwafokea Sela na mama yake.
“Baba Sela, nani kasema huu ni msiba wangu? Tutautwaa pamoja. Huyu ni mtoto wetu, sio maradhi. Tutaondoka ndio; lakini elewa uchungu wa mwana ajuaye ni mzazi.” Mama yake Sela alitoa kauli yake.
Maswali
- Shule ya Askofu Timotheo imejengwa katika msingi wa kidini. Fafanua. (alama 2)
- “.. sisi hufanya tuwezavyo kuwalinda wanetu,..” Kulingana na kifungu eleza jinsi wazazi na walimu wanavyolinda wana wao. (alama 4)
- Mwalimu mkuu alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuwajibikia kwa wanafunzi katika vitendo vyao. Taja matokeo tatu ya kutowajibika kwa Sela. (alama 3)
- Kwa kutolea sifa mbili, eleza hulka ya Mzee Batili. (alama 2)
- Taja mtindo uliotumika katika kauli hii: Boma la Mzee Butali liligeuka jahanamu… (alama 1)
- Eleza maana ya: (alama 2)
- alitia udibaji
- majojo
- Kipe kifungu hiki anwani mwafaka. (alama 1)
UFUPISHO
Hapana shaka yeyote kuwa, ujio wa teknolojia nchini ulibadilisha ufumo wa kimaisha uliokuwepo hapo awali. Binafsi, ni miongoni mwa kizazi kilichozaliwa na kulelewa wakati hakukuwa na teknolojia yoyote katika jamii. Pengine teknolojia kubwa iliyokuwepo nyakati hizo ni redio na saa. Njia kuu ya mawasiliano ilikuwa uandishi wa barua.
Shirika la Posta Kenya lilikuwa na umuhimu mkubwa sana, kwani idadi kubwa ya wananchi ambao hawangemudu gharama ya kupiga simu za serikali walikuwa wakilazimika kuandika barua kuwatumia wapendwa wao. Si wengi walimudu kutumia simu hizo, kwani nyingi zilikuwa katika maeneo ya mijini. Kwa hivyo ili kutumia ingemlazimu mtu aliye katika maeneo ya mashambani kutenga siku fulani kusafiri hadi mjini ili kuitumia simu fulani.
Hata hivyo, mwanzoni wa 2000, hali ya mawasiliano ilianza kubadilika nchini kutokana na ujio wa simu za rununu. Wale walimudu kununua simu hizo walionekana kama matajiri . Lilikuwa jambo la kipekee kumwona mtu akiwasiliana kwa kutumia kisanduku kidogo kilicho bonyezwabonyezwa vidude kwa vidole . Miaka ilivyosonga, mawasiliano yaliendelea kurahisika .Bei za simu zikashuka pakubwa . Miundo ya simu pia iliimarika, kiasi kwamba kwa sasa,ni vigumu kumwona mtu yoyote bila simu hata watoto. Kwa sasa ,mtu yeyote anayemiliki simu isiyo na intaneti huonekana kama”aliyebaki nyuma”.
Si intaneti tu, simu za sasa ni kama ofisi ndogo. Kando na intaneti,zina huduma nyingi ambazo hupatikana katika saibakefu,kwani ndiko kuna tarakilishi zilizounganishwa na intaneti. Sababu ya urejeleo ni kuonyesha jinsi teknolojia na mawasiliano yalivyo badili katika jamii. Kilicho wazi ni kuwa ,ujio wa simu za kisasa umerahisisha sana mawasiliano na jinsi tunavyopata habari kuhusu matukio tofauti duniani kwa muda mfupi. Licha ya manufaa hayo yote,kuna tatizo kubwa kuhusu simu hizo: uwepo wa baadhi ya apu na mitandao ya kijamii.
Ukweli ni kuwa baadhi ya apu zilizo katika simu hizo zinatishia kuvuruga maadili katika jamii. Kwa mfano, muundo wa apu ya Tiktok humruhushu mtu kurekodi video na kuiweka mtandaoni. Hilo huwapa nafasi maelfu ya watu kutazama video husika na kuifurahia. Wengine hueleza hisia zao kuhusu video husika.
Hata hivyo kile kinachohitajika ni kuhakikisha kuwa sawa na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook , Instagram, Twitter au Whatsapp, kanuni na masharti ya kuutumia yanafuatiliwa kuhakikisha uzingatiaji ili usivuruge mustakabali wa kimaadili kwa kizazi cha sasa na vile vijavyo.
- Kwa maneno 80 fupisha aya tatu za kwanza. (alama 8)
matayarisho
jibu - Fupisha ujumbe wa aya tatu za mwisho kwa maneno 70. (alama 7)
Matayarisho
jibu
MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
- Andika neno lenye sauti zifuatazo (alama 1)
- Kipasuo-kwamizo sighuna cha kaakaa gumu,irabu ya juu,nyuma,irabu ya juu,nyuma ,kikwaruzo ghuna cha masine,irabu ya chini,kati tandaze
- Dondoa sauti mwambatano katika maneno yafuatayo na uainishe mahali pa kutamkia. (alama 1)
Tamba
Afya - Linganua irabu katika neno;mavue. (alama 1)
-
- Onyesha muundo wa silabi kwenye kiima katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Mwalimu aliwasili kwa gari ili awasilishe ripoti ya wanahabari. - Eleza tofauti kati ya sauti mwambatano na silabi mwambatano.Thibitisha kwa mfano. (alama 2)
- Onyesha muundo wa silabi kwenye kiima katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
- Weka shadda panapofaa katika maneno yafuatayo. (alama 1)
- katakata (kugawavipande.)
- katakata (kabisa kabisa)
- Bainisha dhamira inayoibuliwa na sentensi ifuatayo. (alama 1)
- Ombeni bila kusita.
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo. (alama 1)
- Mofimu ya nafsi ya tatu wingi,hali timilifu ,mzizi,kauli ya kutendwa,kauli ya kutenda(kiishio).
- Kwa kutunga sentensi,tumia ‘a’unganifu kuonyesha dhana zifuatazo; (alama 2)
- uhusiano wa cheo/kazi
- uhusiano wa wakati
- Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.
- Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo. (alama 2)
(Bila kutumia vitenzi visaidizi) - Mwalimu huwaadhibu wanafunzi wapotovu.Mwalimu huwarekebisha wengi. (alama 2)
(unganisha kuwa sentensi changamano;Anza kwa kiunganishi) - Maandalizi yalifanywa kwa wakati ufaao.Wanajeshi walishinda vita hivyo. (alama 2)
(Tumia ‘ki’ ya masharti kuunda sentensi moja) - Michuano itaanza juma lijalo.Wakufunzi wanaendelea kuwatia makali wachezaji. (alama 2)
(Unganisha kuwa sentensi moja inayoanza kwa: Wakufunzi…)
- Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo. (alama 2)
- Tunga sententensi ukitumia aina zifuatazo za maneno. (alama 2)
- nomino ambatano
- nomino ya kitenzijina
- Tunga sentensi ukitumia kivumishi cha pekee cha nyongeza (alama 1)
- Tunga sentensi ukitumia shina -w-kama ; (alama 2)
- kitenzi kisaidizi
- kitenzi kishirikishi
-
- Eleza dhana ngeli. (alama 1)
- Tunga sentensi kwa kutumia nomino zifuatazo na ubainishe upatanisho wa kisarufi. (alama 1)
- simanzi
- wino
- Andika sentensi ifuatayayo katika hali ya ukubwa wingi; (alama 2)
Mama huyo aliicheza tarumbeta kwa vidole na midomo . - Kwa kutolea mifano bainisha miundo miwili ya ngeli ya KI-VI. (alama 2)
- Pambanua sentensi ifuatayo kwa mishale, (alama 3)
Bwalo ambalo lilisakafiwa litafunguliwa mwakani. - Iandike upya sentensi ifuatayo ukianza kwa shamirisho kipozi. (alama 1)
Alila aliwakatakatia mifugo wale nyasi kwa upanga. - Eleza dhana chagizo. (alama 1)
- Tunga sentensi yenye muundo ufuatao; (alama 1)
KN(Ꝋ)+KT(T) - Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo. (alama 2)
Hawa ni watoto wa marehemu Bwana Nzovu na Bi.Makambo. - Tunga sentensi moja kutofautisha sahibu na shaibu. (alama 1)
- Taja visawe viwili vya ,kata kamba , (alama 1)
ISIMUJAMII
Wewe ni chifu wa kata la Mawindoni. Umealikwa kuhutubia wanakijiji kuhusu swala la usalama. Fafanua mtindo wa lugha utakayotumia. (alama 10)
MWONGOZO
UFAHAMU
Majibu
- Shule ya Askofu Timotheo imejengwa katika msingi wa kidini. Fafanua. (alama 2)
- Imepewa jina linalohusishwa na dini-Askofu Timotheo
- Maombi ya asubuhi yalifanywa.
- Msamiati Sista
- “.. sisi hufanya tuwezavyo kuwalinda wanetu,..” Kulingana na kifungu eleza jinsi wazazi na walimu wanavyolinda wana wao. (alama 4)
- Kuwakumbusha wanafunzi majukumu yao.
- Kuwakumbusha wanafunzi umuhimu wa kuwajibika- kuwashauri
- Kuwapeleka watoto shule
- Kuwalipia watoto karo
- Kuwatunza
- Mwalimu mkuu alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuwajibikia kwa wanafunzi katika vitendo vyao. Taja matokeo tatu ya kutowajibika kwa Sela. (alama 3)
- Alipata uja uzito
- Alinyimwa nafasi ya kuendelea kusomea katika shule ya Askofu Timotheo
- Alifurushwa kwao wakiwa na mama yake
- Kwa kutolea sifa mbili, eleza hulka ya Mzee Batili. (alama 2)
- Mpyaro- “…mwana akigeuka afriti”
- Mwenye hasira- aliwafukuza Sela na mama yake
- Taja mtindo uliotumika katika kauli hii: Boma la Mzee Butali liligeuka jahanamu… (alama 1)
sitiari - Eleza maana ya: (alama 2)
- alitia udibaji-alianzia kusema
- majojo- fujo kuu
- Kipe kifungu hiki anwani mwafaka. (alama 1)
Uwajibikaji/ Changamoto za malezi
UFUPISHO
- (alama 7, 1 mtiririko)
jibu
ujio wa teknolojia ulibadilisha mfumo wa kimaisha
teknolojia kubwa iliyokuwepo ni redio na saa
njia kuu ya mawasiliano ilikuwa barua
idadi kubwa ya wananchi haingemudu alama ya kupiga simu
simu nyingi zilikuwa katika maeneo ya mijini.
Hali ya mawasiliano ilbadilika kutokana na ujio wa simu
Miaka ilivyosonga bei ya simu ilishuka
Miundo ya simu iliimarika
Asiye na simu iliyo na intaneti huonekana kama aliyebaki nyuma. - Fupisha ujumbe wa aya tatu za mwisho kwa maneno 70. (alama 6, 1, mtririko)
jibu
simu sasa ni kama ofisi
ujio wa simu ulirahisisha mawasiliano
simu huwezesha kupata habari kwa muda mfupi
simu zina huduma nyingi ambazo hupatikana saibakefu
baadhi ya apu zinahatarisha kuvuruga maadili
kanunu na masharti ya kutumia apuyafuatiliwe
MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
- Andika neno lenye sauti zifuatazo (alama 1)
- Kipasuo-kwamizo sighuna cha kaakaa gumu,irabu ya juu,nyuma,irabu ya juu,nyuma ,kikwaruzo ghuna cha masine,irabu ya chini,kati tandaze
-
- Chuuza
-
- Dondoa sauti mwambatano katika maneno yafuatayo na uainishe mahali pa kutamkia. (alama 1)
Tamba mb-midomoni
Afya fy-mdomo-meno,kaakaagumu - Linganua irabu katika neno;mavue. (alama 1)
- /a/ chini, kati
- /u/ nyuma,juu,viringwa
- /e/ mbele,wastani
- Kipasuo-kwamizo sighuna cha kaakaa gumu,irabu ya juu,nyuma,irabu ya juu,nyuma ,kikwaruzo ghuna cha masine,irabu ya chini,kati tandaze
-
- Onyesha muundo wa silabi kwenye kiima katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
Mwalimu aliwasili kwa gari ili awasilishe ripoti ya wanahabari.- mwalimu -mwa-li-mu -KKI+KI+KI
- Eleza tofauti kati ya sauti mwambatano na silabi mwambatano.Thibitisha kwa mfano. (alama 2)
- sauti mwambatano ni sauti yenye kosonati mbili au zaidi bila irabu na hutamkwa kama sauti moja ilhali silabi mwambatano ni sauti yenye kosonanti mbili au zaidi na irabu na hutamkwa kama silabu maja. mfano:neno mwalimu
- mw-sauti
- mwa-silabi
- sauti mwambatano ni sauti yenye kosonati mbili au zaidi bila irabu na hutamkwa kama sauti moja ilhali silabi mwambatano ni sauti yenye kosonanti mbili au zaidi na irabu na hutamkwa kama silabu maja. mfano:neno mwalimu
- Onyesha muundo wa silabi kwenye kiima katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
- Weka shadda panapofaa katika maneno yafuatayo. (alama 1)
- katakata (kugawavipande.) kata'kata
- katakata (kabisa kabisa)ka'takata
- Bainisha dhamira inayoibuliwa na sentensi ifuatayo. (alama 1)
- Ombeni bila kusita.
- agizi/agiza/amrishi
- Ombeni bila kusita.
- Andika maneno yenye miundo ifuatayo. (alama 1)
- Mofimu ya nafsi ya tatu wingi,hali timilifu ,mzizi,kauli ya kutendwa,kauli ya kutenda(kiishio).
- wamepigwa
mwalinu atathmini majibu ya mwanafunzi
- wamepigwa
- Mofimu ya nafsi ya tatu wingi,hali timilifu ,mzizi,kauli ya kutendwa,kauli ya kutenda(kiishio).
- Kwa kutunga sentensi,tumia ‘a’unganifu kuonyesha dhana zifuatazo; (alama 2)
- uhusiano wa cheo/kazi
- kiongozi wa chama amekaribishwa
- uhusiano wa wakati
- masomo ya asubuhi yalifana
- uhusiano wa cheo/kazi
- Andika upya sentensi zifuatazo kulingana na maagizo.
- Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo. (alama 2)
(Bila kutumia vitenzi visaidizi)- wachezaji watashinda mchezo wa leo
- Mwalimu huwaadhibu wanafunzi wapotovu.Mwalimu huwarekebisha wengi. (alama 2)
(unganisha kuwa sentensi changamano;Anza kwa kiunganishi)- ingawa mwalimu huwaadhibu wanafunzi wapotovu, huwarekebisha wengi
- Maandalizi yalifanywa kwa wakati ufaao.Wanajeshi walishinda vita hivyo. (alama 2)
(Tumia ‘ki’ ya masharti kuunda sentensi moja)- maandalizi yakifanywa kwa wakati ufaao wanajeshi watashinda vita hivyo
- Michuano itaanza juma lijalo.Wakufunzi wanaendelea kuwatia makali wachezaji. (alama 2)
(Unganisha kuwa sentensi moja inayoanza kwa: Wakufunzi…)- wakufunzi wanaendelea kuwatia makali wachezaji kwa kuwa/ kwa vile/kwa sababu michuano itaanza juma lijalo
- Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo. (alama 2)
- Tunga sententensi ukitumia aina zifuatazo za maneno. (alama 2)
- nomino ambatano
- mwanariadha alipewa tuzo kwa kushinda
- nomino ya kitenzijina
- kuimba kwake kunapendeza
- nomino ambatano
- Tunga sentensi ukitumia kivumishi cha pekee cha nyongeza (alama 1)
- tumia-ingine
- Tunga sentensi ukitumia shina -w-kama ; (alama 2)
- kitenzi kisaidizi
- mwalimu alikuwa anafundisha somo
- kitenzi kishirikishi
- mkulima alikuwa shambani
- kitenzi kisaidizi
-
- Eleza dhana ngeli. (alama 1)
- ngeli ni uainisho wa nomino za kiswahili katika makundi yenye sifa maalum
- Eleza dhana ngeli. (alama 1)
- Tunga sentensi kwa kutumia nomino zifuatazo na ubainishe upatanisho wa kisarufi. (alama 1)
- simanzi
- simanizi ilimpata mwombolizaji
- simanzi iliwapata waombelezaji
- wino
- wino ulimwagika
- wino ulimwagika
- simanzi
- Andika sentensi ifuatayayo katika hali ya ukubwa wingi; (alama 2)
Mama huyo aliicheza tarumbeta kwa vidole na midomo .- majimama hayo yaliyacheza majitarumbeta kwa majidole na majidomo
- majidole na majidomo
- Kwa kutolea mifano bainisha miundo miwili ya ngeli ya KI-VI. (alama 2)
- chakula -ch
vyakula -vy - kiatu -ki
viatu -vi
- chakula -ch
- Pambanua sentensi ifuatayo kwa mishale, (alama 3)
Bwalo ambalo lilisakafiwa litafunguliwa mwakani.- s -KN+KT
- KN-N+S
- N-bwalo
- S-ambalo lilisakafiwa
- KT-T+E
- T-litafunguliwa
- E-mwakani
- Iandike upya sentensi ifuatayo ukianza kwa shamirisho kipozi. (alama 1)
Alila aliwakatakatia mifugo wale nyasi kwa upanga.- nyasi zilikatakatiwa mifugo wale na alila kwa upanga
- Eleza dhana chagizo. (alama 1)
- chagizo ni sehemu ya sentensi inayochukuliwa na kielezi
- ni kielezi
- Tunga sentensi yenye muundo ufuatao; (alama 1)
KN(Ꝋ)+KT(T)- anaandika
- Eleza maana mbili za sentensi ifuatayo. (alama 2)
Hawa ni watoto wa marehemu Bwana Nzovu na Bi.Makambo.- bwana nzovu ni marehemu lakini bi makambo yu hai
- wazazi wote wawili ni marehemu
- Tunga sentensi moja kutofautisha sahibu na shaibu. (alama 1)
- sahibu-rafiki shaibu-mwanaume mzee
- Taja visawe viwili vya ,kata kamba , (alama 1)
- kata roho
- aga dunia
- enda jangameo
- piga dunia teke
- enda zake
- ipa dunia mkono wa buriani
- enda kuzimuni
- ipa dunia kisogo
- tangulia mbele ya haki
- fuata njia ya marahaba
- koma moyo
ISIMUJAMII
Wewe ni chifu wa kata la Mawindoni. Umealikwa kuhutubia wanakijiji kuhusu swala la usalama. Fafanua mtindo wa lugha utakayotumia. (alama 10)
- Msamiati uoane na mada
- Lugha yenye heshima/ unyenyekevu
- Lugha isiyo na mzaha wala utani
- Kuchanganya ndimi/kubadilisha msimbo
- Kutumia wakatiuliopo zaidi
- Kujirudiarudia/ takriri/ uradidi
- Matumizi ya tamathali
- Lugha shawishi
- Kutaja vyeo hasa mwanzoni
- Matumizi ya ishara/viziada lugha
Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Wahundura Boys Mock Examination 2023.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students