Click the link below to download as a full set with all the subjects. (PDF)
https://downloads.easyelimu.com/details/35-Alliance_High_School_Pre_Trial_Examination
SHULE YA UPILI YA ALLIANCE
KIDATO CHA NNE MUHULA WA PILI, 2018, MWIGA-MWIGO
KISWAHILI 102/2 (Ufahamu, Ufupisho, Matumizi ya Lugha, Isimu-Jamii)
Jibu maswali yote. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali.
Karatasi hii ina kurasa 11. Watahiniwa ni lazima waangalie kama kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
- Ufahamu (Alama 15)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali.
Aisee, umeyasikia haya? Nafahamishwa kuwa mwenzetu huyu hapa mtaani, mwenye kiburi cha tausi, amepata funzo la mwaka. Naambiwa aliapa kuwa katu hatayafanya aliyoyafanya usiku ule.
Kisa na maana ni kuwa Athumani alipata mwaliko wa kwenda kufanya mahojiano kule katika jiji kuu. Nasikia kazi aliyotarajia kupata baada ya mahojiano ilikuwa na donge si haba. Huyo hangekuwa mwenzetu tena angeipata kazi hiyo. Nafikiri angezidisha madaba maradufu.
Athumani hakutaka mtu yeyote kujua kwamba anaenda kufanya mahojiano. Alipanga mambo yake kisirisiri. Akaamua kuomba idhini ya siku moja kutoka kazini akisingizia kuwa alikuwa mgonjwa ambaye angempeleka hospitalini siku hiyo. Akapanga kusafiri kwa basi la usiku ili kuwahi jijini asubuhi, kufanya mahojiano na kurudi jioni
Kama kawaida, mabasi ya usiku huondoka hapa kuanzia saa mbili. Madereva nao wana tabia za kuyasimamisha katika eneo fulani njiani ili abiria wenye baja wajisaidie na angaa kupata kitu kidogo cha kutuliza tumbo.
Basi liliposimama, Athumani alishuka kama abiria wenzake. Akaenda msalani kisha mkahawani. Alikuwa na uraibu wa maziwa ya mtindi. Akanunua pakiti moja na kuifungua harakaharake; ungedhani anashindana na mtu. Akayagugumia kana kwamba angenyang'anywa. Akaitisha na pakiti ya pili ya maziwa yao hayo na kuyagugumia kamna ya kwanza. Abiria wenzake wakastaajabu, lakini kwa kuwa kila mtu alikuwa na hamsini zake, hawakumjali.
Baada ya muda, abiria wakarudi garini. Basi likang'on nanga. Kitambo cha nusu saa bivi, tumbo likaanza kumchafuka Athumani Akahangaika na kuhangaika pale kitini jasho likaanza kumtoka. Alipoona hayavumiliki tena, alichapuka kitini himahima hadi kwa dereva. Kutokana na mkazo aliokuwa nao, akasahau kutumia lugha ya adabu. Baada ya kumwamrisha dereva kusimamisha basi, dereva naye akaongeza mwendo. Alihofia kuwa yaenda anayemwamrisha ni mmoja wa majambazi wa barabarani ambao wana mazoea ya kumtuma mmoja wao asafiri pamoja na abiria wengine kama mmoja wao. Wenzake huwa shika eneo fulani ambapo jambazi abiria ataomba basi lisimamishwe ili ajisaldie. Dereva akilisimamisha basi pale alipoombwa, majambazi hutoka vichakani na kuwavamia. Huwaumiza na kuwafilisi abiria, dereva na tingo
Athumani alielidelea kuhangaika. Hatimaye, dereva aliamua na liwe liwalo alipomwona Athumani amechutama huku jasho likimtiririka Akaliegesha basi kando ya barabara na kumpa Athumani nafasi ya kujisaidia. Athumani hakungoja basi lisimame kabisa wala wtingo kufungua mlango. Aliufungua harakaharaka na kufyatuka nje kama risasi na kujitoma kichakani. Akavua suruali yake upesiupesi na kutekeleza matilaba bila kufahamu kuwa pale alipokuwa anatekeleza shughuli hizi alikuweko kuchakulo; mnyama mdogo ambaye kinga yake anapoingiliwa na adui ni kumcha maji yenye harufu mbaya. Karibu Athumani amalie kuchakulo yule bila kujua kutokana na mkazo aliokuwa nao. Kuchakulo akasonga kidogo na kumrushin Athumani maji yale mavazini mwake. Athumani hakuyahisi haya.
Athumani alichukua muda pale kichakani hata abiria wakasikika wakilalamika. Aliporudi basini huku amechangamka kwa kulitua zigo lililomlemea, abiria wote walizishika pua zao wakisema mfuuul Athumani hakujua kuna nini.
Basi liliendelea na safari huku abiria wakishikilia pua zao. Kila wakijaribu kuziachilia, ndivyo harufu iliyohanikiza ilivyozidi kuwaathiri. Wakashindwa kuuhimili uvundo. Wengi walidhani kuwa Athumani alijininihii. Wakaamrisha atupwe nje au wote washuke warejeshewe nauli zao. Kwa kuwa baridi ina msimamo kwa kondoo mwenye manyoya haba, njia rahisi ilikuwa kumshusha Athumani aliyekuwa peke yake badala ya abiria katika basi zima. Alishushwa katika kitongoji kimojawapo.
Athumani aliposhushwa, alichanganyikiwa asijue la kufanya. Hakujua alikoshushwa wala wa kumwendea kumuomba msaada. Alipokuwa akiwaza na kuwazua afanye nini, genge la majambazi lilitokea na kumvamia Likampora, kila kitu mkoba wake, stakabadhi, pesa na hata kumvua mavazi aliyokuwa nayo. Wakamwacha uchi wa mnyama katika eneo asilojua mtu wa kumwauni. Baridi ya usiku ikamvamia vilivyo.
Athumani aliokolewa siku iliyofuata na madereva a magari ambao hapo awali alikuwa akiwabeza. Wakamtafutia mavazi na kumbeba hadi nyumbani. Hakuweza kufanya yale mahojiano. Alipokumbuka yaliyomfika siku huo, alikula yamini kuwa katu hatakunywa wala kula chakula chochote akiwa safarini.
Maswali- Tambua sifa tatu hasi za Athumani (alama 3)
- Thibitisha kuwa Athumani ni msiri (alama 1)
- Onesha changamoto za safari za mabasi kulingana na kifungu (alama 3)
- Jadili mafunzo aliyopata Athumani.. (alama 2)
- Kwa nini Athumani alikataa mtu yeyote kujua kwamba anaenda kufanya mahojiano? (alama 1)
- Jadili sifa mbili za dereva (alama 2)
- Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (alama 3)
- gugumia
- ng'oa nanga
- himili
- Ufupisho (Alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ufupishe habari kulingana na maswali uliyopewa.
Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.
Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa kuwa waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaa ya wateule waungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri, vitumbua na kadhalika na akina yahe hawangeweza kuigharamia.
Watafiti wa masuala ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa hivi haina virutubishi vyovyote. Halikadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kuwa ni kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya asidi mwilini yenye supo inayoathiri siha.
Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Kwanza, huchangia kuoza na kuharibika kwa meno pamoja matatizo ya meno kuuma. Pili, sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugoajwa wa ghafla wa kuumwa upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Pia, sukari huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na ambao unatokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii ya kolestroli inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda moyo ukachoka na kukoma kufanya kazi.
Madhara haya ya sukari ndiyo yanayowafanya watu wengi kukiri kuwa sukari, ingawa ni tamu, ni sumo mwilini.
Wataalamu wa lishe wamependekeza ulaji wa vyakula kama nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia.
Fauka ya hayo, sukari inayotoka katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamini, madini na amino asidi. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Mathalani, asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo. Licha ya hayo, asali huuchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo husaidia watoto kukua vizuri. Huweza kuzidisha kiwango cha himoglobini, hivyo kupunguza uwezekano wa watoto kuwa na anemia (upungufu wa damu). Halikadhalika, asali husaidia katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.
Asali pia inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumiwa kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing'are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikakatika. Halikadhalika, asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
Maswali- Eleza madhara ya sukari (maneno 120) (alama 9)
- Eleza manufaa ya asali ya sukari kwa maneno 70 ) (alama 6)
- Matumizi ya lugha (Alama 40)
Jibu maswali yote yafuatayo.- Andika sauti moja sighuna ambayo ni kikwamizo cha ufizi (alama 1)
- Andika neno lenye muundo wa silabi ya irabu tatu pekee. (alama 1)
- Jadili sifa mbili za kimadende zinazohusisha ulimi (alama 2)
- Eleza maana ya sauti mwambatano kisha utoe mfano itamkiwayo ufizini(alama2)
- Andika sauti zenye sifa zifuatazo ( alama 2)
- Nazali ya kankaa laini
- Kikwamizo ghuna cha mdomo na meno
- Irabu ya nyuma wastani
- Kiyeyusho cha kaakaa gumu
- Akifisha sentensi hii ili kuleta maana mbili tofauti kwa kurejelea kiimbo..
Jirani yangu amewasili (alama2) - Huku ukitoa mfano, fafanua dhana nne za mzizi wa neno (alama 4)
- Andika neno moja lenye mofimu zifuatazo:
Nafsi ya kwanza wingi, wakati uliopita, yambwa wingi, mzizi wa kitenzi imba, kauli tendesha, kauli tenda (alama 1) - Onyesha matumizi ya kiambishi na kama kiambatanishi (alama 1)
- Eleza matumizi ya kiambishi 'ki katika sentensi hii. (alama 1)
Njia hii haipitiki - Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata hivyo baadhi majina haya huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi. Orodhesha majina matano kama hayo, kisha uonyeshe viambishi hivyo tofauti vya ngeli katika umoja na wingi) (alama2)
- Kanusha sentensi hii. (alama 1)
Kila achezapo Kaissa, huumiza mkono wake - Andika sentensi ifuatayo upya ukizingatia kinyume cha maneno yaliyopigiwa mistari
Ubora wa kazi zao ulifichika baada ya kuanzishwa kwa mradi ule. (alama2) - Andika kwa ukubwa
Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka (alama 1) - Tumia nomino, ya jamii kuwakilisha maneno yaliyopigiwa mstari (alama 1)
Nzige wengi sana walivamia na kuharibu mimea. - Yaandike maneno yafuatayo katika ufupi wake (alama 2)
- Shangazi zako
- Mama zako
- Tunga sentensi kubainisha matumizi ya (alama 2)
- -enye
- enyewe
- Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: (alama 2)
KN (N) + KT (T+E) +U+KN (N) + KT(T+E) - Tunga sentensi moja yenye nomino dhahani na nomino ya jamii (alama2)
- Tumia viwakilishi badala ya nomino zilizopigiwa mistari (alama 1)
Mtalii atazunu mbuga - Andika sentensi ifuatayo katika umoja.(alama 2)
Hao wenyewe hawakuzingatia mafunzo ya lishe bora. - Andika kwa ukubwa wingi (alama 1)
Nyoka hatari wamepanda mtini. - Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi (alama 2)
- Kula uyundo
- Kula uhondo
- Akifisha:
Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza sijaona (ala. 2)
- Isimu jamii (alama 10)
- Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo yanavyodhibiti mitindo ya lugha.
- Mazingira (alama 4)
- Madhumuni (alama 2)
- Malezi (alama 4)
- Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo yanavyodhibiti mitindo ya lugha.
Download Kiswahili Paper 2 - Alliance High School Pre-Trial Examination 2018.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students