Click the link below to download as a full set with all the subjects. (PDF)
https://downloads.easyelimu.com/details/35-Alliance_High_School_Pre_Trial_Examination
SHULE YA UPILI YA ALLIANCE
MTIHANI WA MWIGA-MWIGO, 2018
KISWAHILI
KARATASI YA 3, FASIHI, MUHULA WA PILI
MUDA: 21/2
MAAGIZO
- Jibu maswali manne pekee.
- Swali la kwanza ni la lazima
- Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki
- Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
SEHEMU YA A
- "Mjukuu wangu, masomo ni jambo muhimu sana. Ufikapo shuleni na kuanza maisha ya shule ya upili, usijingize katika mambo ya dunia anasa na raha nyingi. Vifanye vitabu rafiki wa karibu. Wasikiza Walimu na uzingatie wanayoyasema, saidiana na wenzako na utie bidii za mchwa katika masomo. Kumbuka kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha mema hapo usoni."
- Tambua kipera cha Fasihi Simulizi kinachohusishwa na kifungu hiki. (ala. 2)
- Jadili sifa nane za kipera hiki (ala. 8)
- Jadili vipengele vinane vya kuzingatia katika uchanganuzi wa hadithi (ala. 8)
- Jadili sifa mbili za vitanza ndimi (ala.2)
SEHEMU YA B: KIDAGAA KIMEMWOZEA
- "...usiniweke pembeni kama tanbihi..."
- Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Fafanua mbinu mbili za uandishi zilizotumika hapa (alama 2)
- Hakiki usawiri wa wahusika wa kike katika riwaya hii (alama 14)
au
- Wananchi wa Tomoko wamesalia katika ndoto ya uhuru. Dhibitisha ukweli wa kauli hii kwa mifano kumi. (alama 20)
SEHEMU YA C KIGOGO
- "Si dawa ya deni ni kulipa"
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Onesha umuhimu wa msemaji katika kujenga tamthilia ya Kigogo (alama 6)
- Fafanua vile kauli hii inafiki matukio katika tamthilia ya kigogo. (alama 10)
AU
- Jadili mbinu ambazo Majoka anatumia kujidumisha mamlakani (alama 20)
SEHEMU YA D: TUMBO LISILOSHIBA
Hadithi fupi: Tumbo lisiloshiba na Hadithi Nyingine
- "Mtihani wa Maisha"" (Eunice Kimaliro)
"...Ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa."- Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
- Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili (Alama 6)
- Onesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili. (Alama 10)
- Nizikeni papa hapa -Ken Walibora
"Kauli yake ni kama maji ya moto yasiyoweza kuchoma nyumba."- Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
- Taja na ueleze umuhimu wa tamathali moja ya usemi iliyotumika katika dondoo.(Alama 3)
- Fafanua sifa za wanaorejelewa katika dondoo hili. (Alama 7)
- Jadili dhima ya anayedokezwa katika dondoo. (Alama 6)
SEHEMU YA E: Ushairi
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Watafuta Riziki- Watafuta riziki, watokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula wahakiki, visipungue vinyuani. - Watafuta riziki, wahangaikao mijini
Kutwa kile na hiki, kama watanga na mipini
Japo hawasikiki, hawakosi kujiamini. - Watafuta riziki, wazalendo wa nchi hii
Kamwe hawajadhiki, tamaa za moyo kutii
Bali huafiki, kupingana na ulaghai. - Watafuta riziki, pato ambalo la halali
Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali
Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali
- Fafanua sifa tano za watu wanaozungumziwa katika shairi hili. (ala 5)
- Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili (ala 6)
- Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi (alama 6)
- Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifutavyo: (alama 3)
- Idadi ya mishororo katika beti
- Mpangilio wa vina
- Mpangilio wa maneno
- Watafuta riziki, watokwa jasho vijijini
Download Kiswahili Paper 3 - Alliance High School Pre-Trial Examination 2018.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students