Kiswahili Paper 1 Questions and Answers- Mokasa 1 Joint Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp
MAAGIZO:
  • Andika insha mbili.  Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
  • Insha zote sharti ziandikwe katika nafasi ulizoachiwa kwenye kijitabu hiki.

 

  1. LAZIMA
    Wewe ni Mkuu wa Utumishi wa Umma na katibu wa Baraza la Mawaziri katika Gatuzi la Matopeni. Utendakazi na mienendo ya baadhi ya mawaziri hauridhishi.  Waandikie Arifa/Memo ukiwaonya dhidi ya jambo hili.
  2. Wewe ni msomaji wa  Gazeti la Tujuzane. Andika barua kwa mhariri ukitoa maoni yako kuhusu namna mabadiliko ya hali ya anga yanavyoathiri maisha ya wananchi.
  3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
    'subira huvuta heri. '
  4. Andika insha itakayomalizika kwa :
    ……….. aliangalia nyuma alikotoka lakini hakuona chochote, macho yaliingia kiwi. Ukweli ulikuwa umejiandika kila mahali alikoangaza. 

MARKING SCHEME

  1. Wewe ni Mkuu wa Utumishi wa Umma na katibu wa Baraza la Mawaziri katika Gatuzi la Matopeni. Utendakazi na mienendo ya baadhi ya mawaziri hairidhishi.  Waandikie Arifa ukiwaonya dhidi ya jambo hili.
    Arifa pia huitwa memo. Huu ni utungo wa kiuamilifu; vipengele viwili vikuu vya utungo wa aina hii vishughulikiwe
    1. Sura
    2. Maudhui

      Sura Arifa
      Mtahiniwa azingatie muundo wa juu(sura) ya memo
      Vipengele vifuatavyo  vya kimsingi  vizingatiwe
      1. Nembo na anwani ya Gatuzi la Matopeni iandikwe juu katikati mwa ukurasa wala si pambizoni kama ilivyo katika barua rasmi
      2. Nambari ya marejeleo.
        KUMB. /REJ. GM/ARIFA/BARAZA/23
      3. Tarehe inaweza kuandikwa pambizoni kwenye mstari na nambari ya kumbukumbu. Kielelezo
        Jina hili liandikwe katikati mwa ukurasa k.m.
        F4SwaDMokMP12023Q1
      4. Mtajo. Mfano
        KUTOKA:  MKUU WA BARAZA LA MAWAZIRI
        KWA:         MAWAZIRI
        MADA:       MIENENDO NA UTENDAKAZI DUNI
      5. Utangulizi
        Mtahiniwa atangulize kwa kiini cha arifa. Mtindo ufuatao unaweza kufuatwa.
      6. Mwili- hapa ndipo hoja zitakapojadiliwa. Hoja zote zipangwe ki-aya
      7. Hitimisho (kimuundo)
        Mtahiniwa ahitimishe utungo wake
        Hapa anaweza kujumuisha hatua ambazo zitachukuliwa dhidi ya mawaziri ambao wanadhihirisha mienendo na utendakazi duni
      8. Kimalizio- Muundo wa mwisho wa arifa udhihirike kama ifuatavyo.
        1. Sahihi
        2. Jina 
        3. Cheo  (si lazima)
          Insha ikikosa maudhui lakini iwe na sura ikadiriwe katika kiwango cha D+ 04/20
          Kwa vile ni onyo, mtahiniwa anahitajika kutumia lugha yenye toni kali
          Kaida nyingine zote za usahihishaji wa karatasi hii zizingatiwe

GATUZI LA MATOPENI

MEMO

REJ.          GM/MEMO/BARAZA/03/23
KUTOKA:  MKUU WA UTUMISHI WA UMMA
KWA:         MAWAZIRI
MADA :      UTEPETEVU KAZINI
TAREHE:   14/03/2023

MAUDHUI/HOJA MUHIMU
Hoja zifuatazo ziJadiliwe.

  1. Kuchelewa kazini.
  2. Kuondoka mapema kazini.
  3. Kuzembea kazini.
  4. Matumizi mabaya ya rasilimali za wizara
  5. Mahusiano yasiyoruhusiwa
  6. Kutozingatia mitindo ifaayo ya mavazi
  7. Kudai malipo kwa kutumia stakabadhi ghushi.
  8. Kutoa siri za serikali
  9. Kueneza fitina na chuki baina ya wafanyakazi au mawaziri
  10. Mapendeleo kazini – kuhusiana na utoaji wa nafasi za kujiendeleza kimasomo,vyeo nk
  11. Utoaji na upokeaji wa rushwa.
  12. Kutoheshimu/kutozingatia haki za wafanyakazi wenye mahitaji maalum.
  13. Kutumia muda wa shughuli za wizara kampuni kujiendeleza masomoni bila kufidia.
  14. Kukosa kuratibu mikakati ya jinsi ya kuimarisha wizara
  15. Matumizi ya vileo kazini
  16. Kukosa kuafikia na kutimiza makataa yaliyowekwa
  17. Kutoa zabuni kwa njia ya mapendeleo
  18. Kukosa kuwajibikia makosa pale yanapotokea.
  19. Kuendeleza dhuluma za kimapenzi.
  20. Kutumia mali na rasilimali za kampuni bila idhini

Hitimisho

  • Hitimisho linaweza kujumuisha hatua za kinidhamu kulingana na sheria za Baraza la Mawaziri
  • Kutoa onyo.
  • Kusimamishwa kazi kwa muda.
  • Kutoa himizo kwa mawaziri kuzingatia maadili ya kikazi

Tanbihi

  • Kwa vile ni onyo tumia lugha yenye toni kali au inayohimiza nidhamu kazini.
  • Mtahiniwa anaweza kufafanua kosa na papo hapo akataja hatua za kinidhamu kwa kosa husika.

Wenu mwaminifu,

F4SwaDMokMP12023Q2

Karamu Kambe
MKUU WA UTUMISHI WA UMMA

TANBIHI: Hoja kamili itiliwe mkwaju, hoja kamili ni ile ambayo itatambulisha tatizo na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mhusika

  1. Wewe  ni mhariri mkuu wa Gazeti la Tujuzane. Andika tahariri kuhusu namna mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri maisha ya wananchi.

    MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
    Tahariri ni maelezo ya mhariri wa gazeti kuhusu mawazo, maoni na msimamo wa chombo cha habari anachowakilisha. Tahariri huhusu suala maalumu na muhimu.
    Sura ya tahariri iwe na:
    Kichwa cha gazeti: GAZETI LA TUJUZANE
    Tarehe chini ya kichwa
    Mada, kwa mfano, ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI
    Utangulizi utakaotoa maelezo mafupi kuhusu suala linaloangaziwa
    Mwili – sehemu inayojibu swali. Hoja zijitokeze hapa. Kila hoja iandikwe kwenye aya yake.
    Maoni au msimamo wa mhariri waweza kuwepo.
    Aya tamati yaweza kutoa ushauri kwa jumla au muhtasari wa suala linaloangaziwa.
    Hitimisho: Jina la mhariri na wadhifa wake.
    Baadhi ya hoja
    • Kufurika kwa mito na maziwa na hivyo kusabibisha maangamizi makubwa na uharibifu wa mali.
    • Misimu kubadilika kiasi cha kutotabirika.
    • Magonjwa ya aina mbalimbali kuwa kero kwa wananchi, magonjwa kama saratani.
    • Kiangazi kinachodumu kwa muda mrefu katika maeneo mengine, tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
    • Hali ya joto kuongezeka na hivyo kusababisha vianzo vingi vya mito na maziwa kukauka.
    • Kilimo kuathirika kutokana na kuzuka kwa magonjwa mapya ya mimea yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
    • Vivutia utalii kuathirika kwa kiwango kikubwa; sehemu za fuo za bahari kulika kwa kuongezeka kwa kiwango cha maji baharini.
    • Ufugaji wa samaki maziwani kuathirika kwa sababu ya  hali ya joto kuwa ya juu sana kwenye maziwa na hivyo kuangamiza samaki wanaofugwa. Kiwango cha hewa ya oksijeni hupungua kwa kiwango kikubwa.
    • Miundo msingi kuathirika na mabadilko ya hali ya hewa kwa sababu ya maporomoko ya ardhi, maji kuenea sehemu ambazo awali zilikuwa miundo msingi muhmu ya jamii kama vile barabara, viwanja vya michezo nk.
    • Ukosefu wa chakula cha watu na cha wanyama kwa sababu ya mimea ya chakula.
  2. Methali: Subira huvuta heri'.
    • mtahiniwa aonyeshe pande zote mbili za methali; mhusika akiwa na subira /uvumilivu na jinsi hatimaye anavyopata heri/nafuu/fanaka.
    • Akionyesha upande mmoja atakuwa amepotoka kwa hivyo atapata bakshishi.
    • Kisa kiwe cha kiwango cha juu cha ubunifu.
    • Kisa kinaweza kuwa kwa nafsi ya kwanza au tatu (mtahiniwa mwenyewe awe mhusika awe asimulie kisa cha mtu mwingine).
    • Mtahiniwa asilalie upande mmoja wa methali;pande zote mbili zijitokeze wazi.
  3. MWONGOZO                                                                                                                         
    Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa ahitimishe kwa maneno aliyopewa.                                         
    Kisa kirejelee mtu ambaye hakutumia fursa zake vizuri aushini mwake na sasa anajutia kwa kuwa nafasi hizo pengine hazipo tena au yeye amepitwa na wakati. Kuangalia nyuma alikotoka > ni hali ya kukumbuka maisha yake ya awali. Kutoona chochote > ni hali ya kutokuwa na ufanisi wowote. Macho kuingia kiwi > kujutia / kutokuwa na mbele wala nyuma / kushindwa pa kuanzia

    Hali zifuatazo zinaweza kujitokeza:                                                                                                                         
    1. Mhusika alikuwa na kazi nzuri / mshahara mkubwa lakini alikosa kuwekeza au kujiendeleza. Anatanabahi wakati kazi inakwisha kuwa hakuwa na chochote.                                                                           
    2. Mhusika alikuwa na nafasi nzuri ya kusoma. Mazingira na mandhari mazuri ya kujiendeleza kimasomo lakini akazembea na kujihusisha na mambo yasohusu masomo. Anatanabahi muda umekwisha na hajajiandaa vilivyo kwa mitihani.
      Yafuatayo yazingatiwe:                                                                                                                                                                               
      1. Mhusika ni mmoja katika nafsi ya tatu                                                                                             
      2. Kisa kisimuliwe katika wakati uliopita                                                                                                                                             
      3. Hisia mseto zidhihirike waziwazi 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers- Mokasa 1 Joint Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?