Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2023

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU (Alama 15)
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
    Katika karne hii, juhudi zetu za kushughulikia changamoto za usalama zimeimarishwa zaidi kwa matumizi ya teknolojia. Kuimarika kwa ufungaji milango, matumizi ya vifaa vya kamsa, njia za kisasa za utambuzi, utafiti na uchunguzi wa kiuhalifu ni baadhi tu ya maendeleo yaliyoafikiwa na jamii ili kujihami. Sasa hivi huduma zinazotolewa na polisi kwa umma zimewafikia watu kwa njia rahisi. Hata hivyo, maendeleo haya ya kiteknolojia yamehusishwa na hatari fulani. Baadhi ya mifumo inaweza kutumiwa vibaya au ikawa na athari zisizotarajiwa kama vile kumdhuru mtu asiyekusudiwa.

    Matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuukabili uhalifu wa jinai si suala geni. Tangu kuvumbuliwa kwa kikosi cha askari polisi katika karne ya kumi na tisa, utendakazi na maendeleo yake yamepimwa kwa kigezo cha kuimarisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika harakati za utoaji huduma kwa raia. Tumeshuhudia maafisa wetu wakitumia vifaa vya utambuzi kwa alama za vidole na  matumizi ya vifaa visivyotumia nyaya katika mawasiliano. Lakini kutokana na kuimarika kwa ubunifu wa wahalifu, pana haja ya vikosi vyetu kujipiga msasa zaidi ili kuzuia au kuzima kabisa njama za kihalifu. Matumizi ya teknolojia katika kuzuia visa vya uhalifu yameanza kukubalika na wanajamii kama sehemu ya maisha yao. Leo hii kuna vifaa vya kuchunguza iwapo mtu ana kifaa chochote cha chuma hususan silaha ndogondogo wakati aingiapo kwenye kumbi za umma au anapoabiri magari ya uchukuzi wa umma. Kifaa hiki kimezuia pakubwa uhalifu wa utekaji nyara  uliokuwepo awali hasa miongoni mwa magari ya umma mijini.Aidha vifaa vya kudhibiti kasi ya magari vimeimarisha usalama barabarani. Uwekaji wa taa za umeme kwenye viunga vya miji huuhakikishia umma usalama wao na vilevile kuchangia kuwafichua wavamizi.

    Kamera za siri kwenye ofisi za kibinafsi, majengo ya umma na kwenye baadhi ya barabara za miji mikuu huwa hifadhi ya matukio anuwai na hivyo kuwa muhimu wakati wa kesi zinazohusisha uvamizi au uhalifu mwingine wowote. Vifaa vidogo vinavyotumia mawimbi ya kielektroniki na ambavyo hutiwa mifukoni ni muhimu wakati wa mawasiliano ya dharura. Huwasaidia sana watu wenye umri mpevu ambao huwa ni windo jepesi la wahalifu. Aidha huwapa hakikisho la kuwa huru kuyaendesha maisha yao kinyume na awali ambapo maisha yao yalitawaliwa na unyanyapaa baada ya kusikia au kuhusika katika visa vya uhalifu. Kwa sasa teknolojia inayotumia miale kufichua silaha haramu zilizofichwa au kumtambua mtu anayenuia kupenyeza mihandarati kwa kumeza vidonge inagonga ndipo. Njia hii hufanya hivi bila kumkaribia mshukiwa na kuepuka hali ya kuhatarisha maisha ya afisa wa ukaguzi. Aidha huwezesha mshukiwa kutambulika mara moja na hatari husika kutandarukiwa bila ajizi. 

    Licha ya ufaafu wa teknolojia ya kisasa katika kuzuia au kuzima kabisa visa vya uhalifu, athari zake hasi zimeweza kushuhudiwa. Kwa mfano matumizi ya vifaa vya kwenda kwa kasi kuwafuata wahalifu yanaweza kuwa hatari kwa mtumiaji, mshukiwa au hata raia asiyehusika.

    Kifaa cha kuzima kasi ya magari kwa mbali kinaweza kulisimamisha gari ghafla na kusababisha maafa makubwa. Matumizi ya mwangaza mkali au gesi kama njia ya kumdhibiti mhalifu yanaweza kusababisha ulemavu wa kuona au hata kupumua. Baadhi ya vifaa ambavyo hutumia miale vinaweza kuwa na athari ya kudumu na hata kusababisha maradhi ya kansa.Inapendekezwa kuwa matumizi ya teknolojia kuangamiza uhalifu yazingatie haki za binadamu. Aidha njia husika iwe nafuu , pawe na uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake na vilevile matumizi yake yazingatie maadili.
    Maswali
    1. Kwa mujibu wa kifungu wahalifu bado wanazizidi nguvu asasi za kiusalama katika jamii. Eleza. (alama 1)
    2. Onyesha jinsi teknolojia imeimarisha usalama katika sekta ya usafiri. (alama1)
    3. Ni kwa njia gani teknolojia imesaidia kupatikana kwa haki? (alama 2)
    4. Eleza manufaa ya kutumia miale kama njia ya kuzuia uhalifu. (alama 3)
    5. Taja mambo mawili ambayo yanafaa kuiongoza jamii wakati wa kuteua mbinu ya kuukabili uhalifu. (alama 2)
    6. Teknolojia ya kisasa katika kuukabili uhalifu imeelezwa kuleta changamoto zipi?    (alama 3)
    7. Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumiwa kwenye kifungu. (alama 3)
      1. Viunga
      2. Zinazolanguliwa
      3. Unyanyapaa
  2. Muhtasari (Alama 15)
    Sikukuu ya wafanyikazi huadhimishwa na wafanyikazi kote ulimwenguni kwa minajili ya kukumbushana na kutanabahishana umuhimu wa mshikaniano na umoja katika kudai na kutetea maslahi na inaendeleo yao. Kwa jumla wafanyakazi hukongamana kwa nia ya kutafakari kuhusu bali yao ya baajaye.

    Kwa sababu ya jyrnuhjmu hin wafanyakazi hunata kila nui va sababu va kuienzi siku Kwao ni siku yao ya kufanya tathmini ya jinsi wanavyotimiza wajibu wao wa kutoa kuzalisha mali pamoja na kutambua changamoto zinazowasakama kwa lengo la kubuni kuzikabili.

    Aidha siku hii hutoa jukwaa kwa wafanyakazi na viongozi wao kuwapa tuzo wenzao waliobobea katika nyanja mbali mbali za kazi zao. Yaani, ni wakati wa mathali, meheza kwao hutuzwa au la, huangaliwa kupata muktadha wa matumizi. Hata hivyo, ukweli mmoja ni kuwa sio wote waliotamba huweza kutuzwa madhali ni muhali kumtuza kila mtu. Ama thamani na manufaa ya tuzo hupatikana katika uchache wake. Jambo muhimu na la kukumbukwa ni kwamba kila mfanyakazi ni mchapa kazi, atuzwe asituzwe!

    Jambo ambalo wafanyakazi hawapaswi kufunzwa, labda kukumbushwa tu, ni kuwa waendelee kufanya kazi kwa ari, umahiri na weledi wa bali ya juu. Mradi ni lazima watambue kuwa nafasi yao katika kuleta maendeleo ya kitaifa ni kubwa mno wala haimithilishwi na chochote.

    Ni kutokana na kuelewa umuhimu mkubwa wa wafanyakazi ambapo katiba za nchi nyingi kote duniani husabili sahifa nyingi kuangazia inasuala ya wafanyakazi. Baadhi ya masuala yanayofafanuliwa ni wajibu wa wafanyakazi na waajini pamoja na haki za kila kundi ambapo wajibu wa kundi moja ni haki za kundi lingine. Hata hivyo, haiwezekani katiba za nchi kushughuulikia masuala yote ya wafanyakazi. Kwa sababu hii, stakabadhi zingine kama sheria za nchi husika hii adhimu. huduma na mikakati yahufafanua zaidi kuhusu masuala ya waajiri na waajiriwa. Nyaraka hizi zote huandaliwa katika misingi ya maazimio ya Shirika a Wafanyakazi Duniani yaani ILO.

    Haimhitaji mweledi kutambua kwamba wajibu mkubwa wa kila mwajiri ni kuhakikisha ya kuwa maslahi ya wafanyakazi yamepewa nafasi ya kwanza katika mipango yake yote. Miongoni mwa waajiri wote, serikali ndiyo mwajiri mkubwa. Hivyo basi, serikali inastahili kuwa kwenye msitari wa mbele katika kutunza na kutekeleza maslahi ya wafanyakazi wake.

    Jambo linalotamausha ni kushuhudia na kusikia kuhusu visa vingi vya migomo ya wafanyakazi kote duniani wakilalamikia mazingira duni ya kutenda kazi, mishahara midogo, marupurupu madogo na machache, ukosefu wa muda wa mapumziko na kadhalika. Na shani kubwa ni kwamba aghalabu niwajiri anayesusiwa huwa ni serikali. Hofu kubwa hapa ni kwamba serikali zikikosa kujali maslahi ya wafanyakazi wao, waajiri wengine katika sekta ya kibinafsi kama mashirika, taasisi na watu binafsi, hawataona haja ya kufanya hivyo. Na katika hali kama hii basi msemo kwamba kazi isiyo kipimo, mwishowe watu huteta huwa kitulizo kikubwa kwa waajiriwa.

    Wanapofikia na kufikishwa katika kiwango hiki, wafanyakazi hupandwa  na jazba na kariha isiyoruhusu wala kusikiliza ama yoyote ya vitisho au ushauri ila tu utekelezaji wa matakwa yao!
    Maswali 
    1. Eleza umuhirnu wa kuadhirnishwa Sikukuu ya wafanyakazi unavyodhihirika katika aya tatu za kwanza. Maneno 45-50   (alama 5)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Kwa kurejelea aya zilizosalia, andika hoja kuu zinazozungurnziwa. (alama 9)  (Maneno 90— 100)
      Matayarisho 
      Jibu
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Sauti /ch/ ina sifa zipi?          (alama 2)
    2. Akifisha kifungu kifuatacho: baba kwa mshangao salale umechoma shati langu yaya akitetemeka samahani si kosa langu     (alama
    3. Tambua miundo yoyote minne ya nomino za ngeli ya A-WA. Toa mifano.      (alama 2)
    4. Nyambaka alimwambia Ochiel kuwa angemlipa pesa zake siku hiyo jioni. Andika katika usemi halisi.   (alama 2)                                  
    5. Vitaje na uvinyambue vitenzi vyovyote viwili vyenye asili ya kigeni katika kauli ya kutendeana.     (alama 2)                                          
    6. Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: Tulipikiwa pilau kwa chungu.         (alama 3)
    7. Tunga sentensi moja iliyo na chagizo ya namna halisi na ya namna hali.                 (alama 2)
    8. Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo: Ingawa hajalipwa mshahara, angali anaikimu familia yake.  (alama 3)                                      
    9. Kanusha sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa wingi: Hiki kijiti  kilitolewa kwenye mti ule mrefu.       (alama 3)                                   
    10. Tumia neno haraka kama nomino na kielezi katika sentensi moja.         (alama 2)
    11. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia visanduku: Rosamaria alipata kitabu chake kipya kilichopotea jana.     (alama 4)                
    12. Tambua na uainishe viwakilishi katika sentensi ifuatayo: Aliniitisha zawadi uliyokuwa umenituma nimpelekee Hadija. (alama 2)           
    13.  
      1. Kishazi ni nini?    (Alama 1)
      2. Tunga sentensi iliyo na kishazi huru na kishazi tegemezi.            (alama 2)
    14. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kiambishi ‘ku’.           (alama 2)
    15. Tambua hali na wakati gani katika sentensi ifuatayo: Zawadi atakuwa anasoma nitakapofika.           (alama 2)
    16. Tofautisha silabi funge na silabi wazi. Toa mfano mmoja mmoja kwa kila mojawapo.         (alama 3)

  4. ISIMUJAMII (alama 10)
    1. Eleza maana ya istilahi zifuatazo:
      1. Linguafranka
      2. Sajili
      3. Lahaja
      4. Uwili lugha
      5. Lugha sanifu
    2. Eleza majukumu yoyote sita ya Kiswahili nchini Kenya. (alama 6)

MWONGOZO 

  1. UFAHAMU ( ALAMA 15)
    1. Kwa mujibu wa kifungu wahalifu bado wanazizidi nguvu asasi za kiusalama katika jamii. Eleza.      (alama 1)                           
      • Wahalifu wanawazidi polisi kwa ubunifu wao na kuendelea kutekeleza uhalifu. Pana haja ya vikosi vya polisi kujiimarisha zaidi ili kuwazidi wahalifu.                        1x1= 1
    2. Onyesha jinsi teknolojia imeimarisha usalama katika sekta ya usafiri.          (alama 1)
      • Matumizi ya kifaa cha kuwakagua abiria kama wana silaha haramu na matumizi ya miale ya kielektroniki kukagua uwepo wa silaha hatari kabla ya kuabiri kifaa cha kusafiria.       2x½= 1
    3. Ni kwa njia gani teknolojia imesaidia kupatikana kwa haki?         (alama 2)
      • Kamera za siri huweka kumbukumbu za matukio mbalimbali hivyo kutumiwa mahakamani kama njia ya kuutoa ushahidi dhidi ya wahalifu. 1x1= 2
    4. Eleza manufaa ya kutumia miale kama njia ya kuzuia uhalifu. (alama 3)
      • Ni njia ambayo haikosei katika ufichuzi wa silaha au dawa haramu, Huhusisha ukaguzi mtu akiwa mbali na kumwepushia mkagiuzi uwezekano wa kuathiriwa kwa vyovyote, Matokeo yake hubainika mara moja hivyo hatua za tahadhari kuchukuliwa mapema.                                                                                                                   3x1= 3
    5. Taja mambo mawili ambayo yanafaa kuiongoza jamii wakati wa kuteua mbinu ya kuukabili uhalifu.         (alama 2)
      • Matumizi ya njia yoyote ile yazingatie haki za binadamu, yazingatie maadili ya jamii, pawepo na uwazi na uwajibikaji katika matumizi yake. Zozote                              2x1= 2
    6. Teknolojia ya kisasa katika kuukabili uhalifu imeelezwa kuleta changamoto zipi?            (alama 3)
      • Kuwaletea watu maradhi kama vile kansa, kulathiri asiyehusika na uhalifu, inaweza kuleta maafa hasa matumizi ya vifaa vya kasi vya kuuzuia uhalifu                       3x1= 3
    7. Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotumiwa kwenye kifungu.         (alama 3)
      1. Viunga - sehemu nje ya mji ambazo huwa ni makazi ya watu.
      2. Zinazolanguliwa - kuuza dawa haramu/kupenyeza na kusambaza dawa hizo haramu
      3. Unyanyapaa - woga unaoletwa na tendo au hali fulani.                                3x1=3

  2. MUHTASARI
    1.  
      1. kukumbushana na kutanabishiana umuhimu wa mshikamano/umoja katika kutetea maslhi na maendeleo ya wafanyakazi.
      2. Hukongamana ili kutafakari kuhusu hali yao ya baadaye.
      3. Kufanya tathimini ya njisi wanavyotimiza wajibu wao wa kulra huduma na kuzalihsa mali.
      4. Kutambua changamoto zinazowasakama kwa lengo la kubuni mikakati ya kuzikabili.
      5. Hutoa kikwaa kwa wafanyakazi na viongozi wao kutuza waliobobea katiak kazi zao.
    2.  
      1. Wafanyakazi waendelee kufanya kazi kwa ari, umahiri na waledi.
      2. lazima watambue kuwa wana nafasi kubwa katika kuleta maendeleo.
      3. Katiba zanchi nyingi duniani huangazia masuala ya wafanyakazi.
      4. baadhi ya maswala ni wajibu wa wafanyakazi na waajiri na haki zao.
      5. sheria za nchi husika hufafanua zaidi masaula ya waajiri na wajiriwa.
      6. Sheria /nyaraka hizi huandaliwa katika misingi ya maazimio ya shirika la wafanyakazi duniani.
      7. Wajibu  wa kila mwajiri ni kuweka maslahi ya wafanyakazi mbele
      8. Serikali inastahili  kuwa msitari wa mbele katika kutunza maslahi ya wafanyakazi wake.
      9. Kuna visa vingi vya migomo ya wafanyakazi duniani.
      10. Serikali zisipojali maslahi ya wafanyakazi wao waajiri wengine hawatafanya hivyo.
      11. Wakifikishwa kiwango hiki hukosa kusikiliza vitisho/ushauri wowote.

  3. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
    1. Sauti /ch/ ina sifa zipi?                       (alama 2)
      • Ni sauti/konsonanti hafifu.
      • Ni kipasuo kwamizo.
      • Hutamkiwa kwenye ulimi na kaakaa gumu.                                  Zozote 2×1=2
    2. Akifisha kifungu kifuatacho: baba kwa mshangao salale umechoma shati langu yaya akitetemeka samahani si kosa langu  (alama 3)
      • Baba: (Kwa mshangao) Salale! Umechoma shati langu?
      • Yaya: (Akitetemeka) Samahani. Si kosa langu.                           Vitahiniwa 6×½=3
    3. Tambua miundo yoyote minne ya nomino za ngeli ya A-WA. Toa mifano.               (alama 2)
      • Ki-Vi Kwa mfano: Kipepeo – Vipepepo. 
      • M-Mi Kwa mfano: Mtume – Mitume.
      • M/Mw- Wa Kwa mfano: Mtu – Watu.       
      • Ch –Vy Kwa mfano:Chura – Vyura.
      • Zinazochukua kiambishi ma- katika wingi: Daktari – Madaktari.
      • Zisizobadilika katika umoja na wingi: Punda – Punda.                                       Miundo 4×½=2
    4. Nyambaka alimwambia Ochiel kuwa angemlipa pesa zake siku hiyo jioni. Andika katika usemi halisi.      (alama 2)         
      • “Nitakulipa pesa zako leo jioni,” Nyambaka alimwambia Ochiel.                  Vitahiniwa 4×½=2
    5. Vitaje na uvinyambue vitenzi vyovyote viwili vyenye asili ya kigeni katika kauli ya kutendeana.                                                                                                                         (alama 2)
      • Vitenzi vyenye asili ya kigeni ni vile vinavyoishia kwa irabu –i, -e au –u.
      • Kwa mfano: Hubiri – hubiriana, Amini – aminiana, Saliti – salitiana, Samehe – sameheana, abudu – abudiana.
                                                                                                Kutaja kitenzi 2×½=1, Kunyambua vitenzi 2×½=1
    6. Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo: Tulipikiwa pilau kwa chungu.               (alama 3)
      • Tu (sisi) ni shamirisho kitondo/yambwa tendewa.
      • Pilau ni shamirisho kipozi/yambwa tendwa.
      • Chungu ni shamirisho ala/yambwa kitumizi.                                                    Vitahiniwa 3×1=3
    7. Tunga sentensi moja iliyo na chagizo ya namna halisi na ya namna hali.                 (alama 2)
      • Mwanafunzi aliyecheka sana/mno/kupindukia aliadhibwa vikali/vibaya.        Vitahiniwa 2×1=2
    8. Ainisha vitenzi katika sentensi ifuatayo: Ingawa hajalipwa mshahara, angali anaikimu familia yake.      (alama 3)                   
      • Hajalipwa ni kitenzi halisi.
      • Angali ni kitenzi kisaidizi.
      • Anaikimu ni kitenzi kikuu.
      • Angali anaikimu ni vitenzi sambamba.                                                     Vitenzi vyovyote 3×1=3
    9. Kanusha sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa wingi: Hiki kijiti  kilitolewa kwenye mti ule mrefu.                                                                                                                                  (alama 3)
      • Haya majiti/majijiti yalitolewa kwenye majiti yale marefu.                            Vitahiniwa 6×½=3
    10. Tumia neno haraka kama nomino na kielezi katika sentensi moja.         (alama 2)
      • Haraka yake ilimfanya atembee haraka kwenda kazini.
            N                                                                                                                   Vitahiniwa 2×1=2
    11. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia visanduku: Rosamaria alipata kitabu chake kipya kilichopotea jana.     (alama 4)

                                                                                  S                            
       KN                                                 KT                                     
       N  T                           KN           S
        Rosamaria   Alipata  N  V  V   kilichopotea jana.
       kitabu  chake kipya 
                                                                                                                                                Vitahiniwa 8×½=4
    12. Tambua na uainishe viwakilishi katika sentensi ifuatayo: Aliniitisha zawadi uliyokuwa umenituma nimpelekee Hadija. (alama 2)           
      • A – kiwakililishi cha nafsi ya tatu umoja, U – kiwakilishi cha nafsi ya pili umoja, U – kiwakilishi cha nafsi ya pili umoja, Ni – kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja.                                                                                                             Vitahiniwa 4×½=2
    13.  
      1. Kishazi ni nini?                                                                                                       (Alama 1)
        • Ni kipashio cha kimuundo chenye kiima na kiarifu.                                    Maana 1×1=1
      2. Tunga sentensi iliyo na kishazi huru na kishazi tegemezi.                                      (alama 2)
        • Mwalimu aliyeajiriwa mwaka jana alitoweka bila na fedha zetu. (Tathmini majibu ya wanafunzi)               Vishazi 2×1=2
    14. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili tofauti ya kiambishi ‘ku’.           (alama 2)
      • Kucheka kwake kulituudhi sana.                                                                Matumizi yoyote 2×1=2
    15. Sentensi ifuatayo iko katika hali na wakati gani?: Zawadi atakuwa anasoma nitakapofika. 
      • Wakati ujao hali ya kuendelea.   Kutaja wakati = 1, Kutaja hali = 1
    16. Tofautisha silabi funge na silabi wazi. Toa mfano mmoja mmoja kwa kila mojawapo.
      • Silabi funge ni silabi inayoishia kwa konsonati. Kwa mfano: Dak-ta-ri. Silabi wazi ni silabi inayoishia kwa irabu. Kwa mfano: Ba-ba.                       Kutofautisha silabi 2×1=2, Kutoa mifano 2×½=1
  4. ISIMUJAMII (alama 10)
    1. Eleza maana ya istilahi zifuatazo:
      1. Linguafranka                                                                                                                 (alama 1)
        • Ni lugha inayotumiwa baina ya watu ambao wanazungumza lugha tofauti kabisa za kwanza.
      2. Sajili                                                                                                                              (alama 1)
        • Ni mtindo wa lugha ambao hutumika katika muktadha mahsusi.
      3. Lahaja                                                                                                                          (alama 1)
        • Ni namna tofauti tofauti ya kuzungumza lugha moja kutegemea eneo au tabaka fulani.
      4.  Uwili lugha                                                                                                                   (alama 1)
        • Ni hali ambapo mzungumzaji mmoja anaweza kutumia lugha mbili.
      5. Lugha sanifu                                                                                                                  (alama 1)
        • Ni lugha au lahaja iliyochaguliwa na kufanyiwa marekebisho ya kimatamshi, kisarufi, kimaana na kimaandishi ili iweze kutumika katika shughuli rasmi.
    2. Eleza majukumu yoyote sita ya Kiswahili nchini Kenya.                                            (alama 5)
      • Ni chombo cha mawasiliano, maingiliano na maelewano baina ya Wakenya.
      • Ni nyenzo ya kuwaunganisha Wakenya wote wenye asili mbalimbali na kuwafanya kuwa kitu kimoja.
      • Ni chombo cha kushirikisha umma katika shughuli zote za taifa.
      • Ni kitambulisho cha Wakenya wote.
      • Hutumiwa na serikali ya Kenya kupitisha sera zake kwa wananchi.
                                                                                                                    Hoja zozote 5×1=5
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Form 3 Term 3 Opener Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest