MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
MASWALI
- Wewe ni Gavana wa kaunti ya Zaoni. Andika hotuba utakayotoa katika sherehe ya siku ya ufanisi ukieleza hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zimepigwa katika gatuzi lako.
- Wanawake ni nguzo muhimu katika ustawi wa taifa. Jadili.
- Ivushayo ni mbovu. Dhihirisha ukweli wa methali hii.
- Hitimisha insha yako kwa maneno yafuatayo.
………. Nilipoamka kutoka usingizini, nilitamani ndoto hiyo yangu ingekuwa ukweli.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
-
- Miradi
- Hospitali au zahanati
- Shule au miundo msingi
- Elimu – msaada wa karo, vitabu, vifaa nk.
- Nguvu za umeme.
- Mabwawa ya maji ya kunywa na utumizi viwandani.
- Barabara na madaraja .
- Kilimo – miche, mbegu, mbolea nk.
- Vituo vya polisi – usalama
- Burudani k.v. kumbi mbalimbali, viwanja vya michezo
- Mazingira – kupanda miti, kuondoa/ kuzoa takataka, kuondoa maji taka n.k.
- Tanbihi
- Muundo wa hotuba sharti uzingatiwe.
- Miradi
- Maendeleo yanayoweza kufanikishwa na wanawake nchini yagusie yale.
- Ya kijamii
- Ya kiuchumi
- Ya kisiasa
- Mtahiniwa azingatie utaratibu ufuatao:
- Kichwa
- Maana na matumizi ya methali k.v ivushayo ni daraja au chombo chochote kama mashua kinachomwezesha mtu kutoka ng’ambo moja hadi ya pili. Aghalabu baada ya mtu kuvushwa huishia kubeza au kudharau kilichomvusha. Methali hii hurejelea mtu anayemdharau mtu Fulani aliyewahi kumfaa maishani na kumwona bure maana sasa hamhitaji.
- Kisa kidhihirishe ukweli wa methali.
- Pande zote za methali zizingatiwe kwa kiwango sawia kila upande.
- Hitimisho iwe nzuri.
- Urefu unaofaa utiliwe maanani.
- Mkaguzi atathmini kazi ya mtahiniwa akizingatia mdokezo uliotolewa kwenye swali.
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Form 4 Term 2 Opener Exams 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students