Tumbo Lisiloshiba Dondoo Questions and Answers
Maswali haya hujitokeza kwa namna ya maneno yaliyodondolewa kutoka kwenye kazi ya Fasihi. Dondoo hunukuliwa kisha maswali yanayohusiana na dondoo hilo huulizwa. Dondoo laweza kuwa maneno ya mhusika mmoja ambaye hatatajwa au maelezo katika kazi. Maswali huenda yakarejelea matukio yaliyotokea kabla au baada ya dondoo. Katika kulijibu swali la muktadha wa dondoo, mtahiniwa huhitajika kuangazia mambo yafuatayo;
- Kumtaja msemaji wa maneno haya
- Kumtaja msemewa(anayerejelewa)
- Kueleza mahali yalikofanyika mazungumzo haya.
- Kueleza kiinisababu ya mazungumzo haya kutokea.
Swali la dondoo 1
“… Ningeondoka…..mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana”
- Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
- Onyesha vile Kinaya kinavyojitokeza katika dondoo hili (Alama 2)
- Kinaya kimetumika kwingine katika hadithi husika. Thibitisha kwa kutumia hoja tisa. (Alama 9)
- Eleza umuhimu wa msemaji katika hadithi hii. (alama.5)
Majibu ya dondoo 1
-
- Haya ni maneno ya Jairo.
- Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu.
- Sherehe hii ilifanyika shuleni.
- Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kumpatia atumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii
- Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa atumaini maishani badala ya kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana ni lazima aibe na aue.
-
- Ni kinaya kwa Jairo kudai ili mtu awe wa maana, athaminiwe na kuitwa mheshimiwa na kuwa bingwa lazima aibe, apore au aue.
- Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
- Ni kinaya pia kwa mwalimu Mosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosa badala ya kumsifu.
- Ni kinaya kwa Jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili mkewe kama zawadi.
- Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa pombe ni kiiwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masibu ya maisha ya kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
- Ni kinaya kwa mkewe Jairo kukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
- Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa afuska ndio raha ya maisha na kuwa uaadilifu haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
- Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi,Sera kukubali na kumkaribisha mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake. (Hoja Zozote 9 Alama 9)
-
- Ni kielelezo cha utovu wa nidhamu miongoni wa wanafunzi. Anakunywa pombe na hata kujihusisha katika ufuska
- Kupitia kwake uwajibikaji wa mwalimu Mosi unajitokeza. Kama mwalimu alimkanya kunywa pombe na hata ufuska
- Ametumiwa kudhihirisha ukweli wa methali “asante ya punda ni mateke.”
Swali la dondoo 2
Shibe inatumaliza : Salma Omar Hamad
“Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
- Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)
Majibu ya dondoo 2
-
- Maneno haya yanasemwa na Mbura
- alikuwa anazungumza na Sasa
- walikuwa kwenye sherehe iliyoandaliwa na mzee Mambo
- walikuwa wanazungumza kuhusu ‘kula kwao’ 4 x 1 = 4
- Sifa za Mbura
- ni mzalendo - anafanya kazi kwa bidii katika wizara yake kama njia ya kuonyesha uzalendo
- mwenye tamaa - anajaza sahani kwa chakula na kukila chote
- mwenye utu - anataka wananchi wale kwa niaba ya viongozi kama vile wao wamekuwa wakila kwa niaba yao
- ni fisadi - amepokea kazi kwa afisi ya serikali kwa njia isiyo halali
- mzembe - baada ya kula sahani tatu za vyakula kwenye sherehe analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini
- mtetezi wa haki
- mvumilivu
- mpyoro
- msema kweli zozote 6 x 1 = 6
-
- hulipwa mishahara mikubwa sana na serikali jambo linalochangia ubadhirifu wa mali ya umma
- sherehe kubwa za viongozi wa kiserikali huchangia pakubwa ubadhirifu
- viongozi hutumia raslimali za nchi kwa manufaa yao ya kibinafsi
- magari ya serikali
- raslimali zilizotumiwa katika kuvinunua vyakula na vinywaji vingetumika katika kuendeleza asasi tofauti za kijamii
- DJ na wenzake wanapata mabilioni ya fedha kutokana na kuwatumbuiza wageni katikasherehe kama hizi
- viongozi wanawachukua baadhi ya watu wao wa karibu na kufanya juu chini kuona kwamba wanajifaidi na mali na raslimali za wananchi pasipo kuzitolea jasho kamwe
- upeperushaji wa matangazo katika vyombo vya habari ya sherehe za kiongozi binafsi ni njia ya kuendeleza ubadhirifu wa raslimali za umma
- Mbura na Sasa wanaendeleza ubadhirifu pale wanapoamua kuchukua vyakula kupita kiasi katika sherehe za mzee Mambo
- kuwaajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika sekta tofauti za umma
- vibaraka na vikaragosi kupewa mali ambayo ingewafaidi wananchi zozote 10 x 1 = 10
Swali la dondoo 3
Ndoto ya mashaka
“Sasa nimechoka mja. Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Taja mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (alama 4)
- Mzungumzaji alikuwa na haki ya kuradua kufa. Thibitisha. (alama 12)
Majibu ya dondoo 3
-
- Haya ni mawazo ya Mashaka.
- Yuko chumbani mwake.
- Anakumbuka hali yake ngumu ya maisha na mashaka tele.
- Anamkumbuke mkewe, Waridi, alivyomtoroka na wanawe.
- Anayaona maisha kutokuwa na thamani tena kiasi kwamba anaona kifo kingemfaa. (4×1= 4)
-
- Takriri- nimechoka
- Uzungumzi nafsi- sasa nimechoka… (2×2= 4)
- Mashaka alikuwa na haki ya kuradua kufa kwani alikuwa amepitia matizo mengi:
- Mamake mzazi, Ma Mtumwa, aliiaga dunia punde tu baada ya kumkopoa.
- Baada ya kifo cha mamake, babake alishindwa kuvumilia naye akaaga dunia.
- Mashaka alilelewa na Biti Kidebe asiyekuwa mamake mzazi.
- Mamake mlezi, Biti Kidebe naye alihitaji kulelewa. Daima alilalamikia miguu yake.
- Mashaka alilazimika kufanya vijikazi ili kumsaidia mamake mlezi kupata chohcote cha kutumia.
- Mashaka na Biti Kidebe walipanda mabokoboko ambayo wengi waliamini si ndizi.
- Biti Kideba alienda jongomeo pindi tu Mashaka alipomaliza chumba cha nane.
- Mzee Rubeya na Shehe Mwinyimvua wanawafungisha Mashaka na Waridi Ndoa ya Mkeka bila kupenda kwao.
- Mzee Rubeya wanawakimbia Mashaka na Waridi na kurudi kwao Yemeni ili Mashaka wasije kuwaaibisha.
- Kazi ya Mashaka ilikuwa ya kijungu meko- ya kupigania tumbo.
- Mashaka na Waridi waliishi sehemu kuchafu kule Tandale, Kwatumbo, eneo la Uswahilini.
- Walikosa vyoo wakawa wanatumia karatasi kwa haja zao zote.
- Mashaka na Waridi walipata watoto wengi, saba, ambao wanawashinda kuwakimu.
- Mashaka alilazimika kuomba jikoni kwa jirana yake, Chakupewa, ili wanawe wa kiume wapate mahali pa kulala.
- Chumba chao kiliingiza maji mvua iliponyesha.
- Mashaka alifanya kazi ya usiku katika Shirika la Zuia Wizi Security (ZWS).
- Waridi anamtoroka Mashaka maisha yanapokuwa magumu. (12×1= 12)
Kila hoja ifafanuliwe kikamilifu
Swali la dondoo 4
Mame Bakari
“Una nini? Umeshtuka mwanangu! Unaogopa? Uaogopa nini?
- Weka dondoo hili katika muktadha wake. al 4
- Eleza sifa za mrejelewa. al 6
- Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo. al 2
- Eleza umuhimu wa msemaji. al 4
- Tambua maudhui yanayojitokeza katika kifungu hiki. al 1
- Fafanua maudhui katika swali la (e) kwa kurejelea hadithi nzima. al 3
Majibu ya dondoo 4
-
- Msemaji ni babake Sara.
- Akimwambia Sara.
- Wakiwa hospitalini kwenye chumba cha daktari.
- Sara alikuwa ameenda kufanyiwa vipimo vya ujauzito na Beluwa alipowakuta wazaziwe wakisubiri katika chumba hicho
- sifa za mrejelewa.(Sara)
- mpenda masomo
- ni mwoga
- mwenye busara
- mwenye mapenzi ya dhati
- mwenye utu hakutaka kuavya mimba
- ni msiri
- mwenye maadili
- mwenye majuto
- ni mvumilivu.
(kila sifa itolewe maelezo. Mwanafunzi akitaja sifa tu asituzwe)
Hoja Zozote 6 (6x 1 = 6)
-
- Swali la balagha; una nini?
- Takriri; unaogopa, unaogopa
- umuhimu wa msemaji (babake Sara)
- Kupitia kwake tunapata habari ya ukali kupita kiasi kwa wazazi kwa wanao.
- Ni kielelezo cha wazazi ambao hawako tayari kubadili msimamo wao mkali kwa watoto wao.
- Anaonyesha umuhimu wa wazazi kushirikiana katika malezi.
- Anaonyesha umuhimu wa kuweka siri katika masuala tata ya familia.
- Ni kielelezo cha wazazi wanaouenzi utamaduni wa jamii yao.
-
- Malezi
- mapenzi
-
- Malezi- Babake Sara anakuwa mkali kwa sara. Babake Sara anadalika na kumwonyesha mapenzi.
- Mapenzi - Kuna mapenzi ya dhati kati ya sarana salime. Salime anamsaidia sara anapokuwa mjamzito. Salime aidha anamsaidia sara kuweka siri ya ujauzito.
Swali la dondoo 5
“Tulipokutana Tena” (Alifa Chokocho)
Halikuwa jambo la kawaida maana maji yalikuwa hayapatikani karibu pale kijijini petu. Sharti mtu aende masafa marefu kuyatafuta. Na sabuni? Sabuni ilikuwa kitu cha anasa kwa familia yetu. Wazazi wangu hakuwa na uwezo wa kununua Sabuni. Labda mara moja moja siku za sikukuu.
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza majukumu mawili ya takriri katika dondoo hili. (alama2)
- Kwa kurejelea hadithi Tulipokutana Tena jadili jinsi haki za watoto zinavyokiukwa.(alama 6)
- Jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa ukirejelea hadithi zifuatazo: (alama 10)
- Masharti ya Kisasa
- Ndoto ya Mashaka
Majibu ya dondoo 5
-
- Maneno haya ni ya Bogoa.
- Anawambia msimulizi na Kazu.
- Wako katika club Pogopogo.
- Bogoa na msimulizi wanakutana baabaya miaka 41 baada ya kutoroka kwasababu ya kuwa mtumwa wa nyumbani kwa Bi. Sinai.
-
- Imetumika kuchimuza hali ya umasikini kwani hata sabuni hawangeweza kununua.
- Imetumika kuendeleza maudhui ya umasikini
- Imetumika kusisitiza wazo. Mfano kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni isipokuwa siku ya sikukuu.
- Imetumika kuendeleza tamathali nyingine za semi mfano chuku. Kuthamini sabuni sana na hata kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni.
-
- Kutengwa na familia- Bogoa alikuwa na umri mdogo wa miaka mitano na hakuta kakutengwa na baba,mama, ndugu, kaka na dada zake. Uk 114
- Kuamrishwa kufanya vitu bila hiari ya Bogo uk. 115
- Bogoa alitwishwa mambo yote ya nyumbani alikuwa mtoto mdogo. Uk 115
- Watoto masikini hawapaswi kusoma shuleni. Uk 116
- Bogoa hakuwa na uhuru wakucheza na watoto wa Bi. Sinai.
- Kutishiwa maisha- Bi. Sinai alimtisha Bogua kuwa angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yake ya ndani.
- Kuadhibiwa kwa kuchomwa- Bi. Sinai alimchoma viganja Bogoa kwa kosa la kuchoma maandazi.
- Kutoambiwa ukweli- Bogoa anawalaumu wazazi wake kwa kumdanganya Alama 6×1=6
Masharti ya Kisasa
- Masharti katika ndoa
- Ukosefu wa uaminifu
- uhuru
- Taasubi ya kiume/ utamaduni
- Wivu
- Utabaka
- Ukengeushi
Ndoto ya Mashaka
- Ndoa ya lazima
- Utabaka
- Umaskini
- Upangaji wa uzazi
- Usaliti
Swali la dondoo 6
`..........Lakini shogake................. shogake.................. shogake dada nikamwona ana ndevu’.
- Eleza muktadha wa dondoo hili. alama 4
- Bainisha sifa tatu za `shoga ‘ anayezungumziwa katika dondoo hili. alama 6
- Jadili umuhimu wa `dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi. alama 10
Majibu ya dondoo 6
-
- Haya ni maneno ya lulua
- Anamwambia mamake Bi. Hamida
- Wamo nyumbani mwao wakila chomcha.
- Lulua anamweleza jinsi alivyoingia katika chumba cha safia na kumkuta akiwa amelala kitandani na kimwana. (4x1=4)
-
- Msiri- Wazazi wake safia hawakuwahi kuiona sura yake kwa sababu alipenda kuvaa buibui ili asijulikane kuwa ni mwanamume.
- Mzinifu- Anazini na safia na kumpachika mimba
- Mjanja – Anajifunika buibui na kujifanya jinsi ya kike
- Dada anayerejerewa ni safia
- Ni kiwakilishi cha uoza katika jamii. Anawahada wazazi wake kuwa kimwona ni shogake kumbe ni mpenziwe na kiume.
- Ametumiwa kukosoa malezi ya wazazi. Wazazi wake Bwana Masudi na Bi Hamida walimwamini sana hadi wakawa wanamsifu tu badala ya kungumza naye ili kumpa mwelekeo ufaao maishaini.
- Kuendeleza maudhui ya elimu. Alikuwa mwerevu shuleni. Kila mtihani aliofanya aliongoza katika darasa lao.
- Ni kielelezo cha wanawake wanaoavya mimba kuuficha uovu huo. Safai anajaribu kuavya mimba ili wazazi wake wasijue lakini anakufa.
- Suala la unafiki linajitokeza kupitia kwake. Alijifanya mzuri kwa zazazi wake hhadi wakamwamini kwa kila jambo kumbe alikuwa mwovu- anawahadaa wazaziwe kuwa kimwana ni shogaye ilhali ni mpenziwe wa kiume.
- Ni kielezo cha athari za mapenzi kabla ya ndoa. Anafanya mapenzi na kimwana.Anapachikwa mimba na kwa sababu ya kuhofia matokeo yake anaamua kuiavya ile iwe siri lakini anakufa. ( 2x5=10) Taja = 1, Kueleza = 1, Jumla = 2
Swali la dondoo 7
Ndoto ya Mashaka
"...dunia imenikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza fimbo yake aushi yangu yote."
- Eleza muktadha wa dondoo hili (al.4)
- Tambua na ueleze mbinu ya lugha iliyotumiwa katika dondoo.(al.2)
- Eleza jinsi dunia ilimcharaza fimbo msemaji kwa kutolea hoja kumi na nne. (al.14)
Majibu ya dondoo 7
-
- Maneno ya Mashaka
- Katika ndoto
- Yumo chumbani mwake.
- Anaota kuhusu kurudi kwa ua lake baada ya kupotea kwa karne moja.
-
- Tashihisi - dunia kunikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza
-
- Mamake Mashaka kufariki punde tu baada ya kumkopoa.
- Babake pia anafariki punde tu baada ya mamake.
- Kuambulia mama mlezi maskini.
- Kuanza kufanya kazi za kijungu jiko kujikimu yeye na mama mlezi.
- Licha ya bidii yao mara kwa mara walikosa ikamlazimu Kidebe kutumia akiba yake.
- Kufiwa na mama mlezi.
- Kufungishwa ndoa ya mkeka na Mzee Rubeya.
- Kudharauliwa na wazazi wa Waridi kwa sababu ya umasikini wake.
- Kuishi katika mtaa duni.
- Chumba chake ni duni - kinavuja paa inyeshapo.
- Alikosa samani chumbani – hana meza,viti,kitanda wala godoro.
- Kazi ya usiku.
- Mshahara duni.
- Kukopoa pacha mara tatu.
- Kulazimika kuomba nafasi ya malazi ya wana kwa jirani.
- Mazingira yenye harufu mbaya ya chooni.
- Mke na wana kumkimbia. Zozote 14
Swali la dondoo 8
Nizikeni papa hapa–Ken Walibora
“Ndugu yangu tahadhari na hawa.........”
- Eleza muktadha wa dondoo (al.4)
- Eleza sifa za msemewa (al.4)
- Taja naufafanue maudhui sita katika hadithi hii (al.12)
Majibu ya dondoo 8
-
- Maneno ya rafiki ya Otii
- Msemewa ni Otii
- Walikua katika klabu moja Mombasa
- Ni baada ya Otili kuanza urafiki na Rehema Wanjiru
- Sifa za Otii
- Bidii
- Mvumilivu
- Mchunguzi
- Tamaa
- Mapuuza
- Mpenda starehe
- Msimamo dhabiti
- Hasira
- Kumbulazi
-
- Ukimwi
- Ajali Barabarani
- Usafiri
- Utekelezajichezaji soka
- Ukalili/Dhuluma
- Usaliti
- Uanahabari
- Teknolojia
- uzalendo
Swali la dondoo 9
“Rasta twambie bwana!”
- Weka dondo katika muktadha (alama 4)
- Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (alama 2)
- Nikwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe? (alama4)
- Je, mtihani wa maisha niamwani faafu ya hadithi hii? (alama10)
Majibu ya dondoo 9
-
- Maneno ya wanafunzi wa shule ya Busukalala.
- Akimwambia Rasta/ Samueli Matandiko.
- Walipokuwa shuleni.
- Samueli alikuwa ametoka katika afisi ya mwalimu mkuu kuchukua matoke yake ya mtihani.
- Marafiki waliomjua wanamtaka awaelezee alama zake.
-
- Utohozi -rasta
- nidaa-Rasta twambie bwana! c)
-
- Mwalimu mkuu wa shule ya Busukalala hakuwahi kumwamini Samueli hata siku moja kama anaweza kufaulu mtihani
- Mwalimu mkuu hakuamini Samueli aliposema kuwa amelipa ada mpaka alipohakikisha kwa kuangalia nyaraka na kumbukumbu zake.
- Anamwonyesha Samueli dharau kwa kumrushia karatasi kama mbwa; anarejelea kile alichokuwa akifanya na kumpuuza.
- Mwalimu mkuu hakumpa ushauri wowote Samueli ambo unmgemsaidia kupokea matokeo yake ambayo hayakuwa mazuri hata kidogo.
- Mwalimu mkuu alimjibu Samueli kwa karaha, alipomwita kuwa ni fidhuli.
- Anamjibiza kwa kuuliza iwapo wanafunzi wengine wanalipa mawe au majani.
- Mtihani wa Maisha ni anwani ambayo imesawiri maudhui ya hadithi hii kwa kiwango kikubwa.
- Samueli anafanya mtihani wake wa shule ya upili na kuenda kuyachukua matokeo. Kabla ya kufikia zamu zake Samueli anajichunguza na kujipima uwapo ameufanya vizuri. Mawazo kuhusu mtihani huo yanamtawala.
- Alianza kuwachunguza wanafunzi waliokuja kuchukua matokeo ya mtihani wanaopotoka mlangoni ili kujaribu kuona iwapo wamefaulu au la.
- Samueli anajaribu kujiaminisha kuwa yeye atakuwa amefaulu mtihani wakati akiwa kwenye foleni ya kuchukua matokeo.
- Samueli anajiaminisha kuwa yeye ni mjanja na angemshangaza mwalimu mkuu.
- Anagundua kuwa amefali mtihani huo. Safu za alama ya D na ilimkodolea macho. Herufi hizo zilimfedhesha na akalemewa.
- Nyumbani baba yake aliyengoja matokeo kwa hamu hakuyapata.
- Samueli anadanganya kwamba ana salio la karo.
- Baba anarauka na kutembea kilomita sita kwenda kuchukua matokeo ya mtihani.
- Anapogundua ni uwongo anapandwa na hamaki.
- Samueli anaamua kujitosa bwawani ili aondokane na athari za kufeli mtihani huu wa kitaaluma. Hata hivyo amaokolewa na mpita njia.
- Mama yake anamwambia kuwa ingawa amefeli mtihani wa shule, asikate tamaa, bado ana mtihani wa maisha ambao anaweza kufaulu.
- Anwani hii inafaa sana
Swali la dondoo 10
TUMBO LISILOSHIBA (S.AMOHAMMED)
``Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’’
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama4)
- Tambua tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama2)
- Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinacho rejelewa katika dondoo hili.(alama10)
- Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. (alama4)
Majibu ya dondoo 10
-
- Hii ni kauli ya mwandishi
- anarejelea tukio la ulafi wa Jitu
- mahali ni katika mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
- watu wamepigwa na butwaa kwa tendo la ulafi wa Jitu.(4x1=4 b)
-
- nahau- kukitegua kitendawili (alama 2)
- jazanda - neno kitendawili kurejelea jambo fulani lililofichika (yoyote: kutaja alama 1, kutoa mfano mmoja alama 1)
- Chanzo
- Kuwepo kwa uvumi na nong'ono kuhusu uwezekano wa kunyakuliwa ardhi ya Wanamadongoporomoka.
- Mzee Mago kuwahamasisha raia kuhusu haja ya kutetea kazi zao.
- Mikutano ya kuandaa mikakati ya kutetea haki za Wanamadongoporomoko inayofanyika katika mkahawa.
- Jitu kuwasili mkahawa mshenzi na kuzua taharuki
- Jitu kuamrisha kuhudumiwa na kula chakula chote kilichoandaliwa.
- Watu kupigwa na butwaa kwa ulafi wa jitu na kuwazia tendo hili
Hatima - Jitu kuahidi kurudi keshoye kula maradufu ya siku hiyo.
- Hatimaye jitu kufika na mabuldoza
- Askari wa baraza kuandamana na jitu
- Jeshi la polisi kuwalinda askari wa baraza
- Watu kupigwa virungu bila hatia
- Vibanda kubomolewa
- Watu kujenga upya vibanda mshezi zaidi ya hapo awali (Hoja zozote 5 za chanzo na 5 za hatima jumla ni alama 10)
-
- Wazalendo halisi wanaendeleza harakati za kupigania haki zao za kumiliki na kukomboa ardhi yao.
- Wenye bidii: hawasiti /hawakomi kuandaa mikakati ya kupigania haki zao. mfano: mikutano yao.
- Wenye umoja na ushirikiano : wanashirikiana kwa kukutana na kupanga utetezi wa haki zao.
- Wakakamavu/ jasiri: wanakaidi hatua ya Jitu na kuikomboa ardhi yao iliyonyakuliwa.
- Wenye hekima/ busara: wanabaini hila za wenye nguvu kutaka kunyakua ardhi yao na kujiandaa kukabiliana nao. (zozote 4X1-4)
Swali la Dondoo 11
”Jijini ni kuzuri.Kuna majumba makubwa , utapanda magari mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari.Utapelekwa shule kusoma na kuandika.”
- Jadili mukadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza taswira zinazojitokeza katika dondoo kwa kutoa mifano. (alama 3
- Aliyoambiwa msemewa ni kinyume cha yaliotokea .Eleza.(alama 8)
- Wahusika mbalimbali katika dondoo hili wametumia njia nyingi kukabiliana na matatizo yanayowakumba.Zijadili.(Alama 5)
Majibu ya Dondoo 11
- Jadili mukadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Msemaji ni Babake Bogoa
- Wanoambiwa ni kina Sebu , Kazu ,Temu na Sakina
- Wako katika club Pogopogo
- Bogoa alikuwa anawasimulia yaliomfika kabla ya kutolewa kwao.
- Eleza taswira zinazojitokeza katika dondoo kwa kutoa mifano. (alama 3)
- Taswira oni-majumba makubwa makubwa
- Taswira mwonjo-utakula vyakula vitamu
- Taswira mwendo-utapelekwa shule
- Aliyoambiwa msemewa ni kinyume cha yaliotokea .Eleza.(alama 8)
Masaibu ya Bogoa- Kula kwa viage/sufuria wengine wakila kwa sahani
- Kuchomwa kwa kijinga alipokuwa akioka maandazi halafu akalala
- Kukatazwa asiende shule kama watoto wengine
- Kunyimwa ushirika wa watoto wa Bi, Sinai, wasicheze pamoja
- Kufanyishwa kazi ngumu kama kuteke maji, kuchanja kuni, kufua
- Kuchapwa sana alipochelewa kurudi baada ya kupewa nafasi ya kutoka kidogo
- Kutishiwa kukatwa ulimi iwapo angesema kwa yeyote yaliojiri humo nyumbani
- Kunyimwa ushirika na wazazi wake walipokuja kumwona
- Kulazimika kuamka mapema kama mtoto mdogo
- Kula makoko ya chakula ua makombo
Zozote 8*1=8
- Wahusika mbalimbali katika dondoo hili wametumia njia nyingi kukabiliana na matatizo yanayowakumba.Zijadili.(Alama 5)
- Bogoa kupelekwa kulelewa kwa Bi. Sinai kwa sabau ya uamskini
- Kuhama kwa Bogoa kutoka kwa Bi, Sinai ili kuyaepuka mateso
- Bogoa kumwaga dukudku zake kwa kina Sebu ninjia ya kutoa kihoro cha aliyopatia kwa Bi.Sinai
- Bogoa kutia bidii katika maisha yake kama sonara ili kujitoa katika hali ya uchochole
- Bogoa alimwoa Sakina ili amwondolee upweke pale Tinya.
- Bogoa kuwasemehe wazazi wake na bi.Sinai
Swali la Dondoo 12
“Lakini hajawahi kuniamini huyu hambe. Lakini mimi mwenyewe najiamini. Lazima mtu ajiamini. Au sio? Leo ndio siku yangu ya kuthibitisha ukweli wa mambo Leo mwalimu atajua kuwa mkataa biu hubiuka. ….”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
- Bainisha mbinu nne za kimtindo katika dondoo hili. (Alama 4)
- Bainisha toni ya dondoo hili. (Alama 2)
- Thibitisha ukweli wa kauli, “Leo ndio siku yangu ya kuthibitisha ukweli wa mambo,” kama alivyosema mzungumzaji. (Alama 12)
Majibu ya Dondoo 12
“Lakini hajawahi kuniamini huyu hambe. Lakini mimi mwenyewe najiamini. Lazima mtu ajiamini. Au sio? Leo ndio siku yangu ya kuthibitisha ukweli wa mambo. Leo mwalimu atajua kuwa mkataa biu hubiuka….”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
- Haya ni maneno ya Samueli Matandiko. Anajiambia nafsini. Yupo katika mlango wa ofisi ya mwalimu mkuu. Amekuja ili kuchukua matokeo yake ya mtihani wa kitaifa. Anasema maneno haya kwani alijua kuwa mwalimu mkuu hakuamini uwezo wake masomoni.
(zozote 4×1= 4)
- Haya ni maneno ya Samueli Matandiko. Anajiambia nafsini. Yupo katika mlango wa ofisi ya mwalimu mkuu. Amekuja ili kuchukua matokeo yake ya mtihani wa kitaifa. Anasema maneno haya kwani alijua kuwa mwalimu mkuu hakuamini uwezo wake masomoni.
- Bainisha mbinu nne za kimtindo katika dondoo hili. (Alama 4)
- Uzungumzi nafsi- lakini hajawahi kuniamini huyu…
- Balagha- au sio?
- Kinaya- leo ndio siku yangu ya kuthibitisha ukweli wa mambo.
- Methali- Mdharau biu hubiuka.
(zozote 4×1=4)
- Uzungumzi nafsi- lakini hajawahi kuniamini huyu…
- Bainisha toni ya dondoo hili. (Alama 2)
- Toni ya tumaini- mimi mwenyewe najiamini
(kutaja 1, maelezo 1)
- Toni ya tumaini- mimi mwenyewe najiamini
- Thibitisha ukweli wa kauli, “Leo ndio siku yangu ya kuthibitisha ukweli wa mambo,” kama alivyosema mzungumzaji. (Alama 12)
- Ukweli unathibitishwa kwa Samueli kufeli mtihani ilhali aliamini kuwa yeye ni hodari na atamshtua Mwalimu Mkuu. Anapata D na E kwenye kila somo.
- Ukweli unathibitishwa kwa Samueli kudai kuwa anajua Mto Limpopo upo Misri na Mto Zambezi upo Tanzania ambayo inapakana kaskazini na Somalia.
- Ukweli unathibitishwa Samueli anapodai eti anajua Kenya ilipata uhuru 1980. ⮚ Ukweli unathibitishwa kwa Samueli kusema kwamba mimea ya kijani ina kitu kiitwacho umbijani (uk 135). Haya yote ni uongo huku naye akidhani ni ukweli.
- Samueli anashindwa kuwakabili wanafunzi wenzake na kujifungia chooni.
- Ukweli unadhihirika babake Samueli anapoenda shuleni na kutambua kuwa Samueli alikuwa kafeli mtihani vibaya vibaya.
- Samueli anamwepuka mpenziwe Nina baada ya kujua kuwa alikuwa amefeli katika mtihani. Anaogopa kuonwa zuzu.
(zozote 6×2= 12)
Swali la Dondoo 13
“Kwanza nilimwogopa sana…kwa sababu kila siku alinitishia…”
- Fafanua muktadha wa dondoo. (alama 4)
- Eleza sifa zozote nne za msemaji . (alama 4)
- Ni sababu zipi zilichangia msemaji kujikuta katika mikono ya mrejelewa? (alama 4)
- Jadili masaibu wanayopitia watoto huku ukirejelea hadithi hii (alama 8)
Majibu ya Dondoo 13
- haya ni maneno ya Bogoa akimjibu Sebu katika Club Pogopogo.
Sebu alitaka kujua kwa nini Bogoa hakumweleza matatizo yake kwa Bi. Sinai kama kunyimwa nafasi ya kuwaona wazazi wake na kulishwa makombo. (4 x 1 = 4) - sifa za Bogoa
- Msiri;anaficha siri ya kuchomeka viganja, anatororka kisiri kutoka kwa Bi Sinai.
- Mvumilivu;anavumilia mateso ya Bi Sinai hadi kubalaghe
- Mwenye mapenzi;anampenda Sebu sana ndiposa anamwambia siri zake
- Mwenye bidii; anajibidiisha kujifunza usonara na anaifanya kwa bidii
- Karimu;anawanunulia kina Sebu vinywaji katika Club Pogopogo
(Za kwanza 4 x 1 =4)
- sababu zilizomchangia Bogoa kujikuta mikononi mwa Bi. Sinai
- asubuhi moja babake alimwamsha mapema na kumtayarisha kisha babake akamwambia waende mjini amuache kwa marafiki zake/mrejelewa
- babake alimshawishi kuwa jijini ni kuzuri na angekula vizuri na angeenda shuleni kusoma na kuandika .
- babake alimshikia mkwaju na kutishia kumchapa iwapo angekataa kwenda kwa mrejelewa
- umaskini wa wazazi wake uliwapelekea kumpeleka kulelewa kwa mrejelewa
- mjini angepata maisha bora zaidi ya kitajiri
(zozote 4 x 1 = 4)
- masaibu ya watoto
- kutelekezwa wazazi wake bogoa wanayatelekeza majukumu yao ya malezi na kumpeleka kwa Bi Sinai
- kunyimwa usingizi wa kutosha annamshwa mapema kuchoma mandazi na kuyapeleka shuleni kuyauza
- kunyimwa uhuru wa kucheza na watoto wa jirani
- kunyimwa nafasi ya kusoma – Badala ya kupelekwa shuleni na Bi Sinai anamtumia kuchoma mandazi na kuyauza.
- kupigwa sana Bogoa anapoenda kucheza na kuchelewa kurudi Bi Sinai anamtafuta na kumpiga vibaya
- Kutishwa ; Bogoa anatishwa kukatwa ulimi akitoa siri ya nyumba ya Bi Sinai
- Kunyimwa nafasi ya kutangamana na wazazi wao . Bi Sinai anamzuia Bogoa kupatana na wazazi wake wanapomtembelea ili asipate nafasi ya kusimulia madhila anayopitia.
- Kubaguliwa Bi Sinai anawaambia wanawe kuwa watoto wa kimaskini wanastahili kutumwa na hawastahili kwenda shuleni
- kutengwa na watoto wenzao Bogoa anateganishwa na wanuna wake anapopelekwa kwa Bi Sinai
- kulishwa makombo Bogoa anakula makombo ya watu waliokula na kushiba
- maoni yao kutosikilizwa ; babake Bogoa alimtishia kwa mkwaju
- Kulia sufuriani Bogoa anakula kwenye sufuria na vyungu wakati kila mtu alikulia sahanini
- Kufanyizwa kazi. Bi Sinai anamtumikisha Bogoa kuchanja kuni, kufagia, kuteka maji, kufua ilhali ni kitoto cha miaka mitano tu
Swali la Dondoo 14
“Ndugu yangu kula kunatumaliza.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
- Taja na ueleze sifa zozote mbili za mnenewa. (al 4)
- Eleza tamathali ya usemi iliyotumiwa katika dondoo hili. (al 2)
- Kwa kurejelea hadithi ya Shibe Inatumaliza, thibitisha ukweli wa kauli ‘kula kunatumaliza’(al 6)
- Eleza umuhimu wa matumiziya nyimbo katika hadithi ya Shibe Inatumaliza. (al 4)
Majibu ya Dondoo 14
“Ndugu yangu kula kunatumaliza.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)
- Maneno haya ni ya Mbura akimwambia Sasa wakiwa nyumbani kwa Mzee Mambo katika sherehe. Mbura anamhakikishia Sasa kuwa kula kutawamaliza baada ya Sasa kumuuliza ikiwa anahitaji kuongeza vyakula. 4×1= al 4
- Taja na ueleze sifa zozote mbili za mnenewa (al 4)
- Ni msomi- ni waziri wa mipango na mipangilio, wizara inayomhitaji mtu kusoma kwa kina vipengele vya jamii.
- Mwenye bidii- hakuna sekunde iwapitayo akiwa na Mbura bila kufanya kazi
- Mzalendo- wanajituma kwa uzalendo wa taifa lao.
- Mwajibikaji- hufanya kazi kwa hiari yake ama kwa kuamriwa na huyu au yule.
- Mtiifu- anafanya kazi kwa kuamriwa.
- Mdadisi- anamsumbua Mbura na maswali mengi.
- Mlafi- baada ya kupakua anaanza kula bila kunawa na kurudia kuongeza chakula chakula mara tatu. 2×2= al 2
- Eleza tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo (al 2)
- Uhaishaji- kula kunatumaliza
- Jazanda- kula kunatumaliza 1×2= al 2
- Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza, thibitisha ukweli wa kauli ‘kula kunatumaliza’ (al 6)
- Mzee Mambo anachota mshahara ila hatosheki; anaendelea kuchota wananchi wakiteseka.
- Mzee Mambo anapanga sherehe nyingi kwa pesa za umma ila hatosheki nazo.
- Katika sherehe, watu wanakula na kula tena tokea jua lilipochomoza.
- Watu wanakula tu bila kuuliza aliyepika chakula na jinsi chakula kilivyopikwa.
- Sasa na Mbura wanakula hadi wanalala.
- Sasa na Mura wanarudia chakula kwenye foleni mara tatu kabla ya kutafuta mahali pa kutulia kula bila aibu.
- DJ bado anafanya kazi ya kuburudisha hata baada ya kuchota mabilioni ya pesa za serikali, nao wananchi wa kawaida wanateseka.
- DJ na viongozi wengine wanapata huduma zote za msingi bure huku wananchi wa kawaida wakilipia huduma zote.
- Mbura aneleza madhara ya kiafya yanayohusiana na kula kwa wingi bila kutosheka.
- Viongozi wanajali maslahi yao na kunyakua mali kuliko utu na ubinadamu. 6×1= al 6
- Eleza umuhimu wa matumizi ya nyimbo katika hadithi ya Shibe Inatumaliza (al 4)
- Zinatumiwa na viongozi kujitumbuiza baada ya kunyakua mali ya umma. (uk 37)
- Zinatumiwa na viongozi kujiliwaza kuwa mali mtu hupewa na Mungu. (uk 37)
- Zinatumiwa na viongozi kujiondolea lawama baada ya kuchota pesa za umma. (uk 43) Zinatumiwa kuonyesha kuwa wanaonyanyaswa na kutegemea viongozi wataamka na kuwakimbilia viongozi shida zikiwazidia. (uk 43)
- Zinatumiwa kuonyesha kuwa wananchi wa kawaida wanasahau shida zao na viongozi wabaya pindi wanapopokea msaada mdogo.
Swali la Dondoo 15
(Mtihani wa maisha)
‘Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharau biu hubiuka’
- Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
- Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika mktadha huu. (Alama 6)
- Eleza wasifu wa mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 2)
- Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi ya Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla) ala. 8
Majibu ya Dondoo 15
Haya ni maneno ya Samueli matandiko anayejizungumzia.
- Yuko ofisini ya mwalimu mkuu. Amekuja kuchukua matokeo ya mtihani. (4x1)
-
- Uzungumzaji nafsi - Samueli anajizungumzia.
- Kinaya - Ni Samueli aliyeaibika si mwalimu.
- Methali - mdharau biu hubiuka (3x2)
-
- Ni mwongo - Alimdanganya Nina kuwa ni mwerevu shuleni.
- Ni mwoga - Alitaka kutorokea babake.
- Hana matumaini - Anataka kujiua.
- Hana bidii - Anashindwa na masomo (2x1)
-
- Babake Samueli anauza mali yake ili asomeshe watoto.
- Babake Samueli anathamini elimu ya Samueli kuliko dada zake kama mwajuma na Bilha.
- Samueli anatembea muda wa kilomita sita ili atafute elimu.
- Samueli anaogopa kuzungumza na babake kuhusu matokeo yake.
- Mwalimu mkuu alimdharau Samueli kwa kumrushia matokeo yake.
- Samueli hakutaka kuonyesha matokeo yake kwa wenzake alipoanguka.
- Samueli hakutia bidii masomoni mwake kwani hata majibu yake si sahihi.
- Samueli alipoanguka mtihani wake alikosa matumaini na kutaka kujiua.
Swali la Dondoo 16
“Bwana we, huoni kwamba unaniumiza? Katafute mpira uupige shuti, mimi ni binadamu mwenzako.”
- Eleza muktadha wa sdondoo hili. (al. 4)
- Fafanua mbinu za kimtindo zinazobainika katika dondoo hili. (al. 4)
- Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza vile mandhari ya “Hotel Rombeka” inavyokuza maudhui.(al. 4)
- Eleza namna haki za watoto zinavyokiukwa katika hadithi ya “Tulipokutana tena. (al. 8)
Majibu ya Dondoo 16
- msemaji ni Sebu, akimwambia Kazu – akina kazu/ wakiwa hoteli ya Romeo. Sebu anarejelea uchawi wa akina kazu kwama ukalipiga pakacha teke, litalalamika. 1 x 4 =4
- mitindo
- swali la balagha – huchi kwamba unaniumiza?
- utohozi – shuti
- litifati – maneno ya pakacha yanasemwa na sebu
- uhuishi/tashihisi – pakacha lina uwezo wa kusema
4 x 1 =4
- Maudhui ya anasa/raha/starehe/burudani
Maudhui ya urafiki baina ya kazu na sebu
Maudhui ya mapenzi kazu na mkewe /sebu na mkewe
Maudhui ya ushirikiano /uchawi
Maudhui ya kuwajibika – wanaamua kumtafuta Bogoa. 4 x 1 =4 - Ukiukaji wa haki za watoto
- Bogoa hataki kuenda kuishi na rafikiye babake mjini lakini babake anamlazimisha kumpeleka huko, hivyo kumtenga na familia ambayo hakutaka kutengana nayo kamwe.
- Bogoa anapokataa kutenganishwa na familia yake ili kuenda mjini na rafikiye babake, babake anatisha kumpiga kwa mkwaju iwapo hangekubali.
- Bi. Sinai hampeleki Bogoa shuleni. Anamfanyiza kazi tu. Anadai kuwa watoto wa kimaskini hawakustahiki kusoma; wanastahili kutumwa.
- Bi. Sinai anamtumkisha Bogoa, mtoto wa miaka tano. Anamfanyiza kazi kama vile kuchanja kuni, kufagia, kufua, kuteka maji kutoka kisimani na kuuza maandazi shuleni.
- Bogoa akiwa nyumbani kwa Bi. Sinai hakuwa na uhuru wa kucheza ila kwa kutoroka, Bi Sinai alipolala mchana baada ya kula.
- Bogoa alipochelewa kurudi nyumbani kutoka mchezoni, Bi. Sinai alimtafuta na alipompata alimpiga vibaya.
- Bi. Sinai hakumruhusu Bogoa kucheza na wanawe. Alicheza tu na watoto wa majirani kama vile Sebu.
- Bi Sinai alikuwa akimtusi na kumsimbulia Bogoa.
- Wazazi wake Bogoa walipomtembelea, Bi. Sinai alimzuia kuwa pamoja nao ili asiwaeleze dhiki alizokuwa akipitia mikononi mwake.
- Bogoa akiwa nyumbani kwa Bi. Sinai, alikuwa wa mwisho kula wakati kila mtu akiwa ashakula/alikula makombo ya watu waliyoacha baada ya kushiba.
- Bogoaalikula kwenye sufuria na vyungu wakati kila mtu katika familia ya Bi. Sinai alikula sahanini.
- B. Sinai alimtisha Bogoa kuwa angemkata ulimi iwapo angesema chochote kuhusu maisha ya familia yake – hivyo kumhofisha Bogoa kufichua siri kuhusu shida alizozipitia nyumbani kwake.
- Bogoa ambaye ni mtoto wa miaka mitano anaamshwa alfajiri kuchoma maandazi na kuenda kuyauza shuleni huku watu wazima kama Bi. Sinai wakiwa wamelala, hali inayomsababisha kusinzia akichoima maandazi.
- Bi. Sinai anamchoma Bogoa viganja vyake kwa kijinga baada ya kusinzia na kuacha maandazi kuungua.
Swali la Dondoo 17
“Hiyo ni dharau ndugu yangu, kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine”.
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Fafanua sifa za msemaji . (alama 4)
- Tathmini vile viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)
Majibu ya Dondoo 17
-
- Msemaji ni Mbura
- Alikuwa anazungumza na Sasa.
- Walikuwa kwenye sherehe iliyoandaliwa kwa mzee Mambo. (uk44)
- Walikuwa wanazungumza kuhusu ‘kula kwao’ Zozote4×l
- msemaji ni Mbura
- Ni mzalendo- anafanya kazi kwa bidii katika wizara yake kama njia ya kuonyesha uzalendo. ii. Mwenye tamaa- anajaza sahani kwa chakula na kukila chote.
- Mwenye utu- anataka wananchi wale kwa niaba ya viongozi kama vile wao wamekuwa wakila kwa niaba yao.
- Ni fisadi- amepokea kazi kwa afisi ya serikali kwa njia isiyo halali.
- Mzembe- baada ya kula sahani tatu za vyakula kwenye sherehe analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini.
- Mtetezi wa haki
- Mvumilivu
- Mpyaro
- Msema kweli. Za kwanza 6×1
- Tathmini vile viongozi wanavyokuwa wabadhirifu.
- Hulipwa mishahara mikubwa sana na serikali jambo linalochangia ubadhirifu wa mali ya üuma.
- Sherehe kubwa za viongozi wa kiserikali huchangia pakubwa ubadhirifu.
- Viongozi hutumia raslimali za nchi kwa manufaa yao ya kibinafsi- magari ya serikali.
- Raslimali zilizotumiwa katika kuvinunua vyakula na vinywaji vingetumika katika kuendeleza asasi tofauti za kijamii.
- Dj na wenzake wanapata mabilioni ya fedha kutokana na kuwatumbuiza wageni katika sherehe kama hizi.
- Dj kupata huduma za maji, stima, matibabu bure.
- Dj kuuza dawa ambazo zilipaswa kutumika na wananchi katika hospitali
- Viongozi wanawachukua baadhi ya watu wao wa karibu na kufanya juu chini kuona kwamba wanajifaidi na mali na raslimali za wananchi pasipo kujitolea jasho kamwe.
- Upeperushaji wa matangazo katika vyombo vya habari ya sherehe za kiongozi binafsi ni njia ya kuendeleza ubadhirifu.
- Sasa na Mbura wanapoamua kuchukua vyakula kupita kiasi katika sherehe za mzee mambo.
- Kuwaajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika sekta moja ya umma.
- Vibaraka na vikaragosi kupewa mali ambayo ingewafaidi wananchi.
Swali la Dondoo 18
“hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?
- Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
- Tambua mbinu tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili na umuhimu wake (alama 6)
- Onyesha jinsi dhana ya nzi kufia kidondani inabainika hadithini (alama 4)
- Hali ya kutowajibika inajitokeza vipi katika hadithi? (alama 6)
Majibu ya Dondoo 18
“Hebu sikiliza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”
- Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
Kauli ni ya Otii
Msemewa ni rafiki yake
Rafiki yake alikuwa akimtahadharisha dhidi ya wasichana warembo anapotambua ana uhusiano na Rehema.
Otii anasema maneno haya ili kujitetea na kuuhalalisha uhusiano wake na Rehema - Tambua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili na umuhimu wake (alama 6)
- Nidaa - “Sikiliza jo!” Otii anadhihirisha hisa zake za hasira anapokosolewa na rafiki yake.
- Balagha – “Pana hasara gani nzi kufia kidondani. Otii anadhihirisha hisia kuwa tayari anaelewa anachokifanya na rafikiye hana haja ya kuingilia lisilomhusu.
- Methali - methali nzi kufa juu ya kidonda si hasara imedokezwa. Methali hii inatumika kuonyesha kuwa anaelewa hasara zinazoweza kutokana na mahusiano yake na vimanzi.
Pia inadhihirisha mapuuza ya Otii (3 x 2 = 6)
- Dhana ya nzi kufia kidondani inavyobainika katika hadithi (alama 4)
- Otii anaugua maradhi ya ukimwi na kuishia kujutia kitendo chake
- Rehema anaangamia kwa ukimwi katika harakati za kujitafutia raha
- Otii anaishia kuvunjika muundi wake akiwa katika raha za kucheza kandanda.
- Otii anakonda kama ng’onda na kubakia mwembamba kama sindano
(4 x 1 = 4)
- Jinsi hali ya kutowajibika inavyojitokeza katika hadithi (alama 6)
- Hospitali zinashindwa kuwajibikia hali ya wagonjwa.
Otii anarejeshwa nyumbani - Vyombo vya habari vinashindwa kuwajibikia hali ya Otii hasa baada ya kuvunjika muundi. Wanamfuata Otii anapokuwa na afya na umaarufu.
- Serikali inamtelekeza Otii baada ya kuvunjika muundi.
- Otii anakosa kuwajibikia maisha hata baada ya kuonywa na rafiki yake.
- Rehema anakosa kuwajibikia ujana wake. Anaendeleza maradhi ya ukimwi
- Wanachama wa chama cha nyumbani wanapuuza agizo la Otii la kuzikwa Mombasa badala ya nyumbani Sidindi.
- Klabu ya Bandari FC haikumjali mchezaji wao hodari Otii baada ya kuvunjika muundi.
- Hospitali zinashindwa kuwajibikia hali ya wagonjwa.
Swali la Dondoo 19
Tulipokutana Tena Ingawa mimi nilikuwa kitoto cha miaka mitano, nilihisi siku ile ilikuwa mbaya kwangu.
- Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza toni ya dondoo hili. (alama 2)
- Eleza sifa sita za mzungumzaji wa kauli hii. (alama 6)
- Fafanua umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuijenga hadithi ya Tulipokutana Tena. (alama 8)
Majibu ya Dondoo 19
- Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Haya ni maneno ya Bogoa Bakari.
- Anawaambia mkewe Sakina, Sebu na mkewe Tunu, Kazu na mkewe Bi. Temu.
- Wamo katika Club Pogopogo.
- Bogoa anawasimulia hadithi kuhusu jinsi alivyotolewa nyumbani kwao na kupelekwa kwa
Bi. Sinai aliyemtesa sana.
- Eleza toni ya dondoo hili. (alama 2)
Toni ya huzuni- Bogoa anahuzunika anapokumbuka mateso yake mikononi mwa Bi Sinai - Eleza sifa sita za mzungumzaji wa kauli hii. (alama 6)
- Mpenda anasa - Sebu anasema kwamba yeye na Bogoa walikuwa wakienda mjini kucheza densi wakiwa na miaka kumi na minane.
- Karimu-_anashirikiana na Kazu kuwanunua chakula Sebu, Bi.Tunu, Bi.Temu na Sakina.
- Mwenye mapenzi - Baba yake alipotaka kumpeleka mjini akaishi huko alilia kwa maana hakutaka kutengana na mama, baba, ndugu, kaka na dada zake.
- Mtiifu - anatii kila analoambiwa na Bi.Sinai. Kwa mfano, Bi. Sinai anapomtisha kuwa angemkata ulimi iwapo angefichua chochote kuhusu maisha aliyoyapitia nyumbani kwa Bi.Sinai.
- Msiri aliteseka sana nyumbani kwa Bi. Sinai ila hakumwambia rafikiye Sebu licha ya kucheza naye. Aidha, hakuwahi kumtolea mkewe hadithi kuhusu masaibu aliyoyapitia nyumbani kwa Bi.Sinai.
- Mwongo Bi. Sinai anapomchoma viganja kwa sababu ya kuacha mandazi kuungua anamhadaa Sebu kuwa aliungua akiepua maji moto.
- Mwoga anasema kwamba alimwogopa Bi. Sinai kwa sababu ya kumtisha kwamba angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yao ya ndani.
- Mwenye mawazo mapevu - Sebu anapomuuliza kwa nini hakumueleza masaibu yake nyumbani kwa Bi. Sinaj, anamwambia kwamba hangeweza kufanya chochote kwa maana yeye alikuwa mtoto kama yeye.
- Mwenye kisasi anapotoroka nyumbani mwa Bi. Sinai anaamua kurorejea nyumbani kwao na pia kutotaka kumwona mtu yeyote kwa sababu anaona kuwa masaibu aliyoyapitia nyumbani kwa Bi. Sinai yalisababishwa na wazazi wake.
- Fafanua umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuijenga hadithi ya Tulipokutana Tena. (alama 8)
- Inachimuza saula la umaskini - Wazazi wake Bogoa hawana uwezo wa kununua sabuni / Bogoa na baba yake wanatembea kwa miguu, bila ya viatu hadi mjini.
- Inaonyesha masaibu ya wanakijiji Walikuwa na tatizo la maji kwa maana yalikuwa hayapatikani karibu. Walitembea masafa marefu kuyatafuta.
- Imemfumbulia Sebu fumbo alilotaka kufumbua - Amejua sababu ya Bogoa kutoroka nyumbani kwa Bi. Sinai.
- Kusawiri maudhui ya mapenzi Mapezi ya Bogoa kwa nduguze na wazazi wake yalimfanya kutotaka kutengana na familia yake.
- Kusawiri maudhui ya elimu - Baba yake Bogoa anamwambia kwamba angepelekwa shuleni kusoma.
- Kuendeleza maudhui ya ajira ya Watoto - Bi. Sinai alimtumia Bogoa kufanya kazi za Nyumbani.
- Kuonyesha' suala la ukiukaji wa haki za Watoto - Bi. Sinai anamtumia Bogoa kufanya kazi za nyumbani badala ya kumpeleka shuleni.
- Kuonyesha maudhui ya utabaka - Bi. Sinai anawaambia wanawe kwamba Watoto wa maskini hawastahili kusoma; kazi yao ni kutumwa.
- Kuonyesha maudhui ya uwajibikaji - Wazazi wake Bogoa walimtembelea ili kumjulia hali. Kuendeleza maudhui ya siri - Bogoa aliteseka sana mikononi mwa Bi. Sinai ila hakuwahi kumwambia rafikiye Sebu.
- Unajenga ploti/ msuko wa hadithi - Usimulizi wake unachimuza masuala kadhaa kama vile ukiukaji wa haki za Watoto umaskini n.k.
- Kubainisha masaibu ya Bogoa - Bi. Sinai hakumruhusu kutangamana na wazazi wake walipomtembelea, alikula makombo, anatusiwa, anasimbuliwa, anakatazwa kucheza na Watoto wengine.
- Unajenga sifa za wahusika. Kwa mfano, ukatili wa Sinai unabainika kutokana na usimulizi huu. Sinni anamchoma Bogoa mandazi yalipoungua.
Swali la Dondoo 20
Mame Bakari
“Dunia we’ dunia. Dunia ya mwenye nguvu, si ya mimi dhaifu wa nguvu. Dunia ya msumari moto juu ya donda bichi. Hao watu je?”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Fafanua mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)
- Thibitisha kauli “Dunia ya msumari moto juu ya donda bichi” ukirejelea Hadithi ya Mame Bakari. (alama 6)
- Fafanua jinsi mwanamke alivyosawiriwa katika hadithi hii. (alama 6)
Majibu ya Dondoo 20
MAME BAKARI
-
- Muktadha wa dondoo
- Haya ni maneno ya Sara katika uzungumzi nafsia.
- Anawaza akiwa nyumbani kwao
- Anawazia dhuluma ambazo angepata baada ya kubakwa na janadume.
-
- Mbinu za kimtindo katika dondoo
- Uradidi/takriri …dunia dunia
- Jazanda…dunia ya msumari moto juu ya kidonda
- Balagha…hao watu je?
- Kadiria. Zozote 2x2=4
- Kudhibitisha kauli “Dunia ya msumari moto juu ya donda mbichi”
- Sara angetengwa,kusutwa na kukashifiwa kwa kosa lisilo lake
- Babake ‘angemchinja’au amfukuze nyumbani
- Kukosa kuaminika.Sara anahofia babake huenda asimwamini
- Kufukuzwa shuleni. Sara anahofia kuwa angefukuzwa shuleni
- Kupata ujauzito. Sara anaambulia ujauzito baada ya kubakwa na janadume
- Dhiki za kisaikolojia
- Janadume linapatikana likijaribu kumbaka msichana mwingine,baada ya kumnajisi Sara
Tanbihi .Hoja zizingatie masaibu ya Sara baada ya kubakwa. Zozote 6x1=6
- Mwanamke alivyosawiriwa katika hadithi.
- Anadhulumiwa kimapenzi –Sara
- Anatumiwa kama chombo cha kumridhisha mwanamme
- Msiri -Sara
- Mwenye kuwajibika – Beluwa
- Mwenye busara –mamake Sara
- Kiumbe dhaifu –Sara baada ya kubakwa
Kadiria zozote 6x1=6 - TULIPOKUTANA TENA
Swali la Dondoo 21
Mohammed Khelef Ghassany “Mame Bakari”
“……… Bwana na Bibi hawawezi kukuvunja,”
- Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 3)
- Fafanua jinsi wazazi wa msemewa hawakumvunja. (alama 7)
Jadili ‘mitihani’ katika hadithi ya ‘Mtihani wa maisha’ (alama 10)
Majibu ya Dondoo 21
- Aliyosema maneno haya ni Sarina
- Akimwambia Sara
- Walikuwa wanatafuta suluhisho kwa ujauzito wa Sara. (alama 3)
- Wazazi wa Sarah walienda hospitali na kumsubiri kuona daktari.
- Waliweza kugharamia matibabu ya Sara.
- Walimzungumzia kwa upole kule hospitali
- Hawakumuonyesha kughadhabika kwao hata baada ya kujua kuwa aliwaficha
- Wanamnyamazisha anapolia katika chumba cha daktari.
- Walifahamu juu ya uzito wake kutoka kwa rafikiyo Sara na lakini hawakumgombeza.
- Walimpa mtoto jina Mame Bakari.
- Walimwandalia sherehe kumkaribisha mtoto nyumbani kwa kuchinja mbuzi na hata kuwaalika majirani.
(alama 7 x 1=7)
- ‘Mitihani’
- Mtihani halisi alioufanya shule ya upili na kufeli .
- Samueli kueleza matokeo kwa wazazi, inabidi adanganye kwamba hajakamilisha kulipa karo.
- Mtihani kwa Samueli kubaini aliyokuwa akiwaza nira.
- Samueli kuwaeleza wenzake kuhusu matokeo yake ya mtihani.
- Kutoweza kukabiliana na maisha baada ya kufeli mtihani na kutaka kujitoa uhai. Kujitosa maishani.
- Babake Samueli anafeli mtihani wa kuonyesha mapenzi kwa mwanaye baada ya kufeli mtihani shuleni. Anampa kamba ili atoe uhai wake.
- Mamake anafaulu katika mtihani kwa kuwa mlezi bora kwa kumnasua alipotaka kujitosa.
- Wanakijiji wanashughulika kumwokoa Samueli alipotaka kujitosa majini.
- Mwalimu mkuu anafeli mtihani wa maisha kwa kumwona Samueli kama mtu asiyefaa. Anamtupia matokeo.
- Wazazi wa Samueli walikuwa na mtihani wa kukubali kuwa pesa zao za karo zilipotea bure.
Swali la Dondoo 22
- “Pom poom! pom poom! pom poom…Honi ya muuza samaki hiyo. Alibonyeza mpira wa honi ili kuashiria kwamba sasa yumo njiani juu ya baiskeli yake, anapita akitembeza samaki.
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Bainisha vipengele vitatu vya kimtindo katika dondoo hili. (alama.3)
- Bainisha aina tatu za taswira katika dondoo hili. (alama 3)
- ”….mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana. “Thibitsha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi ya Masharti ya kisasa. (alama 10)
Majibu ya Dondoo 22
-
-
- Msemaji – msimulizi
- Msemewa – Akimrejelea Dadi
- Mahali – Njiani akitemebeza samaki.
- Ni baada ya miaka tisa katika ndoa. Ndoa ambayo Dadi ana hisi kuwa mkewe ndiye aliyevunja masharti kwa kumwendea kinyume.
4x1=4
-
- Tanakali ya sauti – pom poom! pom poom!
- Mdokezo – pom poom….Honi.
- Takriri – pom poom! pom poom, samaki
3x1=3
-
- Taswira hisi – pom, poom! pom poom….Honi ya muuza samaki huyo.
- Taswira mwendo – anapita akitembeza samaki.
- Taswira usikivu- Honi ya muuza samaki huyo.
3x1=3
-
-
- Dadi ndiye mchuma riziki – yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kulisha jamaa yake. Pesa za mkewe ni za kununua fasheni mpya na mapambo.
- Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.
- Kidawa hakubali kuwa mwanaume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya kazi za ndani ni hisani tu.
- Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui
- Dadi anaosha nyumba, kufagia na hata kupiga nguo pasi.
- Wanandoa kujiwekea masharti ya uzazi. Wanahiari kumzaa mtoto mmoja tu kutokana na athari za usasa.
- Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja. Kila mara mkewe anapofanya hivyo anaumia sana.
- Dadi kushuku mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu mkuu. Hali hiyo inampa wasiwasi sana hata anashindwa kula
- Kila mara Dadi alitarijiwa kuwa baada ya kula anageviondoa vyombo mezani na hata kuvisafisha.
- Dadi anapoamua kuzua mpango wa kupeleleza uhusiano wa mkewe na mwalimu mkuu, anafumaniwa na watu akiwa amepanda paipu na anaanguka na kuumia.
Swali la Dondoo 23 (Mtihani wa Maisha)
’Kusema kweli lakini hata mimi sikuwa na nadhari katika kumpenda msichana huyu … Nilimpenda kufa! Lakini! Kwao bure tu!’
- Eleza mkutadha huu. (Alama 4)
- Taja mtindo wa lugha uliotumika katika mkutadha huu. Alama 4
- Taja sifa mbili za mzungumzaji. (Alama 2)
- Onyesha maudhui ya umaskini katika hadithi fupi ya Ndoto ya mashaka.
Majibu ya Dondoo 23
- Haya ni maneno ya Samueli matandiko anayejizungumzia.
Yuko ofisini ya mwalimu mkuu. Amekuja kuchukua matokeo ya mtihani. (4x1) - Uzungumzaji nafsi - Samueli anajizungumzia.
Kinaya - Ni Samueli aliyeaibika si mwalimu.
Methali - mdharau biu hubiuka (3x2) - Ni mwongo - Alimdanganya Nina kuwa ni mwerevu shuleni.
Ni mwoga - Alitaka kutorokea babake.
Hana matumaini - Anataka kujiua.
Hana bidii - Anashindwa na masomo (2x1) -
- Babake Samueli anauza mali yake ili asomeshe watoto.
- Babake Samueli anathamini elimu ya Samueli kuliko dada zake kama mwajuma na Bilha.
- Samueli anatembea muda wa kilomita sita ili atafute elimu.
- Samueli anaogopa kuzungumza na babake kuhusu matokeo yake.
- Mwalimu mkuu alimdharau Samueli kwa kumrushia matokeo yake.
- Samueli hakutaka kuonyesha matokeo yake kwa wenzake alipoanguka.
Samueli hakutia bidii masomoni mwake kwani hata majibu yake si sahihi. - Samueli alipoanguka mtihani wake alikosa matumaini na kutaka kujiua.
Swali la Dondoo 24
“Maswali ya sampuli hiyo yanafaa kuulizwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza”
- Eleza muktadha wa dondoo hili (Al 4)
- Fafanua sifa tatu za msemaji wa dondoo hili (Al 6)
- Tadhmini namna maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi ambamo dondoo hili limetolewa (Al 10)
Majibu ya Dondoo 24
”Maswali ya sampuli hiyo yanafaa kuulizwa na wanafunzi wa kidato ch kwanza”
- Eleza miktadha ya dondoo hili
- haya ni maneno ya dkt. Mabonga
- anamwambia mwanafunzi wake
- wamo darasani katika chuo kikuu cha kivukoni
- anamwambia hivi baada ya kumuuliza swali kuhusu namna fasihi inavyoielekeza jamii
- Fafanua sifa tatu za msemaji wa dondoo hili
msemaji ni dkt. Mabonga. Ana sifa zifuatazo:- mshairi bora – anawahimiza wanafunzi chuoni kivukoni kujitegemea na kusuta ukupe
- Mwenye kiburi – anapoulizwa swali na mwanafunzi wake anamjibu kuwa maswali ya sampuli hiyo yalifaa kuulizwa wanafunzi wa kidato cha kwanza
- Mapujufu/mpyaro – anamwita mwanafunzi anayetaka kuuliza swali ‘Mama’
- Mwenye madharau – anamcheka mwanafunzi wake kicheko kikubwa kabla ya kumpa nafasi ya kuuliza swali
- Tathmini namna maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi ambamo dondoo hili limetolewa
- kazi – wazazi wa dennis ambao ni maskini wanawalimia matajiri mashamba yao ili kupata hela za kujikimu kimaisha
- utengano – tunaambiwa kwamba maskini na matajiri wametengana kama ardhi na mbingu chuoni – dennis ingawa wama chuoni kimoja na wafabya masomo pamoja
- mavazi – wnanafunzi kutoka familia za kitajiri hawavai vitenge kutoka mataifa ya afrika kama Ghana, na senegali kama wenzao. Wanavaa mavazi kutoka uingereza, ujerumani, marekani na ufaransa
- vifaa vya kielektroniki – wanafunzi kutoka familia za kitajiri wanamiliki simu za thamani, vipakatalishi na ipad huku wanafunzi maskini kama dennis machora wakiwa hawana hata vifaa kimojawapo. Wanasalia kuvimezea mate tu
- shule – wanafunzi kutoka tabala la juu wanasomea kwenye shule za mikoa na kitaifa huku wanaotoka katika tabaka la chini kama dennis wakisomea katika shule za vijijini
- ndoa – ni nadra mtu wa tabaka la chini na tabaka la juu kuoana – wazazi wake penina wanapinga ndoa ya penina na dennis kwa sababu ya dennis anatoka katika familia ya kimaskini huku wao wakiwa matajiri
- pesa za matumizi – wanafunzi kutoka familia za kitajiri wanatumiwa pesa nyingi za matumizi huku maskini wakitaabika. Kwa mfano, penina anatumiwa shilingi elfu tano kila wiki huku maskini dennis wakinywa uji bila sukari kwa kukosa pesa
- mahali pa kuishi – mtaa wa new Zealand wanakoishi wazazi wa penina ni mtaa wa watu wenye mapato ya kadri
- kukataa uchumba – wazazi wa penina wanamkataza penina kuchumbiwa na dennis kwa sababu ya dennis kuwa maskini huku kwao wakiwa matajiri
- tabaka la chini linakejeliwa. Wazazi wake dennis wanakejeliwa na kila mtu kwa sababu ya kuwa maskini
- magari – tabaka la juu linamiliki magari makubwa makubwa huku tabaka la chini kama dennis likiishia kubaki likitamani magari hayo kwa maana halina uwezo wa kuyanunua
- wanafunzi kutoka tabaka la juu wanataka kuacha masomo ambayo wanadai kuwa ni magumu ili kufanya kazi zinazomilikiwa na wazazi wao huku maskini kama dennis hawana la kufanya hata kama masomo hayo ni magumu. Kwa mfano, kuna mmoja anayetaka kuenda kuwa manamba katika magari ya babake.
- wanafunzi wa tabaka la chini wanaoishi maisha ya taabu chuoni huku wa tabaka la juu wakiishi maisha mazuri. Kwa mfano, dennis analalia shuka zilizochanika mbali na kuwa na shida ya kupata chakula huku matajiri kama penina wakitumiwa shilingi elfu tano kila wiki na wazazi wao
- wanafunzi wa tabaka la juu hawali Baadhi ya vyakula wanavyoichukulia kuwa duni huku maskini kama dennis wakivila. Kwa mfano, penina apoingia chumbani mwa dennis anashangaa kwa nini dennis anakunywa uji ishara kwamba yeye hanywi uji kwa sababu ni wa tabaka la juu
- utabaka ni chanzo cha mtu kujidunisha kwa mwingine. Dennis anayetoka katika tabaka la chini anaogopa kuwa mpenziwe penina anayetoka katika tabaka la juu hataki kuolewa na mwanamume asiye na kazi ya mshahara kubwa/mwanamume wa tabaka la chini, hivyo kuuvunja uchumba wao.
- watoto kutoka tabaka la juu wanajinaki kwa wenzao kuhusu kazi wanazozifanya wazazi wao. Kwa mfano, dennis anakumbuka shakila akajinaki kwamba mama yake ni mkurugenzi mkuu wa shirika la kuchapisha magazetini
- watu wa tabaka la juu wanaoishi jijjini huku maskini mashambani. Kwa mfano akina shakila wanaishi kijiijini kivukoni huku dennis akiishi mashambani.
Swali la Dondoo 25
“…madonda ya tumbo obesiti, ni kulatu ! “
- Eleza muktadha wa dondoo hili ( alama 4 )
- Taja na ueleze sifa mbili za msemewa ( alama 4)
- Taja na utoe mifano miwili ya mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo ( alama 2)
- Jadili maudhui matano yanayojitokeza katika hadithi husika. (alama 10)
Majibu ya Dondoo 25
- Maneno ya Mbura akiwambia sasa .
Wako katika sherehe za kumea meno kwa mtoto wa Mzee Mambo na wa pili kujiunga na shule ya chekechea. Sherehe inayofanyika nyumbani kwa Mzee Mambo.
Haya yanatokea baada ya vijana hawa kula kila kitu kisha kuanza kujadiliana ubora wa vyakula walivyovila na madhara yake. - Sifa za msemewa.
Mlafi..anakula bila kujali
Mzembe… baada ya kula sahani tatu analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini. - mbinuzalugha
utohozi… obesity
nidaa… kulatu !
jazanda - uongozi mbaya…. Mzee Mambo na DJ wanaongoza umma vibaya kwa kutumia mali ya umma kuandaa sherehe isiyowafaidi wananchi.
Tamaa na ubinafsi….. DJ ananyakua dawa za wagonjwa na kuziweka kwa duka lake binafsi.
Ufisadi. Mzee Mambo na DJ wanavuna mabilioni ya pesa za umma kwa sherehe isiyo na manufaa yoyote kwa umma.
Matumizi mabaya ya vyombo vya dola…. Televisheni ya kitaifa inatumika kupeperusha sherehe ambazo hazi na manufaa yoyote kwa umma.
Athari ya bidhaa zinazoingizwa inchini kutoka mataifa ya ughaibuni… mchelewa basmati ambao ni plastiki unawasababishia walaji( wanainchimaskini ) magonjwa kama vile saratani na obesiti.Matumizi mabaya ya mamlaka…Mzee Mambo anatumia gari za serikali kusafirisha vyakula , wageni na ata maji katika sherehe yake binafsi.
Swali la Dondoo 26
“… Na ati tuliopewa hatupokonyeki…”
- Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (al 4)
- Taja mbinu mbili za sanaa zilizotumika katika dondoo hili (al 4)
- Fafanua sifa zozote nne za mzungumzaji (al 2)
- Kwa kurejelea hadithi ‘shibe inatumaliza’ tathmini jinsi ubadhirifu wa mali ya umma umesawiriwa katika hadithi hii (al 10)
Majibu ya Dondoo 26
-
- Haya ni maneno yake mbura
- Alikuwa katika uwanja wa sherehe ya mzee mambo ya kusherehekea mwanawe kuingia nasari. Anajihisi ya kwamba
- amezinduka na kugundua jinsi walivyokuwa wakiwanyanyasa wananchi ambao wangezinduka. (al 4)
-
- Yaweke maneno hayakatika muktadha wake.
- kejeli – matumizi ya neno ati
- kinaya- tuliopewa ni kinaya kwa kuwa walikuwa wamenyakuwa kutoka kwa wananchi kimabavu (al 4)
- Fafanua sifa zote nne za mzungumzaji.
Mzungumzaji ni mbura- ni mlafi-wanaunga foleni na kula sana
- Mwenye mapuuza-ingawa wanafahamu uzembe uliopo na unyakuaji wa mali ya umma na hawafanyi kitu
- Mbadhirifu-wamehusika katika kufisidi hazina ya taifa
- Ni mkweli/ aliyezinduka -anatambua makosa yao kama viongozi
- Ni mbinafsi- anakula chakula bila kujali wananchi wengine
- (zozote nne) (al 4)
- Kwa kurejelea hadithi ‘Shibe inatumaliza’ tathmini jinsi mwandishi amelishughulikia suala la ubadhirifu wa mali ya umma. (al 8)
- Sasa na mbura kulipwa mshahara kwa kushikilia wizara ambayo ingefanywa na mtu mmoja
- Sasa na mbura kula kwa niaba ya watu wengine
- Dj kuuza dawa ambazo zilipaswa kutumika na wananchi katika hospitali za kiserikali
- Dj kutolipia huduma za umeme na maji.
- Dj kulipwa mabilioni kutumbuiza watu katika sherehe za kibinafsi
- Mzee mambo kulipwa mshahara mwingi bila kazi
- Magari ya serikali kutumika katika sherehe za kibinafsi kubeba Watoto
- Watu wanakula kupita kiasi katika sherehe ya mzee mambo -sasa na mbura
- Vyombo vya Habari kupeperusha sherehe ya kibinafsi
Swali la Dondoo 27
- Hakuna aliyeweza kukitegua kitendawili chenyewe lakini…’
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama4)
- Tambua mitindo uliyotumiwa katika dondoo hili. (alama2)
- Fafanua chanzo na hatima ya kitendawili kinachorejelewa katika dondoo hili.(alama 6)
- Eleza wasifu wa warejelewa katika dondoo hili. (alama4)
- Huku ukirejerea hadithi ya Tulipokutana tena eleza namna unyanyashaji umeshughulikiwa(alama 4)
Majibu ya Dondoo 27
- uk. 47
-
- Hii ni kauli ya mwandishi
- anarejelea tukio la ulafi wa Jitu
- mahali ni katika mkahawa mshenzi wa Mzee Mago
- watu wamepigwa na butwaa kwa tendo la ulafi wa Jitu.4x1=4
-
- nahau-kukiangua kitendawili
- jazanda -neno`kitendawili’kurejelea jambo Fulani lililofichika
- mdokezo- chenyewe lakini..(zozote 2x1)
-
- Chanzo
- Kuwepo kwa uvumi na nong`ono kuhusu uwezekano wa kunyakuliwa ardhi ya Wanamadongoporomoka.
- Mzee Mago kuwahamasisha raia kuhusu haja ya kutetea kazi zao.
- Mikutano ya kuandaa mikakati ya kutetea haki zaWanamadongoporomoko inayofanyika katika mkahawa.
- Jitu kuwasili mkahawa mshenzi na kuzua taharuki
- Jitu kuamrisha kuhudumiwa na kula chakula chote kilichoandaliwa.
- Watu kupigwa na butwaa kwa ulafi wa jitu na kuwazia tendo hili (zozote 3x1)
- Hatima
- Jitu kuahidi kurudi keshoye kula maradufu ya siku hiyo.
- Hatimaye jitu kufika na mabuldoza
- Askari wa baraza kuandamana na jitu
- Jeshi la polisi kuwalinda askari wa baraza
- watu kupigwa virungu bila hatia
- Vibanda kubomolewa
- Watu kujenga upya`vibanda mshezi’zaidi ya hapo awali
(Hoja zozote 3x1)
- Chanzo
- Wasifu wa warejelewa katika dondoo hili.
- Wazalendo halisi;wanaendeleza harakati za kupigania haki zao za kumilikina kukomboa ardhi yao.
- Wenye bidi:hawasiti/hawakomi kuandaa mikakati ya kupigania haki zao. mfano:mikutano yao.
- Wenye umoja na ushirikiano:wanashirikiana kwa kukutana na kupanga utetezi wa haki zao.
- Wakakamavu/jasiri:wanakaidi hatua ya Jitu na kuikomboa ardhi yao
(zozote 4x1)
-
-
- Bogoa anatenganishwa na jamaa wake anapopelekwa kuishi na Bi Sinai
- Bogoa kufanyishwa kazi nyingi na ngumu na Bi Sinai-kuna nazi ,kupara na kutoa matumbo ya samaki nk
- Kuamshwa mapema kuliko wengine ili kuchoma mandazi ya kuuza shule.
- Bogoa kunyimwa elimu ya shule na Bi Sinai .
- kunyimwa haki ya lishe bora kwani analazimika kula makoko na makombo yaliyobaki.
- Bogoa kuchomwa viganja vya mkono kwa moto anapounguza mandazi aliyokuwa akichoma.
Swali la Dondoo 28
“Alipokuwa kiguu na njia akimwinda kama kunguru mwerevu, moyoni mwake alidhani anafuata nyuki apate kula asali.”
- Weka dondoo katika muktadha wake. (alama 4)
- Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
- Eleza sifa za anayerejelewa kama kunguru mwerevu. (alama 6)
- Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho. (alama 8)
Anamwona baba akilini akifoka kama hayawani aliyejeruhiwa. Hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Familia yao si ya watu mbumbumbu. Dada zake Samueli walipasi mtihani huo huo wa kidato cha nne pasi hatihati kwenye shule hiyo ya Busukalala miaka michache iliyopita. Yule mkubwa, Bilha ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta naye Mwajuma anasomea ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Eregi. Kwa hivyo, shule si sababu wala udhuru. Ingawa baba yao anayaonea fahari mafanikio ya binti zake, aliwaona wanawake tu. Fahari yake ya dhati imo katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Baba alisadiki kwamba pindi walw mabinti wakishaolewa, hana satua tena juu yao na amatumizi yao ya fedha zao. Samueli ndilo tegemeo, nguzo hasa. Alijuzu kuwa tegemeo na nguzo ya familia yake.
Yaani akiwa mtoto wa pekee wa kiume alitegemewa kuwategemeza na kuwahami wazee wake na kulidumisha jina la ukoo wa babake…Ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa. Lo! Iweje yeye mwanamume kushindwa na dada zake, wanawake..!
Majibu ya Dondoo 28
“Alipokuwa kiguu na njia akimwinda kama kunguru mwerevu, moyoni mwake alidhani anafuata nyuki apate kula asali.” (uk 56)
- Weka dondoo katika muktadha wake. (alama 4)
Ni maneno ya msimulizi/mwandishi. Anamrejelea Dadi alipokuwa na msukumo wa kumtaka Kidawa kuwa mpenzi wake. Kidawa alikuwa amemwambaa Dadi. Dadi alikuwa kufa kupona kumtafuta Kidawa. - Tambua mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. (alama 2)
- Nahau. Alipokuwa kiguu na njia
- Sitiari/jazanda. Maneno kunguru na nyuki ni jazanda inayomrejelea Kidawa.
- Tashbihi/tashbiba- kama kunguru mwerevu
- Changanua mtindo katika kifungu kifuatacho. (uk 136) (alama 8)
Anamwona baba akilini akifoka kama hayawani aliyejeruhiwa. Hayawani ambaye anaweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima. Familia yao si ya watu mbumbumbu. Dada zake Samueli walipasi mtihani huo huo wa kidato cha nne pasi hatihati kwenye shule hiyo ya Busukalala miaka michache iliyopita. Yule mkubwa, Bilha ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta naye Mwajuma anasomea ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Eregi. Kwa hivyo, shule si sababu wala udhuru. Ingawa baba yao anayaonea fahari mafanikio ya binti zake, aliwaona wanawake tu. Fahari yake ya dhati imo katika kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. Baba alisadiki kwamba pindi walw mabinti wakishaolewa, hana satua tena juu yao na amatumizi yao ya fedha zao. Samueli ndilo tegemeo, nguzo hasa. Alijuzu kuwa tegemeo na nguzo ya familia yake. Yaani akiwa mtoto wa pekee wa kiume alitegemewa kuwategemeza na kuwahami wazee wake na kulidumisha jina la ukoo wa babake…Ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa. Lo! Iweje yeye mwanamume kushindwa na dada zake, wanawake..!- Taswira –Anamwona baba akilini akifoka
- Nahau-kumwona mwanawe wa kiume akifua dafu. …anayaonea fahari
- Chuku- baba kuweza kumrarua mtu na kumla mzimamzima
- Takriri/urudiaji- nguzo, tegemeo kuonyesha matumaini makubwa kwa Samueli
- Tashihisi. Ilmuradi mawazo yanamwadhibu
- Mdokezo- jina la ukoo wa babake…/wanawake..!
- Uzungumzinafsia- mawazo haya yatokea mawazoni mwa Samueli
- Nidaa-Lo! wanawake...!
- Tabaini – familia yao si ya watu mbumbumbu
Swali la Dondoo 29
Wako wapi?Wamepuuzwa tu kulee! Futari kwa niaba.Sikukuu kwa niaba.Harusi kwa niaba.
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama4)
- Tambua mbinu za kimtindo katika dondoo hili (alama 3)
- Fafanua sifa za mnenaji ( alama3)
- Jadili maudhui yanayojitokeza katika dondoo kwa kurejelea hadithi nzima (alama5)
- Kwa kutoa hoja tano jadili ufaafu wa anwani ya hadithi husika. ( alama5)
Majibu ya Dondoo 29
-
- Mnenaji – Mbura
- Mnenewa – sasa
- Wapi – Nyumbani kwa mzee Mambo
- Mzee Mambo alikuwa ameandaa sherehe kwa mtoto wake wa kwanza anaingizwa nasari na wa pili ameanza kuota meno
( 4 x1 = 4)
- Balagha – wako wapi
Nidaa – wamepuuzwa tu kulee!
Urudiaji (takriri) kwa niaba
Kudumisha sauti – kulee!
Zozote 3 x1 = 3 - Mlafi – alikula chakula kingi
- Mtetezi wa haki za wanyonge anasema kuwa kula kwa niaba ya maskini ni dharau.
- Mwenye busara – anaelewa kuwa shibe ilikuwa ikiwamaliza kwa namna mbalimbali m.f magonjwa n.k
- Mzalendo anawatetea wanyonge wa nchi yake na kuupanda mchele wa kwao Mbeya
- Ni mweye utu – anataka wananchi pia wale kwa naiba ya viongozi
- Ni mtambuzi – anatambua kwamba wananchi wanaendelea kukumbwa na dhiki hukuviongozi wakiendela kujifaidi
Zozote 3 x1 = 3
-
- tabaka la utawala limejawa na ubinafsi – wanakula kwa niaba yaw engine.
- Mambo anatumia raslimali ya taifa kuandaa sherehe za watoto wake
- DJ anapata huduma zote za kimsingi kama maji, umeme bila malipo ilhali maskini hulipia yote
- DJ anapata dawa za duka lake kutoka kwa bohari ya serikali anasema hajali
- Mwandishi anasema waliopewa hawapokonyeki
- Ubinafsi unawamaliza wabinafsi na kuwaletea magonjwa kama saratani, presha n.k
- Sasa anafurahishwa na tabia yao ya kula kwa niaba ya watu wengine
- Katika sherehe watu walikula na kurudia tena na tena hadi wengine wakabeba kama Mbura
- Sasa anasema kuwa walio navyo walikula kwa niaba ya wengine waliopo na watakaozaliwa kwa hivyo kizazi kijacho hakitapata raslimali
- DJ na wenzake wanachota mabilioni ya serikali katika sherehe
(Zozote 5 x 1 = 5)
- Kwa sababu ya kula watu wamepata magonjwa mbalimbali kama presha…
- Kwa ajili ya kula wameleta vifo kwa kuuana mabomu, risasi na kunyongana
- Kula kumewafanya wauane kufikiria kimawazo hivyo basi wanabaki nyuma kiamendeleo
- Shibe inawamaliza kupitia watu kunyang’anyana vitu vinavyoonekana na visivyoonekana kama haki, heshima, utu na uhuru
- Waliopo wanakula kwa niaba ya wengine waliopo na watakaozaliwa; watakaozaliwa hawatapata chochote ila matatizo ya kulipia mikopo
- Mzee mambo anaandaa sherehe zisizo na maana kwa taifa lake. Maandalizi haya yanafanywa kwa kutumia raslimali za umma
- Kwenye sherehe walikula vyakula vya kila aina, vitamu, vichacho, vikali ana baridi, mchele wa basmati. Plastiki matokeo yake ni maradhi ya kila aina na vifo.
Swali la Dondoo 30
Ingawa mimi nilikuwa kitoto cha miaka mitano, nilihisi siku ile ilikuwa mbaya kwangu.
- Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza toni ya dondoo hili. (alama 2)
- Eleza sifa sita za mzungumzaji wa kauli hii. (alama 6)
- Fafanua umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuijenga hadithi ya Tulipokutana Tena. (alama 8)
Majibu ya Dondoo 30
-
- Haya ni maneno ya Bogoa Bakari.
- Anawaambia mkewe Sakina , Sebu na mkewe Tunu , Kazu na mkewe Bi. Temu.
- Wamo katika Club Pogopogo.
- Bogoa anawasimulia hadithi kuhusu jinsi alivyotolewa nyumbani kwao na kupelekwa kwa Bi. Sinai aliyemtesa sana.
4x1=4
- Toni ya huzuni- Bogoa anahuzunika anapokumbuka mateso yake mikononi mwa Bi Sinai
-
- Mpenda anasa – Sebu anasema kwamba yeye na Bogoa walikuwa wakienda mjini kucheza densi wakiwa na miaka kumi na minane.
- Karimu – anashirikiana na Kazu kuwanunua chakula Sebu, Bi.Tunu , Bi.Temu na Sakina.
- Mwenye mapenzi – Baba yake alipotaka kumpeleka mjini akaishi huko alilia kwa maana hakutaka kutengana na mama, baba, ndugu , kaka na dada zake.
- Mtiifu – anatii kila analoambiwa na Bi.Sinai . Kwa mfano , Bi. Sinai anapomtisha kuwa angemkata ulimi iwapo angefichua chochote kuhusu maisha aliyoyapitia nyumbani kwa Bi.Sinai.
- Msiri – aliteseka sana nyumbani kwa Bi. Sinai ila hakumwambia rafikiye Sebu licha ya kucheza naye. Aidha, hakuwahi kumtolea mkewe hadithi kuhusu masaibu aliyoyapitia nyumbani kwa Bi.Sinai.
- Mwongo – Bi. Sinai anapomchoma viganja kwa sababu ya kuacha mandazi kuungua anamhadaa Sebu kuwa aliungua akiepua maji moto.
- Mwoga – anaseama kwamba alimwogopa Bi. Sinai kwa sababu ya kumtisha kwamba angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yao ya ndani.
- Mwenye mawazo mapevu – Sebu anapomuuliza kwa nini hakumueleza masaibu yake nyumbani kwa Bi. Sinai, anamwambia kwamba hangeweza kufanya chochote kwa maana yeye alikuwa mtoto kama yeye.
- Mwenye kisasi - anapotoroka nyumbani mwa Bi. Sinai anaamua kurorejea nyumbani kwao na pia kutotaka kumwona mtu yeyote kwa sababu anaona kuwa masaibu aliyoyapitia nyumbani kwa Bi. Sinai yalisababishwa na wazazi wake.
6x1=6
-
- Inachimuza saula la umaskini – Wazazi wake Bogoa hawana uwezo wa kununua sabuni / Bogoa na baba yake wanatembea kwa miguu , bila ya viatu hadi mjini.
- Inaonyesha masaibu ya wanakijiji - Walikuwa na tatizo la maji kwa maana yalikuwa hayapatikani karibu . Walitembea masafa marefu kuyatafuta.
- Imemfumbulia Sebu fumbo alilotaka kufumbua – Amejua sababu ya Bogoa kutoroka nyumbani kwa Bi. Sinai.
- Kusawiri maudhui ya mapenzi – Mapezi ya Bogoa kwa nduguze na wazazi wake yalimfanya kutotaka kutengana na familia yake.
- Kusawiri maudhui ya elimu - Baba yake Bogoa anamwambia kwamba angepelekwa shuleni kusoma.
- Kuendeleza maudhui ya ajira ya Watoto – Bi. Sinai alimtumia Bogoa kufanya kazi za Nyumbani.
- Kuonyesha suala la ukiukaji wa haki za Watoto – Bi. Sinai anamtumia Bogoa kufanya kazi za nyumbani badala ya kumpeleka shuleni.
- Kuonyesha maudhui ya utabaka – Bi. Sinai anawaambia wanawe kwamba Watoto wa maskini hawastahili kusoma; kazi yao ni kutumwa.
- Kuonyesha maudhui ya uwajibikaji – Wazazi wake Bogoa walimtembelea ili kumjulia hali.
- Kuendeleza maudhui ya siri – Bogoa aliteseka sana mikononi mwa Bi. Sinai ila hakuwahi kumwambia rafikiye Sebu.
- Unajenga ploti/ msuko wa hadithi – Usimulizi wake unachimuza masuala kadhaa kama vile ukiukaji wa haki za Watoto umaskini n.k.
- Kubainisha masaibu ya Bogoa – Bi. Sinai hakumruhusu kutangamana na wazazi wake walipomtembelea, alikula makombo, anatusiwa, anasimbuliwa, anakatazwa kucheza na Watoto wengine.
xiii. Unajenga sifa za wahusika. Kwa mfano, ukatili wa Sinai unabainika kutokana na usimulizi huu. Sinai anamchoma Bogoa mandazi yalipoungua.
Swali la Dondoo 31
“Usiteketeze umati kama kuni zinavyoteketeza moto. Rudi, rudi kwa Mola wako.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
- Eleza tamathali mbili za usemi zinavyojitokeza katika dondoo hili (ala 2)
- Eleza madhara yanayotokana na vitendo vya mnenewa vya kuteketeza umma. (ala 8)
- Eleza umuhimu wa mnenaji wa maneno haya. (ala 6)
Majibu ya Dondoo 31
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (ala 4)
- Haya ni maneno ya mkumbukwa
- Alikuwa akimwambia Mkubwa
- Walikuwa nyumbani kwa Mkubwa
- Alimwambia maneno haya bada ya kutoka kororkoroni na akawa ameamua kuwachana na biasahara haramu ya kusambaza dawa za kulevya biashara aliyoajiriwa na Mkubwa
- Eleza tamathali mbili za usemi zinavyojitokeza katika dondoo hili (ala 2)
- Takriri- Rudi, rudi
- Tashibihi- Usiteketeze umati kama kuni
- Jazanda- kuteketeza umati
- Eleza madhara yanayotokana na vitendo vya mnenewa vya kuteketeza umati. (ala 8)
- Dawa za kulevya zinawadhoofisha kiafya vijana wanaozitumia. Tunaelezwa kuwa vijana wamekonda na kukondeana.
- Vijana wanaishia kuwa wezi ili wapate pesa za kununulia dawa za kulevya
- Vijana wengi wanakamatwa na kusalia korokoroni kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya
- Vijana wanaotumia dawa hizi za kulevya wanafanya vitendo vichafu vya kaumu luti kama wanyama
- Dawa za kulevya zinmawafanya watu wengi kupoteza maisha yao. Mkumbukwa anamweleza Mkubwa wazi kuwa watu wengi wanaangamia kutokana na matumizi ya dawa hizi za kulevya
- Dawa za kulevya zinawafanya vijana kuwa wapyaro. Kijana mmoja anamwuuliza mkubwa ikiwa walikula kwa babake na kumwita makande.
- Dawa za kulevya zinawafanya vijana kuwa mazuzu.
- Dawa za kulevya zinawafanya watu kukosa raha kwa ujumla
- Vijana wanatokwa na denda midomoni kutokana na matumizi ya dawa hizi za kulevya
- Watumizi wa dawa hizi wanasinzia mchana kweupe na hata kupatwa na ndoto za mchana.mfano kijana mmoja anaota akielekea kwa Obama na kudai kuwa Mkubwa amemkatizia safari yake. (Hoja zozote 8x 1 =ala 8)
- Eleza umuhimu wa mnenaji wa maneno haya. (ala 6)
- Ametumiwa kuonyesha watu wenye bidii maishani. Mkumbukwa anafanya kazi yake ya kumfanyia mkubwa kampeni hadi anapigiwa kura.
- Anawakilisha watu fisadi katika jamii. Anawahonga wapiga kura wakishirikiana na Bi. Kibwebwe.
- Anaendeleza maudhui ya usaliti. Mkumbukwa ana msaliti M,kubwa anapodinda kwendelea na biashara haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
- Ni kielelezo cha watu wanaoongozwa na tamaa na baadaye kujipata matatani. Tamaa yake ya kutajirika inamfanya kushiriki katika biashara ya uuzaji wa dawa za kulevya na baadaye anatiwa mbaroni.
- Ametumiwa kufichua uozo uliopo katika jela zetu. Pale watuhumiwa wanakaa katikas mazingira mabovu na hatass kupokwa chakula na walinzi.
- Anaonyesha watu wanaojutia matendo yao na kuuamua kubadilika maishani. Mkumbukwa anajutia kushiriki katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya na baadaye anaiasi biashara hiyo.
- Anawakilisha watu wapyaro kwenye jamii. Anamtusi mkubwa anapokuwa akiikataa kazi ya uuzaji wa dawa za kulevya.
Swali la Dondoo 32
“Na kwa nini hazitaki kuukemea mfumo huu wa maisha? Mfumo wa mwenye nacho kuendelea kupata na msinacho kuendelea kukosa?”
- Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
- Fafanua maudhui mawili yanayodhihirika katika dondoo hili (alama 4)
- Tambua na ueleze sifa sita za msemaji (alama 6)
- Eleza athari ya “msinacho kuendelea kukosa” katika jamii husika (alama 6)
Majibu ya Dondoo 32
- Mawazo ya Mashaka baada ya mkewe kumtoroka akiwaza kuhusu umaskini unaozikumba nchi za Kiafrika kama vile Kenya na Tanzania.
-
- Utabaka-anazungumzia mfumo wa mwenye nacho na msinacho kumaanisha matajiri na maskini.
- Umaskini-kuna watu maskini ambao anawarejelea kama msinacho
- Ubinafsi-kuna watu ambao wanaendelea kutajirika ilhali wengine wanaendelea kuselelea katika lindi la umaskini
(Zozote mbili: kutaja-alama moja, kueleza alama moja)
-
- Mwenye bidii-anafanya vibarua anui ili kukidhi mahitaji yake na Bi. Kidebe
- Msomi-anaelimika hadi chumba cha nane
- Mwenye kutamauka –mkewe anapomtoroka anatamauka kwani anasema kuwa amechoka kungoja
- Mwenye mapenzi-anampenda mkewe kwani anamlinganisha na ua la waridi
- Mwenye tamaa-anatamani mabadiliko ya kumtoa katika hali yake ya umaskini
- Mwenye mtazamo finyu-wanapata watoto wengi ilhali wanafamu kuwa hali yao ya kiuchumi haitawaruhusu kuwakimu
- Mvumilivu-anavumilia hali yake ya umaskini kwa muda mrefu
(Zozote 6×1=6)
- Athari ya umaskini:
- Utengano –Waridi anamtoroka Mashaka kwa misingi ya kuwa maskini
- Majuto-Mashaka anajutia hali yake ya umaskini na kutamani kuwa angekuwa tajiri kwani mkewe hangemtoroka
- Aibu-Mzee Rubeya-babake Waridi anatorokea Yemeni kwa vile bintiye ameolewa na mtu maskini
- Kukatiziwa elimu-Mashaka anaacha kundelea na masomo ya juu kwa kukosa pesa
- Ajira ya watoto-Mashaka akiwa na umri mchanga analazimika kufanya ajira ya watoto ili apate mahitaji yake
- Kutamauka-Katika ndoto, Mashaka anawaona wanyonge wakiandamana huku wakisema kuwa afadhali wafe
- Hali duni ya maisha-tunaelezwa kuwa makazi ya watu wa Tandale yalivyochafuka na kwamba hakuna mfumo mwafaka wa kusafisha
- Dharau-Mashaka anasema kuwa laiti angekuwa tajiri mkewe angemheshimu
Download Maswali na Majibu ya Dondoo katika Tumbo Lisiloshiba.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students