Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2008) Kiswahili Paper 3

Share via Whatsapp

(LAZIMA )      USHAIRI

 1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata. 

  WASAKATONGE

  1. Wasakatonge na juakali

  Wabeba zege ya maroshani,
  Ni msukuma mikokoteni,
  Pia makuli bandarini,
  Ni wachimbaji wa migodini,
  Lakini maisha yao chini.

  2.  Juakali na wasakatonge 

  Wao ni manamba mashambani, 
  Ni wachapa kazi viwandani, 
  Mayaya na madobi wa nyumbani,
  Ni matopasi wa majaani, 
  Lakini bado ni masikini

  3. Wasakatonge na juakali 

  Wao huweka serekalni, 
  Wanasiasa madarakani," 
  Dola ikawa mikononi, 
  Wachaguliwa na ikuluni,
  Lakini wachaguaji duni.

  4. Juakali na wasakatonge 

  Wao ni wengi ulimwenguni, 
  Tabaka lisilso ahueni,  
  Siku zote wako matesoni, 
  Ziada ya pato hawaoni,
  lakini watakomboka lini? 

  (Mohammed Seif Katib)

  1. "Shairi hili ni la kukatisha tamaa". Fafanua rai hii kwa kutoa mifano minne. (alama 4)

  2. Taja tamathali ya usemi iliyotawala katika shairi zima na uonyeshe mifano miwili ya jinsi ilivyotumika. (alama 3)

  3. Eleza umbo la shairi hili. (alama 5)

  4. Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari. (alama 4)

  5. Onyesha mifano miwili ya maadili yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 2)

  6. Eleza maana ya maneneo yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. (alama 2)

   1. Manamba

   2. Tabaka lisilo ahueni

    TAMTHILIA

    Jibu swali la 2 au la 3.

 2. Kithaka wa Mberia: Kifo Kisimani
  Ukitumia mifano, onyesha matumizi matano ya mbinu ya ishara kama ilivyotumiwa katika tamthilia ya Kifo Kisimani.  (alama 20)

 3. "Kwa hakika, mzazi hana kifani katika Butangi nzima. Na pengine hata katika ulimwengu mzima."

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

  2. "Watu waliojiita washauri wa mzee Bokono walikuwa si washauri halisi bali wanafiki waliomdanganya." Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano mitano. (alama 16)

   RIWAYA 

   Jibu swali la 4 au la 5 

   Z. Buhari: Mwisho wa Kosa.

 4. Wanawake katika riwaya ya Mwisho wa Kosa wamepewa nafasi ndogo katika masuala ya maendeleo ya kijamii." Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (alama 20)

 5. Eleza jinsi wahusika wafuatao wanavyoafiki anwani ya riwaya ya Mwisho wa Kosa: 
  1. Ali   (alama 10)

  2. Asha (alama 10)

   HADITHI FUPI

   K.W. Wamitila
   (Mhariri): Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine.

 6. "Umdhaniaye ndiye, kumbe siye."
  Kwa kurejelea hadithi zote tano katika diwani ya Mayai Waziri wa Maradhi na hadithi Nyingine, onyesha ukweli wa kauli hii. (alama 20)

           FASIHI SIMULIZI

 7. Fafanua sifa zozote kumi za mtambaji bora wa ngano. (alama 20)

 

          
         
          

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2008) Kiswahili Paper 3.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest