Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2008) Kiswahili Paper 2

Share via Whatsapp
 1. UFAHAMU
  Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
         Kuna aina kuu za hisia zinazotawala na kuongoza makala na kuongoza maisha ya mwanadamu: kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kunusa. Ni vigumu kusema ni hisia gani muhimu kuliko nyingine ingawa ni dhahiri athari kubwa humuangukia mahuluku asiyeweza kuona. Inasemekana kuwa mishipa ya fahamu inayounga ubongo na macho ni mikubwa zaidi kuliko mishipa ya fahamu inayounga ubongo na viwambo vya masikio. Na katika misha na nyendo za kila siku kuona hupewa uzito mubwa minghairi ya kusikia. Pengine basi sio ajabu, kama intakavyobainika punde baadaye, kuwa kazi nyingi za fasihi andishi zimeelemea mno katika hisia hii kana kwamba zile nyingine kuu hazipo kabisa. Hakika hili ni kosa. Maana kusikia, kugusa, kuonja na kunusa nako ndiko humkamilisha mwanadamu aweze kuyafaidi maisha yake. Na hata mbele ya sheria, ushahidi huweza kutolewa mintaarafu ya kusikia, kugusa, kuonja na kunusa alimradi shahidi awe amesikia, kugusa, kuonja na kunusa mwenyewe Ushahidi wa kuambiwa haukubaliwi.

  Kwa hivyo basi kazi ya sanaa ambayo itazituma fikira za msomaji zihisi kuona, kusikia, kuonja, kugusa na kunusa  matendo na mazingira yanayosimuliwa humpeleka msomaji huyo katika  mipaka na nyanja za juu za ufahamu na furaha.

  Kila hisia ina umuhimu wake kutokana na mazingira ya tukio linalohusika au kusimuliwa. Maana kazi zote za sanaa hutokana na matendo na maisha ya watu ambao katika matukio, visa na mazingira yao hutumia hisia zao zote tano ama kwa pamoja au kwa nyakati mbalimbali. Ili basi msomaji aweze kupata mandhari kamili, na hata yeye mwenyewe ashiriki kwa matukio yenyewe kwa kuchukia, kuonea huruma, n.k, muhimu kabla ya yote, apate hisia zote hizo tano. Kazi ya sanaa inayojihusisha na hisia moja tu au mbili huwa muflisi kisanii kwa vile inashindwa kuwasilisha mandhari za hali halisi kwa msomaji. Je, mara ngapi nyoyo zetu husononeka au kuripukwa kwa maya kwa sababu ya sauti ndogo tu ya ndege aliaye pekee nyikani, au nyimbo za zamani? Sauti ya ndege huweza kuleta majonzi ya miaka nyingi mno ya utotoni wakati ambapo mtu alifiwa na mzazi, ndugu, jamaa au sahibu wake. Kadhalika nyimbo ya kale huweza kuchimbua ashiki ya zamani baina ya wapenzi au kutonesha jeraha la masaibu na madhila yaliyopita. Na wala sio nyimbo na sauti ya ndege tu, pengine pia hata harufu ya maua huwa na kumbukumbu za nguvu kubwa mno.

  Licha ya yote hayo, matumizi ya hisia nyingi yanasaidia kujenga mandhari kamili ya tukio katika akili ya msomaji. Mathalan badala ya kuelezwa tu paliandaliwa chakula kizuri, msomaji anaelezwa vitu ambavyo vimeandaliwa pamoja na harufu yake. Au badala ya kuambiwa mtu fulani alikuwa na wajihi wa kutisha, huelezwa na kuelewa vyema zaidi kwa kuainishia jinsi pua, macho, rangi, nywele, mdomo na meno ya mtu huyo yalivyo. Na hivyohivyo kwa mifano mingine kadha wa kadha kama vile hasira na ucheshi. Kutokana na maelezo ya kutosha ya hisia, msomaji huweza kumuashiki janabi, au akadondokwa na ute kutamani chakula ambacho hakipo mbele yake.

  Na sio hivyo tu. Hisia zinazotumiwa huweza kumfanya msomaji atafakari zaidi. Ataweza kufikia uamuzi kuhusu picha zinazochorwa kutokana na hisia mbalimbali na wala sio kauli za mkatomkato za mwandishi kama ilivyogusiwa hapo juu. Kauli ya mkatomkato sio tu hudumaza sanaa, bali pia hudhalilisha hata akili ya msomaji: kwani umbuji wa mwandishi ni pamoja na kufanya matendo na mazingira anayoyasimulia yawakilishe na kuwakilisha fikra za wahusika wake na hata zake mwenyewe.

  Hivyo ni dhahairi kwamba hisia humsaidia msomaji kuzama katika matendo ya kuelewa fikra za mwandishi mwenyewe, asili na makazi yake, kuwadadisi na kuwaelewa wahusika wenyewe, n.k.  

           Makala kutoka:     Saffari A.J'Hisia Katika Fasihi Andishi'
                                     Katika Mulokozi, M.M na Mung'ong'o (Wah)
                                     (1993:33) Fasihi, uandishi na uchapishaji
                                     Dar-es-Salaam: Dar-es-Salaam Univ. Press 

  1. Taja na ueleze uwanja ambao hutilia mkazo hisia zote. (alama 3)

  2. Kwa mujibu wa kifungu hiki, ni nini matokeo ya kusistiza hisia ya kuona katika fasihi andishi? (alama 2)

   1. Mwandishi ana maoni gani kuhusu kazi  nzuri ya sanaa? (alama 2)
   2. Maoni hayo yana umuhimu gani? (alama 4)

  3. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika kifungu ulichosoma. (alama 4)

   1. muflisi kisanii ........................................................................................
   2. jeraha la masaibu ...................................................................................
   3. kumuashiki janabi ...................................................................................
   4. umbuji ....................................................................................................

 2. UFUPISHO

  Uchumi ya soko huria ni hali ya kiuchumi ambapo itokeapo amali, shughuli na harakati zote za kiuchumi ghairi ya zile ambazo ni za lazima kwa serikali au dola kama ulinzi, sheria na mpangilio mzima wa jamii, huwa huria kwa watu binafsi. Msingi wa soko huria, sifa kuu ya utandawazi, ni kuibua na kudumisha mazingira na hali zinzochochea na kumruhusu mtu yeyote kuongozwa na hawaa au matamanio ya kibiashara anayoyaona sawa pasi na hofu ya kuingiliwa na udhibiti wa serikali.

  Mazingira hayo yanawapa watu satua ya kufanya maamuzi kuhusu hatima yao ya kiuchumi, uamuzi kuhusu suala la ajira yao., matumizi ya mtaji - kipato na harija zake, na uwekezaji mzima. Suala mojawapo linaloibuka kuhusiana na mfumo wa soko huria ni kuweka mipaka bainifu na wazi baina ya amali na shughuli zinazohusishwa na serikali na zile ambazo huachwa huria na watu.  Kwa mfano inaaminiwa kuwa haki ya kuishi na kulindwa dhidi ya shambulizi, liwe la kijambazi au la kigaidi ni ya kimsingi ambayo haiwezi kuhusishwa na uwezo wa kiuchumi wa mtu binafsi. Aidha huduma za kimsingi za afya nazo zaingia katika kumbo hili. Ikiwa huduma hizi zitaachwa huria, pana uwezekano mkubwa kuwa zitaisha kuwa istihaki kwa wenye mtaji wa kipato cha juu tu. 

  Licha ya kuwepo kwa sheria au kanuni huria kutoka nyanja maalum, hutokea hali ambapo udhibiti wa kiserikali ni lazima. Hili hutokea pale ambapo ipo haja ya kuyalinda mazingira hasa kutokana na uchafuzi wa viwanda au tasnia. Aidha udhabiti huo ni lazima pale ambapo haki za watu wengine zinahusika: yaani ikiwa uhuru wa hata mtu mmoja unaadhirika kutokana na sera hizo, pana haja ya kuingilia ili kuisawazisha hali yenyewe.
   
  1. Andika kwa muhtasari maana ya uchumi wa soko huria kulingana na taarifa hii. (maneno 25 -30)                            (alama 5, 1 ya mtiririko)

  2. Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika aya ya pili na ya tatu. (maneno 70-75)      (alama 10, 1 ya mtiririko)


 3. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Tambua mzizi katika neno .........................................................................................(alama 1)
   "msahaulifu"

  2. Tunga sentensi ukitumia kivumishi cha nomino.                      (alama 1)

  3. Andika kinyume cha:
   Wasichana watatu wanaingia darasani kwa haraka. (alama 2)

   1. Fafanua maana ya"mofimu huru". (alama 1)
   2. Toa mfano mmoja wa mofimu huru. (alama 1)

  4. Tambua kiambishi awali na tamati katika neno alaye. (alama 2)

  5. Tumia kirejeshi -amba kuunganisha sentensi zifuatazo.
   1. Mwanafunzi yule ni mrefu.
   2. Mwanafunzi yule amepita mtihani. (alama 2)

  6. Sahihisha sentensi hii:
   Waya yangu imepotea .............................................................................................(alama 1)

  7. Taja aina ya yambwa iliyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo: 
   Mpishi amempikia mgeni wali vizuri.  (alama 1) 

  8. Neno "Chuo" lina maana "Shule inayotoa mafunzo maalum ya kazi fulani". 
   Tunga sentensi mbili kubainisha matumizi mengine mawili ya neno hili. (alama 2) 

  9. Ibadilishe chagizo ya mahali kuwa ile ya wakati katika katika sentensi ifuatayo:
   Mchezaji aliucheza mpira mjini Malindi. (alama 1)

  10. Eleza maana mbili ya sentensi: (alama 2)
   Yohana alimpigia Husha mpira.

  11. Kanusha: 
   Sisi tumemaliza kujenga nyumba ambayo ingalikuwa yake angalifurahi. (alama 1)

  12. Unda nomino kutokana na:
   1. Zingua .................................................................................... (alama 1)
   2. Tosa ..........................................................................................( alama 1)

  13. Ichoree vielelezo matawi sentensi: 
   Paka mdogo amelala mchungwani. (alama 4)

  14. Tumia kihusishi badalia kutunga upya sentensi hii:
   Mgeni  yupo katika nyumba.            (alama 1)

  15. Unda sentensi kutokana na neno "sahili" ..............................................................(alama 1)

  16. Eleza tofauti kati ya sauti [z] na [d]  (alama 2)

  17. Tambua aina ya kitenzi kilichopigiwa mstari katika sentensi.
   Mzee huenda anacheza kamari. (alama 1)

  18. Badilisha kiwakilishi kimilikishi kuwa kuwa kiwakilishi kionyeshi kaika sentensi:
   Chake kilipatikana chini. (alama 1)

  19. Tumia mfano mmoja mmoja kutofautisha baina ya sentensi sahili na ambatano. (alama 4)

  20. Tunga sentensi itakayodhihirisha kuwa matumizi ya kielezi cha nomino. (alama 1)

  21. Andika wingi wa: Mvua imebomoa nyumba ya jirani. (alama 1)

  22. Akifisha kifungu kifuatacho:
   huenda serikali iwazie kudhibiti  bei ya petroli hatuwezi kuyaruhusu makampuni ya petroli kuunyanyasa umma alisema waziri wa kawi bei ya petroli imeongezwa mara nne katika kipindi cha mwezi mmoja.         (alama 4) 

 4. ISIMU JAMII

  Eleza huku ukitoa mifano sifa tano za kimsingi zinazotambulisha sajili ya mazungumzo. (alama 10)

    

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kenya Certificate Of Secondary Education (KCSE 2008) Kiswahili Paper 2.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest