KCSE 2011 Kiswahili Paper 2 Questions with Marking Scheme

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU (alama 15)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
    Changamoto kubwa inayowakabili watu wengi katika mataifa yanayoendelea ni suala la chakula. Suala hili linaweza kuangaliwa katika sawia mbili tofauti. Kuna tatizo linalofungamana na uhaba wa chakula chenyewe. Uhaba huu unaweza kutokana na utegemezi mkubwa kwa zaraa kama nyenzo kuu ya uzalishaji chakula.

    Zaraa katika mataifa mengi hususan yanayoendelea, hutegemea mvua. Kupatikana kwa mvua huathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni. Matendo na amali za watu kama ukataji wa miti na uchafuzi wa mazingira huwa na athari hasi kwenye tabianchi hiyo. Mabadiliko ya tabianchi huweza kuvyaza ukame kutokana na ngambi ya mvua.

    Kibinimethali hutokea wakati mafuriko yanapotokea na labda kuyasomba mazao mashambani na kusababisha baa la njaa. Hali hizi mbili husababisha matatizo makubwa ya chakula na kuathiri pakubwa suala zima la usalama wa chakula. Ili kuzuia uwezekano wa kuwepo kwa shida hii, pana haja ya kuwepo kwa mikakati na sera kuhakikisha kuna usalama wa chakula. Kwa mfano, pana haja za kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua. Kwa pande mwingine, sharti zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.

    Changamoto nyingine inahusiana na usalama wa chakula chenyewe. Chakula kilichosibikwa na vijasumu au kwa njia nyingine ile huweza kumdhuru anayehusika. Msibiko wa chakula unatokana na vyanzo tofauti. Mathalan, uandalizi wa chakula kuchafuliwa na choo, kutozingatia mbeko za usafi, uaandaji wa chakula na kukiweka katika hali ya uvuguvugu kabla ya kukipakua – hali inayochochea ukuaji wa viini na ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.
    Ili kuepuka uwezekano wa kuadhirika, pana haja ya kuzingata usafi wa chakula na uandalizi unaofaa. Fauka ya hayo, vyombo vya uandalizi viwe safi, kanuni za usafi zifuatwe upikaji na uaandaji uwe kamilifu. Hali hii isipozingatiwa, siha za raia wenyewe zinaadhirika pakubwa.

    Maswali
    1. Taja aina mbili za kuangalia suala la chakula katika mataifa yanayoendelea. (alama 2)

    2. Taja hatua mbili zinazoweza kuchukuliwa kupambana na tataizo la chakula. (alama 2)

    3. Eleza jinsi nne tofauti namna chakula kinavyoweza kuwa si salama? (alama 4)

    4. Kwa nini inahalisi kukipakua chakula baada ya kukiandaa tu? (alama 1)

    5. Ni mapendekezo gani anayoyatoa mwandishi kuhakikisha kuwa chakula kinafaa? (alama 2)

    6. Eleza maana ya maneno haya jinsi ilivyotumiwa:
      1. Ngambi ya mvua ………………………………………………………..
      2. Adha …………………………………………………………………….


  2. MUHTASARI

    Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili. Uwazaji huu umekitwa kwenye kwenye matumizi ya michakato kama makini, upangiliaji, uteuzi na tathmini. Hata hivyo, uwazaji huu si mchakato mwepesi bali ni mchakato changamano.
    Mchakato wa uwajazi tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti. Mathalan, kuweza kutambua na kubainisha misimamo ya watu wengine, hoja wanazozua na uamuzi waliofikia, kutathmini au kupima ushahidi uliopo ili kubainisha mitazamo tofauti. Vilevile uwazaji tunduizi hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki pamoja na kutambua yaliyofichwa au ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu. Hali kadhalika, uwazaji tunduizi hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia misimamo fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi. Aidha, uwazaji huu huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi kufikia uamuzi kama hoja zinazotumiwa zina mashiko au zinakubalika kuwa nzuri. Zaidi ya hayo kuna uwazaji tunduizi unahusisha kuwasilisha mtazamo kwa njia yenye uwazaji mzuri na inayoshawishi.

    Uwazaji tunduizi una manufaa anuwai. Mosi, unasaidia kujenga makini ya utendaji. Pili, hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya usomaji huo uwe na malengo wazi. Fauka ya hayo, unamsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katika matini au ujumbe fulani bila ya kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni. Uwazaji huu unasaidia kuchonga uwezo wa kuikabili na kuiitikia hali fulani na kukuza stadi za uchanganuzi. Mwanadamu huwa mtu tofauti na bora anapoujenga na kuuimarisha uwazaji tunduizi wake.

    Maswali
    1. Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwanzo. (Maneno 70 – 80) (alama 10; alama 2 za utiririko)
    2. Andika kwa muhtasari mambo muhimu katika aya ya tatu. (Maneno 35 – 40) (alama 5; alama 1 ya utirirko)


  3. MATUMIZI YA LUGHA.

    1. Tumia mzizi ‘-enye-‘ katika sentensi kama: (alama 2)
      1. Kivumishi ……………………………………………
      2. Kiwakilishi …………………………………………..

    2. Andika sentensi ifuatayo katika ukubwa:
      Paka mweusi amenasw mguuni. (alama 2)

    3. Taja mfano mmoja wa sauti zifuatazo:
      1. Kiyeyusho ……………………………………………
      2. Kimadende ………………………………………….. (alama 1)

    4. Onyesha shamirisho kitondo, kipozi na ala katika sentensi ifuatayo.
      Kipkemboi alimbebea mwalimu mzigo kwa gari. (alama 3)

    5. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali.
      Maria alipika taratibu huku mama akimwelekeza vizuri. (alama 4)

    6. Nomino ‘furaha’ iko katika ngeli gani? (alama 1)

    7. Andika kinyume cha sentensi:
      Watoto wameombwa waanike nguo. (alama 2)

    8. Andika sentensi ifuatayo upya kufuata maagizo uliyopewa.
      Mama alishangilia arusi ya mwana.
      Anza: Mwana ……………………………………………. (alama 2)

    9. Tumia kirejeshi ‘O’ katika sentensi ifuatayo.:
      Mtu ambaye hutupa tope hujichafua mwenyewe. (alama 2)

    10. Kanusha sentensi ifuatayo:
      Mgonjwa huyo alipona na kurejea nyumbani. (alama 2)

    11. Ainisha vihusishi katika sentensi:
      Ame aliwasili mapema kuliko wengine halafu akaondoka. (alama 2)

    12. Tunga sentensi mbili kuonyesha maana tofauti za neno “chuma”. (alama 4)

    13. Unda nomino kutokana na kitenzi ‘tafakari’ ……………………….(alama 1)

    14. Eleza maana mbili za sentensi:
      Tuliitwa na Juma. ………………………………………. (alama 2)

    15. Ainisha viambishi katika kitenzi:
      Tutaonana ………………………………………………… (alama 2)

    16. Tunga sentensi moja ukitumia kiunganishi cha kinyume. (alama 2)

    17. Huku ukitoa mifano eleza miundo miwili ya silabi za Kiswahili. (alama 2)

    18. Akifisha kifungu kifuatacho.
      Mzee alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwa babu yako angalau umjue mtoto aliuliza nani babu? (alama 4)

  4. ISIMU JAMII
    1. Bainisha changamoto tano zinazoikabili lugha ya Kiswahili kama somo katika shule za upili nchini Kenya. (alama 5)

    2. Eleza namna tano za kukabiliana na changamoto ulizozibainisha hapo juu. (alama 5)

MAAKIZO

  1.  UFAHAMU  
    1.    
      1. Uhaba wa chakula/Ukosefu wa chakula/Upungufu wa chakula
      2. Usalama wa chakula chenyewe
        (Hoja 2 x 1=2)
    2.      
      1. Kuwepo kwa mikakati ya kuhakikisha kuna usalama wa chakula/kukuza kilimo cha umwagiliaji ili kuepuka adha inayosababishwa na ukosefu wa mvua/zichukuliwe hatua mufidi za kuzuia na kupambana na athari za gharika.
      2. Kuwepo kwa sera za kuhakikisha kuna usalama wa chakula
        (Hoja 2 x 1 = 2)
    3.     
      1. Uandalizi wa chakula kilichochafuliwa na choo;
      2. Kutozingatia mbeko za usafi; 
      3. Kukiandaa chakula na kukiacha katika hali vuguvugu kabla ya kukipakua; (iv)
      4. Ulaji wa chakula kisichoandaliwa vyema.
        (Hoja 4 x 1 = 4)
    4. Kuzuia hali inayochochea ukuaji wa viini/kuhakikisha kuwa chakula hakitakuwa na viini
    5.        
      1. Pana haja ya kuzingatia usafi wa chakula;
      2. Uandalizi unaofaa;
      3. Vyombo vya undalizi viwe safi;
      4. Kanuni za usafi zifuatwe;
      5. Upikaji na uandalizi uwe kamilifu.
        (Hoja 4 x 1 =4)
    6.      
      1. Ngambi ya mvua --Uhaba, upungufu, shida, ukosefu, uchache
      2. Adha - Shida, kero mashaka, usumbufu, dhiki, matatizo, taabu, janga
        (Hoja 2 x 1 = 2)
        • Kuadhibu
          • Ondoa alama 3 za makosa ya hijai yanapotokea kwa mara ya kwanza, yaani 12 alama hadi kufikia makosa 6.
          • Ondoa 2 alama kwa kila kosa la sarufi kufikia 1/2 ya alama alizopata katika kila kisehemu.
  2. MUHTASARI
    1.          
      1. Uwazaji tunduizi ni tendo ambalo huhusisha matumizi ya akili.
      2. Umekitwa kwenye mizizi ya michakato kama makini, upangiliaji, uteuzi na tathmini.
        Au
        Umekitwa kwa mizizi ya michakato mbalimbali.
      3. Uwazaji si mchakato mwepesi.
        Au
        Uwazaji ni mchakato changamano
      4. Uwazaji tunduizi unahusisha stadi na mikabala tofauti.
      5. Hushirikisha kupima hoja za upinzani na ushahidi uliopo kwa njia ya haki/ukweli uliofunikwa na taswira ya juu juu.
      6. Hujumuisha kutambua mbinu zinazotumiwa kufikia msimamo fulani kwa mvuto zaidi na kwa matumizi ya mbinu za kishawishi.
      7. Huhitaji kutathmini masuala kwa mtindo ulio wazi kufikia uamuzi.
      8. Huhusisha kuwasilisha mtazamo kwa njia yenye uwazaji mzuri na inayoshawishi.
        (Hoja 8 x 1 = 8)
    2.     
      1. Unasaidia kujenga makini ya utendaji
      2. Hupevusha uwezo wa usomaji kwa kuufanya uwe na malengo wazi
      3. Humsaidia mtumiaji kutambua hoja kuu katika matini/kutambua ujumbe fulani bila kuzongwazongwa na hoja duni za pembeni
      4. Unasaidia kuuchonga uwezo wa kuikabili hali fulani/unasaidia kuitikia hali fulani.
      5. Unasaidia kukuza stadi za uchanganuzi.
      6. Binadamu huwa mtu tofauti na bora anapojenga na kuuimarisha uwazaji tunduzi wake.
        (Hoja 6 x 1 = 6) .
        • Mtindo wa kutuza
          KisltCS2011p2qa2b
        • Kuadhibu
        • Ondoa makosa 6 ya hijai yotokeapo mara ya kwanza kwa kuadhibu k alama kwa kila kosa yaani alama 3 Ondoa alama 3 kwa makosa 6 ya mwanzo ya sarufi(s)
        • Ondoa alama 1 kwa ziada (z) ya maneno 10 ya mwanzo kisha endelea kuondoa 2 alama kwa kila ziada ya maneno 5 hadi mwisho wa jibu lake
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.              
      1. Mfano - Mwanafunzi mwenye tabia nzuri hupendeza
      2. Mfano - Mwenye gari amewasili
        Mwenye kula kwa pupa hafaidi utamu
        Amesema lenye maana
        (Hoja 1 x 2 = 2)
    2.            
      1. Paka jeupe limenaswa guuni.
      2. Jipaka jeupe limenaswa jiguuni.
      3. Paka jeupe limenaswa jiguuni.
      4. Jipaka jeupe limenaswa guuni.
        (Alama 1 x 2 = 2)
    3.         
      1. /y/na/w
      2. /r/
        (Alama 12 x 2 = 1)
    4. Kitondo - Mwalimu
      Kipozi -Mzigo
      Ala -Gari
      (Alama 1 x 3 = 3)
    5.    
         S    
        S1  U S2
      KN KT    KN KT
       N  T  E  N  T  E
      Maria  alipika  taratibu huku mama akimwelekeza vizuri
        
    6. 1-1
      (Alama 1 x 1 = 1)
    7.      
      1. Neno watoto lisibadilike - Likibadilishwa ondoa 11 alama
      2. Wameombwa
        • Wameamrishwa
        • Wamelazimishwa
        • Wameshurutishwa
      3. Waanike - Waanue (Alama 2 x 1 = 1)
    8.        
      1. Mwana alishangiliwa arusi na mama.
      2. Mwana alishangiliwa arusi yake na mama.
      3. Mwana alishangiliwa arusi na mamake.
        (Alama 2 x 1 = 2)
    9.    
      1. Mtu atupaye tope hujichafua mwenyewe.
      2. Mtu anayetupa tope hujichafua mwenyewe.
      3. Mtu atupaye tope ndiye ajichafuaye/mwenyewe.
      4. Mtu anayetupa tope ndiye anayejichafua.
      5. Mtu ajichafuaye mwenyewe ni yule atupaye tope.
        (Alama 2 xl=2)
    10.     
      1. Mgonjwa huyo hakupona wala kurejea nyumbani.
      2. Mgonjwa huyo hakupona na hakurejea nyumbani.
      3. Mgonjwa huyo hakupona wala hakurejea nyumbani.
      4. Mgonjwa huyo hakupona na kurejea nyumbani.
        (Alama 2 x 1 = 2)
    11.     
      • Kuliko: Kihusishi kilinganishi
      • Halafu: Kihusishi cha wakati
        (Alama 1 x 2 = 2)
    12. Chuma : Madini, mtu mwenye nguvu nyingi, tungua/tundua, tafuta mali. * Sentensi zidhihirishe maana mojawapo ya hizo zilizoelezwa. (Mbili zozote 2 x 2 = 4)
    13. Tafakuri, kutafakari, utafakari. (Alama 1 x 1 = 1)
    14.         
      1. Juma alituhitaji kwenda kwake.
      2. Mimi pamoja na Juma tuliitwa na mtu fulani.
      3. Sisi pamoja na Juma tuliitwa na mtu fulani.
      4. Juma aliwaita watu wengine kwake.
      5. Watu wengine pamoja na Juma waliitwa na mtu fulani.
        (Alama zozote 1 x 2 = 2)
    15.        
      1.      
        • tu - Kiambishi cha nafsi ya kwanza wingi 
        • ta - Kiambishi cha wakati ujao
        • on - 
        • an - Kiambishi cha mnyambuliko au kauli ya kutendana
        • a - Kiishio (kauli tenda)
          Au
      2.    
        • tu - Viambishi awali
        • ta 
        • an - Viambishi tamati (alama 1 kwa kila kiambishi)
        • a  (1 x 4 = 4)
    16. Viunganishi vya kinyume - lakini, ijapokuwa, japo, ingawa, ila, bali, ilhali, hata kama hata hivyo (Alama 2 x 1 = 2)
    17.        
      1. Irabu pekee - kwa mfano - O-a
      2. Konsonanti pekee - kwa mfano - m tu
      3. Konsonanti na irabu - kwa mfano ba - ba
      4. Konsonanti konsonanti irabu - kwa mfano -mba-vu
      5. Kiyeyusho na Irabu wa-ya
        (Mbili zozote, alama 1 x 2 = 2)
    18. Mzee alimwambia mwanawe, “Njoo nikupeleke kwa babu angalau umjue." Mtoto aliuliza, "Nani babu?"(Alama 4)
  4. ISIMUJAMII
    1.      
      1. Kukua na kuenea kwa lugha ya Sheng'.
      2. Watu wengi kutothamini lugha ya Kiswahili.
      3. Watu wengine kutawaliwa na kasumba ya kigeni hadi kupenda Kiingereza na lugha zingine za kigeni na kudunisha Kiswahili.
      4. Vyombo vya mawasiliano vinapotosha Kiswahili sanifu.
      5. Shughuli nyingi shuleni zafanyika kwa Kiingereza.
      6. Lugha ya Kiingereza kutumika kufunzia masomo mengi. Kiswahili kinafunza lugha ya Kiswahili tu.
      7. Ukosefu wa walimu waliofuzu katika Kiswahili katika baadhi ya shule
      8. Ukosefu wa vitabu katika baadhi ya shule
      9. Vipindi vichche vya kufunza Kiswahili
      10. Uhaba wa wakaguzi na waelekezaji waliohitimu katika Kiswahili
      11. Athari za lugha ya kwanza.
      12. Kutohusishwa kwa lugha ya Kiswahili katika masuala ya kisayansi na teknolojia.
        (zozote 5 x 1 = 5)
    2.     
      1. Kuwahimiza vijana kutumia lugha mwafaka ya Kiswahili kutegemea muktadha
      2. Kuwahimiza wanafunzi kukionea Kiswahili fahari
      3. Kiswahili kiwe lugha rasmi na kitumiwe katika shughuli zote za kiserikali
      4. Kuundwa kwa asasi ya kudhibiti matumizi mwafaka ya Kiswahili kwenye vyombo vya mawasiliano
      5. Sera bora za matumizi ya Kiswahili shuleni ili kukipa Kiswahili hadhi sawa na Kiingereza
      6. Kuweka sera ambapo Kiswahili kitatumika kufundishia baadhi ya masomo kama vile dini, stadi za kimaisha, ujasiri na kadhalika
      7. Serikali kuhakikisha kuwa imewaajiri walimu wa Kiswahili waliohitimu katika shule zetu zote
      8. Mashirika ya uchapishaji yachapishe vitabu vingi kwa lugha ifaayo na kwa gharama nafuu
      9. Vipindi vya kufundishia Kiswahili viongezwe
      10. Serikali ihakikishe kuwa kuna wakaguzi wa kutosha kukabiliana na idadi ya shule zinazozidi kuongezeka 
      11. Matumizi yafaayo ya lugha ya Kiswahili yahimizwe kuanzia shule za msingi
      12. Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika masuala ya kisayansi na teknolojia (zozote 5 x 1 = 5)
        • Kuadhibu
        • Ondoa ½ alama kwa kosa la hijai (h) litokeapo kwa mara ya kwanza hadi kufikia makosa 6; yaani alama 3 katika swali zima.
        • Ondoa ½ alama kwa kosa la sarufi(s) litokeapo mara ya kwanza hadi kufikia makosa 6, yaani alama 3 katika swali zima. 
Join our whatsapp group for latest updates

Download KCSE 2011 Kiswahili Paper 2 Questions with Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest