KCSE 2011 Kiswahili Paper 3 Questions with Marking Scheme

Share via Whatsapp

SEHEMU A: TAMTHILIA

KITHAKA WA MBERIA: Kifo Kisimani
  Swali la lazima

  1. “Alijiona pwagu. Lakini Butangi ina pwaguzi pia.”
    Eleza tofauti baina ya wahusika wanaoejelewa. (alama 20)

    SEHEMU B: RIWAYA
    S.A MOHAMED
    : Utengano
    Jibu swali la 2 au la 3

  2. Eleza mbinu zifuatazo zizlivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Utengano:
    1. Kwelikinzani
    2. Sadfa (alama 20)

  3. “Uhuru alioutaka na ulimwengu alioufahamu Maimuna umemdhuru hatimaye.”
    Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (alama 10)

    SEHEMU C: USHAIRI
    Jibu swali la 4 au la 5

  4. KUJITEGEMEA

    1 Nchi ni ile ambayo, imekuwa ardhini
    Siyo ile iombayo, ghaibu na majirani
    Taratibu siyo hiyo, wanachi twambizaneni
    Daima kukaa chini, maganja ya upewaji

    2 Chumo lote la mitaji, leo limo maganjani
    Bepari na wanyonyaji, wasalie maguguni
    Shime utekelezaji, vingine havifanani
    Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

    3 Twaishije tujihoji, wanachi humu nchini
    Kila tunachohitaji, kupatakwe ugenini
    Hiyo ni tete haviji, tongo tupungusaneni
    Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

    4 Kuomba wataalamu, ni mwendo haulingani
    Tupate wa humu humu, wajuzi wa kila fani
    Mbele washike hatamu, kwa mapimo na makini
    Daima hukaa chini, maganja ya upewaji

    5 Tuufuate wongozi, pamwe na nyingi imani
    Tushiriki kila kazi, na mambo yaliyomkini
    Mikopo ina kinyezi, si kitu cha tumaini
    Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

    6 Yote huyatimizi, alotimiza ni nani
    Lakini tuwe maizi, tusizurure mijini
    Tukamshabihi cozi, kipanga au kunguni
    Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

    7 Shujaa itakiwavyo, aonekane vitani
    Na sisi vita tunavyo, roho kwa roho ugani
    ‘Kutegemea’ vilivyo, kondo tujiamueni
    Daima hukaa chini, maganja ya mpewaji

    Boukhet Amana: Malenga wa Mrima
    Mwinyihatibu Mohammed
    Oxford University Press
    1977


    1. Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani? (alama 2)

    2. Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu moja. (alama 2)

    3. Eleza maneno matatu ambayo mshairi anashauri nchi ifanye ili kujitegemea. (alama 3)

    4. Taja aina moja ya idhini ya kishairi iliyojitokeza kwa wingi zaidi katika shairi na utoe mifano mitano ya matumizi yake. (alama 7)

    5. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)

    6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kamaa yalivyotumiwa katika shairi.:
      1. Ghaibu
      2. Tukamshabihi (alama 2)


  5. HAKI

    1. Haki watatuitisha, usikuandame, kwa matendo yetu,
    Watukorofisha, tusikwandame, kila penye kitu,
    Mbona watugwisha, mwiba ituchome, kwenye huu mwitu,
                         Tutokwe na utu!

    2. Hatukukufanya, mwana kwa mvyele, aliyemzaa,
    Haki watunyima , machumi ya mbele, na nyingi hadaa,
    Tuchumayo nyanya, uchungu umbele, hatuna wasaa,
                       Haki twashangaa!

    3. Na kambi nzima, kunaiyenea, hasa hapa petu,
    Tukatazamana, kwa kuuliza, kuweza thubutu,
    Na kwenye milima, ilotueka kupandia watu,
                     Usipande katu!

    4. Sio hao mabwana, walioteuliwa, kupata mwangaza,
    Haki wakubana, liliotarajiwa, kwenye hichi kiza,
    Ndevu kuchomana, wengine kuliwa, tukijiingiza,
                  Kambi yatuviza!

    5. Haki huna njia, kizuizi mali, ndio njia panda,
    Tukiifatia, hatufiki mbali, tunaganda,
    Sio yetu nia, lakini akili, mali ishapenda,
                 Haki yatuponza!

    6. Wala hutasemwa, sababu ni nyoyo, kisha haribika,
    Ya mali kuchumwa, vyovyote iwavyo, itakavyopatika,
    Wakati mtumwa, ushatumwa ndivyo, na ushatufika,
                Kwetu ni mashaka!

    7. Haki hufanyiki, paitapo mambo, na vikubwa visa,
    Watu hawataki, kutenda kijambo, tunu yao pesa,
    Sisi kwetu dhiki, yatunisha tumbo, wao hata hisa,
                  Na ndio ya sasa!

    8. Haki husimami, kwa viumbe sisi, tuvyojaaliwa,
    Na huna ulimi, kuweza tukisi, tukageukiwa,
    Zama za uchumi, zishashika kasi, nguvu zishapewa,
                  Haki wauliwa!

    9. Iwe hivi haki, hakuna mmoja, akukumbukae,
    Hatuna ashiki, kuvuta la haja, haki ituvae,
    Mbona hatutaki, twalia na tija, haki iambae,
                  Haki tamati!

                     Suleiman A. Ali:
                      Malenga Wapya


    1. Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 2)

    2. Huku ukitoa mfano, eleza aina ya shairi hili. (alama 3)

    3. Taja na ufafanue tamathali ya usemi inayotawala katika shairi hili. (alama 3)

    4. Kwa kutoa mfano mmoja mmoja, onyesha aina tatu za idhini ya kishairi katika shairi hili. (alama 6)

    5. Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)

    6. Mshairi ana maana gani kwa kusema:
      1. Kambi yatuviza
      2. Kuweza kutukisi (alama 2)

        SEHEMU D: HADITHI FUPI

        K. W. WAMITILA
        : Mayai Waziri Wa Maradhi na Hadithi Nyinginezo.

        Jibu swali la 6 au la 7


  6. “Cheche ndogo hufanya moto mkubwa.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

    2. Fafanua maudhui manne yanayohusiana na chanzo cha tukio linalorejelewa katika dondoo hilo. (alama 8)

    3. Eleza matokeo manne ya tukio linalorejelewa katika dondoo. (alama 8)

  7. “Mganga na wateja wake wote wlikosa busara.” Fafanua ukweli wa kauli hii kwa mifano kumi kutoka hadithi ya ‘Siku ya Mganga.’ (alama 20)

    SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

    1. Eleza maana ya malumbano ya utani. (alama 2)

    2. Bainisha sifa nne za malumbano ya utani. (alama 8)

    3. Fafanua majukumu matano ya malumbano ya utani katika jamii. (alama 10)

MAAKIZO

  1. KIFO KISIMANI(LAZIMA) SEHEMU YA A
    • Pwagu ndiye Mwelusi na pwaguzi ni Gege. Wahusika hawa ni watoto wa mama mmoja lakin walitofautiana. Mtahiniwa pia anaweza kutambulisha dondoo - Maneno haya yanasemwa na Gege kwa {Batu) kuhusu Mwelusi/ wanaorejelewa ni Mwelusi na Gege. (maelezo)
    • Pwanguzi pia anaweza kuwa Bokomo
      Mwelusi Gege
      -Alikuwa na mitazamo maalumu kuhusu maisha. Amezinduka k.m Anawachochea watu kususia mkutano. -Alikuwa na mtizamo finyu kuhusu maisha /kwake maisha bora ni kuoa mke na kupata watoto wake mwenyewe.
      -Alifikiria hali ya umma wa Butangi/ mazingira; maji. -Fikira zake zilifungwa na mahitaji yake ya kibinafsi/ ya kimsingi k.v kuwvutia wasichana
      -Alikuwa na msimamo thabiti kuhusu mambo/ anakataa vishawishi vya Batu. -Alikubali kushawishiwa na Mweke na Talui akamuua Mwelusi.
      -Aliwaheshimu watu, mfano kumtaja Kaloo kwa jina la mama. -Aliwakosea watu heshima hasa mamake, anajibizana naye.
      -Alikuwa na mahusiano mazuri na wanawake k.m Atega, walifanya kazi kwa pamoja/ uhusiano wa kisiasa. -Aliamini maisha yalikuwa ni wanawake kumpa sifa/ raha na kuoa.
      -Alikuwa mwanaharakati aliyepigania ukombozi wa raia k.m kuteswa gerezani -Nia yake ni kujikomboa kiuchumi.
      -Aliwajali watu wengine/ kuhakikisha wanapata maji -Alijijali yeye mwenyewe/ ana ubinafsi. Anatengneza ala badala ya kwenda kumtembelea Mwelusi.
      -Alifahamu ukweli wa mambo kuhusu haki za wananchi/ alipinga utawala wa Bokono. -Aliunga mkono utawala wa Bokono.
      -Mzalendo - Anakataa kutoroka Butangi. -Ni mzalendo wa kijinga (Msaliti). Anausaliti udugu wake kwa Mwelusi kwa kumuua.
      -Jaşiri - hata anapoteswa gerezani anakataa kusema anampenda Bokono. -Mwoga - anpoitwa na Mweke anadhani anaitiwa adhabu.
      -Mwenye utu - anawazia Butangi vyema (usalama, amani, maendeleo, chakula. -Katili - anainuua Mwelusi.
      -Mwenye maarifa/ busara -- aligundua ujanja wa Batu alipomwambia atatuzwa. -Mjinga - alidanganywa kwa urahisi kuwa atamwoa Alida/ anakubali ahadi ambazo hajaziona.
      -Mpenda mabadiliko/ mwanamapinduzi, -Mhafidhina - anataka utawala wa Bokomo uendelee.

      -Mkweli -- Anamwambia Gege kuwa kuwaza xiv) kuwa maisha ni kuoa na kupata watoto ni kujitia katika kiwango cha nyani..

      -Mnafiki/ mwongo - anamdanganya mamake kuwa sasa hana kinyongo na Mwelusi.

    • Maana ya Pwagu na Pwaguzi; ni kuwa kuna mwizi na kuna mwizi stadi. Pwagu hushindwa na pwaguzi; Bokono alimuua Mwelusi hatimaye ambaye alikuwa ndiye pwagu.(maelezo)
      Mwelusi Bokomo 
      Kujali masilahi ya Wanabutangi km kuhakikisha wamepata maji. Kuwakandamiza. K.m. kuwanyima maji.
      Ni Mzalendo halisi. Anateswa gerezani lakini haikani Butangi Ni msaliti/mzalendo hasi. Kutawala kwa mabavu. Wapende wasipende.
      Alijali mazingira . km ukataji miti, maji.  Aliruhusu miti kukatwa na mmomonyoko wa udongo kuongezeka.
      Alipenda haki: wazalendo wapewe maji. Alikiuka haki za wanabutangi k.m. kumfungia Mwelusi gerezani.
      Mkweli: anasema Butangi haiongozwi
      vyema.
      Mwongo: anasema anapendwa, kina Batu wanasema sifa za uongo kumhusu.
      Heshima kwa wanawake. K.m. Alifanya kazi pamoja na Atega/ kisiasa. Ana jicho la nje k.m. kumtamani Kaloo; ana hawara; yule mwananke aliyepigwa na Nyalwe.
      Jasiri: kukataa kusema anampenda Bokono anapopigwa. Mwoga; anaota ndoto za kuzikwa akiwa hai, anaweka mikakati ya kumuua Mwelusi.
      Mwanaharakati wa kukomboa nchi yake.
      Anataka Butangi yenye uswa kwa
      wote.isiyo na bughudha.
      Kukandamiza wananchi k.m. anatumia propaganda eti anapenda watoto na huku anagawa kiwanja chao cha kuchezea.
      Anajali masilahi ya umma. Anakubali
      kuteswa ili awakomboe.
      Anakataa kuwasikiliza raia. Anasema Mama Agoro asiende kumwona, anakubali uwanja wa watoto kuchukuliwa.
      Angelitaka haki itendeke kwa kila mwanabutangi (usawa). Angelipenda kuwafaidi wachache. Anawakinga wahalifu kama vile Askari II.
      Maarifa/ busara - aligundua ujanja wa Batu alipokuwa gerezani. Mjinga - alikataa/ pinga ushauri wa Nyalwe/ kuwa aache uongozi mbaya.
  2. UTENGANO. SEHEMU YA B
    1. Kwelikinzani
      1. Kwelikinzani -- (maelezo) mbinu ya kuonyesha maneno yanayojipinga yenyewe lakini ukichunguza yana ukweli fulani. Usahihishaji pia ulilkubali maelezo ya kinaya
      2. Maimuna kujifanya anachagua kuwa huru ilhali uhuru wenyewe haumsaidii. Anajikuta taabani hata akiwa nje ya kasri
      3. Maksuudi kudai awapenda na kuwajali wanajamii na familia kuwa awasaidia huku anawaibia na kuwatesa.
      4. Maksuudi kujifanya mwanadini muumini kiasi cha kwenda kwa ibada huku anatenda maovu (km usherati, ufisadi)
      5. Kazija mwanzoni anachorwa kama kwamba anawachukia wanaume huku akiwa anajitayarisha kumpokea mmoja wao na hata anampokea Mussa papo hapo.
      6. Wanasiasa wanadai kuwa wanajali umma: watawasaidia raia lakini walikuwa wanajitakia makuu – mfano Maksuudi/ Zanga.
      7. Ndugu wawili Inspekta Fadhili na Maksuudi/wanachorwa kuwa ndugu lakini mahusiano yanaonyesha kinyume. Damu hapo si nzito kuliko maji. Uk. 76 (kufukuzwa kwa Inspekta Fadhili/ makaribisho)
      8. Maksuudi kudai kuwa anampa Inspekta pesa za bure kuwa hamna kosa la kufichwa (makosa ya jinai) alikuwa na hatia.
      9. Kazija kumkaribisha Maksuudi na kusema mambo ni shwari lakini amempangia mabaya.
      10. Biti Kocho kudai Maimuna ametafutwa kote kote ilhali anajua alipo Maimuna.
      11. Farashuu kumtorosha Maimuna na mwishowe Maimuna kuolewa na mjukuu wake Kabi,
      12. Maksuudi kukataa na kitoto eti kitakufa njaa na mwishowe kinafia kwake.
      13. Maksuudi alipokuta kitoto kimezaliwa, badala ya kufurahia anainchapa na kumtaliki Tamima.
      14. Kitoto cha Maksuudi kinapozaliwa kuonjeshwa shubiri na asali.
      15. Maimuna kuambiwa na Biti Kocho mapenzi ni kitu kizuri ilhali mapenzi ya wazazi wao ni majonzi.
      16. Dunia ni kitu si kitu ..... Maneno ya mwandishi Maksuudi anapoenda pale hospitalini.
        Zozote 5 x 2 = 10
    2. Sadfa
      1. (Maelezo) Kutokea kwa mambo mawili kana kwamba yamepangwa ilhali hakuna matayarisho wala maagano ya namna yoyote.
      2. Maksuudi kurejea nyumbani bila kutarajiwa kisha anapata mtoto amezaliwa (Bi. Tamima amezalishwa)
      3. Kazija kama mwanamke kuwepo mkutanoni kisha akainuka na kumwuliza maswali Maksuudi.
      4. Maksuudi hakutarajia kukutana na Mussa kule kwa Kazija, pia Mussa hakutarajia.
      5. Mussa, Maimuna, Tamima na Maksuudi wanapokutana mwishowe.
      6. Maksuudi kukutana na Mussa akiwa daktari.
      7. Farashuu kukutana na Maimuna mara ya kwanza kule kwake wanapotafuta Mkunga.
      8. Farashuu akishuhudia kuchumbiana kwa Maimuna na Kabi./ Farashuu ndiye alimtorosha Maimuna na hakutarajia aolewe na Kabi. 
      9. Simu kupigwa nyumbani mwa Maksuudi huku Inspekta Fadhili yupo na alikuwa anaendelea na uchunguzi.
      10. Kusambaratika kwa familia ya Maksuudi kutokea usiku mmoja.
      11. Rashid kuona tangazo gazetini kuhusu Maimuna kule Rumbalola wakati Maksuudi alikuwa anamtafuta.
      12. Maulidi kumsikia Maimuna akiimba na kumpa kazi ya uimbaji huko Rumbalola..
      13. Bi. Tarima kushikwa na uchungu wa uzazi na Farashuu kuitwa kuwa mkunga.
      14. Kabi kukutana na Maimuna Futoni na kupendana na kuoana ilhali wana uhusiano wa kutoka Liwazoni. (kihistoria).
      15. Maimuna kukutana na Kabi wakati anatafuta kitoweo na Kabi kumpa samaki.
      16. Askari kufika kuwakamata Maksuudi na Zanga wakati tu umati umelipuka kutaka kuwaua.
      17. Maimuna amechanganyikiwa na hajui pa kwenda anatokea Dora na kumwelekeza kwa Biti Sururu. 
      18. Wimbo wa Bantus kule Rumbalola - Nilikimbia kwa baba ... uliimbwa wakati Maksuudi alienda kumtafuta Maimuna hapo/Maimuna pia amekimbia kwa babake..
      19. Uchungu wa uzazi unampata Tamina mara tu Maksuudi anapoondoka nyumbani.
        Zozote 5 x 2-10
    3. Uhuru alioutaka Mainuna
      1. Maimuna alijikuta akidhibitiwa na watu wengine. Mfano Mama Jeni, Biti Sururu, James na Shoka.
      2. Aliingizwa kwenye madanguro na ukahaba na kufunzwa kuweka pesa mbele. K.m. kisa cha James.
      3. Walimwengu walimchezea bila. - Hawa ni pamoja na Bi. Farashuu, Mama Jeni na Biti Kocho
      4. Alitarajiwa kufanya kazi. Biti Sururu alilalamika kuwa Maimuna alikuwa analala huku wenzake wanafanya kazi.
      5. Maimuna alikosa jamaa yake. Alilia ndani kwa ndani alipowakumbuka/ Alitengana na jamaa yake.
      6. Alizama kwenye tabia ya ulevi.
      7. Mazingira alimoishi yalikuwa machafu. Kila mahali kulikuwa na mashimo, matope, uvundo wa vyakula panya na mende, kwa mfano kwa Mama Jeni na kwa Biti Sururu.
      8. Maimuna alijikuta kwenye maisha duni yaufukara. Anapata chakula kwa hila kutoka kwa Ashuru. Anapewa samaki na Kabi.
      9. Alifanya kazi duni zenye mapato duni. Alihudumu kwenye vilabu kuuza tembo, kusafisha makopo.
      10. Kwa sababu ya umri mdogo na urembo wake, watu hasa wenye pesa walimtumia kama chombo na kitega uchumi, kwa mfano alitumiwa kama kitega uchumi Rumbalola, Pumziko, Bobea.
      11. Alibobea katika ukahaba. (Kwa sababu ya urembo wake)
      12. Alijikuta kwenye maisha ya uhuni kama vile kung'ang'ania wanaume na kupigana k.m. Kijakazi.
      13. Alikumbwa na matatizo ya jamii ambapo hakuna uhuru kamili, hakuna mwongozo wa maisha, jamii iko katika tanzo la kunyongwa. Alikosa mtu wa kumwelekeza
      14. Alikumbwa na hali ya uhitaji na ufukara. K.m kukopa kwa Ashuru.
      15. Mapigo ya maisha yalimuumbua akapoteza urembo na kupata makovu/kukonda na kuchujuka.
      16. Anapata dhiki ya kisaikolojia. Mwishowe kujiona duni/asiweze kuolewa. Anamwambia Kabi kuwa yeye ni mchafu.
      17. Ulimwengu umembadilisha hadi akawa fidhuli kwa babake/ kukosa heshima. Anamkaripia na kumlaumu pale Bobea.
      18. Kusingiziwa wizi na kufukuzwa kwa Mama Jeni.
      19. Kudharauliwa / kudunishwa na watu, kwa mfano Farashuu/ Kijakazi/ Shoka.
        Zozote 10 x 2 = 20

  3. MASHAIRI SEHEMU YA C
    • KUJITEGEMEA
      1. Umuhumu wa nchi kujitegemea/ tatizo la mikopo na uombaji. ( alama 2)
      2. Aina.
        1. Tarbia-mishororo minne kila ubeti.
        2. Mathnawi – vipande 2 kila mshororo.
        3. Ukara - lina vina vya ndani vina na nje vinafanana/ urari
          Yoyote moja = 2 x 1 = 2 c)
      3. Anashauri nchi
        1. Kupata wataalamu wa ndani ya nchi kuendesha mambo.(ub. 4)
        2. Wananchi washiriki kazi za aina yoyote.(ub. 5)
        3. Wananchi wawajibike. (ub. 2)
        4. Kuepuka na mikopo maana haina faida. (ub. 5)
        5. Ritifaa – kuzungumza moja kwa moja na kitu kisicho hai (Haki)
          Yoyote moja. Kutaja 1 maelezo 2 = 1x3 = 3 d)
      4. Idhini
        1. Matumizi ya msamiati usiokuwa wa kawaida/ kuunda - machumi (ub. 4)
        2. Inkisari; mbinu ya kufupisha maneno. Waloteuliwa (ub. 4) – walioteuliwa; litarajiwa (ub. 4) - lililotarajiwa; ilotueka – iliyotuweka; itavyopatika - itakavyopatikana; tukiifatia- tukiifuatia tukiifuatia
        3. Lahaja - tukiifatia (ub. 5) - tukiifuatia; hichi (ub. 4) - hiki.
        4. Tabdila - kunaiyenea; akukumbukae; ilotueka
        5. Kuboronga sarufi - sio hao mabwana (sio mabwana hao); na vikubwa visa (na visa vikubwa); kwenye hichi kiza (kwenye kiza hichi)
        6. Utohozi - tukisi
          Tatu za mwanzo. 3 x 2 = 6
      5. Haki haifanyiki au haipatikani mahali penye mambo au visa vingi/ watu hawataki kufanya lolote la haki mradi watapata pesa/ sisi tunapata shida kubwa ila wao wako sawa/ haya ndiyo ya leo au siku hizi. AU Watu wanapopatwa na shida/ mikasa/ taabu/ visanga hawatendewi haki/ ili kutendewa haki au kusaidiwa ni lazima walipe pesa hongo]/ wakati wa shida hatuhurumiwi [hakuna utu, tunateseka bure, hawajali, hawana hisia/ Na huo ndio mtindo wa kisasa (na hivyo ndivyo ilivyo siku hizi). (alama 4)
      6. Maana ya maneno
        1. Mahali palipo panatuumiza/ panatutesa/ dunisha/ turudisha nyuma.
        2. Kuweza kufikiri/ kusema/ kukubusu/ kutetea.(alama 2)
  4. MAYAI SEHEMU YA D
    • Cheche
      1. Mbunda/ alikuwa anazungumzia nafsi yake akiwa amejibanza kwenye hoteli mjini/ akiwa anakumbuka tukio ambapo yeye pamoja na wanafunzi wenzake walipanga kuiteketeza shule yao ili kumpa funzo mwalimu mkuu kwa kuwadhibiti. Tukio hili lilisababisha hasara na vifo vingi. Matokeo haya ndiyo yaliyomfanya Mbunda kuungulika moyoni (alama 4)
      2. Chanzo
        1. Utawala mbaya/ ulegevu wa mwalimu mkuu (hakuchukua hatua za tahadhari)
        2. Malezi mabaya - mfano Mbunda anapodai hajawahi kuadhibiwa na wazazi.
        3. Ubabe unaotokana na fikira za ujana wa kupenda mambo yatendeke wanavyotaka. Uk. 126 ... hawezi kutufanya mahabusu wake ...) Madai ya wanafunzi ya uhuru mkubwa.
        4. Ukatili wa wanafunzi wachache kupanga njama ya kuteketeza shule.
        5. Utovu wa nidhamu
          Nne za mwanzo 4 x 2 = 8
      3. Matokeo
        1. Kuteketea kwa majengo ya shule/ uharibifu wa mali.
        2. Vifo vya wanafunzi 68.
        3. Kuvurugika kwa utaratibu wa shule.
        4. Athari za kimhemko kwa waliofika kusaidia au kushuhudia/ wengine hata walizirai.
        5. Athari za kinafsia za walioteketeza shule/ majuto ya akina Mbunda, Musesi na hata kamaliza.
        6. Majonzi kwa familia za waliokufa/ wananchi/ nchi.
        7. Watoto kutozikwa makwao kwa sababu ya kuchomeka na kutotambulika/ kuzikwa kaburi moja. 
        8. Majeruhi - wanafunzi wajeruhiwa.
        9. Mwalimu mkuu kulaumiwa kwa uongozi mbaya.
        10. Jopo kuundwa kuchunguza tukio hilo.
          Nne za mwanzo 4 x 2 = 8
    • Mganga
      1. Kutotambua umuhimu wa kuwapeleka watoto shule
      2. Kutumia wembe mmoja kuwachanja wagonjwa
      3. Hakuelewa maendeleo. Alipoenda mjini anaona jokovu kama sanduku la barafu.
      4. Hakufahamu chochote kuhusu UKIMWI na hakutaka kuuliza. Anasema ni ungonjwa wa mjini, unaosababishwa na kurukaruka
      5. Hakujua jinsi ya kujitangaza
      6. Vifaa alivyotumia havikuwa na maana. K.m, vibuyu, pembe, mbegu
      7. Kutumia maneno ambayo hata mwenyewe hayakuyaelewa
      8. Kutoa tiba ile moja kwa magonjwa yote na wateja wote
      9. Kutumia mimea bila kujali athari kimazingira.
      10. Kunyonya damu kwa imani kuwa anajiongezea
      11. Kutofahamu jina la mpira wa kinga wa ngono.

        Wateja
      12. Kumwachia mganga hela za kununua nyembe ingawa wao ndio walioishi mjini/ Walishindwa au kudhibitisha upya wa nyembe anazotumia
      13. Kumfuata mganga mbali kule porini, badala ya kwenda hospitalini
      14. Ni wasomi lakini walitafuta msaada wa mganga ili kupata cheo
      15. Kutofahamu ugonjwa waliougua hata ulipokuwa na dalili za wazi za UKIMWI
      16. Kukubali kuchanjwa kwa wembe mmoja. Asteria na rafiki yake
      17. Kutafuta msaada wa mganga kwa mambo kama vile mapenzi/biashara/ ndoa
      18. Kumpa mganga maelezo aliyoyatumia eti kuwagangua
      19. Imani kwenye madoido na mbwembwe za mganga.
        Kumi za mwanzo 10 x 2 = 20
  5. FASIHI SIMULIZI . SEHEMU YA E.
    1. Utani ni kipera cha Fasishi Simulizi chini ya uwanja/ utanzu wa mazungumzo Malumbano ya utani ni majibizano kati ya watu au makundi mawili kwa nia ya kutaniana. Hufanywa kwa kutumia maneno ya mzaha ili kuleta ucheshi. Utani ni utaratibu unakubaliwa na jamii. (alama 2)
    2. Sifa za malumbano ya utani
      1. Hutumia lugha ya ucheshi.
      2. Hutolewa kwa njia ya kudunisha/ kejeli
      3. Huwa na mlengwa mahsusi anayejulikana na anayetania/ anayetaniwa.
      4. Huwa na kusudi maalum inapotolewa.
      5. Maneno yanayotumiwa yanaweza kuwa ya aibu au hayazingatii tauria.
      6. Lugha huweza kuwa ya mafumbo/ tamathali za usemi.
      7. Baadhi ya kauli hutumia fomyula, K.m. katika jamii nyingi utani wa babu kwa mjukuu huwa. “Mke wangu, mbona leo ..."
      8. Katika kutaniana, wahusika hujuana na kuheshimiana/ mipaka hudumishwa.
      9. Kupiga chuku.
      10. Hoja zozote za mwanzo 4 x 2 - 8
    3. Umuhimu wa utani
      1. Hujenga mahusiano kati ya wahusika/ umoja/ ushirika/ utangamano,
      2. Huchangamsha/ huburudisha wanaohusika.
      3. Huchemsha bongo.
      4. Hutia ladha mahusiano kwani huchekesha.
      5. Huhifadhi mila/ utamaduni/ desturi/ itikadi/ kitambulisho cha jamii.
      6. Hufunza maadili.
      7. Hukosoa/ huonya.
      8. Kuendeleza historia ya jamii husika.
      9. Hukuza lugha.
      10. Huelimisha jamii.
      11. Hutolewa kwa nia ya kukejeli.
      12. Hukuza vipawa.
      13. Hujasirisha (ujasiri).
      14. Kupitisha wakati
      15. Hukuza ubunifu.
        Za mwanzo 5 x 2 = 10 
Join our whatsapp group for latest updates

Download KCSE 2011 Kiswahili Paper 3 Questions with Marking Scheme.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest