Soma kifungu hiki kisha ujaze mianya.
Upishi ni __1__ambayo watu wengi huichukulia kimzaha. Matokeo ya__2__ mengi ni ya kuudhi. Upishi __3__ huwafanya watu__4__mate na kulamba vidole. Vyakula mbalimbali__5__kwa njia tofautitofauti. Kuna vyakula ambavyo__6__kwa kutumia mafuta. Nyama zinaweza__7__ kwa kutumia makaa au moto. Ugali__8__kwa njia ya utaalamu ili kuhakikisha hakuna __9__. Vyakula vingine kama ndizi vinaweza kuliwa bila kupikwa. Ndizi__10__ kwenye vumbi au majani ili ziwe mbivu.
Ni jukumu__11___ kutunza mazingire yetu. Tunapaswaa kupanda miti ili kuzuia__12__wa udongo na kufanya __13__ ya nchi yawe ya kuvutia. Ushirikiano__14__watu wote utasaidia katika kufanikisha ndoto__15__.
Soma maswali kwa usahihi kulingana na maagizo
- ______huvaliwa shingoni
A.Mkufu na kidani
B. Kishaufu na kekee
C. Wanja na chale
D. Nyerere na udodi - Kamilisha methali hii: Ikiwa hujui kufa tazama
A. kifo
B. kaburi
C. maiti
D. wafu - kitegue kitendawili hiki: Nje nyama ndani ngozi
A. Nyongo
B. Ini
C. Sarara
D. Firigisi
Jaza pengo kwa usahihi
- Kilema ___hajafunga safari.
A. chenyewe
B. chenye
C. mwenyewe
D. mwenye - Sayari ndogo kuliko zote huitwa_____ na yenye pete ni
A. Zaibaki, Zohali
B. Zuhura, Kausi
C. Zohali, Mshtari
D. Mirihi, Dunia - Malipo yanayotolewa kabla wakati wake kuwadia ni _______
A. arshi
B. dia
C. hongo
D. karisaji - Milima inayofuatana huitwa
A. mlolongo
B. safu
C. karne
D.gwaride - Nilijipaka mafuta usoni
A.mwangu.
B. wangu
C. pangu
D. yangu - Nyumba iliyo juu ya nyingine huitwa
A. roshani
B.ghorofa
C. gorofa
D. kasri - Amevaa kitambaa cheupe kama
A. kaniki
B.kizimwili
C. pambo
D. bafta - Wingi wa
Nyani huyu ni
A. manyani hawa
B. wanyani hawa
C.minyani hii
D. vinyani hivi - Andika ukubwa wa sentensi hii
Nguo yak imeshonwa vizuri
A. manguo yake yameshonwa vizuri
B. guo lake limeshonwa vizuri
C. Kinguo chake kimeshonwa vizuri
D. kiguo chake kimeshonwa mzuri - Tumia "amba" kwa sentensi: Bakuli huoshwa huwa safi.
A. ambayo B. amako
C. ambapo D. ambalo - Chagua sentesi yenye vielezi peke yake.
A. Wanne, hizo, mzuri, vizuri
B. Mno, vibaya, sana, haraka.
C. Lo, do, lahaula, shabashi.
D. Safi, dhaifu, bora, duni. - Maumbo haya huitwa
A. duara na pembe nne
B. kipenyo na tiara
C. kitovu na uru
D. nusu kipenyo na shungaza
Soma makala haya kisha ujibu maswali 31-40
Siku moja Juma aliporudi kutoka shuleni, aliwakuta watu wenye nguo zilizokunjana wamesimama karibu na lango la babu yake. Nyumba ya babu yake lilikuwa imeungua moto. Juma aliweza kuona makaa na jivu.
Hapo alishtuka sana kwa maana alijua bayana kuwa si jengo tu lililoungua, bali hata vitu vyote vilivyokuwamo ndani.Machozi yalimtiririka michirizi michirizi, alipowaza na'kuwazua jinsi angepata chakula na mahali pa kulala. Akamwuliza babu yake kwa jitimai, "babu, kuna vitu vilivyosalia?"
Mzee kazmwendo alimtazama kwa huzuni kisha akamjibu, "Mjukuu wangu, Juma, ni vitu vichache tu tulivyoifaulu kuvitoa nje lakini vingine vyote vimeteketea kabisa. "Kisha aliyaelekeza macho mahali palipokuwa na vigae vya chungu ambacho kiliteketea katika moto ule. Akachukua vile vigae akasema, "Juma, waona vigae hivi vya uhuni?" Juma akajibu "Naam babu" Kazamwendo akaendelea, "Kilikuwa chungu ambamo nilitia fedha za sarafu na noti ambazo nilizinduliza kila wiki. Nilikuwa nikizipata kwa kuuza pamba. Ingawa pengine nilipata
fedha kichele tu, sikufuja mali ila nilijinyima mengi na kuziweka ili zinifae wakati wa dhiki. Nilikuwa nikikumbuka methali isemayo" Akiba haiozi."Chungu hicho nilikificha darini ili kisifikiwe na mtu yeyote. Sasa nimekuwa fukara fakiri.
Juma alipotaka kujua ni pesa ngapi baabu yake alizokuwa akiziweka kila juma na kwa muda gani, alimjibu kuwa alikuwa akiweka shilingi elfu tano kila wiki kwa muda wa mika minne. Juma akasema, "Babu, uliamua vyema kujiwekea fedha ila hukujua mahali salama pa kuziweka fedha hizo."
Kusikia haya, mzee Kazamwendo akashika tama akaketi chini ya kivuli huku amekunja uso amabao ulikuwa na makunyunyu kama ngozi ya kifaru. Kisha akamwelekea Juma akamwuliza," umesema sikujua mahali pa usalama pa kuweka fedha hizo? Ningeziweka wapi? Tangu zama za zama za baba na babu zetu walioanza kutumia pesa hakuna aliyeziweka kwa namna nyingine ila kuziweka katika chungu au kuzichimbia chini ardhini. Pukachaka! Sasa wataka kuniambia nini mtoto wa jana?" Mzee alikuwa amepandwa na mori kweli.
Juma akainamisha kichwa chini kama mtu anayefikiria kujibu, bila kukawia akasema, "Baba, kunradhi! sikuwa na maana ya kukudharau, hata! ila siku hizi kuna njia bora zaidi za kujiwekea akiba. Juma akapata wakati mwafaka wa kumwelimisha babu. Akamwambia kuwa njia mojawapo ni kuziweka benkini kwa sababu hazitaibiwa na utakuwa ukipata riba ya kila mwaka.
Mzee Kazamwendo akamshukuru mjukuu wake kwa kumwelimisha Juma akamtuliza babu yake akasema, “Ingawa majuto ni mjukuu, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Iwapo tutaziweka fedha zetu benkini,jasho letuhalitazidi kupotea."
Mwaka uliofuata baada ya kupitia kipindi kigumu cha kukimiwa na wahisani akaenda kuziweka fedha katika benki. Tangu wakati huo hakuwa na kiherehere kwani fedha zake zilikuwa salama u salimini.
- Watu waliookuwa karibu na lango walikuwa wakifanya nini kwa fikira zako?
A. Kuuzima moto
B. Kuonyesha furaha
C. Kujitangazia sifa
D. Kuiba - Juma alikwa akimtegemea nani?
A. Baba
B. Mama
C. Babu
D. Shangazi - Unadhani chungu kilitumika kwa kazi gani?
A. Kupikia
B. Kutulia maji
C. Kuhifadhia pesa
D. Kupikia pure - Pukachaka ni
A. kivumishi
B. kihusishi
C.kielezi
D. kihisishi - Faida yakuweka pesa benkini ni
A. utapata riba na ni salama
B. utapata riba tu
C. utapata nuksi na riba
D. utapata riba nafuu - Kwa nini uso wa Kazamwendo ulikuwa na makunyunyu?
A. alikuwa amekasirikaa
B. ndivyo alivyozaliwa
C. alikuwa amezeeka
D. alikuwa amechomekewa - Tendo la kuhifadhi mali ya thamani kubwa nyumbani inafaa?
A. Haifai
B. Unailinda vizuri
C. Pengi si salama
D. Wevi hawataipata - Methali: hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho ina maana kuwa?
A. Zito hufuatwa na jepesi
B. Kamba hukatikia pembamba
C. Hakuna mwisho wa shida
D. Hakuna msiba usiokuwa ma mwisho - Babu anasema kuwa amukuw fukara fakiri-hivi ni kusema?
A. anachungulia kaburi
B. yeye si wa maji si wa uji
C. yeye ni mnobe na hawinde
D. hatii wala hatoi - Makala haya yanaweza kuelezewa kwa methali
A. msiba wa kujitakia hauna kilio
B. akili ni nywele
C. pema usipopepma si pema pa mwenzio
D. ajali haina kinga wala kafara.
Soma ufahamu huu kisha ujibu 41-50
Safari ilikuwa ndefu. Hawakuwa na budi kuenda masia kwa sababu licha ya magari kuadimika kama barafu ya kukaanga, hapakuwa na tariki. Kulikuwa na vijia msituni ungedhani vilitengenezewa panya.
Msitu ule ulikuwa umejaa wanyama tena wa kila aina. Ilikuwa nadra sana kumwona mtu akitembea peke yake. Yamkini waliamini kuwa kifo cha watu wengi ni arusi. Wanaume kwa wanawake walikuwa kwenye charo. Walikuwa wakigura sehemu ile kwa sababu walihofia kuvamiwa na wanyama pori. Kila walipopanda mazao yao yalikuwa chakula cha tembo, mbogo na wanyama ambao hula mazao ya shambani. Usiku ulikuwa wa kutishaa.
Hawakupata hata lepe la usingizi kwa sababu mifugo yao ilikuwa katika hatari ya kushambuliwa na chui, duma na simba. Masaibu yaliwasibu na kuwazingira. Wakaamua kuacha migunda yao ingawa ilkuwa na rotuba ya kupigiwa mfano.
Wanaume waliangata mizigo yao nao wanawake waliitwika. Watoo walielekea na safari ikauma mchanga alfajiri na manyera huku umande ukiwalowesha. Jua liliangaza lakini ukali wa miale yake haukuwasumbua. Safari ilipoanza kunoga ghafla bin vuu, walikifumania kikundi cha mbogo. Mbogo hawa walikuwa wakinywa maji. Bila kuboroga wasaa nyati waliwakabili vilivyo. Kila mtu alitundika guu begani. Ulikuwa wajibu wa mtu kuyaokoa maisha. Vumbi lillitifuliwa. Walipoona maji yamezidi unga, walikwea juu ya miti. Nyati walipita wangu wangu na hatua chache baadaye, walikutana na simba. Simba waliamini kuwa mlo umejipeleka wenyewe. Mbogo wa kwanza alishikwa na kutoa sauti ya kutisha. Vita kamili vilizuka dhidi ya simba na nyati. Simba alipambana na kujipatia shibe ilhali nyati alikuwa na nia ya kuyanusuru maisha yake. Katika shamrashamra hizo, nyati walikimbia wakifuatwa kwa kasi na simba.
Hatimaye wasafiri walipata muda wa kuendelea na safari yao. Walikuwa wachovu kupindukia na wenye jitimai. Siku ilianza kukuchwa na hawakuwa na makao maalum ya malazi. Iliwalazimu kuwasha moto mkubwa na kutengeneza malazi karibu na moto huo. Sehemu ile haikuwa na wanyama. Miti ilikuwa mifupi ilibidi kutembea kwa muda mrefu ili kupata mvua. Mvua iliponyesha ilikuwa ya kuondoa vumbi tu. Mimea ilinawiri kwa muda kisha ikakaushwua na jua lililoleta joto ungedhani ni tanuri.
- Si kweli kuwa
A. baraste zilikuwa nyingi
B. vijia vidodgo vidogo vilitumika
C. safari ilikuwa ndefu
D. kulikuwa na uhaba wa magari - Kisawe cha "Kuenda masia" ni
A. Kuenda chemba
B. kupiga milundi
C. kuenda kwa mesiya
D. kupiga miluzi - Wasafiri walisafiri kwa makundi ili
A. kuandamana
B. kuhofiana
C. kuhimizana
D. kulindana - Maana ya neno charo ni
A. kundi la wanyama pori
B. kuhama
C. kundi la wasafiri
D.msafara wa ng'ombe - Wasafiri walipata nafasi ya kuendelea na safari wakati
A. kulipokucha
B. nyati walipokimbizwa na simba unyounyo
C. walipofumania mbogo wakinywa maji
D.umande ulipohinikiza nyasini - Watu walihofia nini hasa ndiposa wakagura?
A. mvua kupunguka kwa kiasi kikubwa
B. mmomonyoko wa udongo ulizorotesha rotuba
C. kushambuliwa na wanyama pori kila mara
D. wanyama pori walianza kula wapita njia - "walikuwa wachovu kupindukia na wenye jitimai."maana
A. walikuwa na wavune na majonzi ya kutwa
B. walikuwa wakihofia wanyama pori usiku.
C. walikuwa na makao maalum ndiposa walichoka
D. walikaribia kufika walikokuwa wakihamia - Sentensi ipi inayoonyesha sababu kamili iliyowafanya watu wakose usingizi usiku?
A. mazao ya mashamba yalikuwa finyu
B. uchovu wa kutembea muda mrefu
C. hawakuwa na vitanda
D. iliwapasa walinde mifugo yao - Simba aliamini kuwa shibe imejipeleka yenyewe, ina maana
A. wanyama wengine walikuwa shibe ya simba
B. walitegemea masiya safarini
C. walitembea kwa miguu
D. walikuwa wameshiba kutokana na shibe - Vita vilizka dhidi ya simba na mbogo. Je, ni methali gani ingetumiwa kudhihirisha haya?
A. vita vya panzi furahha ya kunguru
B. Hasira ya mkizi furaha ya mvuvi
C. Angurumapo simba mcheza ni nani?
D. Meno ya mbwa hayaumani
INSHA
Umepewa mwanzo wa insha. Iandike kwa kutumia maneno yako mwenyewe na uifanye iwe ya kusisimua uwezavyo
Baada ya kumaliza na kupita mtihani wa KCPE, nilipewa fursa satua ya kuzuru mji niliopenda kwa moyo...........................................................................
MAJIBU
Download KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 2.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students