KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 3

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo kutoka nafasi 1 hadi 15. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale manne uliyopewa. 

Alfajiri kuu mwanafunzi alikuwa__1__katika lepe__2__ la usingizi. __3__ ya kutwa iliyotangulia __4__yu hoi__5__si kidogo usingizi__6__kwa nguvu akalala fo wala hakujipindua __7__ kitanda chake cha teremka tukaze mpaka alfajiri. Alikuwa__8__ misono mikubwa __9__ ghafla na sauti ya kitoto kichanga akazinduka. Akatega sikio kwa makini.

KISWA SET 3 1

Ni jukumu kwa kila mzazi__10__ watoto wake. __11__ yafaayo hushughulikia mtoto kwa njia__12__ Lazima__13__kwamba, mtoto anafundishwa kuwa na__14___ kwa lolote ambalo__15__.

KISWA SET 3 2

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi kulingana na maagizo

  1. Nomino'werevu' ni nomino ya
    A. mguso.
    B. maalumu
    C. fungamano
    D. dhahania
  2. Ni nini wingi na ukubwa wa sentensi ifuatayo. Kinywa chake ni chembamba.
    A. Vinywa vyao ni vyembamba.
    B. Jinywa lake ni embamba.
    C. Majinywa yao ni membamba.
    D. Jinywa lake ni jembamba.
  3. Tumia kimilikishi cha nafsi ya tatu.
    Nyumba __ ni nzuri sana.
    A. zetu
    B. yake
    C. zenu
    D. yako
  4. Mtu anayetumiwa na kiongozi mwengine kwa manufaa ya kiongozi huyo ni
    A. karagosi.
    B. fashisti.
    C. balozi.
    D.mkimbizi.
  5. Chagua orodha ya viunganishi pekee.
    A. Pengine, Yake, Sembuse.
    B. Ingawa, Isipokuwa, Maadamu.
    C. Vipi, Lini, Wapi.
    D. Ila, Wala, Hii.
  6. Panga nyakati zifuatazo jinsi zinavyofuata na katika siku.
    A. Macheo, Alasiri, Adhuhuri, Machweo.
    B. Machweo, Adhuhuri, Alasiri, Macheo
    C. Macheo, Adhuhuri, Alasiri, Machweo.
    D. Machweo, Adhuhuri, Alasiri, Macheo.
  7. Ni ipi tarakimu tasa kati ya hizi
    A. 9
    B. 12
    C. 15
    D. 11
  8. Chagua kimilikishi katika sentensi hii.
    'Msichana huyu wako anacheza vizuri."
    A. huyo.
    B. vizuri.
    C.msichana.
    D. wako.
  9. Chagua kitenzi kinachotokana na jina au nomino
    "shujaa"
    A. Shujaisha.
    B. Shujiisha.
    C. Shajira.
    D. Shajari.
  10. Anayetunza fedha au hazina ni mhazini.
    Anayetunza maktaba pamoja na vitabu vya maktabani ni …
    A. katibu.
    B. mkataba.
    C. mkutubi.
    D. hatibu.
  11. Bwaloni ni ukumbini pa____ chakula.
    A. kula
    B. kukulia
    C. kulia
    D. kukula
  12. Jina litumiwalo na mjomba kumwita mtoto wa ndugu yake wa kike ni_
    A. mpwa.
    B. mkoi.
    C. binamu.
    D. shemeji.
  13. Biwi la ghubari ni tamathali gani?
    A. Majina ya pekee.
    B. Majina ya makundi.
    C. Tashbihi.
    D. Methali.
  14. Chagua kivumishi kisicholingana na vingine?
    A. Dhalimu.
    B. Safi.
    C. Zuri.
    D. Madhia.
  15. Ni sayari gani ndogo zaidi kuliko zote?
    A. Zaibaki.
    B. Mshatarii.
    C. Sarteni.
    D. Kausi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Wote walilewa katika karia moja huko Janibu za Maragwa. Walikuwa wa hirimu moja wakahudhuria shule moja na kuhitimu wakati mmoja. Kamani alifua dafu masomoni naye Kogotho akauma mchanga. Yaelekea nyota ya Kagotho haikuwa masomoni kwani hakufeli kutokana na ulazaji wa damu wala utovu wa makini. La hasha! Lakini hayo ni ya kawaida hapa duniani, kwani hata wahenga walitoa lulu kuwa bidii si pato. Waambao waliamba. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa mapishi. Kigotho hakusalimu amri. Alijiliwaza kuwa kuteleza sio kuanguka bali ni kwenda mbele. Alianza biashara ya kubahatisha ya kuuza mboga na makaa. Akawa kijana mwenye bidii mithili ya nyuki huku akizingatia ya wahenga kuwa achanikaye kwenye mpini wa jembe hafi njaa. Shababi Kigotio aliendelea kuishi pale Kayani. Alishirikiana na wanakaya kwa heri na kwa shari, kwa baridi na kwa joto. Alielewa kuwa upweke ni uvundo na mkataa wengi ni mchawi.

Miaka ya mwanzo, shughuli zake hazikumwendea mserego. Juhudi na jitihada zake zikawa zimetumbukia nyongo. Licha ya hayo, hakubwaga silaha. Papo hapo, kamba hukata jiwe. Polepole, alifanikiwa na wengi wakaamini kuwa zito hufuatwa na jepesi.

Mbali na chudi zake za mchwa, Kigotho alikuwa na taadhima zake. Alielewa fika kuwa heshima si utumwa. Jambo hilo lilimnasia wasena tumbi nzima kwani jina jema hung'aa gizani. Wengi wakwasi walimpiga jeki. Waama sifa njema yakaribia utajiri. Baada ya muda mrefu wa kujifunga mkwiji, alijipata akiogelea katika bahari ya ubwanyenye. Alipata nyumba na kujiendeleza aushini. 

Kamani nae aliendelea kulisukuma na kulibiringisha gurudumu la masomo. Skulini, alionyesha mafanikio ya ufanisi mkubwa. Alizidi kunawiri na kushamiri shuleni. Hata hivyo, ushamiri wake uliishia hapo kwani kwake heshima ilikuwa ni utumwa. Alikuwa na kichwa kikubwa. Kuwa na adabu likawa ni jambo la mwiko. Licha ya elimu yake, hakuwa na chembe ya adabu. Alisahau kuwa elimu yake pekee pasi adabu na nidhamu haingemfaa. Wakwasi wa lugha walinena kuwa elimu bila adabu ni sawa na mtu kuvaa tai huku akiwa uchi wa mnyama. Badala ya kuitumia elimu kuwaheshimu wenzake, alitumia kuwazebeza na kuwatweza. Alipoajiriwa, aliingiwa na shauku ya kuvuka hadi ng'ambo ya utajiri huku akiyapuuza ya wahenga kwamba kawia ufike. Alitiwa mbaroni kwa makosa ya ufisadi na akaonyeshwa paa. Fauka ya hayo, alifikishwa mahakamani kula kalenda jelani kwa miaka mitatu na kufanya kazi ya dharubu na sulubu. Yakini heshima, adabu na subira ní vigezo dhabiti maishani.

  1. Kulingana na kifungu, ni methali gani ambayo haikutumika.
    A. Achanikaye kwenye mpini wa jembe hafi njaa.
    B. Kwa heri na kwa shari.
    C. Papo kwa hapo, kamba hukata jiwe.
    D. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa mapishi.
  2. Ni sahihi kusema Kamani na Kagotho
    A. walionyesha bidii katika shughuli zao.
    B. walikuwa na kichewa kikubwa.
    C. walikuwa na heshima.
    D. walisoma hadi kiwango cha juu.
  3. Ni kwa nini Kigotho aliyakatiza masomo yake?
    A. Alikosa karo.
    B. Hakupasi mtihani wa shule ya msingi.
    C. Hakupendelea kusoma.
    D. Alifukuzwa shuleni.
  4. Mwanzoni Kagotho alishughulika na yapi?
    A. Kilimo cha mboga.
    B. Biashara ndogondogo.
    C. Ubwanyenye.
    D. Kuuaza asali.
  5. Nahau "kulaza damu' limetumika, maana yake ni
    A. hakufaulu.
    B. hakulala.
    C. hakujitahidi.
    D. hakuzembea.
  6. Ni sababu ipi ilivochangia sana kwa Kagotho apendwe na wengi?
    A. Bidii zake.
    B. Utajiri wake.
    C. Haiba yake.
    D. Kazi yake.
  7. Ni tabia ipi ilisababisha Kamani kujipata gerezani?
    A. Tamaa ya kutajirika haraka.
    B. Kichwa kikubwa.
    C. Utovu wa heshima na adabu.
    D. Kupenda kusoma sana.
  8. Kwa mujibu wa mwandishi ni kweli kusema:
    A. elimu pekee inatosha.
    B. heshima bila elimu ya juu haifai.
    C. bidii bila elimu ni bure bilashi.
    D. elimu pasipo nidhamu ni bure bilashi.
  9. Ni kweli kusema kuwa Kamani na Kigotho walikuwa
    A. somo.
    B. mahasimu.
    C.pacha.
    D. marika.
  10. Kati ya methali zifuatazo, ni ipi iliyotiliwa maanani na Kagotho na kupuuzwa na Kamani?
    A. Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
    B. Mvumilivu hula mbivu.
    C. Penye nia pana njia.
    D. Mtaka yote hukosa yote.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50

Mama Buibui alikuwa na watoto wanne, jioni moja marafiki wanne, kila mmoja, waliwaalika watoto hao kwa chakula. 

"Mna bahati sana wanangu kwa kualikwa jioni hii! Sina chakula chochote nyumbani. Sasa mnakula vyakula vizuri lakini mimi nitashinda njaa tu" usilie mama," Wanawe walimwambia, ingawa ninalo wazo linalofaa zaidi. Sikizeni! Nitajifunga kiuno kwa kamba moja. Mnapoingia nyumbani kwa marafiki wetu, mtaona ikiwa chakula ni kitamu au la. Kikiwa kitamu uvute sana kamba yako. Nikikazwa na kamba moja, nitajua chakula kilicho bora
zaidi. Basi nitaenda kwa nyumba hiyo na bila shaka nitapewa chakula."

"Umwerevu sana mama. Tunaelewa. "Kwa hivyo waliondoka.Mtoto wa kwanza hakuona chakula kilichokuwa tayari bali alinusa harufu ya chakula kitamu kikipikwa nyuma ya nyumba. "Aah! Vyema sana. "Aliwaza na kuvuta kamba. Mamake aliwaza "Ha! Huko ndiko nitakakoenda." Lakini wakati huo huo wale watoto wengine watatu walikuwa wakiingia nyumbani mwa marafiki wao watatu. Wote waliona vyakula vingi vitamu vikiwangojea. Kwa hivyo walizivuta kamba zao kwa nguvu. Mama yao alivutwa sehemu nne tofauti na hangeweza kwenda popote. Kila mtoto alivuta kwa nguvu ili mamake aende kwa chakula chake. Maskini mama alisikia uchungu mwingi sana. Alikuwa katika maumivu "Acheni, Acheni," alipiga kelele, mnaniuaaaa
Bila shaka wanawe hawangesikia. Dakika kadhaa baadaye waligundua kuwa kulikuwa na balaa fulani, na wakaacha kuvula kamba zao.

Mama yao hakufa, lakini kiuno chake kilifinywa sana na kikabaki vivyo hivyo, chembamba.

  1. Mialiko hiyo ilipangwa vipi?
    A. Marafiki wanne walimwalika mtoto mmoja kila mmoja.
    B. Rafiki mmoja aliwaalika watoto wanne.
    C. Mtoto mmoja alialikwa na marafiki wane tofauti.
    D. Mama alialikwa na mmoja wa marafiki.
  2. Mama buibui alikuwa na madhumuni gani katika mpango wake?
    A. Alitaka kualikwa kwa chakula kilichokuwa kitamu zaidi ya vyote.
    B. Alitaka kualikwa kwa chakula kilichokuwa kingi zaidi.
    C. Alitaka kula katika kila nyumba.
    D. Alitaka kujikinga na njaa.
  3. Mama buibui alifanya kosa gani katika mpango wake?
    A. Alikaza sana zile kamba kwenye kiuno chake.
    B. Alisahau kuwa huenda watoto wote wakaamua kuwa vyakula vyote walivyopewa vilikuwa vitamu.
    C. Hakuwaambia marafiki zake kuhusu mpango huo.
    D Hakufahamu kuwa huenda mmoja wa wanawe akaivuta sana kamba, kushinda wale wengine.
  4. Katika habari neno 'maumivu' limepigwa msitari. Neno hili lina maana ya:
    A. kuhisi uchungu mwingi.
    B. kushikwa na hofu.
    C.kutoweza kupumua.
    D. kutokuwa mchangamfu.
  5. Hadithi hii ni hadithi ya Kiafrika ya zamani. Ni funzo gani la muhimu inalonifundisha?
    A. Kutokula chakula katika nyumba za watu wengine.
    B. Kutokuwa walafi.
    C. Kutopiga mayowe kabla ya kuumizwa.
    D. Kutoogopa buibui.
  6. Sifa itakayomfaa sana Buibui na wanawe ni:
    A. mashujaa.
    B. werevu.
    C.wapumbavu.
    D. waoga.
  7. Chagua methali itakayomfaa sana huyo mama Buibui
    A. Mla na mla leo,mla jana kalani.
    B. Mtegemea nundu haachi kunona.
    C. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
    D. Mtaka yote hukosa yote.
  8. Kati ya vichwa vifuatavyo ni kipi kitakachofaa sana kupewa habari hii?
    A. Buibui na wanawe.
    B. Buibui mlafi.
    C. Mwaliko kwa chakula.
    D. Buibui mwerevu.
  9. Ijapokuwa Buibui hakufa, alifikwa na mkasa ambao hatausahau milele. Ni mkasa gani huo?
    A. Ijapokuwa alikuwa na njaa sana, hakufaulu kula chakula mahali popote.
    B. Alifinywa sana kiuno kikawa chembamba sana na kubaki hivyo.
    C. Alisikia maumivu mengi sana.
    D. Alikatika vipande vinne.
  10. Kichwa kingine kingalichofaa habari hii ni:
    A. kilichomfanya buibui kuwa mdudu indogo.
    B. buibui na wanao wanavyopendana.
    C.kilichowafanya buibui kuwa na viuno vyembamba.
    D. buibui walivyo wadugu wapumbavu.

INSHA

Endeleza insha ifuatayo. Insha yako isipungue ukurasa mmoja na nusu.

Maandalizi ya siku yenyewe yalikuwa yashakamilika…………………………………………………………



MAJIBU

KISWAHILI SET 3 MARKING SCHEME

Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI - KCPE 2020 PREDICTION 1 SET 3.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest