Kiswahili - Maranda High School Form 1 End Term 1 2018

Share via Whatsapp

Click the link below to download as a full set with all the subjects.

https://downloads.easyelimu.com/details/32-Maranda_High_School_2018_Form_1_End_Term_1_Past_Papers

KISWAHILI
KARATASI MSETO
SAA 2

SHULE YA UPILI YA MARANDA
KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA 1, 2018

Maagizo

 • Jibu maswali yote katika nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia Kiswahili sanifu
 • Makosa ya tahajia na sarufi yataadhibiwa


1. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)

 1. Tambua sauti zifuatazo: (alama 3)
  1. Irabu ya nyuma wastani.
  2. Irabu ya kati tandazwa.
  3. Kikwamizo sighuna cha ufizi.
 2.  
  1. Huku ukitoa mfano mwafaka, eleza dhana silabi wazi. (alama 2)
  2. Eleza muundo wa silabi katika neno tafrija. (alama 2)
 3. Kanusha:
  Mtoto anaimba na kucheza
 4.  
  1.  Eleza maana ya shadda. (alama 2)
  2. Wekea shadda maneno yafuatayo: (alama 2)
   Karatasi............
   Nzi...................
 5. Geuza kwa udogo: (alama 2)
  Mti ule ulianguka baada ya mvua kubwa.
 6. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi: (alama 2)
  Popo aliruka akatua mgombani.
 7. Sahihisha: (alama 2)
  Tulipofika nyumbani tulimkuta hayuko.
 8. Andika maana mbili tofauti za neno: panda. (alama 2)
 9. Tunga sentensi kudhihirisha matumizi ya ngeli U-I (alama 2)
 10. Bainisha maneno katika sentensi ifuatayo: (alama 2)
  Msichana mrembo ataleta machache
 11. Sabalkheri ni salamu za asubuhi. Jibu lake ni... (alama 1)
 12.  
  1. Eleza maana ya mzizi. .(alama 2)
  2. Onyesha mizizi ya maneno yafuatayo:
   Mdharaulifu..
   Kuombea..
 13. Eleza maana ya methali: mgaagaa na upwa, hali wali mkavu. (alama 2)
 14. Bainisha viambishi katika neno: atampikia. (alama 3)
 15. Tambua aina za sentensi zifuatazo kutokana na kiimbo: (alama 3)
  1. Watu wanakula nyoka.
  2. Watu wanakula nyoka?
  3. Watu wanakula nyoka!
 16. Kamilisha tanakali zifuatazo. (alama 2)
  Shillingi huanguka mchangani......................na Tom amejifunika...........


2. FASIHI SIMULIZI (ALAMA 20)

 1. Eleza maana ya dhana fasihi. (alama 2)
 2. Taja tanzu nne za fasihi simulizi. (alama 4)
 3. Fafanua umuhimu wa hadhira katika fasihi simulizi. (alama 4)
 4. Eleza tofauti tano kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi. (alama 10)

3. ISIMUJAMII (Alama 10)

 1. Eleza maana ya isimujamii. (alama 2)
 2. Eleza sifa nne za lugha. (alama 8)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - Maranda High School Form 1 End Term 1 2018.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest