MASWALI
- Andika barua kwa mhariri wa gazeti la sauti ya mzalendo kuhusu madhara ya janga la korona nchini Kenya.
- Vyama vya wanafunzi shuleni vina manufaa ya kuhusudiwa.Jadili.
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
Mwenye kovu sidhani kapona. - Tunga kisa cha kusisimua na kumalizika kwa …..hivyo ndivyo ukurasa mpya katika kitabu cha maisha yangu ulivyofunguka.
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- Andika barua kwa mhariri wa gazeti la sauti ya mzalendo kuhusu madhara ya janga la korona nchini Kenya.
- Mwanafunzi azingatie muundo wa barua kwa mhariri kikamilifu.
- Madhara ya janga la korona nchini Kenya.
- Kukatizwa kwa elimu
- Vifo
- Kufutwa kazi
- Kudorora kwa uchumi
- Ndoa za mapema
- Mimba za mapema
- Gharama kubwa ya matibabu
- Woga miongoni mwa wananchi
- Kudorora kwa mila na tamaduni za jamii.
- (Mwalimu akadirie maudhui ya wanafunzi)
- Madhara ya janga la korona nchini Kenya.
- Mwanafunzi azingatie muundo wa barua kwa mhariri kikamilifu.
- Vyama vya wanafunzi shuleni vina manufaa ya kuhusudiwa.Jadili.
Manufaa ya vyama vya wanafunzi shuleni.- Hukuza vipawa na kuimarisha stadi za kujieleza
- Huhimiza utangamano miongoni mwa wanachama
- Husaidia mwanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha
- Humfunza mwanafunzi maadili ya kijamii na kidini
- Majukumu ambayo mwanafunzi hupewa hupalilia uwajibikaji,uaminifu na kipawa cha uongozi
- Kupitia vyama hivi mwanafunzi anaweza kuwahamasisha wenzake dhidi y tabia hasi k.v mapenzi ya kiholela n.k
- Shughuli na miradi ya vyama hivi humwezesha mwanafunzi kutumia nishati zake kwa njia ya kunufaisha na kuepuka maovu.
- Vyama vya michezo humwezesha mwanafunzi kuimarisha afya na kujenga misuli.
- Vyama vya michezo huweza pia kuwa msingi wa kupata chanzo cha riziki baadaye.
- Vyama vya wanafunzi ni msingi wa mshikamano na maridhiano.
(Mwalimu akadirie maudhui ya wanafunzi.)
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
Mwenye kovu sidhani kapona.- Msimulizi asimulie kisa kitakachoonyesha ukweli wa methali hii.
- Maana-Mtu ambaye amewahi kuwa mbaya hata akionekana kubadili mwenendo huenda akarudia maovu yake.
- Mtahiniwa aonyeshe:
- Makosa ambayo mhusika alifanya.
- Jinsi makosa hayo yalimfanya kubadili mwenendo wake.
- Kurudia makosa yale au mengine mabaya zaidi.
- Kisa ndicho muhimu si utangulizi
- Tunga kisa cha kusisimua na kumalizika kwa …..hivyo ndivyo ukurasa mpya katika kitabu cha maisha yangu ulivyofunguka.
- Mtahiniwa asimulie kisa kitakachoonyesha mabadiliko yaliyotokea katika maisha yake.mabadiliko haya yaweza kuwa mazuri au mabaya.
- Mtahiniwa atumie wakati uliopita ; aonyeshe matukio yaliyomfikisha katika mabadiliko haya.
- Kisa kioane na mdokezo aliopewa.
maudhui yasipungue 6 x 2 =12
Muundo –alama 4
Lugha -4
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili P1 Questions and Answers - Momaliche 4 cycle Post Mock Exams 2021/2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students