MOKASA Joint Evaluation Examination Kiswahili Karatasi ya 2 2016- Pre MOCK

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU (alama 15)
    Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao. Ni kutokana na kilio cha mwananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo serikali imejitolea sabili kubadili hali katika idara hiyo huku tume mbali mbali zilizobuniwa zikitoa mapendekezo muhimu ya kurekebisha idara hiyo. Matokeo ya hivi punde kutoka kwa shirika la Transparency International liliorodhesha idara ya polisi kama idara fisadi zaidi nchini, maoni ambayo yalisisitiziwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu. Ufisadi bado umekita mizizi katika idara ya polisi tangu mabadiliko yaanze upande wa trafiki na hata ndani ya polisi.

    Serikali imejitolea kupambana na ufisadi unaonekana kuwa kidonda ndugu katika idara ya polisi. Wananchi wanasema kuwa polisi ni mafisadi na kusahau kuwa ufisadi unashirikisha watu wawili na wote wanapaswa kufunguliwa mashtaka, lazima raia na polisi wazingatie hili. Na ili kuleta mabadiliko muhimu katika idara ya polisi, mapendekezo yote pamoja na ya tume zingine za hapo awali lazima yatekelezwa na kwa mujibu wa katiba mpya. Lazima mabadiliko yaanze kuanzia juu kwani maafisa wadogo hulazimiswa kuchukua hongo ili wapelekee wakubwa wao, ni lazima shughuli ya kuwachagua maafisa waliobora ifanyike kisheria ili mabadiliko yaanze kutoka kwa wakuu wa maafisa wa polisi.

    Polisi kidogo wameweza kubadili ile lugha yao ya matusi na ukali kwa rai. Raia nao hawajabadilika, bado wana uwoga dhidi ya polisi na itachukua muda kwani wanadhania kuwa kikosi ni kile kile cha kitambo. Kwa upande wa polisi, hakuna mageuzi yamefanyika. Unaposafiri kuja mjini polisi wangali wana chukua hongo kutoka kwa wenye matatu na kuwaruhusu kubeba kupita kiasi, pia usalama umedorora sana kwani kumekuwa na visa vingi vya mauaji hapa mjini. Ukiangalia maafisa wa polisi hakuna mageuzi makubwa yameshuhudiwa haswa kwa upande wa maafisa wa trafiki bado ni wale wale na ufisadi ungali upo.

    Mabadiliko ambayo tunataka ni ile polisi wasikae mahali kwa muda hadi wanajuana na mafisadi na majambazi. Maafisa wa polisi wanafaa kuhudumu katika kituo kimoja kwa muda usiozidi miaka mitatu. Kwa kufuata njia hiyo mabadiliko yatapatikana. Juhudi nyingi zikielekezwa katika kubadili kikosi cha polisi wananchi wanapaswa kuhamasishwa ili nao waweza kubadilika haswa kuhusuiana na mtazamo wao kwa maafisa wa polisi. Na huku tukijaribu kubadili maafisa wa polisi wananchi pia wanapaswa kuelimishwa ili waweze kubadili mtazamo wao kuhusu maafisa hao. Ni bayana kuwa ili kuweza kuleta mabadiliko ya kutamanika katika kikosi cha polisi na haswa katika kupambana na ufisadi uliokita mizizi wananchi sawia na maafisa wa polisi wanajukumu la pamoja kuleta mabadiliko hayo yatakayopelekea kuwepo kwa mlahaka mzuri kati ya maafisa wa polisi na raia. Hatimaye kuwepo kwa huduma bora itakayochangia pakubwa kuboresha uchumi wa taifa na kuafikiwa kwa ruwaza ya mwaka 2030.

    Maswali

    1. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka. (alama 1)
    2. Thibitisha kwamba ufisadi ni kidonda ndugu ukirejelea makala haya.. (alama2)
    3. Ni vipi ufisadi katika idara ya polisi unaweza kuzikwa katika kaburi la sahau? (alama2)
    4. ‘Wananchi ndio wanapaswa kulaumiwa kwa ufisadi.” Thibitisha. (alama 3)
    5. “ Serikali imepiga hatua katika kuleta mabadiliko katika idara ya polisi”. Onyesha kinaya cha usemi huu.(alama 2)
    6. Taja manufaa yoyote mawili yanayotokana na mabadiliko katika idara ya polisi (alama2)
    7. Eleza maana ya:
      1. Mlahaka
      2. Utepetevu
      3. Kujitolea sabili (alama 3)
  2. UFUPISHO (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata

    Kwa miaka na dahari, nchi nyingi za Asia, Amerika Kusini na Afrika, zimekuwa na mamilioni ya watoto wanaoteseka. Matatizo huwakumba kwenye hali nyingi. Si kielemu, si kiafya, si kiutamaduni na kimakuzi tu, bali hata kiuchumi. Nguvu zao na uwezo wao hufujwa kwa njia zinazokirihisha nyoyo. Wale wanaopenda maendeleo na kutilia nguvu haki za kibinadamu huudhiwa kupindukia.

    Wazazi wengi wa sehemu hizo wamekuwa wakiamini mambo kipuuzi. Wamekuwa wakidhani kuwa wingi ni hoja, lakini wazazi hawa huwapata watoto wengi wasioweza kuwatunza. Isitoshe, huwachukulia watoto kama sehemu ya mali yao badala ya kuwachukulia kuwa ni binadamu wenzao. Akili haziwapigi na kutambua kuwa, hata nao ‘vinyang’arika’, wakitunzwa vizuri na kupewa nafasi mwafaka za kuwainua kimaendeleo, wataweza kuwa watu wa kutajika katika jamii. Wazazi kama hao wanadhania ya leo ni leo tu, msema kesho ni mwongo. Dhana hizo finyu na potovu zimewapelekea kuthamini uzaaji wa watoto wengi ili watoto hawa wawe punda wa dobi. Wazazi hawa wanajihisi matajiri wa kupindukia wanaopata vijana wengi wa kuwasaidia katika kazi zao bure bilashi.

    Baadhi ya watoto hunyimwa nafasi ya kwenda shule. Wale wanaonjeshwa masomo kidogo, huachishwa kisomo hicho mapema. Sababu za kuhinishwa huko kwa kisomo zinafahamika vizuri na wahusika hao. Mara nyingi, huachishwa shule ili wawe mayaya wa watoto wenzao au wakafunge mifugo, kulima shambani, kusaidia biasharani na katika sekta za juakali. Watoto hawana nguvu za kukataa kwani ni kinyume cha utamaduni kuwapinga wazazi. Isitoshe, watoto hawa wanawategemea wazazi hao kwa kila kitu. Utiifu huu, ingawa una uzuri wake unazorotesha maendeleo kupindukia.

    Unyonge wa aina hii umefanya mashirika ya viwanda, ya mashamba kama ya chai, kahawa, ya pamba na ya juakali kuwatumia watoto vibaya bila ya kujali maslahi ya watoto hao. Baadhi ya watu wameanzisha mashirika ya uasherati na utumwa. Watoto wanateswa na kuingizwa kwenye majanga yanayotokana na ukimwi na mengine ya uzinifu. Kutokana na dhuluma hizi, watoto hukandamizwa na kupewa posho duni ya kuwapa uhai tu. Matajiri wamezidi kufutuka kiuchumi kutokana na jasho la watoto hao. Watoto hawapewi kinga zozote za kemikali wala kuonyeshwa jinsi ya kuzitumia kemikali hizo. Wakuu wao hutumia saikolojia duni za watoto kuwawezesha kujikuza kiuchumi. Huwapa viperemende hafifu na viungo ovyo ili watoto waimbe na kucheza ngoma za watu hao. Watoto, kwa kutojua, huwasifu wakuu wao badala ya kuwalaani kwa kuwanyonya hadi mifupani na kupewa vijipesa tu. Kwa kuwa ni watoto hawatambui kuwa wanahiniwa.

    Matajiri nao husahau kuwa watoto hao wakisoma vizuri hadi mwisho, wanaweza kutoa huduma bora nchini. Inadhihirika kuwa lengo potovu la watu hao ni kukwepa kulipa mishahara mikubwa kwa watu wazima. Lakini nasema si sawa kuwanyonya watoto. Matajiri hawa wangehisi vipi kama watoto wao nao wangefanyiwa hivyo? Ama ni yule ya mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu? Serikali zina mikono mirefu. Inafaa ziwachukulia hatua kali wazazi na maafisa wanaotumia watoto kama matambara mabovu. Watoto nao wanafaa kuzinduka na kutaka kusoma kinyuki. Inafaa wajue kuwa vipesa vya ujakazi ni sumu.

    Mashirika ya aina hiyo, inafaa yakipatikana na hatia, yapewe adhabu kali. Yalazimishwe kuwasomesha na kuwakimu watoto hao vilivyo, bila kuwanyanyasa ndipo wasome, kadri ya uwezo wao.

    Maswali
    1. Bila kupoteza maana iliyokusudiwa fupisha aya mbili za mwanzo kwa maneno (45-50) (al. 6, 1 utiririko)
      Maandalizi
      Jibu

    2. Kwa kuzingatia taarifa hii eleza namna maonevu dhidi ya watoto yameendelezwa.. tumia maneno (50-55) (al. 9, 1 utiririko)
      Matayarisho
      Jibu

  3. MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
    1. Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa, taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja. (alama 2)
    2. Bainisha muundo wa silabi katika neno (alama 2)
      Gongwa
    3. Eleza maana ya mofimu funge na kutoa mfano mwafaka (alama 1)
    4.  
      1. Eleza maana ya kiarifu. (alama 1)
      2. Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo (alama 1)
        Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.
    5. Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo. (alama 2)
      Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni.
    6. Bainisha matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika sentensi hii . (alama 2)
      Naomi atakupikia chai halafu aende kule uwanjani.
    7. Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni
    8. Tunga sentensi ukitumia kitenzi ‘-nywa’ katika kauli ya kutendeka. (alama 1)
    9. Tunga sentensi iliyo na kitenzi kishirikishi kilicho na kiambishi nafsi na wakati (alama1 )
    10.  
      1. Eleza dhana ya kishazi. (alama 1)
      2. Onyesha aina za vishazi kwa kutumia sentensi moja. (alama 1)
    11. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale. (alama 4)
      Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.
    12. Yakinisha (alama 2)
      Mgonjwa huyo hakupona wala kurejea nyumbani
    13. Sahihisha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Mgeni ambaye aliyekuja atarudi jana.
    14. Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana
    15. Andika sentensi ifuatayo katika wingi. (alama 1)
      Ua unaozunguka nyumba una ua lililopandwa.
    16. Weka nomino hizi katika ngeli zake (alama 1)
      1. Mbalungi
      2. Mturuki
    17. Andika katika hali ya udogo. (alama 2)
      Alishikwa na jipu ambalo lilivimbisha kidole chake cha mguu mithili ya pera.
    18. Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
      “Lo! Kumbe wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo.
    19. Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo. (alama 2)
      1. Kubahatika
      2. Ubahaili
    20. Eleza maana tatu za sentensi ifuatayo (alama 3)
      Mama alimwimbia mwanawe.
    21. Tunga sentensi moja kutofautisha maana mbili ya neno ziwa. (alama 2)

  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)

    1. Eleza maana ya istilahi hizi; (alama 2)
      1. Usanifishaji
      2. Lahaja
    2. Taja sifa zozote nne za lugha yoyote ile. (alama 4)
    3. Eleza mambo yanayochangia makosa ya kisarufi na ya kimatamshi katika lugha ya Kiswahili (alama 4)

MARKING SCHEME

  • UFAHAMU (alama 15)
    Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao. Ni kutokana na kilio cha mwananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo serikali imejitolea sabili kubadili hali katika idara hiyo huku tume mbali mbali zilizobuniwa zikitoa mapendekezo muhimu ya kurekebisha idara hiyo. Matokeo ya hivi punde kutoka kwa shirika la Transparency International liliorodhesha idara ya polisi kama idara fisadi zaidi nchini, maoni ambayo yalisisitiziwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu. Ufisadi bado umekita mizizi katika idara ya polisi tangu mabadiliko yaanze upande wa trafiki na hata ndani ya polisi.

    Serikali imejitolea kupambana na ufisadi unaonekana kuwa kidonda ndugu katika idara ya polisi. Wananchi wanasema kuwa polisi ni mafisadi na kusahau kuwa ufisadi unashirikisha watu wawili na wote wanapaswa kufunguliwa mashtaka, lazima raia na polisi wazingatie hili. Na ili kuleta mabadiliko muhimu katika idara ya polisi, mapendekezo yote pamoja na ya tume zingine za hapo awali lazima yatekelezwa na kwa mujibu wa katiba mpya. Lazima mabadiliko yaanze kuanzia juu kwani maafisa wadogo hulazimiswa kuchukua hongo ili wapelekee wakubwa wao, ni lazima shughuli ya kuwachagua maafisa waliobora ifanyike kisheria ili mabadiliko yaanze kutoka kwa wakuu wa maafisa wa polisi.

    Polisi kidogo wameweza kubadili ile lugha yao ya matusi na ukali kwa rai. Raia nao hawajabadilika, bado wana uwoga dhidi ya polisi na itachukua muda kwani wanadhania kuwa kikosi ni kile kile cha kitambo. Kwa upande wa polisi, hakuna mageuzi yamefanyika. Unaposafiri kuja mjini polisi wangali wana chukua hongo kutoka kwa wenye matatu na kuwaruhusu kubeba kupita kiasi, pia usalama umedorora sana kwani kumekuwa na visa vingi vya mauaji hapa mjini. Ukiangalia maafisa wa polisi hakuna mageuzi makubwa yameshuhudiwa haswa kwa upande wa maafisa wa trafiki bado ni wale wale na ufisadi ungali upo.

    Mabadiliko ambayo tunataka ni ile polisi wasikae mahali kwa muda hadi wanajuana na mafisadi na majambazi. Maafisa wa polisi wanafaa kuhudumu katika kituo kimoja kwa muda usiozidi miaka mitatu. Kwa kufuata njia hiyo mabadiliko yatapatikana. Juhudi nyingi zikielekezwa katika kubadili kikosi cha polisi wananchi wanapaswa kuhamasishwa ili nao waweza kubadilika haswa kuhusuiana na mtazamo wao kwa maafisa wa polisi. Na huku tukijaribu kubadili maafisa wa polisi wananchi pia wanapaswa kuelimishwa ili waweze kubadili mtazamo wao kuhusu maafisa hao. Ni bayana kuwa ili kuweza kuleta mabadiliko ya kutamanika katika kikosi cha polisi na haswa katika kupambana na ufisadi uliokita mizizi wananchi sawia na maafisa wa polisi wanajukumu la pamoja kuleta mabadiliko hayo yatakayopelekea kuwepo kwa mlahaka mzuri kati ya maafisa wa polisi na raia. Hatimaye kuwepo kwa huduma bora itakayochangia pakubwa kuboresha uchumi wa taifa na kuafikiwa kwa ruwaza ya mwaka 2030.

    Maswali

    1. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka. (alama 1)

       Mabadiliko katika idara ya polisi

    2. Thibitisha kwamba ufisadi ni kidonda ndugu ukirejelea makala haya.. (alama2)

      -Ufisadi ni kero ambalo linaendelea kutatiza kila mtu katika maisha ya kila siku
      -Ufisadi kuonekana ..kama kitu ambacho ni ngumu kulitatua kabisa..

    3. Ni vipi ufisadi katika idara ya polisi unaweza kuzikwa katika kaburi la sahau? (alama2)

      -Lazima mabadiliko yaanzie katika maafisa wa juu zaidi kabla ya kuwafikia maafisa wadogo. Kwa sababu wao huchukua hongo zinazochukuliwa na wadogo wao
      -Raia waweza pia kuwajibika wanapojiingiza katika ufisadi ......

    4. ‘Wananchi ndio wanapaswa kulaumiwa kwa ufisadi.” Thibitisha. (alama 3)

      -Raia wanatoa hongo kwa polisi
      -Uwogo wa wananchi dhidi ya polisi

    5. “ Serikali imepiga hatua katika kuleta mabadiliko katika idara ya polisi”. Onyesha kinaya cha usemi huu.(alama 2)

      -Polisi wa trafiki wanachukua hongo barabarani
      -Usalama kudorora mijini

    6. Taja manufaa yoyote mawili yanayotokana na mabadiliko katika idara ya polisi (alama2)

      -Kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya polisi na raia
      -Uchumi kuimarika

    7. Eleza maana ya:
      1. Mlahaka

        -uhusiano mzuri

      2. Utepetevu

        -ulegevu

      3. Kujitolea sabili (alama 3)

         kujitolea kabisa

  • UFUPISHO (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata

    Kwa miaka na dahari, nchi nyingi za Asia, Amerika Kusini na Afrika, zimekuwa na mamilioni ya watoto wanaoteseka. Matatizo huwakumba kwenye hali nyingi. Si kielemu, si kiafya, si kiutamaduni na kimakuzi tu, bali hata kiuchumi. Nguvu zao na uwezo wao hufujwa kwa njia zinazokirihisha nyoyo. Wale wanaopenda maendeleo na kutilia nguvu haki za kibinadamu huudhiwa kupindukia.

    Wazazi wengi wa sehemu hizo wamekuwa wakiamini mambo kipuuzi. Wamekuwa wakidhani kuwa wingi ni hoja, lakini wazazi hawa huwapata watoto wengi wasioweza kuwatunza. Isitoshe, huwachukulia watoto kama sehemu ya mali yao badala ya kuwachukulia kuwa ni binadamu wenzao. Akili haziwapigi na kutambua kuwa, hata nao ‘vinyang’arika’, wakitunzwa vizuri na kupewa nafasi mwafaka za kuwainua kimaendeleo, wataweza kuwa watu wa kutajika katika jamii. Wazazi kama hao wanadhania ya leo ni leo tu, msema kesho ni mwongo. Dhana hizo finyu na potovu zimewapelekea kuthamini uzaaji wa watoto wengi ili watoto hawa wawe punda wa dobi. Wazazi hawa wanajihisi matajiri wa kupindukia wanaopata vijana wengi wa kuwasaidia katika kazi zao bure bilashi.

    Baadhi ya watoto hunyimwa nafasi ya kwenda shule. Wale wanaonjeshwa masomo kidogo, huachishwa kisomo hicho mapema. Sababu za kuhinishwa huko kwa kisomo zinafahamika vizuri na wahusika hao. Mara nyingi, huachishwa shule ili wawe mayaya wa watoto wenzao au wakafunge mifugo, kulima shambani, kusaidia biasharani na katika sekta za juakali. Watoto hawana nguvu za kukataa kwani ni kinyume cha utamaduni kuwapinga wazazi. Isitoshe, watoto hawa wanawategemea wazazi hao kwa kila kitu. Utiifu huu, ingawa una uzuri wake unazorotesha maendeleo kupindukia.

    Unyonge wa aina hii umefanya mashirika ya viwanda, ya mashamba kama ya chai, kahawa, ya pamba na ya juakali kuwatumia watoto vibaya bila ya kujali maslahi ya watoto hao. Baadhi ya watu wameanzisha mashirika ya uasherati na utumwa. Watoto wanateswa na kuingizwa kwenye majanga yanayotokana na ukimwi na mengine ya uzinifu. Kutokana na dhuluma hizi, watoto hukandamizwa na kupewa posho duni ya kuwapa uhai tu. Matajiri wamezidi kufutuka kiuchumi kutokana na jasho la watoto hao. Watoto hawapewi kinga zozote za kemikali wala kuonyeshwa jinsi ya kuzitumia kemikali hizo. Wakuu wao hutumia saikolojia duni za watoto kuwawezesha kujikuza kiuchumi. Huwapa viperemende hafifu na viungo ovyo ili watoto waimbe na kucheza ngoma za watu hao. Watoto, kwa kutojua, huwasifu wakuu wao badala ya kuwalaani kwa kuwanyonya hadi mifupani na kupewa vijipesa tu. Kwa kuwa ni watoto hawatambui kuwa wanahiniwa.

    Matajiri nao husahau kuwa watoto hao wakisoma vizuri hadi mwisho, wanaweza kutoa huduma bora nchini. Inadhihirika kuwa lengo potovu la watu hao ni kukwepa kulipa mishahara mikubwa kwa watu wazima. Lakini nasema si sawa kuwanyonya watoto. Matajiri hawa wangehisi vipi kama watoto wao nao wangefanyiwa hivyo? Ama ni yule ya mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu uchungu? Serikali zina mikono mirefu. Inafaa ziwachukulia hatua kali wazazi na maafisa wanaotumia watoto kama matambara mabovu. Watoto nao wanafaa kuzinduka na kutaka kusoma kinyuki. Inafaa wajue kuwa vipesa vya ujakazi ni sumu.

    Mashirika ya aina hiyo, inafaa yakipatikana na hatia, yapewe adhabu kali. Yalazimishwe kuwasomesha na kuwakimu watoto hao vilivyo, bila kuwanyanyasa ndipo wasome, kadri ya uwezo wao.

    Maswali
    1. Bila kupoteza maana iliyokusudiwa fupisha aya mbili za mwanzo kwa maneno (45-50) (al. 6, 1 utiririko)
      Maandalizi
      Jibu

    2. Kwa kuzingatia taarifa hii eleza namna maonevu dhidi ya watoto yameendelezwa.. tumia maneno (50-55) (al. 9, 1 utiririko)
      Matayarisho
      Jibu

  • MATUMIZI YA LUGHA (alama 40)
    1. Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa, taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja. (alama 2)

      Vipasuo - /p/,/b/,/t/,/d/,/j/,/k/,/g/
      Kipsuo-kwamizo /ch/
      Kitambaza /l/
      Kimandende /r/

    2. Bainisha muundo wa silabi katika neno (alama 2)
      Gongwa

      Go – KI
      Ngwa – KKI

    3. Eleza maana ya mofimu funge na kutoa mfano mwafaka (alama 1)

       Mofimu ambazo haziwezi kujisimamia. Mfano a-na-som-a

      1. Eleza maana ya kiarifu. (alama 1)

         Sehemu ya sentensi ambayo hutoa habari kuhusu kiima

      2. Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo (alama 1)
        Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.

         Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu

    4. Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo. (alama 2)
      Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni.

      Mwanafunzi – shamirisho kitondo
      Dawati – shamirisho kipozi

    5. Bainisha matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika sentensi hii . (alama 2)
      Naomi atakupikia chai halafu aende kule uwanjani.

      Atakupikia –nafsi ya pili
      Kule-mahali

    6. Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni

      Mgeni-kivumishi cha nomino
      Na-kuhusishi cha

    7. Tunga sentensi ukitumia kitenzi ‘-nywa’ katika kauli ya kutendeka. (alama 1)

       Maziwa haya yananyweka.

    8. Tunga sentensi iliyo na kitenzi kishirikishi kilicho na kiambishi nafsi na wakati (alama1 )

       Wairia amekuwa stadi katika Kamari

      1. Eleza dhana ya kishazi. (alama 1)

         Fungu la maneno lenye uhusiano wakiima na kiarifu ambalo linaweza kujisimamia ama kutojisimamia kimaana.

      2. Onyesha aina za vishazi kwa kutumia sentensi moja. (alama 1)

         Mwanafunzi aliyesoma kwa bidi alipita mtihani.

    9. Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale. (alama 4)
      Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.

      S→KN+KT
      KN→W
      W→O(KAPA)
      KT→T+KN+E+S
      T→alimwona
      N→mamba
      E →majini
      S→ alipopigambizi

    10. Yakinisha (alama 2)
      Mgonjwa huyo hakupona wala kurejea nyumbani

      -Mgonjwa huyu alipona na kurejea nyumbani.

    11. Sahihisha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Mgeni ambaye aliyekuja atarudi jana.

      Mgeni ambaye alikuja alirudi jana.
      Au
      Mgeni aliyekuja alirudi jana.

    12. Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2)
      Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana

      Juma: Maria, ulimwona Farida?
      Maria: La, hakuwepojana.

    13. Andika sentensi ifuatayo katika wingi. (alama 1)
      Ua unaozunguka nyumba una ua lililopandwa.

       Nyua zinazozunguka majumba zina maua yaliyopandwa.

    14. Weka nomino hizi katika ngeli zake (alama 1)
      1. Mbalungi

         U-I

      2. Mturuki

         A-WA

    15. Andika katika hali ya udogo. (alama 2)
      Alishikwa na jipu ambalo lilivimbisha kidole chake cha mguu mithili ya pera.

       Kilishikwa na kijipu ambacho kilikivimbisha kijidole chake cha kiguu mithili ya kipera.

    16. Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
      “Lo! Kumbe wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo.

      Omari alishangaa baada ya kumwona kisura yule kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa.
      Au
      Baada ya kumwona kisura yule,Omari alishangaa kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa.

    17. Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo. (alama 2)
      1. Kubahatika

        -kubahatika kama mwana aliyezaliwa Ijumaa

      2. Ubahaili

         –mkono birika

    18. Eleza maana tatu za sentensi ifuatayo (alama 3)
      Mama alimwimbia mwanawe.

      Kwa niaba ya
      Sababu ya
      Kuelekeza wimbo kwa mwanawe

    19. Tunga sentensi moja kutofautisha maana mbili ya neno ziwa. (alama 2)

  • ISIMU JAMII (ALAMA 10)

    1. Eleza maana ya istilahi hizi; (alama 2)
      1. Usanifishaji

        -Hali yakuchukua lugha moja au mojawapo ya lahaja na kuifanyia marekebisho ya kimatamshi, kisarufi na kiisimu ilikitumike katika muktadha rasmi.

      2. Lahaja

        -Lahaja ni namna mbalimbali ya kuzungumza lugha moja
        Au
        -Vijilugha vidogovidogo vinavyoibuka kutoka lugha kuu

    2. Taja sifa zozote nne za lugha yoyote ile. (alama 4)

      -kila lugha inasauti zake zilizo tofauti na nyingine
      -Lugha ina uwezo wa kukua
      -Lugha inaweza kufa kwa msamiati wake kupotea
      -Lugha zote ni sawa

    3. Eleza mambo yanayochangia makosa ya kisarufi na ya kimatamshi katika lugha ya Kiswahili (alama 4)

      -makosa ya kimakusudi
      -kutofahamu kanuni za kisarufi
      -Mtu kuzungumza haraka
      -Uhamishaji wa kanuni za lugha moja hadi nyingine
      -Hali ya kiakili wakati mtu anapotumia lugha
      -Ujumuishaji wa kanuni zinazotawala sarufi katika muktadha mmoja
      -Athari za lugha ya kwanza

Join our whatsapp group for latest updates

Download MOKASA Joint Evaluation Examination Kiswahili Karatasi ya 2 2016- Pre MOCK.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest