KISWAHILI KARATASI YA 1 - 2020 KCSE PREDICTION SET 1 (QUESTIONS AND ANSWERS)

Share via Whatsapp

MAAGIZO

 • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
 • Kisha changua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400
 • Kila insha ina alama 20
 1. Insha ya lazima
  Andika tahariri kwa gazeti la raia ukielezea hatua zinazochukuliwa nchini ili kumwendeleza kielimu Mtoto msichana.
 2. Ufisadi ndicho kikwazo kikuu katika maendeleo ya uchumi wa taifa lolote. Thibitisha
 3. Matikiti na matango ndiyo maponya njaa.
 4. Andika insha itakayomalizikia kwa;
  ........aha! kumbe mwungwana akivulianguo huchutama. Sitaisahau siku hiyo kwani sijawahi kufedheheka maishani kama nilivyoaibika.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Swali la kwanza
  Tahariri kwa gazeti la raia
  1. sura
   -iwe na kichwa
   -Iwe na tarehe
   -Iwe na utangulizi
   -Iwena mwili/maelezokiaya
   -Yaweza kuwa na maoni au msimamo wa mhariri au msimamo wa gazeti
   -Iwe na hitimisho k.mjinala mhariri na wadhifa wake
  2. MAUDHUI; kuendeleza msichana kielimu
   -kupiga vita ndoa za mapema
   -kupigamarufukuajira ya watoto
   -wasichana wapewe nafasi ya kuendelezana masomo ya baada kujifungua
   -alama za kujiungana vyuo vikuukupunguzwe kwa wasichana
   -elimu bila malipo kwa watoto wa shule za msingi na za upili
   -kutoa msaada wa karo kwa familia maskini
   -kujenga shule zaidi za wasichana
   -mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga shule na vyuo
   -kuhamasisha wazazi kuhusu umuhimu wa elimu ya mtoto msichana
   -adhabu kali kwawabakaji
 2. Swali la pili
  1. ufisadi kama kikwazo
   -hii ni insha ya hoja
   -hoja ziungemkono kauli hii
   -mtahiniwa akubali anena kauli hii
   -mtahiniwa ahusishe ufisadi unavyodumaza uchumi wa nchi
  2. hoja
   -watu kupewa kazi wasizoweza
   -wanaostahili kazi hawapati
   -Biasharaharamuhuwapunja raia
   -Wawekezajihuvunjwa moyo
   -Miradi ya maendeleo kukwama /kutomalizwa
   -Baadhi ya maeneo ya nchi kupuuzwa kimaendeleo
   -Nchi kukosa misaada
   -Taifa hutumia pesa nyingi kurekebisha ufisadi-Sifa za nchi kuharibika
   -Uhalifu kuenea/kukosa usalama
 3. Swali la tatu
  1. methali;matikiti na matango ndiyo maponya njaa
   - Hii ni methali
   - Mtahiniwa atunge kisa/visa kuonyesha ukweli wamethali hii
   - Kisa kionyeshe sehemu mbili za methali
   1. upuuzaji/kudunishakitu jambo au mtu
   2. kitu ,mtu au jambo hilo lijeliwe ni la manufaa Baadaye wakati wa shid
  2. msamiati wa methali
   -matikiti na matango= aina ya vyakula visivyothaminiwa sana
   -maponya=yanayookoa/yanayofaa
   -njaa=shida
  3. maana ya methali
   vitu tunavyodunisha/tunavyo puuza huweza kuwa na msaada mkubwa wakati wa shida .kitu tulichonacho mkononi mwetu ndicho kinaweza kututoa taabuni wakati wa shida hivyo basi tusiidharau
 4. Swali la nne
  1. insha ya mdokezo
   -hii ni insha ya mdokezo na mdokezo huu ni wa kumalizia
   -mtahiniwa atunge kisa kinachomalizikakwa dondoo hili
   -mtahiniwa ajihusishe katika kisa hiki
   -Mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza
   -kisa kiwe na tendo/jambo bayakisiri
   -Jambo hili linawekwa wazi
   -Mhusika anakosa uso yaani anaaibika sana
  2. methali; muungwana akivuliwa nguo huchutama
   Maana; uovu wa mtu anayedhaminiwa ni mwema unapofichuliwa yeye huaibika
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI KARATASI YA 1 - 2020 KCSE PREDICTION SET 1 (QUESTIONS AND ANSWERS).


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest