Maagizo
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine kutoka tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20..
MASWALI
- Wewe ni mhariri wa gazeti la Msemakweli. Andika tahariri kuhusu athari za baa la njaa na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo hili.
- Matumizi ya afyuni katika taasisi za masomo nchini ni suala muhali kutatuliwa. Jadili.
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali: Mtaka yote hukosa yote.
- Tunga kisa kinachoanza kwa maneno haya:
Ilinichukua muda mrefu kusadiki niliyoyapata......
MARKING SCHEME
SWALI LA LAZIMA
Ni insha ya kiuamilifu.
Sura /mtindo wa tahariri uzingatiwe
- Kichwa- Kiandikwe kwa herufi kubwa
- Jina la gazeti - Msemakweli litumiwe.
- Tarehe.
- Jina la mhariri
Athari za baa la njaa
- Vifo vya mifugo.
- Shule kufungwa kutokaba na ukosefu wa chakula.
- Kuhama kwa jamii kutafuta chakula.
- Vifo vya binadamu/watu
- Maradhi mbalimbali kwa mfano utapiamlo.
- Pato kubwa la kitaifa linatumiwa kushughulikia njaa.
- Kudumaa kwa maendeleo ya wananchi na taifa.
- Wanasiasa na mataifa kujinufaisha wakitumia fursa hii.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUKABILIANA NA BAA LA NJAA
- Wakulima kuhimizwa kupanda mimea inayochukua muda mfupi kukomaa katika sehemu zinazopata mvua chache.
- Wakulima kupewa mbegu za kupanda bila malipo.
- Serikali kutangaza baa la njaa kama janga la taifa.
- Kubuniwa kwa wizara ya mipango maalum inayoshughulikia katizo hili miongoni mwa mengine.
- Misaada ya chakula kwa wahasiriwa kutoka kwa serikali na wahisani wengine.
- Serikali kuwahimiza wafugaji kuuza mifugo wao ili kuepuka ukosefu wa nyasi/lishe na maji.
- Serikali kununua mifugo kutoka kwa wakulima/wafugaji walioathiriwa na baa la njaa.
- Wakulima kupanda mimea inayoweza kuhimili ukame kama vile mihogo na mtama.
- Serikali kujenga mabwawa ya maji ili kukusanya maji wakati wa mvua ambapo wakulima wataweza kunyunyizia mimea tao maji wakati wa kiangazi.
- Serikali kutenga pesa ili kuwezesha shirika la nafaka nchini kununua na kuhifadhi mazao kutoka maeneo yanayojitosheleza kwa mvua.
SWALI LA PILI
KUUNGA MKONO
- Shinikizo la rika kuwasukuma vijana kutumia afyuni.
- Sheria hafifu inayowaruhusu wauzaji na watumizi kuendelea na shughuli zao.
- kuporomoka kwa maadili ya jamii na kushindwa kwa wazazi kuwathibiti watoto wao kwa kutowapa mawaidha.
- Ukosefu/ Uchache wa wataalamu wa kutoa nasaha na mwelekeo kwa wanafunzi shuleni.
- Vyombo vya habari vinachangia pakubwa katika kuwashawishi vinajana kutumia afyuni. Kama vile redio, runinga.
- Upungufu wa vielelezo/mifano katika jamii.
- Ufisadi -Wananaowauzia vijana mihadarati hutumia hongo kufanikisha maovu haya.
KUPINGA.
- Kutumia sheria kali zitakazowazuia watumiaji na wauzaji wa afyuni kuendeleza shughuli zao.
- Kuwashauri wazazi kuwa mstari wa mbele kuwazungumzia na kuwashauri watoto wao.
- Kuthibiti vyombo vya habari katika harakati za kupigana na matumizi ya afyuni.
- Kuwaajiri na kuongeza wataalamu wa ushauri shuleni na vijijini.
- Serikali kukabiliana na ufisadi katika vitengo vyote.
- Kuwashauri wanafunzi kujisimamia kimawazo na kuepuka shinikizo la rika.
- Vijana kupewa nasaha kuhusu athari za matumizi ya afyuni.
TANBIHI
- Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kuunga na moja/zaidi za kupinga.
- Mtahiniwa anaweza kuwa na hoja nyingi za kupinga na moja /zaidi za kuunga.
- Mtahiniwa atoe msimamo wake.
- Anayekosa kushughulikia pande zote mbili asipitishe alama 10.
- Mtahiniwa anaweza kutoa hoja sawa pande almuradi atoe msimamo wake.
- Kadiria hoja zingine za mtahiniwa.
SWALI LA TATU.
- Kisa kinafaa kioane na methali
- Mwanafunzi aonyesha sehemu zote mbili za methali.
- Dhana ya mtaka yote ionekane vizuri.
- Dhana ya kukosa yote ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja.
Maana : Anayetaka vitu vingi kwa tamaa hawi na mwisho mzuri.
SWALI LA NNE
- Mtahiniwa aweze kujenga kisa ambacho kinamhusisha yeye mwenyewe kama mhusika mkuu.
- Akimjenga mhusika mkuu mwingine atakuwa anepotoka na hivo basi atuzwe 03/20.
- Mtahiniwa asibadili wakati uliohusika katika swali .Akifanya hivyo atakuwa amepotoka.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bunamfan Post Mock 2021 Exams.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students