Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Bunamfan Post Mock 2021 Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO KWA MTAHINIWA

  • Jibu maswali yote.
  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Ushauri na uelekezaji ni mojawapo ya mikakati ambayo inatumiwa na taasisi na mashirika mengi katika kurekebisha tabia. Msimamo wa kijadi kuwa adhabu kali ndiyo njia mufti ya kumshinikiza binadamu kuacha mienendo hasi unaendelea kufifia na mahali pake kutwaliwa na nasaha na ushawishi. Hata katika mazingira magumu kama gerezani, ushauri na uelekezaji umeonekana kuzaa matunda kwa kuwasaidia wafungwa kubadili mienendo hasi na kukabiliana na makali ya matendo yao.

    Kila mwanajamii, wazee kwa vijana, wake kwa waume, wenye furaha kwa wenye majonzi huhitaji nasaha. Nasaha humwezesha mtu kustahimili hali ngumu katika maisha. Wanaougua magonjwa sugu kama vile iri huhitaji ushauri ili kuishi kwa mitazamo chanya na kupunguza makali ya unyanyapaa na hali ya kujihurumia inayotokana na maradhi hayo.

    Halikadhalika, binadamu huhitaji mawaidha wakati anapovuka kutoka daraja moja la maisha hadi jingine. Kila awamu katika maisha ya binadamu huwa na changamoto, majukumu na matarajio yake. Maarusi, kwa mfano, huhitaji nasaha ya kuwawezesha kukabiliana na changamoto za ndoa. Aidha vijana wanaotiwa jandoni hihitaji ushauri wa kuwasaidia kuyamudu majukumu ya utuuzima. Si ajabu kuwa tangu jadi manyakanga wamekuwa wakiwausia wanaotiwa jandoni kuhusu kunga za utuuzima.

    Ingawa kila mwanajamii anahitaji ushauri na uelekezaji, vijana ndio wanaouhitaji zaidi kwa sababu hawana uzoefu mpana wa maisha. Vijana wanaohitimu masomo ya shule za upili, kwa mfano, wanahitaji kuelekezwa kuhusu taaluma katika vyuo vikuu, umuhima na mahitaji ya taaluma hizo. Isitoshe, wakati wa kukfanya mitihani vijana huhitaji nasaha.

    Mazingira ya binadamu hubadilika, nayo maisha yake hutwaa mabadiliko yanayotokana na hali mpya. Baadhi ya watu wanapojipata katika mazingira mageni wasiyoyaweza, hupatwa na woga au unyonge Fulani ambao huenda ukawaathiri. Wengine, pengine kwa sababu ya maisha duni ya awali, huweza kuathiriwa na kujiona kuwa wenye thamani ya chini wakijilinganisha na wenzao. Kuna wanafunzi au hata wafanyikazi ambao kwa sababu ya kutofikia malengo yao shuleni au kazini, hufa moyo na hata kutaka kuiacha shule au kazi hiyo. Watu kama hawa huhitaji nasaha ili wajikubali jinsi walivyo na hata waweze kutumia udhaifu wao kuboresha maisha yao ya usoni.

    Wengi hudhani kuwa wanaohitaji nasaha ni wale wenye matatizo tu. Ukweli ni kwamba, hata wale ambao wanaonekana kuwa na furaha na vyeo wanahitaji ushauri wa aina Fulani. Wenye mali, kwa mfano, wanaweza kushauriwa kuhusu namna ya kuwekeza ili wasifilisike. Viongozi nao wanahitaji nasaha ili waandame sera bora za uongozi pamoja na jinsi ya kuishi kwa mwamana na wanajamii wenzao.

    Ushauri na uelekezaji, kwa hakika, unahitajika katika nyanja zote za maisha. Ni muhimu kukumbuka kuwa ushauri huanzia nyumbani. Mzazi au mlezi ndiye mshauri wa kwanza. Haifai wazazi kuchelea kuwashauri watoto wao mapema, kwa maana mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.

    Maswali
    1. Ipe taarifa hii anwani mwafaka. (alama 1)
    2. Tofautisha urekebishaji tabia wa kijadi na wa kisasa. (alama 2)
    3. Taja mazingira yoyote manne ambapo binadamu huhitaji nasaha na uelekezaji. (alama 4)
    4. Eleza umuhimu wa kushauri watu wafuatao: (alama 2)
      1. Viongozi.
      2. Wenye mali.
    5. Wazazi wasiowausia watoto wao wataathirika vipi hatimaye? (alama 2)
    6. Andika methali yoyote inayohusiana na nasaha. (alama 1)
    7. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika taarifa: (alama 3)
      1. Unyanyapaa.
      2. Manyakanga
      3. Mitazamo chanya.
  2. UFUPISHO (ALAMA 15)
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali:
    Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha husitawisha ufahamu wetu wa mambo tusomayo. Mazoezi katika kuandika husitawisha ufahamu katika kusoma kwa sababu katika kuandika ni lazima tujaribu kuyatumia maneno vizuri na kufahamu ugumu wa usemi. Twajifunza matumizi ya kugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine wakizungumza. Lugha tusomayo ikiwa imeandikwa hasa huwa ni aina ya lugha ya mazungumzo vile vile. Kuna ujuzi mwingi katika kuzungumza upatikanao katika shule – kama vile michezo ya kuigiza, hotuba, majadiliano na mazungumzo katika darasa na haya yote husaidia katika uhodari wa matumizi ya lugha.

    Ujuzi wa kila siku hutasaidia katika maendeleo ya kusoma na usitawi wa msamiati. Ikiwa mwanafunzi amemwona ndovu hasa, atakuwa amejua maana ya neno ndovu vizuri zaidi kuliko mwanafunzi ambaye hajapata kumwona ndovu bali ameelezwa tu vile alivyo. Vile vile ujuzi wa kujionea sinema au michoro husaidia sana katika kusoma. Kwa hivyo kwa njia fulani mambo yote juu ya ujuzi wa kila siku husaidia kufahamu mambo yaliyoandikwa. Ikiwa mwanafunzi ana huzuni au ana furaha, akiwa mgonjwa au amechoka au amesifiwa, haya yote ni ujuzi. Wakati ujao mwanafunzi asomapo juu ya mtu ambaye amepatikana na mambo kama hayo hana budi kufahamu vizuri zaidi.

    Karibu elimu yote ulimwenguni huwa imeandikwa vitabu lakini lugha zote hazina usitawi sawa kuhusu fasihi. Kwa bahati mbaya lugha nyingine hazijastawi sana na hazina vitabu vingi lakini katika lugha nyingine karibu mambo yote yanayohusiana na elimu huweza kupatikana katika vitabu. Inambidi mwanafunzi anayejifunza asome vitabu au majarida juu ya sayansi au siasa au historia, lakini haimbidi kusoma tu juu ya taaluma fulani anayojifunza. Inafaa asome juu ya michezo, mambo ya shani, na juu ya mahali pageni ili kupata ujuzi wa mambo mengi mbali mbali.

    Maswali
    1. Fupisha aya za kwanza mbili kwa kutumia maneno 65. (alama10,2 za utiririko)
      Nakala chafu
      Jibu:
    2. Kwa kuzingatia habari zote muhimu na bila kupoteza maana asilia, fupisha aya ya mwisho.
      Maneno 30, alama 5, 1 ya utiririko).
      Maandalizi:
      Jibu:
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1.  Andika maneno yenye sifa zifuatazo za sauti:
      1. Kilainisho ghuna cha midomo, irabu ya mbele-juu, kipua ghuna cha midomo, kizuiwa ghuna na irabu ya nyuma-wastani. (alama 1)
      2. Kikwaruzo hafifu cha ufizi, irabu ya chini-kati, kikwamizo cha mdomo-meno hafifu, irabu ya mbele-juu. (alama 1)
    2. Tunga sentensi ukitumia nomino ya ngeli ya KU pamoja na kirai husishi cha uhusiano. (alama 2)
    3. Ainisha uamilifu wa kisarufi wa mofimu katika kitenzi hiki. (alama 3)
      Kilivijisha.
    4. Yakinisha kwa udogo ukitumia kiambishi cha masharti ya uwezekano. (alama 2)
      Mtoto aliyeiba kitabu hajakamatwa.
    5. Andika upya sentensi kulingana na maagizo. (alama 1)
      Kiroboto huyo alituuma.Kiroboto aliuawa.(Tumia kivumishi kirejeshi cha kati kuunganisha sentensi hizi.)
    6. Eleza Matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mola atakukirimu ukimtolea sadaka.
    7. Andika upya sentensi hii kwa wakati ujao hali katavu. (alama 2)
      Mwanariadha alishiriki mbio za Tokyo.
    8. Tunga sentensi moja kutofautisha vitate mji na mchi. (alama 2)
    9. Unda kitenzi kutokana na nomino maskani, kisha ukitungie sentensi. (alama 2)
    10. Bainisha kiima na yambwa katika sentensi hii. (alama 2)
      Omari alipewa vipuli na fundi stadi kwa bahasha.
    11. Tunga sentensi katika hali ya wastani ukitumia kihusishi cha hali. (alama 2)
    12. Ainisha aina za vishazi katika sentensi hii. (alama 2)
      Marekebisho ya katiba ya BBI yatapita iwapo wananchi watahusishwa.
    13. Changanua sentensi hii kwa kielelezo cha mstari. (alama 2)
      Zohali na Zuhura ni majina ya sayari.
    14. Tunga sentensi moja ya kuonyesha Matumizi mawili ya vielezi vya silabi moja. (alama2)
    15. Andika kinyume cha maneno yafuatayo. (alama 2)
      1. Dhahiri………………………………………………………………
      2. Kavu…………………………………………………………………
    16. Tambua hali katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
      Ukulima wa sampuli hii wasumbua wengi.
    17. Eleza maana ya msemo shika sikio. (alama 1)
    18. Tumia kibadala cha kiasi cha kuonyesha nafasi katika orodha kwenye sentensi. (alama 2)
    19. Andika kwa wingi sentensi hii. (alama 2)
      Ukwato wa mnyama huyo aliufikisha ufuoni.
    20.  
      1. Tunasema baraza la wazee……………………wa wagomaji na ………..…………la nafaka. (alama 2)
      2. Audhubilahi ni tunapoapa………………….tunapokana na …………………………...tunapohimiza. (alama 2)
  4. ISIMU JAMII ( ALAMA 10)
    Mtu 1: Je, familia ya mahabusu huyo imetoa bond?
    Mtu 2 : Idont think so. Na wakiendelea kuchelewa huyo atapandishwa...
    1. Tambua sajili ya kifungu hiki. ( alama 2)
    2. Bainisha sifa nane za sajili hii. ( alama 8)

MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU
  2. UFUPISHO
    1.  
      1. Kila jambo tufanyalo kuhusiana na lugha hustawisha ufahamu wetu.
      2. Mazoezi ya kuandika hustawisha ufahamu wa kusoma.
      3. Twajifunza matumizi ya lugha katika kuzungumza na kuwasikiliza wengine.
      4. Lugha iliyoandikwa ni aina ya mazungumzo.
      5. Ujuzi mwingi katika kuzungumza hupatikana shuleni.
      6. Ujuzi wa kila siku husaidia katika maendeleo ya kusoma na msamiati.
      7. Husaidia kufahamu yaliyoandikwa.
      8. Hali ya mwanafunzi (pia) ni ujuzi. (8x1=8)
    2.  
      1. Karibu elimu yote imeandikwa vitabuni.
      2. Lugha zote hazina ustawi sawa.
      3. Zingine hazina vitabu vingi/zina vitabu vingi.
      4. Mwanafunzi anayesoma afaa kusoma mengi kando na taaluma anayoisomea. (4x1=4)
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Andika maneno yenye sifa zifuatazo za sauti:
      1. Kilainishoghuna cha midomo, irabuyambele-juu, kipuaghuna cha midomo, kizuiwa ghuna na irabu ya nyuma-wastani.(alama 1/0)
        • wimbo
      2. Kikwaruzo hafifu cha ufizi, irabu ya chini-kati, kikwamizo cha mdomo-meno hafifu, irabu ya mbele-juu.(alama 1/0)
        • safi
    2. Tunga sentensi ukitumia nomino ya ngeli ya KU pamoja na kirai husishi cha uhusiano.
      Kucheza kwa mtoto kutamfaidi.(alama 2/0)
            N         RH
      Kulima kwa bidii kunaleta mazao.
      Mtahiniwa sharti atumie nomino ya kitenzijina.
    3. Ainisha uamilifu wa kisarufi wa mofimu katika kitenzi hiki.
      Kilivijisha.
      Ki-mofimu ya ngeli
      li-mofimu ya wakati
      vi-mofimu ya watendwa/yambwa
      j-mzizi/shina
      ish-kauli tendesha
      a-kiishio
      (alama½ 3)
    4. Yakinisha kwa udogo ukitumia kiambishi cha masharti ya uwezekano.
      Mtoto asiyeiba Kitabu hajakamatwa.
      Kitoto kingeiba kitabu kingekamatwa. (alama 2/0)
    5. Andika upya sentensi kulingana na maagizo.
      Kiroboto huyo alituuma.Kiroboto aliuawa.(Tumia kivumishi kirejeshi cha kati kuunganisha.)
      Kiroboto huyo aliyetuuma jana aliuawa. (alama 1/0)
    6. Eleza matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
      Mola atakukirimu ukimtolea sadaka.
      Ku-nafsi ya pili umoja, ki-kuonyesha masharti (alama 1
    7. Andika upya sentensi hii kwawakati ujao hali katavu.
      Mwanariadha alishiriki mbio za Tokyo.
      Mwanariadha atakuwa hashiriki mbio za Tokyo.(alama
    8. Tunga sentensi moja kutofautisha vitate mji na mchi.
      1. Mji-makazi ya watu
      2. Mchi-kipande maalum cha mti kinachotumika kutwangia vitu kwenye kinu.
        Mfano
        Mama alitwanga mchele kwa mchi akiwa kwenye mji wa Kisumu.
        (alama 1
    9. Unda kitenzi kutokana na nomino maskani, kisha ukitungie sentensi.
      Maskani-sakini
      Sakini-kaamahali/fanya makazi
      Mfano
      Watalii wa Uingereza walisakini nchini mwetu kwa miaka miwili.
      Tathmini jibu la mtahini.(
      alama 1
    10. Bainisha kiima nayambwa katika sentensi hii.
      Omari alipewa vipuli na fundi stadi kwa bahasha.
      Fundi stadi-kiima
      Omari-yambwa tendewa
      Vipuli-yambwa tendwa
      Bahasha-yambwa ala
      (alama½
    11. Tunga sentensi kwa hali ya wastani ukitumia kihusishi cha hali.
      Vihusishi vya hali ni: kwa niaba ya, miongoni mwa, pamoja na
      Mfano
      Alitoa hotuba kwa niaba ya kiranja mkuu.
      Alikuwa miongoni mwa waliopewa zawadi.
      (alama
    12. Ainisha aina za vishazi katika sentensi hii.
      Marekebisho ya katiba ya BBI yatapita iwapo wananchi watahusishwa.
      Marekebisho ya katiba ya BBI yatapita-kishazihuru
      Iwapo wananchi watahusishwa-kishazitegemezi
      (alama 1
    13. Changanua sentensi hii kwa kielelezo cha mstari.
      Zohali na Zuhura ni majina yasayari.
      S-KN1(N+U+N) + KT(t+KN2(N+H+N))
      (alama KN=1/0, KT-1/0)
    14. Tunga sentensi moja ya kuonyesha matumizi mawili ya vielezi vya silabi moja.
      Alipokuja tulipokuwa tulifurahia. (po ya wakati na mahali)(alama 1
    15. Andika kinyume cha maneno yafuatayo.
      1. Dhahiri-siri
      2. Kavu-nyevu(alama 1
    16. Tambua hali katika sentensi ifuatayo.
      Ukulima wa sampuli hii wasumbua wengi.
      Hali isiyodhihirika/hali ya a (alama 1/0)
    17. Eleza maana ya msemo shika sikio.
      Shika sikio-jutia jambo/kupata funzo (alama 1/0)
    18. Tumia kibadala cha kiasi cha kuonyesha nafasi katika orodha kwenye sentensi.
      Wa kwanza/wa nne/wa kumi wameingia jukwaani. (alama 2)
    19. Andika kwa wingi sentensi hii.
      Ukwato wa mnyama huyo aliufikisha ufuoni.
      Kwato za wanyama hao walizifikisha fuoni. (alama 2)
    20.  
      1. Tunasema baraza la wazee mzengwe wa wagomaji na shuke/shazi la nafaka. (alama 1
      2. Audhubilahi ni tunapoapa la hasha!/kamwe!/hata!/ata!/mawe!/la! tunapokana na harambee! tunapohimiza. (alama 1)
  4. ISIMUJAMII
    1. Sajili ya kituo cha polisi
    2. matumizi ya:
      1. lugha ya adabu
      2. urasmi hudumishwa
      3. matumizi ya misimu
      4. kuchanganya ndimi
      5. kukosa usanifu na usarufi
      6. lugha ya matusihasa kwa washukiwa wakiwa ndani ya seli
      7. lugha ya kuhoji
      8. lugha ya kutisha
      9. istilahi za kisheria
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Bunamfan Post Mock 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest